Saturday, August 14, 2010
HABARI
Saturday, August 14, 2010
huzuni
BW. STAREHE PENDAEL MUSHI AL-MAARUFU KWA JINA LA MC BONKE WA JIJINI MWANZA ANATOA TAARIFA ZA MSIBA WA MAMA YAKE MPENDWA SCHOLASTICA MANGALE (PICHANI) AU MAMA PENDAEL ALIYEFARIKI DUNIA USIKU WA TAREHE 12.08.2010.
MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMATATU YA TAREHE 16.08.2010 SHAMBANI KWAO MIYUJI DODOMA MJINI.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
TANZANIA INA VIVUTIO VINGI VYA KITALII. LAKINI HAVIJATUMIKA IPASAVYO KULETA MAENDELEO TARAJIWA KWA WANANCHI WAKE. KWA MENGI MAZURI NILIYOJIONEA KATIKA SAFARI YANGU KISIWA CHA UKEREWE LAITI KAMA YANGETUMIKA VYEMA, HAKIKA MAENDELEO YANGEKUWA KWA KASI KATIKA KISIWA HICHO CHENYE RASILIMALI NA UTAJIRI WA KUTOSHA.
KWANI KUPITIA UTALII NA BIASHARA, MAMBO YA USAFIRI, BARABARA NA HUDUMA ZA KIJAMII YOTE YANGEBORESHWA TOFAUTI NA SASA. MMH!!
HANDEBEZYO HILL SEHEMU ILIYO JUU YA KILELE CHA KILIMA CHA PANGO LA BENKI YA WATEMI. ENEO AMBALO LILITUMIKA KWA AJILI YA ULINZI NA USALAMA WA KISIWA, KUONA MAADUI WANAOKUJA KUVAMIA NA KADHALIKA. UKISIMAMA ENEO HILI UNAONA SEHEMU KUBWA YA KISIWA CHA UKEREWE.
MFANO WA ENEO KUBWA UNALOWEZA KULIONA UKIWA HANDEBEZYO HILL.
TIZAMA MAHALA HAPA PANAVYOPOTEA. KUNA NCHI ZENYE VIVUTIO VICHACHE DUNIANIKAMA BOTSWANA NA MAURITIUS LAKINI NCHI HIZO ZIMEFAULU KUVIBORESHA, KUVITANGAZA VIVUTIO VYAKE VYA UTALII NA KUJIINGIZIA MAPATO MAKUBWA CHACHU YA MAENDELEO KWA NCHI. TANZANIA INASHINDWA NINI?
KATIKA POZI MASUPER STAR WA KESHO KUTOKA KUSHOTO MELI, MTEBA, MSEKWA, NYEBHUNU, CHIFYWE NA EMMANUEL.
LIKIWA NA MVUTO WA KIPEKEE HILI NI KANISA LA KWANZA LA ROMAN CATHOLIC LILILOJENGWA ENZI ZA UKOLONI KTK KISIWA CHA UKARA WILAYANI UKEREWE.
JIWE LA MSINGI LA MAKUMBUSHO YA OLWEGO LILILOWEKWA NA MKUU WA WILAYA BW. T.A.K MSONGE KWA MAENDELEO YA TAIFA LA TANZANIA. JE! LENGO LIMEFIKIWA?
JIWE HALISI LA MSINGI LILILOWEKWA NA BW. T.A.K MSONGE.
KWA NYUMA MUONEKANO WA PANGO LA BENKI YA WATEMI WA UKEREWE MAHALA AMBAPO WATEMI HAO WALIKUWA WAKIHIFADHI MALI ZAO ZA THAMANI, VITO, FEDHA, MADINI NA KADHALIKA, NA KILA MTEMI ALIKUWA NA SEHEMU YAKE YA HIFADHI. CHINI YA ULINZI WA UHAKIKA.
MLANGO WA KUINGIA PANGO LA BENKI.
MVUTO ENEO LA MBELE BARAZANI LANGO KUU LA BENKI YA WATEMI UKEREWE.
MAANDHALI YA KIPEKEE MVUTO WA KITALII PEMBEZONI MWA HIMAYA YA MAKUMBUSHO YA WATEMI UKEREWE. ENEO LOTE HILI HALINA MLINZI WALA MFANYA USAFI BALI MWANGALIZI ASIYE LIPWA.
KORIDO INAYOTENGANISHA PANGO LA HIFADHI (SEHEMU YA BENKI YA WATEMI) NA UKUMBI WA MAPUMZIKO.
