ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 17, 2012

MUAMBA AZIMIA UWANJANI

Mechi kati ya Kombe la FA kati ya Tottenham na Bolton Wanderers ilisimamishwa ghafula baada ya mchezaji wa Bolton, Fabrice Muamba kuzimia ghafula, na kushindwa kuvuta pumzi.Madaktari walijaribu kwa dakika 10 kumfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aweze kupumua, na hilo liliposhindikana, ilimlazimu mwamuzi Howard Webb kusimamisha mchezo wakati ukiwa 1-1 katika dakika ya 41.

Muamba alizaliwa tarehe 6 Aprili mwaka 1988 mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, na aliimarika kisoka katika chuo cha vijana wadogo cha Arsenal, na akiiwakilisha England katika mechi mbalimbali, tangu zile za vijana wa miaka 16, hadi zile za wale wa miaka 21. Alijiunga na Birmingham mwaka 2007, na kuhamia Bolton mwaka uliofuata.

Tangu kufikishwa hospitali, hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusiana na hali yake ya afya hadi sasa.

MTENGENEZA FILAMU YA KONY ADATA

Mkurugenzi wa filamu, Jason Russell, ambaye filamu yake inayo mshambulia kiongozi wa wapiganaji wa Uganda, Joseph Kony, ilizagaa kwenye mtandao wa internet, inaelekea amepata ugonjwa wa akili.

Shirika lilofanya filamu hiyo, liitwalo "Invisible Children", limesema kuwa Bwana Russell amelazwa hospitali kutokana na machofu, kiwiliwili kuwa kikavu, na njaa.

Shirika la "Invisible Children", lilisema zogo lilozuka baada ya filamu hiyo, limesumbua roho za wanachama wote; na hasa Bwana Russell.

Ripoti zinasema kuwa Jason Russell amekutikana hakujistri sawasawa, akipiga kelele mabara-barani, mjini San Diego, California.

Filamu hiyo ya nusu saa, iliyotoa wito kuwa Joseph Kony akamatwe, ilizagaa kwenye mitandao, na kuwasikitisha wengi, lakini baadhi ya watu wanaona filamu haikueleza vita vya Uganda vilivyo.

Chanzo bbc

WAKUU WA MIKOA MIPYA

Huyu ndiye Mkuu wa Mkoa Mpya wa Geita Magalula Said Magalula
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.

Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2012

Thursday, March 15, 2012

MKUU WA MKOA WA MWANZA ERNEST NDIKILO ASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA HAKI ZA MLAJI

Maadhimisho ya SIKU YA MLAJI DUNIANI ambayo 2012kitaifa yamefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Makongoro yamehitimishwa leo kwa maandamano yaliyofanyika kuanzia ofisi za Halmashauri ya jiji na kuishia eneo la tukio. Kauli mbiu ya mwaka huu ni FEDHA ZETU HAKI YETU (OUR MONEY OUR RIGHT).

Tuliongozwa na brass bendi ya vijana hawa.

Waandamanaji na ujumbe toka Baraza la ushindani.

Walaji wawakilishi toka shule za sekondari.

Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikiro pamoja na meza kuu walipokea maandamano hayo kwenye viwanja vya Makongoro.

"Natoa changamoto kwa NGO, msiishie kwenye kuunda asasi za kupambana na Ukimwi, Watoto yatima na mengine bali pia mjitokeze katika haya ili kuweza kushirikiana pamoja na serikali katika kumtetea mlaji kwani eneo hili linahitaji nguvu kubwa toka kwa asasi zisizokuwa za kiserikali kwani hatujamtetea mlaji vya kutosha" by mkuu wa mkoa.

Mh. Ndikilo akipata maelezo toka kwa bw. Joshua Msona Afisa mwandamizi mtetezi wa walaji pindi alipopata fursa ya kutembelea moja ya mabanda viwanjani hapo.

Wananchi wengi wamekuwa wakilanguliwa sana nauli kwa vituo mbalimbali vya daladala jijini hapa hivyo walipata fursa ya kupata chati za nauli kwa njia zote za safari toka katika banda la SUMATRA CCC kama mama huyu.

