ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 14, 2018

PUNGUZA UZITO NDANI YA SIKU 90 TU.
Wakazi wa Mwanza wanayofursa ya kupunguza uzito na unene ndani ya siku tisini tu ikiwa ni pamoja na kujishindia mizawadi.........
Uzito mkubwa wa kupindukia ni tatizo kubwa la kiafya katika maisha yetu ya kisasa. Uzito unapozidi kiwango ambacho kinahitajika kwa mtu husika kunachangia matatizo mengi ya kiafya. Watu wenye uzito mkubwa wamekuwa wakijaribu njia nyingi tofauti za kupunguza uzito bila ya mafanikio aidha kwasababu ya kukata tamaa mapema kabla ya matokeo au kwa kufuata njia zisizo sahihi na namna zisizo sahihi.

Baadhi ya matatizo yanayosababishwa na uzito mkubwa ni Kisukari ,Shinikizo la Juu la Damu na magonjwa mengine ya moyo. 
Kama nawe unataabishwa na uzito na unene kwa kipindi kirefu na umetumia njia zote zimedunda, sasa kwa matokeo kupitia EDMARK shiriki mpango huu uliosuluhisho la yote hayo.

KATAMBI AMKINGIA KIFUA MAKONDA KISHERIA.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Mkonda kuanzisha kampeni ya kuwataka wakina mama waliokimbiwa na Baba wa watoto wao kujitokeza ofisini kwake kupata msaada wa kisheria wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa maoni yao wapo waliosifu hatua hiyo wengine wakiponda.

Kada wa Chama cha Mapinduzi ambaye alikua Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrobas Katambi amejitokeza na kuunga mkono hatua hiyo akisema Makonda yupo sahihi na mbinu ya kuwatangaza hadharani anayotumia ni kama ile ya kuwatangaza wakwepa kodi (Parade Horribles).

Katambi ambaye kitaaluma ni Mwanasheria amesema, kifungu cha sheria namba 166-167 kinaeleza kuwa itakuwa kosa la jinai endapo wazazi/mzazi ambaye ana wajibu wa kukaa na mtoto akashindwa kumtunza na kumpatia mahitaji yake ya msingi.

" Kanuni ya kipimo cha vinasaba (The Human DNA Regulation act) ya mwaka 2009 kifungu cha 25 kinataja mamlaka ambazo zinaweza kuomba vipimo vya vinasaba vifanyike ni pamoja na Mahakama, Wakili, Afisa ustawi wa jamii, Polisi, taasisi za utafiti, matabibu, Mkuu wa Wilaya na Mkoa, kwa hiyo nyie mnaohoji uhalali wa Makonda kufanya hivyo ni vema mkaenda sambamba na hiki kifungu.

" Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 129 (1), (2) kinasema ni wajibu wa Baba mzazi wa mtoto katika ndoa kumtunza na waliopatikana nje ya ndoa kifungu cha 5 kinasema , watoto wote ni sawa," amesema Katambi.

Kada huyo wa CCM amesema ni vema wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kumuunga mkono mkuu wao wa mkoa na kuwataka wanasiasa wanaojaribu kupotosha waache kufanya hivyo kwani anachokifanya Makonda ni msaada mkubwa kwa akina mama wengi wanyonge ambao wamekuwa wakiteseka kulea watoto peke yao bila msaada wa akina Baba.

" Unajua akina mama wanateseka sana kulea watoto kutokana na waume zao kuwakimbia na wengine kuwatelekeza, kinachofanywa na RC Makonda ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine bila kujalisha itikadi zao za kisiasa, kidini. Wengine wanapaswa kuiga haya yanayofanywa ili kuendana na sera ya Rais wetu John Magufuli ya kutetea wanyonge," amesema Katambi.

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI NAMNA BORA ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI


  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, DODOMA
SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia,  lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama mjini Dodoma mwishoni Aprili 13, 2018, wakati akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma) na Chama cha Waajiri Tanzania, (ATE), kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

Mhe. Waziri alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya kuanzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Waziri.

Aidha Mhe. Waziri alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo  wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba  mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.

Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. 

“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Waziri Jenista Mhagama.

Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.

