Saturday, January 27, 2024
RAIS SAMIA KUTUA MWANZA KUGAWA BOTI NA VIZIMBA VYA SAMAKI
NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amebainisha Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili kuanzia Jumatatu 29-30, 2024 ambapo atazindua Ugawaji wa Boti na Vizimba vya Samaki. Makalla amesema hayo mapema leo januari 26, 2024 wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ukimhusisha pia Ujumbe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Kufuatia Ugeni huo Makalla amewakaribisha wananchi wa Mwanza na Mikoa ya jirani kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza siku ya jumatatu kwa ajili ya kumpokea na kumlaki pamoja na siku ya jumanne kwenye uwanja wa Nyamagana. "Tarehe 30 januari, 2024 Mhe. Rais atazindua Ugawaji wa zana za Uvuvi za Kisasa kwa ajili ya Uvuvi endelevu vikiwemo Boti na Vizimba pamoja na kuzungumza na wananchi wa kanda ya Ziwa kwenye viwanja vya Nyamagana, hivyo basi nawaalika wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza." CPA Makalla. Aidha, amefafanua kuwa Rais Samia baada ya kuwasili Mwanza siku ya Jumatatu atatumia barabara kuu ya kuelekea mjini hivyo wananchi wanaalikwa kumlaki barabarani kuanzia Sabasaba, Pasiansi, Bwiru na Kwenye Mzunguko wa Ziro ili kumshangilia na kumlaki.Friday, January 26, 2024
RC SENDIGA AKABIDHI PIKIPIKI 42 KWA JUMUIYA ZA MAJI RUWASA
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amekabidhi pikipiki 42 kwa jumuiya za watoa huduma za maji katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara ili kurahisisha utendaji kazi kwa watumiaji hao.
Pikipiki hizo zimetolewa na Wakala wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe. Sendiga amesema ni vyema kwa watumishi hao kuzitunza kwani ni mali ya serikali.
Akitoa shukrani zake kwa RUWASA Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange amesema kuwa atasimamia na kufuatilia kwa Ukaribu kama watumisji waliokabidhiwa pikipiki hizo wanazifanyi kazi kama ambavyo kusudio la Serikali ilivyowaagiza.
Amesema kuwa Mkoa wa Manyara unajumla ya Vyombo hivi 88 vinavyosimamia Skimu za maji 346 na kuhudumia wananchi 1,268,239 ambapo mpaka Septemba 30, 2023 zilikusanywa jumla ya Tshs 2,113,232,529", amesema Injinia Kilter.
Ameongeza kuwa RUWASA inaendelea kuvipatia mafunzo jumuiya za watumiaji Maji kama jinsi ya kuandaa mpango wa biashara na ufungaji wa hesabu, vyombo 32 vimeshapatiwa mafunzo hayo mpaka Julai 23, 2023.
KATIBU MKUU WA CCM TAIFA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
VICTOR MASANGU KIBAHA
WAZIRI AWESO AWASHA MOTO HUDUMA KUBORESHWA MAMLAKA YA MAJI ARUSHA,ATOA SIKU 30
RC KUNENGE AMPA KONGOLE RAIS SAMIA KWA KUTOA MATREKA MATATU KWA AJILI YA KILIMO
Wednesday, January 24, 2024
'MALIZIENI MIRADI KWA WAKATI' - RC SENDIGA
Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.
Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiteta jambo na Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini.
Mhe. Sendiga amejionea ujenzi huo huku akiwataka wataalamu hao kumaliza kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote vitavyosababisha ukwamishaji wa ujenzi huo.
Ujenzi huo unaogharimu shilingi Mil. 600 ambapo awamu ya kwanza wamepewa zaidi ya mil. 285 kwa ajili ya ukamilishaji wa Boma, msingi mpaka gorofa ya kwanza na sasa ujenzi umefikia asilimia 21.4.
Aidha Jeshi la Zimamoto Walimemshukuru Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwezesha majeshi ya Tanzania katika kukabiliana na majanga mbali mbali huku wakimshukuru Mhe. Sendiga na ofisi yake kwa ujumla kuweza kuwawezesha katika miongozo mbali mbali.
Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema utekelezaji unaoendelea ni awamu ya Kwanza ambayo ilianza baada ya Serikali kutoa fedha mnamo mwezi Aprili 2023 jumla ya shilingi milioni mia nane tu (TShs.800,000,000.00) ambazo zilipokelewa Polisi Mkoa Manyara.
Amesema kazi zilizofanyika ni ujenzi wa msingi, nguzo na sakafu za ghorofa zote nne huku wakifanya maandalizi ya ujenzi wa kuta za pamoja na kuezeka na ujenzi wa chumba cha mitambo ya lifti ambapo wanatarajia ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi Februari.
Nae Mhe. Sendiga amewapongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kutekeleza mradi kwa vitendo huku akizitaka taasisi nyingine zenye miradi mkoani humo kuiga Jeshi la Polisi.
Aidha Mhe. Sendiga amemtaka mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha ujenzi wa jengo la ofisi ya yake linakamilika kwa wakati maana ujenzi wake umekuwa ukisua sua jambo linaloleta ukakasi kila anapotembelea.
Jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Babati ambapo ujenzi wake umekuwa ukisua sua. (Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara)
TAWIRI NA MUENDELEZO WA TAFITI UGONJWA WA TWIGA ULIOATHIRI ASILIMIA 62 YA TWIGA KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUAHA.
Akizungumza wakati wa ufuatiliaji wa matibabu ya ugonjwa huo katika hifadhi ya Taifa Ruaha, Dkt. Julius Keyyu ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti TAWIRI, amesema ugonjwa wa ngozi wa Twiga uliogundulika katika hifadhi ya Taifa Ruaha mwaka 2000 ni tofauti na ugonjwa wa ngozi wa Twiga katika nchi nyingine duniani
" tumefuatilia ugonjwa huu kwa nchi nyingine duniani na kubaini upo tofauti na hapa nchini" amebainisha Dkt. Keyyu
Dkt.Keyyu amesema asilimia 62% ya Twiga waliopo hifadhi ya Taifa Ruaha wana ugonjwa wa ngozi ambao pia, umeonekana kwa kiwango kidogo katika hifadhi za Taifa za Tarangire na Serengeti, na tafiti za awali zimeonesha madhara ya ugonjwa huo ni pamoja na Twiga wenye ugonjwa kutembea kwa kuchechemea, hivyo kushindwa kukimbia wanapofukuzwa na wanyama wawindao pia hutembea umbali mdogo kwa siku, kwa wiki na kwa mwezi ukilinganisha na Twiga wasio na ugonjwa.
Dkt. Keyyu amesema kwa sasa TAWIRI inaendelea na ufuatiliaji wa matibabu ya ugonjwa huo ili kubaini kisababishi asili cha ugonjwa (_primary agent_) na kupata matokeo ya kushauri nini kifanyike ili kudhibiti ugonjwa huu wa ngozi wa Twiga na kuhakikisha mnyama huyu ambaye ni nembo ya taifa anazidi kuwepo.
Tuesday, January 23, 2024
SERIKALI YAIPONGEZA BARRICK KWA KUENDELEA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA KUPITIA UWEKEZAJI WAKE KATIKA SEKTA YA MADINI.