|
Mwenyekiti wa TACOGA Elias Zizi. |
MWENYEKITI wa
Chama cha Wakulima nchini (TACOGA) na Katibu wake wamekamatwa na
jeshi la Polisi Wilayani hapa baada ya kufanya Mkutano wa hadhara kuzungumzia
umuhimu wa wakulima kutumia Mbegu za manyoya na kukataa kutumia zile zisizo na
manyoya za UK 91(Quton) kutokana na bei yake kuwa shilingi 1,200 kwa kilo moja.
|
Askari polisi walifika na kumsomba mwenyekiti huyo na katibu wake. |
Hatua hiyo ya
kukamwatwa kwa mwenyekiti huyo wa TACOGA Elias Zizi inafuatia kauli ya Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi Erasto Sima kutoa tamko la kuwakamata baadhi ya watu wakiwemo
wanasiasa wanaofanya mikutano ya hadhara na kuwahamasisha wakulima kukataaa
kutumia mbegu bora iliyopitishwa na Bodi ya Pamba nchini.
|
Haooo wakatembea. |
|
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima akijibu maswali ya wananchi. |
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Baiskeli kwa wakulima wawezeshaji 35 kutoka
vijiji 20 vya maeneo ya Wilaya ya Bariadi na Itilima Mkoani Simiyu zilizotolewa
na Bodi ya Pamba nchini kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU) ili kusaidia
kutoa elimu na mafunzo ya kilimo bora cha zao la pamba katika maeneo
mbalimbali.
Sima alisema
kwamba kumekuwa na tabia ya kuwahamasisha wakulima kukataa kutumia mbegu bora
ya Quton ambazo katika maazimio ya vikao mbalimbali vya wadau na Bodi ya pamba
viliadhimia kutumika kwa mbegu hiyo katika msimu wa kilimo unaoanza mwezi
Novemba mwaka huu ili kuboresha pamba na kuwa na tija kwa mkulima.
“Nimepewa taarifa kuwa
Mwenyekiti amekamatwa na askari polisi akiwahutubia watu kwenye mkutano wa
hadhara lakini imeonekana amekiuka kibali chake na kuanza kuwahamasisha
wakulima na wananchi kuwapiga mawe maafisa wa Bodi ya pamba na wataalamu
watakaopeleka mbegu za Quton kwenye vijiji ili kuziuza na kuzipanda” alisema
Mkuu huyo alisema
kwamba taarifa za kukamatwa kwa Zizi hazihusiani moja kwa moja na kile
alichokisema siku moja tu baada ya kukabidhi baiskeli zilizotolewa na Bodi ya
Pamba katika Mradi wa kilimo cha Biashara sehemu ya Pili (TASP II) katika
Wilaya za Meatu, Maswa na Bariadi katika Mkoa wa Simiyu kama ilivyoelezwa na
Mratibu Renatus Luneja.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa TACOGA Zizi alisema kitendo cha kukamatwa kwake kimemushanghaza
sana na kudai kuwa juhudi za kuendelea kuwapigania wakulima
ataendelea nazo kwa kuwa yeye ndiye kiongozi wao aliyepo madarakani kikatiba
kamwe hatarudi nyuma
Naye Katibu wa
TACOGA , George Mpanduji amesema kwamba wakulima wanahaki ya kufahamu kupitia
viongozi wao juu ya nini cha kufanya kabla ya msimu wa kilimo kuanza mwezi
Novemba mwaka huu hivyo kufanyika kwa mikutano hiyo imelenga
kuwahamasisha wakulima kulima na kutumia mbegu bora na si kama inavyodhaniwa.
“Tuwaache
wakulima kuchaguwa mbegu watakazotumia kwenye kilimo badala ya kuwalazimisha
kutumia mbegu za Quton ambazo bie yake ni kubwa kutokana na baadhi yao
kushindwa kumudu bei hiyo kutokana na kuwa na gharama kubwa kuliko uwezo”
alisisitiza Mpanduji .