ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 10, 2017

WIKIENDI NJEMA WADAU.

Kutoka kushoto ni Adolf Nzwalla, Mbaba VC, Dj HQ, Vitus Buyamba, Mokiwa Jumanne na Chriss The Dj.

WATU 14 WAUAWA SOMALIA BAADA YA WANAJESHI KUPIGANA WAKIGOMBANIA CHAKULA.

Kwa uchache watu 14 wameuawa kusini magharibi mwa Somalia wengi wao wakiwa ni raia baada ya kuzuka mapigano baina ya wanajeshi wakigombea chakula cha misaada.

Taarifa zinaeleza kuwa, mapigano hayo ya kugombania chakula ambayo mbali na kusababisha mauaji ya watu 14 yamepelekea pia makumi ya watu kujeruhiwa yalitokea katika mji wa Baidoa ambao una makumi ya maelfu ya raia wanaohitajia misaada ya chakula kutokana na kukabiliwa na ukame na uhaba mkubwa wa chakula.

Mapigano hayo yalizuka baada ya baadhi ya wanajeshi kujaribu kuiba chakula cha misaada ambapo kundi jingine la wanajeshi lilikuja na kuwazuia wenzao hao.

Mohammed Ahmed mmoja wa maafisa katika hospitali kuu ya Baidoa amewaambia waandishi wa habari kwamba, baadhi ya majeruhi wa tukio hilo hali zao ni mbaya, inagawa wanaendelea kupata matibabu.

Wanawake wa Somalia wakiwa katika foleni ya kusubiria chakula cha msaada
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa nchi ya Somalia inakabiliwa na ukame na hivyo kuiongezea matatizo nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa pia na tatizo la njaa na ukosefu wa amani na usalama.
 
Mbali na majanga hayo ya kimaumbile, Somalia inakabiliwa pia  na harakati za kundi la kigaidi la al-Shabaab ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya kigaidi nchini humo.

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, nusu ya raia wa Somalia ambao ni karibu watu milioni sita na laki mbili wanahitajia msaada wa haraka huku watoto laki tatu na elfu 63 wakikabiliwa na hali mbaya sana ya utapiamlo.

ETHIOPIA KUISHIWA NA CHAKULA CHA MISAADA.

Serikali ya Ethiopia na makundi ya misaada ya kibinadamu yametangaza kuwa, nchi hiyo itaishiwa na chakula cha misaada kwa ajili ya watu milioni 7.8 walioathiriwa na ukame mkubwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
 
Wahisani, mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu na serikali ya Ethiopia wanasema kuwa, chakula cha msaada cha zaidi ya watu milioni 7.8 wanaosumbuliwa na ukame kitamalizika kufikia mwishoni mwa mwezi huu huku nchi hiyo ikiendelea kusumbuliwa na uhaba wa misaada ya kifedha.
Uhaba wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa vimesababisha ukame mkubwa nchini Ethiopia na katika nchi nyingine kadhaa za Pembe ya Afrika. Nchini Ethiopia pekee inakadiriwa kuwa, idadi ya watu walioathiriwa na njaa na uhaba wa chakula itaongezeka kwa watu milioni mbili kufikia mwezi ujao.
Ukame umeathiri sehemu kubwa ya Pembe ya Afrika
Mwezi Machi mwaka huu Umoja wa Mataifa ulitangaza kuwa, njaa iliyoyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, Sudan Kusini, Yemen na Somalia imesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu kuwahi kutokea duniani tangu mwaka 1945.

PICHA BASI LA BATCO LILIVYOTEKETEA KWA MOTO LEO.

Basi la BATCO lenye namba za usajili T192DHW limeteketea kwa moto hii leo katika eneo la Kirumi kata ya Bukabwa Wilayani Butama Mkoani Mara. Gari hilo lilikuwa linafanya safari zake kutoka Tarime-Sirari na Mwanza.


Chanzo cha Moto huo bado hakijafahamika.Taarifa za awali kutoka kwa baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo pamoja na abiria wameeleza kuwa baadhi ya mali za abiria zimeteketea kwa moto na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

WATANZANIA WASHAURIWA KUBADILI MTAZAMO KUHUSU UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi (aliyesimama) akizungumza katika Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji. Wengine picha ni watoa mada mbalimbali walioshiriki katika Kongamano hilo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akichangia nafasi ya Benki yake katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jim Yonazi akizungumzia nafasi ya TSN katika kuwezesha juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo alisema kuwa Shirika lake lina uwezo na teknolojia ya hali ya juu katika kuwafikia sehemu kubwa ya watanzania. Alitoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kutumia nafasi hiyo kuwafikia walengwa wa huduma zao.
 Baadhi ya Manaibu Mawaziri wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya wadau wa taasisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi wakifuatilia kwa makini Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji. 
 
