Saturday, August 28, 2010
HABARI
MAMA CELINA VUNA MABOKO ANAYEISHI KIBONDO KIJIJI CHA LUGUNGA LUTALE MKOANI KIGOMA, AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUSHAMBULIWA KWA MAPANGA NA MUMEWE BW. MZONGOLI MABONDO (50) TUKIO HILO LILITOKEA WIKI MOJA ILIYOPITA NYUMBANI KWAKE HUKO KTK KIJIJI CHA LUTALE.
MAJEREHA YA KICHWANI.
KATIKA TUKIO HILO MAMA HUYO LICHA YA KUPATA MAJERAHA MABAYA KICHWANI, ENEO KUBWA LA MGONGONI NA SEHEMU ZA BEGA LA KUSHOTO VILEVILE MWANAMAMA CELINA KAKATWA KABISA MKONO WAKE WA KUSHOTO NA KUBAKIA KIGUTU'.
SABABU ZA KUTOKEA KWA TUKIO HILO LA KIKATILI NI MUME KUDAI MAMA HUYO AMRUDISHIE PESA ZAKE SHILINGI ELFU 40 ALIZOTOZWA KWENYE OFISI YA MTENDAJI WA KIJIJI KUMLIPA FIDIA MAMA CELINA BAADA YA MUME HUYO KUZICHOMA MOTO NGUO (KANGA, VITENGE NA BLAUZI)ZA MKE HUYO WA KWANZA KISA AKIMTUHUMU MAMA HUYO KULA MAHALI ISIYOFAHAMIKA YA BINTI YAO WA KWANZA.
MAJIRA YA SAA 3 MARA BAADA YA CHAKULA CHA USIKU CELINA AKIWA NA MWANAE MDOGO JESKA WALISIKIA MLANGO UKIGONGWA KWA NGUVU NA MUMEWE HUYO BW. NZONGILI MABONDO.
NDIPO MLANGO UKAFUNGULIWA NA MTOTO JESCAR.
MKONONI AKIWA AMESHIKA PANGA BW. NZOGOLI AKAINGIA KWA GHADHABU NDANI YA NYUMBA HIYO NA KUANZA KUMJERUHI KWA PANGA MKEWE CELINA HUKU AKIMKARIPIA "UTANILIPA PESA YANGU ELFU AROBAINI..." MAPANGA YAKAENDELEA TWAAA!, SHWAAA!, PAAA! MWISHOWE MUME HUYO KUONA AKIELEWEKI AKATIMUA NA MKEWE WA PILI ALIYE SINDIKIZANA NAE HADI NYUMBA YA BI MKUBWA KISHA KUACHWA CHINI YA MTI NJE, WAKATI BWANA HUYO AKIFANYA UNYAMA HUO.
DAKIKA CHACHE BAADAE MAJIRANI WAKAFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFUATIWA NA POLISI, NDANI YA NYUMBA WAKIKUTA DAMU ZIKIWA ZIMETAPAKAA NAE MAMA CELINA AKIWA HAJITAMBUI, NDIPO WALIPOCHUKUWA JUKUMU LA KUMKIMBIZA KWA AMBULANCE HADI HOSPITALI YA BUGANDO JIJINI MWANZA.
CELINA AMBAYE KWA HIVI SASA ANAENDELEA KUPATA MATIBABU BUGANDO HOSP ANASEMA ALISHITUKIA YUKO KWENYE KITANDA ASIJUWE WAPI, AKIWA AMEZUNGUKWA NA MADAKTARI. NA ANASEMA ALILIA SANA SIKU YA PILI POLISI WALIPOMLETEA KIPANDE CHA MKONO WAKE WA KUSHOTO KILICHOKATWA AMBACHO HAKIKUWEZA KUUNGIKA TENA. INGAWA HANA MSAADA KWA SABABU NDUGU ZAKE NA MARAFIKI WAKO MBALI, LAKINI HALI YA MAMA HUYO INAENDELEA VIZURI.
MTUHUMIWA AMETOWEKA NA ANASAKWA NA JESHI LA POLISI, NAYE MKE MDOGO YUKO MAHABUSU.
HIMA KWA YEYOTE MWENYE MSAADA.