Wanazuoni nao wakizipitia chati za nauli.

"Aisee unaonaee.. jamaa wanatuibia" akiwa na wenzake alisikika akisema jamaa mwenye t-shirt ya njano mara baada ya kuipitia chati ya bei za nauli kwa ruti za ndani na nje ya jiji la Mwanza.

KWANINI MAMA HUYU ALIFUMUA SHUTI KALI KIASI HIKI KWA MWANAYE? NAHITAJI JIBU TOKA KWA WAJUZI WA SOKA


Mtoto mzuri alikuwa akisumuna gozi kwenye viwanja vidogo vya wazi, probably pretending he's Gareth Barry. Mama yake akaamua kujumuika kucheza naye -- sweet Moses! For some reason she hauls off and blasts the ball right into her son's face from just a few inches away. Why does she kick it that hard?! His jaunty hat pops right off!

The kid, of course, starts to cry and she tries to console him -- thankfully not by launching the ball at him again. Baada ya kutoa machozi kadhaa na tabasamu la mtoto kurejea, mtoto huyo kulingana na uwezo wa nguvu ya mguu wake aliuendea mpira na kuupiga mbali toka eneo alilokuwa mama yake ... kwanini?
NASUBIRI MAJIBU..

GALILE VS MASHALI WATAMBIANA KILA MMOJA KUNYAKUA UBINGWA

MABONDIA Selemani Galile na Thomas Mashali wanatarajia kupanda ulingoni Aprili 9 kuwania mkanda wa ubingwa wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO) litakalofanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese Dar es Salaam.
Mabondia, Selemani Galile kushoto na Tomasi Mashali wakitazamana kwa usongo wa kila mmoja kutaka kuchukua mkanda wa ubingwa wa mchezo wa masumbwi wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini TPBO walipokuwa wakitambulisha mpambano wao. Dar es Salaam jana, utakaofanyika Apri 9.katikati ni Rais wa Oganaizesheni hiyo Yasin Abdallah Mwaipaya.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Pambano hilo linatarajiwa kuwa kati uzito wa kg 75 raundi 10 likiratibiwa na TPBO.
Wakitambiana Dar es Salaam jana, wakati wa kuonyeshwa mkanda huo Galile alisema atahakikisha anafanya mazoezi ya kutosha ili kuweza kuunyakua mkanda huo kwani anauhakika atauchukua kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao. "Mkanda lazima niiuchukue kwani najua Mashali haniwezi na hataweza kunifanya nisichukue mkanda hivyo najiamini na mkanda ni wangu," alisema Galile.

Naye kwa upande wake Mashali alisema raundi 10 ndio zitaamua mkanda ni wanani lakini anaimani ataunyakuwa kwani anamazoezi ya kutosha na bado ataendelea kujifua na kuhakikisha anaibuka bingwa."Ninauwezo, nimejipanga na ninauhakika nitaunyakua mkanda lakini yote raundi 10 ndio zitaamua nani bingwa," alisema.

Upande wake Rais wa TPBO, Yassin Abdalah alisema mkanda huo ulikuwa wazi hivyo wakaamua kuwaambia mapromota ambapo alijitokeza Prospa Rweyomamu ambaye ndio ameandaa pambano hilo hivyo bingwa atakayepatikana ndio utakuwa kwake akisubiri mpinzani

Mbali ya kuwepo na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na huuzwaji wa DVD za Mafunzo ya Mchezo wa Masumbwi wakiwemo mabondia Lenox Lewis, Evander Holfiled, David Haye, Waldmil Klitichiko, Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roj Jones na wengine wengi zitakuwa zikisambazwa kwa ajili ya kuwapa mabondia, mashabiki na marefarii kutambua sheria na kanuni za mchezo huo Duniani ambazo zimeandaliwa na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila Super D Alisema kuwa tangia aanze kutoa mafunzo kwa njia hiyo watu wengi wameanza kuwa na uwelewa wa mchezo wa masumbwi nchini kwa kutambua sheria na mambo mbalimbali ya mchezo alisema Super D boxing Coach ambapo mpaka sasa ameweza kutoa matoleo nane tofauti ya mabingwa wa ngumi Duniani Akichanganya na mabondia wa Nchini.