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wito umetolewa kwa Watanzania hasa kwa wadau wanaojihusisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi kubadili mitazamo juu ya namna sahihi ya kuwawezesha wananchi hao katika kutimiza lengo la serikali la kuwainua wananchi kiuchumi ili kuimarisha kipato na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.
Wakizungumza katika Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji linalofanyika mkoani Dodoma wadau hao wamesema kuwa kuna ulazima wa wadau hao kujua mahitaji sahihi ya wananchi wanaohitaji huduma za uwezeshaji wa kiuchumi kwa kuwa kila kundi lina mahitaji yake.
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unazingatia mahitaji maalumu ya kila sekta ya kiuchumi na kutolea mfano kuwa wakulima nchini hawahitaji rasilimali fedha pekee ili kuongeza tija katika kilimo chao bali wanahitaji masoko ya uhakika ya mazao yao.
“Uzoefu kutoka kwa watekelezaji wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi unaonesha kuwa rasilimali fedha si kila kitu pekee katika kuwawezesha wananchi kiuchumi bali kila kundi linahitaji mahitaji yake, mfano mkulima anahitaji soko la mazao yake ili aweze kuongeza tija kwenye kilimo chake,” alisema Prof. Ngowi.
Akichangia mjadala huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kwa kuwawezesha wananchi kwa kuzingatia mahitaji maalumu kuendana changamoto za kimaeneo hili kuwezesha wananchi kiuchumi nchini ili kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali kuwafikisha wananchi wake kufikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Muundo wa TADB ni tija katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa wakulima wadogo nchini kwani Benki inafanyia kazi mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo kwa kutatua changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji; ukosefu wa mbinu na teknologia za  kisasa; matumizi madogo ya umwagiliaji,” alisema
Aliongeza: “Changamoto nyingine ni ukosefu wa mtaji na upatikanaji wa mikopo kwa wakulima; ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo, pamoja na changamoto zinginezo,” aliongeza.
Kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Kilimo kunaleta suluhisho la changamoto nyingi zilizokuwa zinaikabili sekta kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kama inavyowekwa bayana na dhima ya  Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambayo inalenga kuwaongoza watanzania katika kujenga uchumi wenye nguvu kwa kuboresha mazingira ya kibiashara na kutoa fursa sawa za kiuchumi.
Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji linafanyika katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iliyoundwa mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji namba.16 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

TAARIFA YA IKULU KUHUSU KAMATI YA PILI MCHANGA WA DHAHABU.



Kamati ya Pili iliyoundwa na rais kuchunguza Mchanga wa Dhahabu imekamilisha kazi yake na kwambwa itakabidhi ripoti ya uchunguzi wao Tarehe 12 Juni Mwaka,


ANNA MGHWIRA AMNG'OA KIONGOZI ACT- WAZALENDO

Ikiwa ni Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Act-Wazalendo Anna Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkao wa Kilimanjaro leo ameibuka Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mbeya  Bahati Longopa na kutangaza kujiuzuluzu nafasi hiyo kwa alichodai kutoridhia uteuzi huo.

Longopa amesema  kuendelea kuwa kiongozi wa chama kutampa wakati mgumu kuhamasisha wanachama wapya katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Amesema kuwa kwa hiari yake ameacha nafasi hiyo ndani ya chama kutokana na kitendo cha viongozi wa juu wa Chama hicho kuingia ndani ya Serikali iliyopo madarakani ambayo ni ya chama pinzania kwao wao viongozi wa chini hawataweza kuwashawishi wanachama wapya kujiunga na chama hicho

Kuhusu kujiunga na chama  kingine cha siasa amesema kwa sasa ni mapema mno kuzungumzia hilo kwani   ataendelea kukaa pembeni na kutojihususisha kwenye mambo ya siasa  huku akitafakari nini cha kufanya.

Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo,   Wilaya ya Mbeya, Ally Mbika alisema wamepata taarifa  za chini chini, lakini kama chama bado hawajakabidhiwa barua yoyote kutoka kwa kada huyo kutamka kujiuzulu rasmi.


