MVUA ya upepo mkali yasababisha mlipuko na mapolomoko ya mawe na mmomonyoko mkubwa wa ardhi yaliyotokea Kitongoji cha Sang'ombe Kijiji cha Tatwe Kata ya Goribe Wilayani Rorya Mkubwa wa Mara yaliyosababishwa na mvua kubwa ya iliyoambatana na upepo mkali umesababisha watu 93 kuathiriwa huku kaya kumi zikiathirika zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo (CCM) alitembelea eneo hilo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Charles Ochele na viongozi wengine wa Kata na Vijiji jirani kufika katika eneo la tukio kujionea uhalibifu mkubwa wa ardhi uliopelekea mto na bonde kubwa huku za zaidi ekari 20 za mazao ya wananchi kusombwa na maji na kuharibiwa na mamia ya mawe yaliyoporomoka yenye urefu wa km 2 kutoka eneo la tukio hadi mto Chirya.
Airo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Tatwe alitoa pole kwa wananchi na kusikitisha na tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi na kuwashitua wananchi zaidi 93 kuharibiwa mazao katika mashamba yao yenye urefu wa ekari 20 huku kaya kumi zikipata athari kubwa ikiwemo kupata nyufa kutoka na mlipuko huo.
"Tukio hili limetokea majira ya saa 11:00 jioni Desemba 12 na limeacha janga na hali ya wasiwasi baada ya kupolomoka wa shehena kubwa ya mawe na mmomonyoka mkubwa wa ardhi amapo eneo hilo limekuwa na mto mkubwa ambao unatililisha maji hadi mto Chirya haya ni maajabu lakini tushukuru hayakulenga makazi ya wananchi tungeshuhudia mamia kupoteza maisha," alisema.
Airo aliwaeleza wananchi hao kusikitishwa na tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Saimon Chacha na Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kushindwa kufika katika eneo la tukio na kujionea athari kubwa ya mapolomoko na uharibifu wa ardhi na mazao ya wananchi kusombwa na kufunikwa na mchanga jamb ambalo amesikitishwa na kuwaomba wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki ambacho tukisubilia utaratibu wa serikali baada ya kufika kujionea eneo hilo.
"Nimepokea taarifa za tukio hili kwa mshituko na nilimtaalifu Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ochele na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye ambapo hapa nimekuja na viongozi hawa wa Wilaya wa Chama na tunatoa pole ya Sh milioni 2.3 kwa Kaya tatu zilizoathiriwa na kujihifadhi kwa na jirani huku kaya saba ambazo jumla yake kuzifanya kuwa Kaya kumi kuanza kupata huduma za chakula na malazi wakati tukisubiri wataalamu wa Halmashauri kufanya tathimini ya athari ya tukio hili,
Akikabidhi kiasi cha fedha hizo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi, Mbunge Airo alifafanua kuwa yeye binafsi ametoa kiasi cha Sh milioni moja, Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Ochele ametoa Sh 300,000/- na Mdau wa maendeleo kutoka Wilaya hiyo aliyefahamika kwa jina Orwero aliyechangia Sh milioni moja pia.
Wakizungumzia katika eneo la tukio hilo baadhi ya wathirika wa tukio hilo, Kevin Chacha, Emmanuel Odworu, Rosemary Joseph walieleza kwa nyakati tofauti kuwa siku hiyo ilianza mvua majira ya saa 5:00 asubuhi ikanyesha kisha ikakata badae majira saa 11:00 jioni ikarejea mvua kubwa na kisha kusikika mliyo wa mlipuko mkubwa na kusikika kishindo cha mapolomoko ya maji, mawe na mchanga huku mvua ikiambatana na upepo mkali.
" Mvua hii iliwahi kutokea miaka 1996 lakini haikuwa na madhala kama hii leo tumeshuhudia maafa na mazao kusombwa na mawe na mchanga na tumeshuhudia nyumba mbili zikianguka na ng'ommbe wawili wakisombwa ni jambo ambalo limetuweka katika wasiwasi mkubwa na kuhofia maisha yetu hivyo tunaomba wataalam waje kufanya utafiti kutambua kilichotokea ama kilichosababisha, Alisema Rosemary Joseph
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya, Ochele alisema kwamba tukio hilo limewapa funzo na kuwa Wilaya hiyo ina viongozi wa Serikali wa aina gani kwa kushindwa kufika kujionea athari na uharibifu kwa wakati jambo ambalo watalikemea na kulisema kwa wahusika na kama Chama hawakufurahishwa na hali hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tatwe, Julius Ochwachi aliwashukuru Mbunge Airo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ochele kwa kufika na kutembelea eneo la tukio huku wakiguswa na kutoa msaada kwa waathirika kumi waliopoteza nyumba na mifugo yao huku wananchi wengine 83 wakiwa wameshuhudiwa wakipoteza mazao ya mahindi, mtama, ulezi, mihogo, viazi vitamu, mpunga na maharage katika maeneo mashamba yao zaidi ya ekari 20 huku mapolomoko hayo yakiwa na urefu wa km 2 kutoka eneo la tukio hadi mto Chirya.