Pichani kulia ni mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Mc Shujaaa-Mwanza, Adam Mchomvu akimtangaza mshindi wa shindano la Serengeti Mc Shujaaa, aitwaye Ramastar pichani shoto ndani ya jijini la Mwanza.Shindano hilo limefanyika jioni ya leo kwenye kiota cha maraha cha Clup Lips, Isamilo jijini humo.
Katika mchakato wa shindano hilo kulikuwepo na msisimko mkubwa kwa vijana wengi kujitokeza na kushiriki kikamilifu na kuwa ushindani mkubwa,aidha walijitokeza vijana wapatao 56, kisha 15 na hatimaye kupatikana mshindi mmoja ambaye atakwenda Dar kushindana na wengine kutoka mikoa mbalimbali kwenye kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lililopangwa kufanyika katika viwanja vya Lidaz Club, Kinondoni.
Nikuchanana tu kama sehemu ya misingi husika ya game ya Hip-hop ndani ya Lips Club.
Mashabiki na chata zao za wakali waliotamba katika hip-hop hawakukosekana ulingoni.
Top four ikiwa na Clouds Crew. Baba Jonii (L) na Ncha kali (R)
Hakuna kinyang'anyiro kilichokuwa 'tite' kama hiki cha Ramstar anayemchana Pusha.
Mashabiki walijipanga... ile kisawasawa...
Ni Ramstar(L) na Ramside(R) katika fainali.
Pichani kulia ni mmoja wa majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012,Prodyuza Duke akizungumza machache kabla ya shindano halijaanza,shoto kwake ni jaji mwingine na pia ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akisikiliza kwa makini.
Mc Baba Jonii akirusha shiringi kutafuata nani aanze katika fainali ya Mc Shujaa Mwanza kati ya Ramside kushoto na Ramstar aliyesimama kulia huku kamera ya Clouds Tv ikinasa kinacho endelea..