Saturday, August 28, 2010
BANGO
YULE MBLOGISHAJI MAARUFU NCHINI (LONG TIME KWENYE GAME) ISSA MICHUZI -EI KEI EI- 'ANKAL' LEO NI SIKU YAKE YA KUZALIWA.
Ankal (KULIA) akipongezwa na mgombea ubunge wa Kasulu Mashariki Bw. Jamal Abdallah walipokutana usiku wa kuamkia leo mjini Kigoma. Bw. Abdallah, ambaye ni mdogo wake mchambuzi wa kandanda Dokta Liky Abdallah, alishinda kwa kishindo katika kura za maoni na kumwondoa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Bw. Kilontsi Mpologomyi na wagombea wengine.
SOGGY, TIRA HASSAN NA MAREHEMU MNOMBA ENZI ZA UHAI WAKE.
MNOMBA NJAIDI AMBAYE ZAMANI ALIKUWA MENEJA WA KITUO CHA REDIO TRIPLE A YA MJINI ARUSHA AKISHIRIKI KAMA DJ NA PROMOTER, AMEAGA DUNIA JANA USIKU MJINI CORK, NCHINI IRELAND. INAELEZWA KUWA MAREHEMU ALIPATA STROKE MAJIRA YA USIKU HATA MAUTI KUMKUTA.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
Amin.
HABARI PICHA KWA HISANI YA MICHUZI JR.
Friday, August 27, 2010
HABARI
MWAI KIBAKI AKITIA SAINI.
Kenya imeandika historia mpya ya utawala nchini humo kwa kuidhinisha katiba mpya, iliyotungwa na wananchi wenyewe, baada ya ile iliyokuwa ikiitumia kabla ya kupata uhuru wake mwaka 1963.
Rais Mwai Kibaki, aliwaongoza maelefu ya raia wake walioshuhudia akitia saini katiba mpya ya nchi hiyo katika sherehe zilizofanyika viwanja vya Bustani ya Uhuru mjini Nairobi siku ya Ijumaa.
Baada ya kutia saini nakala sita za katiba hiyo, wimbo wa taifa la Kenya ukapigwa na kufuatiwa na mizinga 21 ya heshima.
Rais Kibaki, Waziri Mkuu Raila Odinga, Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Spika wa bunge na wabunge wamekula kiapo cha kuilinda, kuitetea, na kuiheshimu katiba hiyo mpya kwa manufaa na ustawi wa taifa la Kenya na watu wake.
MWELEKEO MPYA.
Katiba hiyo imepangwa kuzuia aina yoyote ya vurugu kama zile zilizofuatia baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, wakati zaidi ya watu elfu moja waliuawa kutokana na mgogoro wa kupinga matokeo yaliyompa ushindi Rais Kibaki.
Pia ina udhibiti mkubwa kuhusu madaraka ya rais, na inatoa madaraka kwa serikali za majimbo na kuwaongezea uhuru wananchi.
UTATA.
Miongoni mwa viongozi wa mataifa ya kigeni waliohudhuria ni Rais Omar Al Bashir wa nchi jirani ya Sudan ambaye anatakiwa na mahakama ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita, kwa tuhuma za kuendesha mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Kufika kwake katika sherehe hizo kumeonekana kuyakera baadhi ya makundi yakiwemo ya haki za binadamu na mabalozi hususan kutoka nchi za magharibi.
Afisa mkuu wa Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Kenya, Muthoni Wanyeki ni miongoni mwa watu walioishutumu serikali ya Rais Kibaki kumwaalika kiongozi huyo wa Sudan.
Wanyeki amekaririwa akisema " Ni aibu kwa Wakenya ambao waliuchagua utawala ambao unatakiwa kusimamia hazi za binadamu na badala yake wamekiuka hilo, jambo ambalo dhahiri linaashiria mwisho wa kuwaadhibu wakosaji si tu nchini Kenya bali katika ukanda huu wa Afrika.
Amesema, "Si mwanzo mwema wa utekelezaji wa katiba mpya. Katiba Mpya inabainisha wazi kuwa tunawajibika kutekeleza mikataba yote ya kimataifa ambayo tumeridhia, ikimaanisha tunalazimika kushirikiana na mahakama hiyo ya ICC."
Hata hivyo, serikali ya Kenya imetetea uamuzi wake wa kumwalika Rais Omar al Bashir, kuhudhuria sherehe hizo.