“Mimi nilikatika mkono wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye Kampuni ya Reli Tanzania, (TRL), na WCF imenilipa fidia ya mkupuo na inaendelea kunilipa pensheni ya kila mwezi, shilingi 170,000/= kwa maisha yangu yote nitakapokuwa hai.” Alisema Bw.Fortunatus Kiwale

Naye Mfanyakazi mwingine wa Kampuni ya Frank Pile International Project Limited ya jijini Dar es Salaam, Bw. Patrick Millinga, yeye alisema Mfuko umemlipa fidia ya zaidi ya shilingi milioni 31.9 baada ya kupoteza jicho lake la kushoto kutokana na kugongwa na kipande cha chuma wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Petronila Mligo, ambaye yeye alifiwa na mumewe katika ajali ya gari wakati akirejea kituo chake cha kazi jijini Mwanza akitokea Dodoma.

“Mfuko umenilipa fidia ya mkupuo kutokana na kifo cha mume wangu, lakini pia ninaendelea kulipwa pensheni ya kila mwezi mimi na watoto wangu wawili, ambapo kila mtoto analipwa shilingi 175,000/= na mimi ninalipwa shilingi 375,000/=.” Alisema mama huyo mjane ambaye ni mwalimu.

Akiwasilisha mada mbele ya washiriki, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.

“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Eric Shitindi, akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhsuu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (Wanne kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bw. Masha Mashomba, (Wakwanza kushoto), wakisalimiana na wanufaika wa Fidia kwa Wafanyakazi wa (WCF), Bw. Patrick Millinga, (wakwanza kulia) na Bi. Petronila Mligo, (wapili kushoto), wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma, na kufanyika jengo la LAPF mjini Dodoma. Mkuta huo ulilenga kutoa elimu zaidi na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo. Wengine pichani ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Antony Mavunde, (watatu kulia), Mwakilishi wa ATE, Bw. Almasi Maige, (wapili kushoto) na Katibu Mtendaji wa TCCIA-Dodoma, Bw.Iddi Senga.

 Mkutano ukiendelea
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(katikati), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Mashan Mshomba, (kulia), wakimsikiliza Niabu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, wakati wa mkutano wa wadau wa Mfuko, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF-Tawi la Dodoma) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA-Tawi la Dodoma), uliofanyika jengo la LAPF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Mkuta huo ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, ulilenga kutoa elimu zaidi kwa wadau na kujadiliana kuhusu namna bora zaidi ya uendeshaji wa shughuli za Mfuko huo kuhusu masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.

 
 Baadhi ya washiriki
   Baadhi ya washiriki
  Baadhi ya washiriki
 Washiriki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza wakati wa mkutano huo wa majadiliano na wadau.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (kushoto), akiwa na Bw. Mshomba.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, (WCF), Bi. Laura Kunenge, akizungumza jambo wakati wa  mkutano huo.
 Mhe. Waziri Jenista Mhagama, akizungumza na waandishi wa habari.
 Mhe. Waziri akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wakati akiwasili ukumbini.
 Mnufaika wa Fidia, Bi. Petronila Mligo, akitoa ushuhuda wa faida anayopata kutokana na uwepo wa Mfuko, baada ya kufiwa na mumewe akiwa kwenye safarin ya kikazi.
 Bw. Patrick Millinga, naye akitoa ushuhuda kutokana na Fidia aliyopata kutoka WCF baada ya kupoteza jicho lake la kushoto wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi.
 Mhe. Waziri Mhagama akisalimiana namnufaika mwingine wa Fidia, Bw. Fortunatus Kiwale

 Picha ya kwanza ya pamoja.
Picha ya pili ya pamoja.

Friday, April 13, 2018

USHIRIKINA:- WATANO WASHIKILIWA KWA MAUAJI YA KUKATA SEHEMU ZA SIRI ZA WANAWAKE MWANZA

Watu watano Mkoani MWANZA wakiwemo waganga wa jadi WAWILI wanashikiliwa na polisi Wilayani MISUNGWI kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa mauaji ya wanawake kwa imani za kishirikina.

Watuhumiwa hao ambao walikuwa wakitafutwa tangu mwaka 2013 wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya wanawake  wanane kwa kuwakata kwa mapanga, kunyofoa sehemu za siri na matiti na kuziuza kwa waganga wa kienyeji kwa masuala ya kishirikina.

NUSU FAINALI YA UEFA 2018 SASA HADHARANI.

  Wakali wa England Liverpool sasa kukutana uso kwa uso na wababe Baca hapa twawazungumzia AS ROMA.
 Bayern Munchen kuoneshana soka na wakali wa Hispania Real Madrid.
DROO ya kupanga Mechi za Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imechezeshwa leo na timu hizo zimepangwa tayari ambapo Mabingwa watetezi Real Madrid wataanzia ugenini kucheza na Beyern Munich wakati Liverpool wakianza kwa kuikaribisha AS Roma.