ILI KUKUZA MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII, KAMA MCHANGO WA SEKTA HII KWA TAIFA, JUHUDI ZAIDI ZA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA VIVUTIO VYA UTALII SHURTI VIPEWE KIPAUMBELE.
MUHIMU NI KWA SERIKALI NA WAENDESHA SHUGHULI ZA UTALII NCHINI, KUANDAA UTALII KWA WANANCHI ILI WAWEZE KUONA VIVUTIO NA UTAJIRI WA NCHI YAO. OF COZ' SEHEMU YA SOMO LA HISTORIA UTALII NI NJIA NYINGINE YA KUPATA ELIMU.
WENU KATIKA UJENZI WA TAIFA LENYE 'RASILIMALI ZA KUMWAGIRIRU MPAKA KUSAZA'
ALBERT G. SENGO,
MWANZA TANZANIA.
NAOMBA KUWAKILISHA.
Friday, August 13, 2010
BANGO
LEO NI AUGUST 13/2010, NI SIKU ILIYO NA HISTORIA KUBWA KWA MASHABIKI WA MUZIKI AFRIKA MASHARIKI HUSUSANI KANDA YA ZIWA VICTORIA NCHINI TANZANIA KWANI KIJANA WAO ANAYE SIMAMA KAMA BALOZI KUZITAMBULISHA SANAA NA RASLIMALI ZILIZOPO ZONE HIYO FARID KUBANDA AL-MAARUFU 'FID Q', ANAKUMBUKA SIKU ALIYO ZALIWA.
SONGA BROTHER!
BLOGU HII YAKUTAKIA KILA LA KHERI KATIKA HARAKATI ZA MAENDELEO (YAKO NA JAMII KWA UJUMLA).
MWANZA KWANZA!!!
HAPPY BORZDEI NG'WANAMALUNDI!
'MULUNGU AKUGUNANE BHOLE LOSHIKO'
Thursday, August 12, 2010
HABARI
MTARI, KIJANA ALIYE RISISHWA NGUVU YA JIWE HILO LA UKOO.
MJI WA MWANZA.
NILITOKA MWANZA SIKU YA J3 SAA 3:00 NA MV CLARIUS NI MWENDO WA MASAA MA3 HADI KISIWA CHA NANSIO UKEREWE KISHA NIKAELEKEA BUGORORA ENEO LA KIVUKO KINGINE MWENDO WA DK 20 TOKA NANSIO.
SAFARI KUELEKEA UKARA NA MV NYERERE.
ENEO HILI LA BUGORORA NDIPO KINAPOPATIKANA KIVUKO CHA KUELEKEA KISIWA CHA UKARA MWENDO WA SAA 1.
MJI WA BWISHA UKARA.
TOKA BWISHA UKARA SAFARI KWA PIKIPIKI HADI KIJIJI CHA NYANG'OMBE AMBAKO NIKAKUTANA NA KIJIJI CHA MZEE MAKOROKORO. MZEE AMBAYE UMRI WAKE UMEKWENDA MIGUU IMECHOKA AKITEMBEA KWA KUJIVUTA. ANA KIJANA WAKE AITWAE MTARI AMBAYE ALIPOTIMIZA MIAKA 10 ALIRISISHWA KIMILA NGUVU ZA JIWE LA 'BUREBHEKA'.KIJANA SASA ANA UMRI WA MIAKA 20.
WATU WA MTAA WA DUKE WAKICHEZA KARATA SEBULE KUU.
KIJANA MTARI NDIYE ALIYEKUWA MGENI WETU MIE NA DREVA WANGU WA PIKIPIKI, NAE AKATUTOA PALE NYUMBANI HADI ENEO LA JIWE KWA PIKIPIKI MKAO WA MSHIKAKI (MWENDO WA NUSU SAA).
MTAA WA DUKE.
TUKAFIKA ENEO LA JIWE LINALOCHEZA NYAMANGA MTAA WA DUKE MTU AMBAYE ALIKUWA MAARUFU HATA WAKAPACHIKA ENEO HILO JINA LAKE (KAMA DAR ES SALAAM VILE MWANANYAMALA KWA HADIJA KOPA).
HAPA NA PALE MTAA WA DUKE.
MTAA WA DUKE SI MTAA KAMA UNAVYOWEZA KUDHANI KIMJINIMJINI ETI BARABARA, LA-HASHAA! NI ENEO LA UFUKWENI KWA WAVUVI.