Akizungumzia wito wa kuitaka Kenya kumkamata Rais huyo wa Sudan, Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Moses Wetangula, amekaririwa akisema, Rais Bashir yupo nchini hapa kwa mwaliko uliofanywa na serikali ya Kenya kwa jirani zake wote kuwaomba kuhudhuria tukio hili la kihistoria.
Bw Wetangula amesema, "Kenya haijavunja sheria yoyote na ni nchi huru, hivyo ina haki ya kumwalika yeyote inayetaka aje hapa nchini."
Kuhusu kutomkamata Rais Bashir kama ambavyo nchi wanachama wa mahakama ya ICC wanatakiwa kutekeleza agizo la mahakama hiyo, Wetangula amesema, "Huwezi kumdhuru au kumfedhehesha mgeni wako, huu si utaratibu, desturi na maadili ya Kiafrika."
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Friday, August 27, 2010
BANGO
Friday, August 27, 2010
BANGO
ESTER KHERI KUTOKA MUSOMA MKOANI MARA KANITUMIA PICHA NA ANAZUNGUMZA HIVI JUU YA MY HAZBAND WAKE..
"mambo vp mr uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! upo poa naomba nikutumie picha kwa ajili ya bithrday ya ma husband. Anaitwa Kheri Mchume aka baba Mariam"
BLOGU HII INAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA MAISHA YAKO ENDELEA KUITEKETEZA MISHUMAA KAMANDA.
Tuesday, August 24, 2010
HABARI
MWONEKANO KWA PICHA YA KAWAIDA.
MWONEKANO KWA PICHA YA VIDEO.
KWA MARAFIKI AMBAO TULOKUWA TUKISUMBUANA JIWE - JIWE!
HAYA SASA LILE JIWE LINALOCHEZA (NYABULEBHEKA) HILI HAPA INGAWA SIKULINASA VIZURI KWA KIKAMERA CHANGU KIDOGO UKIJUMLISHA NA KUTETEMA KAZI KWELI KWELI!!
Monday, August 23, 2010
BANGO
CHAMA LA MWANANGU MWENYEWE, TEMBELEA KISHA UNAMBIEeee!
Monday, August 23, 2010
HABARI
Serikali nchini Marekani imetoa ruhusa kwa majaribio kufanyika kwa wanaadamu baada ya dawa hiyo kugundulika kuwa tiba kwa tumbili. Ebola ni moja ya maradhi mabaya na yanaua.
Ugonjwa wa Ebola ni hatari zaidi kwa tumbili kuliko binaadamu.Wakipatikana na ugonjwa huu wanafariki dunia.
Lakini kwa majaribio ya dawa hii,asilimia sitini walitibiwa.Matumaini ni kwamba matokeo haya mazuri yatajitokeza au yawe bora zaidi wakati dawa hii itakapotumiwa kwa binaadamu.
Ebola imeua takriban watu elfu moja mia mbili tangu ilipogunduliwa katika miaka ya sabini nchini Zaire,sasa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Mara nyingi mlipuko wa ebola hutokea barani Afrika.
MADAKTARI NDANI YA MAABARA.
Ebola inaweza kuambukizwa kutokana na maji maji ya mwili. Dalili zake ni pamoja na kutapika huku walioathirika wakitoka damu pamoja na viungo muhimu vya mwili kushindwa kufanya kazi kabla hawajafariki dunia. Kutokana na kuwa na athari kubwa inahofiwa kuwa virusi vya ebola vinaweza kutumika kwa ugaidi.
Ufadhili wa utafiti ulitiliwa nguvu Marekani kufwatia mashambulio ya septemba kumi na moja mwaka 2001.
Dawa hii mpya imefanyiwa utafiti na idara ya utafiti ya jeshi la Marekani pamoja na kampuni nyengine binafsi ya AVI-BioPharma.
HABARI KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Sunday, August 22, 2010
SIASA
NAJUA WADAU MWASUBIRI KWA HAMU KUIONA VIDEO JAPO KIDUCHU YA JIWE LA NYABUREBHEKA (JIWE LINALOCHEZA) NAAHIDI SOON KULITUNDIKA.
LAKINI KWA LEO CHEKSHIA AJALI ILIYOMKUTA MSELA WANGU WAKATI AKIJISHAUWA BARABARANI.
KAMWE USIJARIBU!!