KAMPUNI YA STAR MEDIA YAINGIA MKATABA NA TBC


Kampuni ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes pamoja na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) zimetiliana saini Mkataba wa Makubaliano mjini Dodoma. Mkataba huo Mpya utasaidia Kampuni zote mbili kunufaika na ushirikiano huo.

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison  Mwakyembe  amesema kuwa  huu utakuwa ni ukurasa mpya kwa pande zote mbili, “kama alivyosema Waziri Mkuu nina matumaini makubwa sana na Ushirikiano huu, kwa sababu kupitia Ushirikiano huu ndio tutaona TBC ikipanda kiteknolojia, ikipanda kivifaa na ikipanda kwa weledi”, alisema Waziri Mwakyembe.

Waziri Mwakyembe pia alizungumzia kwa upande wa wizara na nafasi yake, “Ni wajibu wa Wizara kuhakikisha yote tuliyokubaliana yanatekelezwa”. Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Dk. Ayoub Rioba amesema kasoro zilizokuwepo awali sasa zimeondoshwa ili kuanza ukurasa Mpya na yeye kwa upande wake atakuwa Mwenyekiti wa Bodi huku TBC ikimiliki asilimia thelathini na tano (35%).

 “Makubaliano haya ambayo tumesainiana leo ni kuondoka kule ambako tumekuwa twende katika muktadha mpya, ambapo Kampuni itaendeshwa kwa uangalizi wa karibu sana, watanzania na mimi kama Mwenyekiti wa bodi tumeshaanza kuanzia hivi ninavyozungumza kuna namna tunafanya mambo tofauti ili tuhakikishe tunasimamia vizuri hiyo Kampuni”.

Prof. Rioba pia alizungumzia upiaji upya wa mikataba ili kuondoa kasoro za awali, “moja ya makubaliano ni kwamba tutapitia upya Mkataba na tumeshaanza,  wao wameshaona mambo ambayo yana kasoro kwa upande wao sisi pia tumeona kwa upande wetu na wote tumeyajadili tumeona kuna kukubaliana kwa hiyo kinachofuata tunaangalia upya ule mkataba wa Ubia ili zile kasoro nyingine za msingi ambazo zilisababisha uendeshaji haukuwa mzuri tunaziondoa ili tuende katika namna ambayo hatutarudia tena kuwa na matatizo ambayo tumekuwa nayo”.

MAKONDA AELEZA MAFANIKIO ZOEZI LA WANAWAKE WALIOTELEKEZWA.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema zoezi la kudai haki za watoto waliotelekezwa limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo kati ya kinababa 226 waliofika kutii wito wake takribani kinababa 205 wamekubali kwa maandishi kuwahudumia watoto wao na 21 wamepimwa DNA.
Makonda amesema tangu kuanza kwa Zoezi hilo zaidi ya kinamama 10,000 wamefika kupata huduma na Kati ya hao Kinamama 4,000 wamesikilizwa ambapo Makonda amesema lengo lake ni kuhakikisha kila aliefika anasikilizwa na mtoto kupatiwa bima ya afya Bure.

Aidha Makonda amesema wiki ijayo itakuwa zamu ya kusikiliza upande wa kinababa waliolalamikiwa sambamba na mwendelezo wa kuwasikiliza kinamama waliosalia.
Pamoja na hayo Makonda ametoa angalizo kwa kinababa watakaokaidi wito wa serikali kuwa watakamatwa popote walipo.


Kwa upande wa kinamama wanaopatiwa huduma wamemshukuru  Makonda kwa kutambua kilio chao ambapo wameonyesha kushangazwa na baadhi ya watu wanaobeza Zoezi hilo ambalo kwao wamesema limewasaidia kupata haki zao na kupata uhakika wa matibabu ya mtoto kupitia kadi za bima za afya zinazotelewa na  Makonda Bure.

Thursday, April 12, 2018

WATU 17 WAFARIKI KWA AJALI KENYA.


Watu 17 wameripotiwa kufariki dunia na wengine 44 kujeruhiwa vibaya  katika ajali iliotokea kwa makosa ya kibinadamu baada ya  dereva wa basi hilo kupoteza muelekea akijaribu kulikwepa lori lililokuwa likijielekeza katika upande wake.

Mkuu wa wilaya ya Narok  nchini Kenya  George  Natembeya amesema kuwa basi hilo lililofanya ajali  lilikuwa na abiria 63.

Miongoni mwa watu waliofarik katika ajali hiyo walikuemo watoto watatu.