Amesema  wanasubiri  kukabidhiwa  rasmi ili kuweza kulizungumzia kwa vyombo vya habari barua na  viongozi wa chama  watapitia katiba yao na kupata mwongozo na kuangalia namna ya  kuziba nafasi hiyo mpaka Uchaguzi  Mkuu  wa  mwaka 2020.
Mbika amesema kuwa kujiengua kwa kada huyo ni pigo kwa chama kwani alikuwa ana mchango mkubwa wa ushawishi na kujenga umoja na mshikamano wa kweli wa ndani na nje ya mkoa

MAMBO 12 YALIYOWAFANYA WABUNGE WASHANGILIE BAJETI KUU YA SERIKALI.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa.

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015.

Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.

Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara.

Simbachawene alisema kutokana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Mei 15, 2017 jumla ya wanafunzi 93,019 ndiyo wenye Sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa kuwa wamefaulu vigezo vyote vya msingi kama vilivyoaibishwa na Wizara ya elimu sayansi na teknolojia ambapo kati ya hao 92,998 ni wa shule na wanafunzi 21 ni wale waliosoma taasisi ya elimu ya watu wazima.

Aidha amewataka wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kuwasili kwa wakati katika shule walizopangiwa July 17 mwaka huu na kwamba hakutakuwa na mabadiliko ya shule walizopangiwa.

"Na kama kuna mwanafunzi ambaye hataripoti kwenye shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 14 nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine," alisema Simbachawene.

Friday, June 9, 2017

WASHUKIWA WALIOJIUNGA NA BOKO HARAM WACHUNGUZWA.

Jeshi la Nigeria linawachunguza watu wanaoshukiwa kujiunga na kundi la kigaidi la Boko Haram nchini humo. 

Lucky Irabor, Kamanda wa oparesheni iliyopewa jina la "Lafiya Dole" huko kaskazini mashariki mwa Nigeria amesema kuwa, baadhi ya wafungwa wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram hivi karibuni watafikishwa mahakamani. Irabor ameongeza kuwa, aghalabu ya waliotiwa mbaroni katika upekuzi uliofanywa na jeshi la Nigeria wamekiri kushiriki katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram.

Lucky Ilabor, Kamanda wa Oparesheni dhidi ya Boko Haram kwa jina la Lafiya Dole.
 
Hadi kufikia sasa watu wasiopungua elfu 20 wameuliwa na wengine zaidi ya milioni mbili na laki sita wamekimbia makazi yao tangu kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram lianzishe mashambulizi na ukatili wake huko kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009. Aidha mashambulizi ya kundi hilo la kitakifiri yameenea huko Chad, Niger na Cameroon kuanzia mwaka 2015.

SERIKALI YATOA SABABU ZINAZOWAFANYA CHADEMA WAPIGWE MARUFUKU KUFANYA SHEREHE VYUONI.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alihoji bungeni sababu za wanafunzi wa CCM kupendelewa kufanya mikutano na sherehe za kumaliza masomo yao huku wanafunzi wa vyama vingine vya upinzani hasa CHADEMA kupigwa marufuku kufanya sherehe hizo.

Akijibu jambo hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kuwa wanafunzi wa Chama Cha Mapinduzi huwa wanafuata utaratibu ndiyo maana huwa wanapewa ruksa kufanya sherehe hizo pindi wanapomaliza vyuo na kusema hao wengine huwa hawafuati utaratibu ndiyo maana wanakuwa wanazuiliwa.

 
"Taratibu ziko wazi kama CCM walikuwa wamefuata utaratibu na kupewa mikutano, chama kingine chochote kinachotakiwa ni kufuata utaratibu zile zile waweze kupewa mikutano lakini wengine kama hawajafanya utaratibu hawatapewa tu kwa sababu CCM walipewa bali watapewa kwa kufuata utaratibu, kuna sehemu zingine CHASO hao hao wamepewa mikutano kwa hiyo linalotakiwa ni utaratibu tu wa kupewa mikutano hiyo" alisema Mwigulu Nchemba


Mbali na hilo Waziri Mwigulu Nchemba alisema mikutano ya hadhara haijazuiwa bali imewekewa utaratibu na kusema duniani kote sifa za mikutano ya hadhara ni kama ambavyo inafanyika hivi sasa Tanzania na kusema kuwa mtu aliyeshinda ndiye anaendelea na majukumu ya kuongoza na aliyeshindwa hapaswi kushukuru kwa wananchi.


