ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 24, 2010

TIGER WOODS NA MKEWE WATALIKIANA.

BINGWA WA MCHEZO WA GOLF DUNIANI TIGER WOODS AMETALIKIANA NA MKEWE ELIN NORDEGREN. HIZI NI HABARI KUTOKA MTANDAO WA MCHEZAJI GOLF NAMBA MOJA DUNIANI.

KWA PAMOJA WALISEMA "Tunasikitika kuwa ndoa yetu imefikia tamati na tunatakiana kila la heri katika mustakabala wetu," WAWILI HAO WALISEMA.


HATA HIVYO WAWILI HAO WAMESEMA WATASAIDIANA MAJUKUMU YA KULEA WATOTO WAO WAWILI. SUALA LA KUGAWANA PESA HALIJAWEKWA WAZI LAKINI TAARIFA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VYA MAREKANI ZINASEMA KUWA BI.NORDEGREN HUENDA AKAONDOKA NA KITITA CHA DOLA MILIONI 100.

WOODS AMEKUWA NA MATATIZO KWENYE NDOA YAKE HALI ILIYOMPELEKEA KITETE HATA KUPATA AJALI PINDI SAKATA LIKIELEKEA KUNUKA, BAADAE MZEE MZIMA MZIGO UKAMWELEMEA AKAOMBA SAMAHANI HADHARANI HUKU AKIKIRI WAZI KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA WANAWAKE KADHAA NJE YA NDOA.

NAAM HAYO NI YA WOODS NA MTALAKA WAKE, KILA LA KHERI KATIKA MAISHA YAO MAPYA KILA MTU KIVYAKEzzz!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.