MFANYABIASHARA MAARUFU ALIYENASWA KATIKA UVUVI HARAMU WILAYANI SENGEREMA


MFANYA biashara na mvuvi mashuhuri Ziwa Victoria wilayani Sengerema mkoani MwanzaJoseph Njako (Njiwa Pori) anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kwa tuhuma za kumiliki zana haramu za uvuvi zilizopigwa marufuku na Serikali,z alizokuwa amezichimbia ardhini katika maeneo ya kiwanja cha makazi yake.

Tukio hilo la kukamatwa mfanya biashara huyo limetokea siku ya jumanne ya wiki hii majira ya saa tisa alasiri katika kitongoji cha KACHU kata ya NAMATONGO wilayani SENGEREMA Ikiwa mi mara ya tatu kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwa kumiliki na kujihusisha na uvuvi halamu ndani ya Ziwa Victoria kama anavyoeleza mkuu wa wilaya hiyo....

Wednesday, April 11, 2018

JUHUDI ZA KUIFIKIA SERIKALI YA VIWANDA KWA JIJI LA MWANZA ZAPIGWA TAFU NA BENKI ABC

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini Mwanza.
 NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO TV
Ili kufikia adhma ya Serikali ya Viwanda wawekezaji wa ndani na nje wametakiwa kuendelea kuwekeza mkoani Mwaza kwa kubuni miradi endelevu kulingana na jiografia ya rasilimali zilizomo ili kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.

 Dona Botha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ABC nchini anayemaliza muda wake amesema kuwa, pamoja na kuendelea kubuni bidhaa mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wateja wake Benki ABC ni benki inayoongoza nchini Tanzania katika huduma ya uhamishaji mihamala ya fedha na ufanyaji manunuzi kwa njia ya mitandao kwa uhakika.


Imman John (pichani kulia), ni Mkurugezi wa Fedha ambaye anayekwenda kukabidhiwa nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji, kwa upande wake, amewataka wananchi kuzichangamkia fursa za benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukuwa mikopo yenye riba nafuu na kuweka akiba kwaajili ya miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo.


Bi. Joyce Malai 
 Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wadogo Bi. Joyce Malai amesema kuwa licha ya benki hiyo kutoa huduma za kawaida, pia imeboresha huduma zake kwa kutoa huduma kwa  kila mtanzania hasa kwa wale wasio na akaunti za Benki, kwa kutoa huduma za kifedha kupitia wakala wa taasisi mbalimbali nchini inayowezesha wateja wake kupata huduma za benki hiyo wakiwa wakiwa popote nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ABC Dona Botha pamoja na Mkurugenzi wa Fedha Imman John (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la tawi linaloashiria ufunguzi huo jijini hapa.
Pongezi kwa kazi nzuri.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akikagua huduma na mazingira ya tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akiwa ameshikilia card ya ATM ya baada ya kufungua akaunti katika tawi jipya la Benki ABC.
Hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akipata maelezo kutoka kwa Bi. Joyce Malai  ambaye ni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wadogo wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.
Mazingira ya benki na jiografia yake.
Safu ya Benki ABC.
Picha ya pamoja.
                                                                  Picha ya pamoja.


Benki ABC ambayo ni moja ya kampuni tanzu za Atlas Mara, inayopatikana sasa katika nchi saba barani Afrika, huku ikijivunia kuwa na tuzo ya kuwa Benki bora Afrika kwa mwaka 2017 ambapo bado imeendelea kujidhatiti na kuenea zaidi hapa nchini kwa kufungua matawi mengi zaidi ambapo mara baada ya kuzindua tawi hili la Mwanza sasa inajiandaa kuelekea mkoani Dodoma ambako nako inakwenda kuzindua tawi lake.

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kueleza kuwa uteuzi huo wa Prof. Jairo unaanza leo Aprili 11, 2018.

Soma hapa chini kwa taarifa kamili.