"Marekani mwaka jana walifanya uchaguzi mmemuona Hillary Clinton anashukuru kwa wananchi? Duniani kote aliyeshinda ndiye anaendesha serikali kwa utaratibu wa kiserikali hili liko wazi duniani kote" alisisitiza Mwigulu Nchemba

MAMBO 12 YALIYOWAFANYA WABUNGE WASHANGILIE BAJETI KUU YA SERIKALI.

Mlipuko wa furaha kutoka kwa wabunge uliojitokeza jana wakati Serikali ilipotangaza kufutwa kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari (motor vehicle licence), ulitosha kuonyesha ukubwa wa kero hiyo uliokuwapo kwa jamii.

Si kero hiyo tu, kelele za furaha kutoka kwa watunga sheria hao pia zilisikika kwa wingi ilipotangazwa kufutwa kwa ushuru wa usafirishaji wa mazao chini ya tani moja, ushuru wa huduma kwenye nyumba za kulala wageni na kutoza ushuru wa forodha wa asilimia sifuri badala ya 25 kwenye malighafi na vifaa vinavyoagizwa mahsusi kwa matumizi ya walemavu.

Zaidi ya mara mbili, Spika wa Bunge, Job Ndugai alilazimika kumtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kurudia alichokisema au kumwambia inatosha na anaweza akaishia hapo kwani wabunge wamemuelewa na hana haja ya kuendelea kuisoma bajeti hiyo.

Ijumaa ya Juni 2, mjadala mkubwa wa kuondolewa kwa ada ya road license uliibuka bungeni, kilio cha wabunge kikiwa ni kuwapo kwa magari ambayo yameegeshwa siku nyingi kutokana na ama ajali au uchakavu wa kutotumika tena hivyo kuitaka Serikali kuifuta ili kuwapa wananchi nafuu na kutoendelea kudaiwa.


Hoja hiyo iliyotolewa na Mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni kwenye kipindi cha maswali na majibu ilichangiwa na wabunge wengi akiwamo Spika bila kujali itikadi zao za vyama vyao.


Hapakuwa na majibu ya uhakika siku hiyo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji ambaye aliishia kusema amelipokea pendekezo hilo na kwamba baada ya kukamilisha taratibu, Serikali itaona hatua sahihi za kuchukua.


Wiki hiyo ikielekea ukingoni, Dk Mpango ametangaza kuifuta sambamba na malimbikizo yake kwa wote waliokuwa wanadaiwa hivyo kuibua nderemo miongoni mwa wabunge hao walioonyesha kufurahishwa baada ya kusikilizwa na kufanyiwa kazi kwa maoni yao. 


“Serikali inatoa msamaha wa kodi, riba na adhabu zinazoambatana na madeni yote ya ada hiyo yaliyolimbikizwa kwa miaka ya nyuma,” alisema Waziri Mpango.

Bunge lilitawaliwa na kelele za CCM… CCM… CCM mara baada ya waziri huyo pia kutangaza kufuta ushuru kwenye usafirishaji wa mazao yasiyozidi tani moja pamoja na kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya walemavu vinavyotengenezwa nchini.


Ilikuwa hivyo pia alipotangaza mpango wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kutoza asilimia sifuri ya ushuru wa forodha kwenye Mashine za Kielektroni (EFD) kutoka asilimia 10 zilizokuwapo.


Hali ilikuwa hivyo pia ilipotangazwa kuondolewa kwa tozo kwa nyumba za kulala wageni.

Kufutwa kwa ada ya ukaguzi wa viwango ukaguzi wa mionzi na ada ya Wakala wa Vipimo kwenye mbolea ni hatua nyingine iliyowafurahisha wawakilishi hao wa wananchi.

WANAFUNZI 93,019 WAMECHAGULIWA KUJIUNG NA KIDATO CHA 5

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene.
Jumla ya wanafunzi 93,019 wamechaguliwa kujiunga kidato cha 5 na vyuo vya ufundi, kuripoti shuleni Julai 17, Waziri Simbachawene atangaza.

