ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 26, 2024

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA AFUNGUKA JINSI WATAKAVYOSHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

VICTOR MASANGU KIBAHA

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa  Dkt. Emmanuel Nchimbi amewahakikishia wana chama kuwa ana  uhakika mkubwa  chama chake kitaibuka na ushindi mkubwa wa zaidi ya asilimia 100  kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa. 

Nchimbi ameyasema hayo wakati  alipokuwa akizungumza katika kikao cha Makatibu wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika kilichofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kwamfipa kilichopo Wilayani  Kibaha Kibaha mkoani Pwani.
"Nchi ya Afrika Kusini na Namibia watakuwa wakifanya uchaguzi wao mkuu, wakati Tanzania, mwaka huu na sisi tutakuwa  tukifanya  uchaguzi wa serikali za mitaa, na mwaka ujao, tutakuwa na uchaguzi mkuu niwahakikishie CCM utKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Emmanuel Nchimbi amesema ana uhakika chama chake kitafanya vizuri kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa zaidi ya asilimia 100.

Ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza katika kikao cha Makatibu wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika kilichofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kwamfipa Kibaha.

"Afrika Kusini na Namibia watakuwa wakifanya uchaguzi wao mkuu, wakati Tanzania, mwaka huu tutafanya uchaguzi wa serikali za mitaa na mwaka ujao, tutakuwa na uchaguzi mkuu niwahakikishie CCM itashinda kwa kishindo kikubwa " alisema Dkt Nchimbi.

Akizungumzia kuhusiana na mkutano huo na uwepo wa ujumbe wa chama Cha Kikomunist Cha nchini China (CPC) alisema, ni muendelezo wa mikutano iliyopita ya kujadili mambo mbalimbali ya vyama vyao. 

Pia alieleza kwamba CPC imekuwa rafiki mzuri na mshirika anayestahili wa vyama hivyo vya Ukombozi  tangu wakati wa mapambano ya ukombozi ya kisasa.

Kwa upande wa shule hiyo ya Uongozi Dkt Nchimbi alisema, kuwepo kwake ni miongoni mwa urithi ambao unazungumza mengi kuhusu muda na misimu yote ya mshikamano wa kindugu huku wakitazamia usaidizi unaoendelea, kwa mustakabali bora kwa manufaa ya pande zote za vyama hivyo.

Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere ni zao la azma ya muda mrefu la vyama vyetu kuwa na taasisi ambayo itatoa mafunzo ya uongozi na itikadi, hasa kwa vijana ambao ni kizazi kijacho kuchukua uongozi wa kuendelea na mapambano, ya kuwakomboa na kuwawezesha watu wetu kiuchumi na maisha bora.

"Nimpongeze mkuu wa shule, Prof. Marcelina Chijoriga, ambaye amekuwa akifanya kazi ya kupongezwa ili kuweka shule kwenye mstari, bila kuathiri maono na dhamira ya shule,"alisema.

Katika hatua nyingine aliwapongeza wafuasi wa Zanu-PF, wanachama, viongozi na watu wa Zimbabwe kwa kufanya uchaguzi mkuu wa kidemokrasia wenye amani, huru na wa haki, ambapo kiongozi kutoka chama hicho Emerson Mnangagwa alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.

Akizungumzia kuhusiana na mkutano huo na uwepo wa ujumbe wa chama Cha Kikomunist Cha nchini China (CPC) alisema, ni muendelezo wa mikutano iliyopita ya kujadili mambo mbalimbali ya vyama vyao. 

Kadhalika alieleza kwamba CPC imekuwa rafiki mzuri na mshirika anayestahili wa vyama hivyo vya Ukombozi  tangu wakati wa mapambano ya ukombozi ya kisasa.

Kwa upande wa shule hiyo ya Uongozi Dkt.Nchimbi alisema, kuwepo kwake ni miongoni mwa urithi ambao unazungumza mengi kuhusu muda na misimu yote ya mshikamano wa kindugu huku wakitazamia usaidizi unaoendelea, kwa mustakabali bora kwa manufaa ya pande zote za vyama hivyo.

Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere ni zao la azma ya muda mrefu la vyama vyetu kuwa na taasisi ambayo itatoa mafunzo ya uongozi na itikadi, hasa kwa vijana ambao ni kizazi kijacho kuchukua uongozi wa kuendelea na mapambano, ya kuwakomboa na kuwawezesha watu wetu kiuchumi na maisha bora.

"Nimpongeze mkuu wa shule, Prof. Marcelina Chijoriga, ambaye amekuwa akifanya kazi ya kupongezwa ili kuweka shule kwenye mstari, bila kuathiri maono na dhamira ya shule,"alisema.
Katika hatua nyingine aliwapongeza wafuasi wa Zanu-PF, wanachama, viongozi na watu wa Zimbabwe kwa kufanya uchaguzi mkuu wa kidemokrasia wenye amani, huru na wa haki, ambapo kiongozi kutoka chama hicho Emerson Mnangagwa alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo.

Dkt. Nchimbi  ameshiriki kikao na  cha siku tatu na Makatibu kutoka vyama vya Ukombozi  Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC cha Afrika kusini, SWAPO cha nchini Namibia, FRELIMO cha Msumbiji, MPLA cha Angola, ZANU - PF cha Zimbabwe na CPC Chama Cha kikomunisty cha nchini China.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.