HUYU NDIYE #EDWARD_MORINGE_SOKOINE SHUJAA WA WANYONGE MZALENDO WA TANGANYIKA, ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE Tangu 1/8/1938 -12/4/1984

HUYU NDIYE #EDWARD_MORINGE_SOKOINE SHUJAA WA WANYONGE MZALENDO WA TANGANYIKA, ADUI WA WAHUJUMU UCHUMI NA WATENDAJI WAZEMBE Tangu 1/8/1938 -12/4/1984
.
. "Ole wao wale wanaotumia nafasi zao za umma na serikali, kuiba, kuhujumu uchumi, kupokea rushwa, maana salama yao ni kudra za Mwenyezi Mungu labda nisiwajue"

Hayo ni maneno aliyowahi kuyatamka hayati kaka na mzalendo wa taifa hili shujaa Moringe Sokoine, wakati akilihutubia kwenye mkutano kikao cha NEC mjini Dodoma 12/04/1984, wakati huo vita ya kupambana na suala la uzembe makazini, ulangunguzi, rushwa na biashara ya magendo, enzi hizo taifa lilikuwa la moto kila sehemu ilikuwa moto, mpaka #WALANGUZI wakamchukia...... lakini mpaka leo kauli yake inaishi, inatumika, inaamsha hali ya uzalendo na maadili ya taifa hasa wakati huu ambapo wanasiasa na serikali kwa ujumla wanaishi kinyume na misingi mikuu ya taifa hili, misingi mikuu ya chama chao na msingi mkuu wa uwajibikaji wa serikali, ingawa Rais #JPM kanyoosha watu si mchezo.
.
.
Leo  tunakumbuka, kifo cha mpendwa wetu huyo kwa yale mazuri aliyoifanyia Tanganyika kwa ujumla wake, lakini pindi tunakumbuka kumbukumbu hii tujiulize je? Je viongozi wetu wanaishi kimatendo kama hayati  Sokoine? 
.
#Tafakari @jembefm

VIGOGO WALIOTELEKEZA WATOTO WATAKIWA KUJISALIMISHA KWA MAKONDA.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa kuanzia kesho Alhamis wanaume wote ambao tayari wametajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito.

Akizungumza na baadhi ya wanawake waliojitokeza kupeleka malalamiko yao, Makonda, amesema kuwa hakutakuwa na kigogo yoyote atakayehitaji kuonana naye kwa siri kama ambavyo wengi wamekuwa wakiomba kufanya hivyo na kueleza kuwa nafasi hiyo haipo.

Amesema kuwa vigogo 107 tayari wametajwa kutelekeza watoto na amewaomba mara wapatapo wito wa barua yake wafike ofisini kwake mara moja kwani watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kesheria.

 Mbali na zoezi hilo Makonda amesema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kusaidia kuwalipia watoto hao Bima za afya ili waweze kumudu gharama za matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Tuesday, April 10, 2018

VODACOM YAKABIDHI BAISKELI 42 KWA MAWAKALA WAKE JIJINI MWANZA.

 Mkuu wa Vodacom kanda ya Ziwa Ayubu Kalufya, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi baiskeli kwa mawakala wa kusajili line za simu jijini Mwanza jana, ambapo baiskeli 42 zilitolewa na Vodacom.
Mkuu wa Oparesheni za kikanda wa Vodacom Domician Mkama, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi baiskeli kwa mawakala wa kusajili line za simu jijini Mwanza jana, ambapo baiskeli 42 zilitolewa na Vodacom.

Mmoja kati ya washindi 42 wa kuwasajili watumiaji wapya wa line za Vodacom Pascal Laurent, akipokea cheti na Baiskeli kutoka kwa  Afisa Masoko wa jiji la Mwanza John Kilunge,baiskeli hiyo itakayomuwezesha kurahisisha kazi yake. kushoto ni Mkuu wa Vodacom kanda ya Ziwa Ayubu Kalufya na Mkuu wa Oparesheni za kikanda wa Vodacom Domician Mkama wakishuhudia.

 Mmoja kati ya washindi 42 wa kuwasajili watumiaji wapya wa line za Vodacom Sostenes Mawazo, akipongezwa na  Mkuu wa Oparesheni za kikanda wa Vodacom Domician Mkama(kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano, kushoto ni  Mkuu wa Vodacom kanda ya Ziwa Ayubu Kalufya na  Afisa Masoko wa jiji la Mwanza John Kilunge(wa pili kulia).
Mmoja kati ya washindi 42 wa kuwasajili watumiaji wapya wa line za Vodacom Witness Christopher, akipokea cheti na Baiskeli kutoka kwa  Afisa Masoko wa jiji la Mwanza John Kilunge,baiskeli hiyo itakayomuwezesha kurahisisha kazi yake.kushoto ni Mkuu wa Vodacom kanda ya Ziwa Ayubu Kalufya na Mkuu wa Oparesheni za kikanda wa Vodacom Domician Mkama wakishuhudia.
 Zawadi za washindi.
 Zawadi za washindi.
 Washindi na zawadi zao. 
 Picha ya pamoja meza kuu na mawakala 
Eneo la tukio.