Thursday, June 8, 2017

HUDUMA YA BIMA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI 'VODACOM JAMII' YAWAFIKIA WAKAZI WA MWANZA


Kupitia masafa yetu 93.7 #jembefm Mwanza #KAZINANGOMA ikishikwa mkono kwa mkono na #JubileeInsuarance chini ya hisani ya kipekee ya #VodacomTanzania kuhakikisha usalama wako wa Afya mwana Mwanza unakuwa na mlinzi hata pale kipato kinapo yumba hata ukasahau machungu ya gharama za matibabu.... 

Sisi tunakwambia simu yako na laini yako ya #vodacom ndiyo usajili wako. 
Jiunge na kifurushi maalum cha matibabu kinachoitwa #VodacomJamii utakachokiona kwenye menu ya #MPesA @precciouschobis CC:- @mansourjumanne & @gsengo and @chrissthedj mpaka 7 kamili CC:- @jembenijembe @mbabavc @gijegije @mkuryamstarabu @bonzbalaa @djmike_beatz_ @deejaykflip @nattyebrandy1 @harith_jaha @mamachobis

WAZIRI MPANGO ATANGAZA KUFUTWA KWA ROAD LICENSE, SASA KULIPWA MARA MOJA.

DODOMA. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ametangaza kufutwa rasmi kwa ada ya mwaka ya leseni ya magari.
 
Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa  katika mafuta ya petroli na dizeli.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi bungeni na Waziri Mpango wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka 2017/18.

 
Pamoja na hayo, Waziri Mpango ameshuha ushuru  kwa mvinyo  unaotengenezwa kwa zabibu zinazozalishwa  ndani kutoka Sh2O2  kwa lita hadi Sh200 kwa lita.

 
Kadhalika ushuru wa bia zinazotengenezwa kwa nafaka za ndani umepanda kutoka Sh429 hadi 450 kwa lita.

 
 Wakati huo, ushuru wa  bia zisizo na kilevi na vinywaji vya kuongeza nguvu kutoka Sh534 hadi Sh564 kwa lita.

Serikali yatangaza neema kwa Wafanyabiashara wadogo wadogo

Serikali imetangaza neema kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi wakiwamo mama lishe na baba lishe, ikiahidi kuwapa vitambulisho maalumu vitavyosaidia kuwatambua rasmi.
 
 Amesema vitambulisho hivyo vitawasaidia kutengewa maeneo maalumu ya kufanyia biashara.

 
Akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kuu leo, Alhamisi kwa mwaka wa fedha 2017/18, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hatua hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara hao ili kukuza mitaji yao.


Usafirishaji madini wa moja kwa moja kutoka mgodini wapigwa stop

Serikali imesema haitaruhusu usafirishaji wa madini moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi na Waziri wa Fedha na Mipango, Phillip Mpango wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti kwa mwaka 2017/18.

Badala yake kutakuwa na viwanja maalumu vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali kabla ya kusafirishwa nje.

“Kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo,” amesema.

Amesema Serikali itatangaza rasmi tarehe rasmi ya kuanza  kwa ada hiyo. 



Watumishi wa tra waonywa na Waziri Mpango

 Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango amewaonya watumishi wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) wanaowatisha na kuwazidishia kodi wafanyabiashara ili kuwakomesha, kuacha mara moja tabia hiyo.
 
Dk Mpango ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/18 na kusisitiza kwamba Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wote watakaobainika.

 
Waziri huyo amewataka wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila hofu yoyote na kwamba Serikali inaendelea kufanya tathmini ya mwenendo wa uchumi nchini licha ya kwamba ripoti mbalimbali zinaonyesha kwamba Tanzania ina mazingira bora ya biashara.

 
“Taarifa ya Benki ya Dunia (WB) inaonyesha kwamba Tanzania ni nchi ya 132 kwa kuwa na mazingira bora ya kufanya biashara ikiwa imepiga hatua kutoka nafasi ya 144 mwaka 2015,” amesema Dk Mpango.

 
Hata hivyo, waziri huyo amesisitiza kwamba Serikali inaamini kwamba sekta binafsi ndiyo mhimili mkuu wa uchumi wa Taifa na kuwa itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara yanakuwa mazuri. 


 Waziri wa Fedha na Mpango Mhe.Dr.Philip Mpango akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2017/18.
 Wabunge wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 Baadhi ya wageni wakisikiliza hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th Juni 2018.
 .Wabunge wakiingia Ukumbi wa Bunge kusikiliza hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/2018 leo Bungeni Mjini Dodoma tarehe 8th June 2018.