Wednesday, March 14, 2012

MAONYESHO SIKU YA MLAJI KILELE CHAKE LEO.

Joshua Msona Afisa mwandamizi mtetezi wa walaji akizungumzia maonyesho ya SIKU YA MLAJI ambayo kitaifa mwaka huu 2012 yanafanyika Mwanza katika viwanja vya Makongoro ambapo leo tarehe 15/03/2012 ndiyo kilele. Kauli mbiu ya mwaka huu ni FEDHA ZETU HAKI YETU (OUR MONEY OUR RIGHT).
NYOTE MNAKARIBUSHWA

MDAHALO WA WAZI KWA WALAJI WAFANYIKA NDANI YA MAADHIMISHO SIKU YA MLAJI KITAIFA MWANZA

"Pamoja na kwamba tunapaswa kuzingatia kuepuka kununua bidhaa feki na kukemea huduma zisizokuwa na viwango pia tunapaswa kulinda miundo mbinu inayo sukuma huduma iwe ya mtu binafsi au serikali kwani inatuhudumia sisi" by Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Ilemela Said Amanzi.

Karibu katika banda la Baraza la Tume ya Ushindani na Udhibiti Bidhaa Bandia.

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Said Amanzi sambamba na wanafunzi akipata maelezo toka kwa msemaji wa Baraza la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA CCC, Erasto Kishe

Wandishi Devota Kabambo na Mtangazaji wa Radio IQRA wakipata maelezo toka kwa mdau wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA CCC)

Karibu katika banda la Baraza la Ushauri Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania. "Lengo kuu ni kujenga msingi imara utakao linda na kuboresha maslahi na haki za watumiaji wa huduma za usafiri wa anga nchini kwa kutengeneza mazingira mazuri ya kushauriana, kuhamasisha utetezi katika mambo yote yanayogusa maslahi na haki za watumiaji wa usafiri wa anga" by msemaji bi Catherine Monarya (L)

KISHA MDAHALO UKAFANYIKA
Katibu Mtendaji Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini SUMATRA CCC, Oscar Kikoyo akijibu maswali kwenye mdahalo.
Mdahalo wa wazi wa watumiaji (Open consumer dialogue) uliowakutanisha wanazuoni, wanafunzi na walaji kwa ujumla ulifanyika kwenye viwanja hivyo vya maonyesho ambapo mambo mbalimbali yaliibuliwa na kupatiwa majibu.

Mdahalo umefanyika leo hapo hapo kwenye maonyesho, Viwanja vya Makongoro jijini Mwanza ambapo ni kitaifa na kesho maonyesho hayo yatahitimishwa.

Picha ya pamoja.

Tuesday, March 13, 2012

MSONDO YENDELEA KUGAWA DOZI ZA KIUTU UZIMA

Waimbaji wa bendi ya Msondo ngoma wakiimba wakati wa onesho lao lililofanyika jumapili katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kutoka kushoto ni Hasani Moshi,Shabani Dede,Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila Super D na mwimbaji Juma Katundu.

Wadau wakila raha....haya twendeeeee!!!!

Msanii Mpya wa bendi ya Msondo ngoma, Shabani Lendi (kushoto) akipuliza Saxphone wakati wa onesho la bendi hiyo iliyofanyika jumapili katika Ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni wengine ni Hamisi Mnyupe, Romani Mngande na Msemaji wa Bendi hiyo Rajabu Mhamila Super D.
(Picha na www.burudan.blogspot.com)

KALIWA BURE........!!!!!

John alimwalika rafiki yake Fred nyumbani kwake kwa ajili ya dinner na vinywaji. Baada ya maakuli na wakati vinywaji vinaendelea, mkewe John (Lisa) na mgeni wao Fred walikuwa wanacheza karata.... Kwa bahati mbaya karata ikaangukia chini ya meza, Fred alipoinama kuichukua akaona nyeti za Lisa ambae hakuwa amevaa chupi. Fred akahamanika kwa aibu, japo John hakukugundua.

