Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini Mwanza. |
Ili kufikia adhma ya Serikali ya Viwanda wawekezaji wa ndani na nje wametakiwa kuendelea kuwekeza mkoani Mwaza kwa kubuni miradi endelevu kulingana na jiografia ya rasilimali zilizomo ili kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.
Dona Botha, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ABC nchini anayemaliza muda wake amesema kuwa, pamoja na kuendelea kubuni bidhaa mbalimbali na zenye kuzingatia mahitaji halisi ya soko kwa wateja wake Benki ABC ni benki inayoongoza nchini Tanzania katika huduma ya uhamishaji mihamala ya fedha na ufanyaji manunuzi kwa njia ya mitandao kwa uhakika.Imman John (pichani kulia), ni Mkurugezi wa Fedha ambaye anayekwenda kukabidhiwa nafasi ya Ukurugenzi Mtendaji, kwa upande wake, amewataka wananchi kuzichangamkia fursa za benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuchukuwa mikopo yenye riba nafuu na kuweka akiba kwaajili ya miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Bi. Joyce Malai |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ABC Dona Botha pamoja na Mkurugenzi wa Fedha Imman John (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la tawi linaloashiria ufunguzi huo jijini hapa.
Pongezi kwa kazi nzuri.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akikagua huduma na mazingira ya tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akiwa ameshikilia card ya ATM ya baada ya kufungua akaunti katika tawi jipya la Benki ABC.
Hapa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mangella akipata maelezo kutoka kwa Bi. Joyce Malai ambaye ni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na wadogo wakati alipokuwa akizindua tawi jipya la Benki ABC jijini hapa.
Mazingira ya benki na jiografia yake.
Safu ya Benki ABC.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Benki ABC
ambayo ni moja ya kampuni tanzu za Atlas Mara, inayopatikana sasa katika nchi
saba barani Afrika, huku ikijivunia kuwa na tuzo ya kuwa Benki bora Afrika kwa
mwaka 2017 ambapo bado imeendelea kujidhatiti na kuenea zaidi hapa nchini kwa
kufungua matawi mengi zaidi ambapo mara baada ya kuzindua tawi hili la Mwanza
sasa inajiandaa kuelekea mkoani Dodoma ambako nako inakwenda kuzindua tawi
lake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.