JIWE LA BUREBHEKA LIKO KILIMANI HIVI JUU YA MIAMBA MIKUBWA MASHARTI KABLA YA KULIFIKIA JIWE KTK MLANGO WAKE WA NJIA UNAVUA VIATU UNAVIACHA HAPO, UNAPANDA HADI KWENYE JIWE.
NJIA KULIFIKIA JIWE.
MTARI AKIWEKA MCHANGA JUU YA FEDHA.
MARA KABAAAAN! JIWE HILI HAPA...TUKAWEKA SH 1000/= KISHA JUU YAKE UKAWEKWA MCHANGA. SHUGHULI IKAANZA KIJANA MTARI (HUKU AKILISUKUMA HIVI KULIZINDUA) AKALIZUNGUMZISHA AKILISIHI KWA LUGHA YA KUKARA KUCHEZA KWANI LIMEPATA WAGENI. DAKIKA KAMA SI SEKUNDE LIKAANZA KUNESA NA LIKAENDELEA ZAIDI NA ZAIDI. SIYO KWAMBA LINA NESA KIUBAVU HAPANA LINA NESA HASWAAA, KUTOKA PEMBE YA FEDHA INAPOWEKWA HADI KULE MBELE KAMA LINAJISUKUMA KUELEKEA ZIWANI. LIKAENDELEA KWA DAKIKA KADHAA KISHA LIKATULIA.
HUKU NIKIBISHA KIMOYOMOYO NAMI NIKAOMBA RUKSA KUJARIBU KULISUKUMA NIKIDHANI KUWA 'SI LINACHEZA KWASABABU KIJANA ANALISUKUMA. ...SUKUMA...SUKUMA... AAAAAH WAPI!! 'NGOMA IMEDINDA' JIWE HALICHEZI NG'O!
UNYAYO WA KAKA YAKE NA NYABUREBHEKA.
SIRI KUBWA YA JIWE LA NYABUREBHEKA KUCHEZA KWA MUJIBU WA MZEE MAKOROKORO ANASEMA KUWA MIAKA YA 1800 (historia haijahifadhiwa vyema) MTU NA KAKA YAKE WALIKUWA KATIKA SAFARI YA KUHAMA KUTOKA KOME UKARA KUELEKEA NYAMANGA MAKAO YAO YA ZAMANI, AMBAPO WALIACHA KUKU NA MBUZI NA MIFUGO MINGINE.(yale maisha ya kuhama hama),SASA KTK SAFARI YA KURUDI MAKAZI YA ZAMANI, MDOGO MTU AKAKANYAGA SEHEMU KWA MGUU WA KUSHOTO AKAPOTEA, KAKAYE AKAFIKA ENEO HILO AKAKANYAGA KWA MGUU WA KULIA HAKUDHURIKA.
KAKA MTU AKAMTAFUTA SANA MDOGO WAKE, KATU ASIPATIKANE. AKAAMUA KUREJEA NYUMBANI KUTOA TAARIFA NAO WAKAFIKA ENEO LA TUKIO, SAKA SANA WASIMPATE KIJANA WAO. HATA SIKU YA 2,YA 3 HADI WIKI, KIJANA KATU ASIONEKANE!
UNYAYO WA NYABUREBHEKA KIJANA ALIYEGEUKA JIWE.
KARAI LA KUNYWESHEA MIFUGO.
NDIPO WAKARUDI NYUMBANI KUFANYA TAMBIKO, TAMBIKO LIKAJIBU KUWA KIJANA WAO KAGEUKA JIWE PINDI TU ALIPO KANYAGA ENEO HILO KWA MGUU WA KUSHOTO.
MGANGA AKASEMA HAKUNA JINSI YA KUMREJESHA KIJANA ZAIDI YA WAO (WANANDUGU) KUMTEMBELEA (JIWE BUREBHEKA) KUFANYA TAMBIKO KILA BAADA YA MIAKA 4 KWA KUCHINJA MBUZI MWEUSI WANAYE MKUZA WAO MBUZI ANAYEKWENDA MALISHONI MWENYEWE WAO WAKIMPA HIFADHI YA KULALA TU.
MIE NA NYABUREBEKA.
INASEMEKANA KIPINDI CHA MIAKA YA NYUMA WAZUNGU WALIFIKA ENEO HILI NA MELI ZAO ZENYE NGUVU WAPATE KUTAFITI KISAYANSI NGUVU HIZO ZA JADI, WAKALIFUNGA MINYORORO NA KULIVUTA KWA MINAJILI YA KULITUPA ZIWANI, WAKACHEMSHA BAADA YA MINYORORO YAO IMARA KUKATIKA.