Baadae kidogo John alipokwenda jikoni kuchukua vinywaji,
Lisa akamuuliza Fred: "Umekipenda ulichokiona?"
Fred: "Ndiyo".
Lisa: Utakipata kwa laki moja, ila iwe ijumaa mchana maana John huenda site visits kwa wateja wake kila ijumaa.
Ijumaa ikafika, Fred akaja kwa John na laki na mchezo ukachezwa. John aliporudi jioni akamuuliza mkewe: "Fred alikuja?"
Lisa akawaza:'Inawezekana alimuona akija au kaambiwa', akajibu: "Ndiyo, alipita hapa mara moja".
John: "Safi, alikuachia laki moja?"
Lisa akawaza: 'Huyu atakuwa anajua'.
Akamjibu mumewe kwa upole: "Ndiyo, kaileta".
John: "Fred ni mwaminifu sana, alikuja asubuhi ofisini akanikopa laki moja na akasema atapita nyumbani akuachie mchana"

Lisa akabaki ametoa macho kumbe ametoa bure!!!

Kituko na Starehe mushi

NILIICHELEWESHA HII: NAPE AJIUNGA TWANGA PEPETA?

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye hivi karibuni alipata fursa ya kipekee kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao mazoezi ndani ya ofisi za Aset.
Anamudu vilivyo gitaa la Solo

Hapa akionyesha mautundu katika Tumba, pembeni yake ni Victor Nkambi na Msafiri Diouf

Asha Baraka akimfurahia Nape wakati akifanya vitu vyake

Akipapasa Kinanda

Kija akimwangalia kwa makini Nape akipiga gitaa la Bass!

Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba.

Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki.

Aidha Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye bendi mara tu atakapo amua kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.

UMUHIMU WA KUDAI RISITI BY EWURA CCC.

Kuwa na risiti kwa huduma mteja aliyopata ni hatua ya kwanza muhimu katika kuwasilisha malalamiko iwapo mtumiaji atakuwa na malalamiko kuhusu huduma aliyopata. Msikilize mr. Erasto Kishe Muelimishaji toka EWURA CCC hili ni Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji ambaye aliyasema hayo jana katika maonyesho ya Siku ya mtumiaji kujifunza jinsi ya kung'amua bidhaa feki ili kutumia bidhaa zenye ubora unaokidhi viwango yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Makongoro jijini Mwanza.

Risiti ni uthibitisho.

PANGA LAISHUKIA KLABU YA YANGA

Wachezaji wa Yanga na sheshe la refa.

Kamati ya mashindano ya TFF imewafungia wachezaji watano wa Yanga kutokana na vurugu zilizotokea hapo siku ya jumamosi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam Fc,

Wachezaji waliofungiwa ni Stephano Mwasika aliyefungiwa mwaka mmoja huku Nadir Haroub na Jerry Tegete wakifungiwa jumla ya michezo sita, Nurdin Bakari na Omega Seme wamefungiwa kila mmoja michezo mitatu.

Huku Yanga ikipigwa faini ya shilingi milioni 4.5.


Hisani ya http://www.shaffihdauda.com/

Monday, March 12, 2012

BIDHAA FEKI ZINAVYOZIDI KUMWONGEZEA UMASIKINI MTANZANIA

SI KATIKA MADAWA, CHAKULA, VIFAA, BIDHAA MBALIMBALI WALA HUDUMA ZA USAFIRI NA UMEME TUSIPOKUWA MAKINI TUTAKWISHALeo Jijini Mwanza kwenye uwanja wa Makongoro kuna maonyesho ya Siku ya mtumiaji (mlaji)kujifunza jinsi ya kung'amua bidhaa feki ili kutumia bidhaa zenye ubora unaokidhi viwango.

Chunguza mjomba kabla hujaliwa... Bidhaa inayotambulishwa kwenye box jina lake ni tofauti na jina la bidhaa ndani ya box.

Kisha Soma kwa makini jina la bidhaa jeh linaandikwa hivi (SUMSNUG)?