KESI YA MMILIKI WA VICENT NA MSAIDIZI WAKE YASOGEZWA MBELE.

ARUSHA. 
Mmiliki wa Shule ya Lucky Vincent,  Innocent  Mosha na Makamu mkuu wa shule hiyo, Logino  Vicent  leo wamepandishwa tena kizimbani kujibu mashtaka matano yanayohusu ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja mwezi uliopita.
Kesi hiyo, imesomwa leo Alhamisi mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa Arusha, Desderi Kamugisha, ambapo Wakili wa Serikali Rose Sulle amesema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa matano tofauti.

Amesema  mmiliki wa shule hiyo, anakabiliwa na makosa matano,  ambayo ni kutokuwa na leseni ya usafirishaji wa gari lake lililopata ajali, kosa la pili ni  kushindwa kuwa na leseni ya barabarani,
makosa mengine ni mmiliki wa shule hiyo kushindwa kuingia mkataba na dereva wake Dismas Joseph aliyepoteza maisha kwenye ajali hiyo, pia  kuzidisha abiria 13 katika gari lililopata ajali.

Sulle amesema, makamu mkuu wa chuo, Vicent anakabiliwa na shtaka moja  la  kuidhinisha kusafirishwa kwa abiria wengi kwenye basi hilo.

Hata hivyo, Sulle aliomba kesi hiyo kupangwa tarehe nyingine kutokana na kutokamilika kwa upelelezi.

Hakimu Kamugisha alikubaliana na ombi la mwendesha mashtaka huyo na kutaka washtakiwa hao warudi tena mahakamani Julai 5, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Ajali ya wanafunzi wa shule hiyo, ilitokea Mei 6, katika eneo la Rhotia wilayani Karatu, mkoani Arusha.

🔴LIVE: YANAYOJIRI BUNGENI:- SERIKALI IKIWASILISHA BAJETI KUU 2017/2018

Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Juni 8, 2017 kipindi cha maswali na majibu.

YANGA YATOLEWA NA AFC LEOPARDS KWA MIKWAJU YA PENATI 2-4 BAADA YA SARE DAKIKA 90.

  Beki wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd
  Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan Katerega, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd
 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd
 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd

 Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd

 Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd

 Winga wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akimfinya beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd

 Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, jana Juni 8, 2017. Picha na kwa hisani ya Montage Ltd


WAINGEREZA WASHIRIKI UCHAGUZI MKUU, WABUNGE 650 KUCHAGULIWA.

Mamilioni ya wananchi wa Uingereza hii leo wanaelekea kwenye masanduku ya kupiga kura kushiriki uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambapo chama tawala cha Kihafidhina kinatazamiwa kuchuana vikali na chama cha upinzani cha Leba.

Wabunge 650 wanatazamiwa kuchaguliwa katika zoezi hilo, ambapo takriban watu milioni 46.9 wametimiza masharti ya kupiga kura. Chama kitakachozoa kura nyingi kitajipatia fursa ya kuunda serikali ijayo ya Uingereza.

Ushindani mkali uko kati ya chama tawala cha Kihafidhina kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa sasa Theresa May na kile cha upinzani cha Leba kinachoongozwa na Jeremy Corbyn.

Corbyn amekuwa akisisitiza kuwa, ni katika manifesto ya chama chake kulitambua mara moja taifa la Palestina iwapo wataibuka na ushindi katika uchaguzi huu wa mapema, sambamba na kushinikiza kusitishwa mara moja mzingiro wa kibaguzi, ukaliaji wa mabavu wa ardhi za Wapalestina na kuendelezwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina.

Thereza May (kulia) na Jeremy Corbyn 
 
Uchaguzi huu unafanyika chini ya anga ya mashambulizi ya kigaidi yaliyoshuhudiwa hivi karibuni katika baadhi ya miji ya nchi hiyo. Shambulizi la hivi karibuni ni lile la Jumamosi iliyopita, ambapo magaidi watatu waliua watu saba katika tukio lililohusisha watu kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu jijini London. 
 
Tukio hilo lilitokea majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa baada ya gaidi kujiripua ndani ya uwanja mmoja wa burudani mjini Manchester.
 
Ni vyema kuashiria hapa kuwa, uchaguzi huu ulipasa kufanyika mwezi Mei mwaka 2020, lakini mwezi jana Theresa May aliitisha uchaguzi wa kabla ya wakati.