ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 31, 2013

MWENYEKITI NA KATIBU WA TACOGA WAKAMATWA BARIADI

Mwenyekiti wa TACOGA Elias Zizi.
 MWENYEKITI wa Chama cha Wakulima nchini (TACOGA) na Katibu wake  wamekamatwa na jeshi la Polisi Wilayani hapa baada ya kufanya Mkutano wa hadhara kuzungumzia umuhimu wa wakulima kutumia Mbegu za manyoya na kukataa kutumia zile zisizo na manyoya za UK 91(Quton) kutokana na bei yake kuwa shilingi 1,200 kwa kilo moja.

Askari polisi walifika na kumsomba mwenyekiti huyo na katibu wake.
Hatua hiyo ya kukamwatwa kwa mwenyekiti huyo wa TACOGA Elias Zizi inafuatia kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima kutoa tamko la kuwakamata baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa wanaofanya mikutano ya hadhara na kuwahamasisha wakulima kukataaa kutumia mbegu bora iliyopitishwa na Bodi ya Pamba  nchini.
Haooo wakatembea.
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Erasto Sima akijibu maswali ya wananchi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Baiskeli kwa wakulima wawezeshaji 35 kutoka vijiji 20 vya maeneo ya Wilaya ya Bariadi na Itilima Mkoani Simiyu zilizotolewa na Bodi ya Pamba nchini kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU) ili kusaidia kutoa elimu na mafunzo ya kilimo bora cha zao la pamba katika maeneo mbalimbali.

Sima alisema kwamba kumekuwa na tabia ya kuwahamasisha wakulima kukataa kutumia mbegu bora ya Quton ambazo katika maazimio ya vikao mbalimbali vya wadau na Bodi ya pamba viliadhimia kutumika kwa mbegu hiyo katika msimu wa kilimo unaoanza mwezi Novemba mwaka huu ili kuboresha pamba na kuwa na tija kwa mkulima.

“Nimepewa taarifa kuwa Mwenyekiti amekamatwa na askari polisi akiwahutubia watu kwenye mkutano wa hadhara lakini imeonekana amekiuka kibali chake na kuanza kuwahamasisha wakulima na wananchi kuwapiga mawe maafisa wa Bodi ya pamba na wataalamu watakaopeleka mbegu za Quton kwenye vijiji ili kuziuza na kuzipanda” alisema

Mkuu huyo alisema kwamba taarifa za kukamatwa kwa Zizi hazihusiani moja kwa moja na kile alichokisema siku moja tu baada ya kukabidhi baiskeli zilizotolewa na Bodi ya Pamba katika Mradi wa kilimo cha Biashara sehemu ya Pili (TASP II) katika Wilaya za Meatu, Maswa na Bariadi katika Mkoa wa Simiyu kama ilivyoelezwa na Mratibu Renatus Luneja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACOGA Zizi alisema kitendo cha kukamatwa kwake kimemushanghaza sana na kudai kuwa juhudi za  kuendelea kuwapigania wakulima ataendelea nazo kwa kuwa yeye ndiye kiongozi wao aliyepo madarakani kikatiba kamwe hatarudi nyuma
Naye Katibu wa TACOGA , George Mpanduji amesema kwamba wakulima wanahaki ya kufahamu kupitia viongozi wao juu ya nini cha kufanya kabla ya msimu wa kilimo kuanza mwezi Novemba mwaka huu hivyo kufanyika kwa mikutano hiyo  imelenga kuwahamasisha wakulima kulima na kutumia mbegu bora na si kama inavyodhaniwa.


“Tuwaache wakulima kuchaguwa mbegu watakazotumia kwenye kilimo badala ya kuwalazimisha kutumia mbegu za Quton ambazo bie yake ni kubwa kutokana na baadhi yao kushindwa kumudu bei hiyo kutokana na kuwa na gharama kubwa kuliko uwezo” alisisitiza Mpanduji .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.