Lucky Irabor, Kamanda wa oparesheni iliyopewa jina la "Lafiya
Dole" huko kaskazini mashariki mwa Nigeria amesema kuwa, baadhi ya
wafungwa wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram
hivi karibuni watafikishwa mahakamani. Irabor ameongeza kuwa, aghalabu
ya waliotiwa mbaroni katika upekuzi uliofanywa na jeshi la Nigeria
wamekiri kushiriki katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko
Haram.
Lucky Ilabor, Kamanda wa Oparesheni dhidi ya Boko Haram kwa jina la Lafiya Dole.
Lucky Ilabor, Kamanda wa Oparesheni dhidi ya Boko Haram kwa jina la Lafiya Dole.
Hadi kufikia sasa watu wasiopungua elfu 20 wameuliwa na wengine zaidi
ya milioni mbili na laki sita wamekimbia makazi yao tangu kundi la
kigaidi na kitakfiri la Boko Haram lianzishe mashambulizi na ukatili
wake huko kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2009. Aidha mashambulizi
ya kundi hilo la kitakifiri yameenea huko Chad, Niger na Cameroon
kuanzia mwaka 2015.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.