"Ndiyo maana mbu hawafi..." says Katu, Wandishi wa habari wakishirikiana kung'amua bidhaa feki kwa dawa ya mbu ya Rungu, kutoka kushoto ni Emmanuel Chacha wa ITV, Fredrick Katulanda wa gazeti la Mwananchi na Mpiga picha wa ITV Steward Duguda.

Sambamba na mapungufu mengi katika bidhaa feki ikiwa ni pamoja na dawa kutokuwa na uwezo wa kuangamiza wadudu kama ilivyo kwa bidhaa halisi, bidhaa feki utaigundua kwa maandishi yake kupishana, baadhi ya maneno au herufi kuachwa au kuongezwa katika jina au nembo ya bidhaa. Fuatilia mfano ufuatao:-
a - hakuna jina la mzalishaji ktk bidhaa feki.
b - kuna jina la mzalishaji ktk bidhaa halali.


Kwa karibu zaidi.

Ufungashaji wa bidhaa huwa siyo bora ukilinganishwa na ule wa bidhaa halisi.

Haki na wajibu wa mlaji.

Maadhimisho haya ambayo kwa mwaka huu kitaifa yanafanyika mkoani Mwanza yanafanywa kwa harakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na maonyesho na kauli mbiu yanataraji kufikia kilele chake tarehe 15/03/2012 chini ya kauli mbiu 'FEDHA ZETU HAKI YETU' ikiwa ni kampeni kuwasaidia wananchi katika kupata huduma bora za kifedha.

WALIO MWIBIA NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI WANASWA

Watu watano wanaotuhumiwa kumuimbia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, wametiwa mbaroni baada ya kukamatwa usiku wa kuamkia jana katika Kata ya Chamwino, Manispaa ya Morogoro. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ( kati kati) akiwafafanulia Waandishi wa Habari ( hawaonekani pichani), namna alivyoibiwa baada ya dirisha la chumba chake kuvunjwa na wezi katika Hoteli ya Kitalii ya Nashera ya Mjini Morogoro. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini , Innocenti Kalongeries na mwingine ni Meneja wa Hoteli hiyo, Eustusi Mtua .( Picha na John Nditi wa Habari leo).
Baadhi ya vitu alivyoibiwa Malima ikiwemo simu na kompyuta mbili vimepatikana katika maeneo ya Kata ya Kichangani na Mafiga.

Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Morogoro, Hamis Seleman, alisema watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Chamwino walikamatwa usiku wa kuamkia jana.

Alidai kuwa vijana hao baada ya kuwibia Malima, vifaa mbalimbali zikiwemo dola za Marekani 4,000 walienda kuzibadilisha dola hizo katika duka la kubadilisha fedha za kigeni eneo la Posta na kupata Shilingi ya Tanzania na kugawana.

Inatajwa kuwa watuhumiwa hao baada ya kuiba simu hizo, walishindwa kuziuza kwa kuwa zilikuwa na picha ya Malima akiwa na mwanawe ambayo walishindwa kuiondoa.

Sunday, March 11, 2012

JAPAN YAKUMBUKA WALIKUFA KWA TSUNAMI

Raia wa Japani walikaa kimya kwa dakika moja kukumbuka siku kama ya leo mwaka mmoja uliopita ambapo tetemeko la ardhi na tsunami lilikumba kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shughuli za usafiri zilisimama hadi Sendai Air Port huku wananchi wakiwakumbuka takriban watu 20,000 waliokufa au kupotea kwenye maafa hayo.

Janga hilo pia lilisababisha miale ya nuclear kuchiririka kutoka kinu cha umeme cha Fukushima na kupelekea Japani kufikiria upya sera zake za nishati.

Wengi walikosa makazi.

Tizama makontena katika yard hii ya moja ya bandari yalivyokusanywa kama viberiti...

Mfalme Akihito na Waziri Mkuu Yoshihido Noda waliongoza maombi ya kitaifa mjini Tokyo. Mfalme alisema kuwa Japani haifai kusahau majanga yaliyoikumba iwapo inataka kuwa taifa salama na lilostawi katika siku za usoni.