ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 11, 2017

MABADILIKO CCM MJUMBE WA KAMATI SOPHIA SIMBA AFUKUZWA UANACHAMA.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Sophia Simba afukuzwa uanachama kwa kosa la usaliti, Adam Kimbisa na Dk Emmanuel Nchimbi wapewa onyo.

VIDEO Koffi Olomide - NYATAQUANCE


Koffi Olomide - NYATAQUANCE [Clip Officiel]

KAFULILA AMTAKA MAKONDA KUONESHA VYETI HADHARANI AU KAMA HANA AJIUZURU ILI WATU WAENDELEE NA MAMBO MENGINE.

ALIYEKUWA Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameibuka na kuongea mambo matano kuhusiana na sakata la vyeti feki linalomuandamana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. 

Kafulila amesema yafuatayo;
"Kwanza ni ushauri wangu kwamba Makonda amsaidie Rais ama kwa kuonesha vyeti vyake vyote kuondoa utata au ajizulu ili serikali iendelee na mambo mengine.

"Obama alipotuhumiwa kuhusu uraia wake USA alifanya kazi ndogo tu ya kuweka vyeti vyake vyote hadharani na akawa amefunga utata wa uraia wake. hivyo ni vema Makonda afanye hivyo kama anavyo au akae pembeni kwani nchi ni muhimu kuliko mahusiano yake na Rais.

"Rais anapaswa kujua kuwa hoja ya jinai ya kughushi vyeti inayopigiwa kelele inahusu pia umakini wa mamlaka yake kama mteuzi wa Makonda kwamba kuna shida ya vetting. hivyo kuondoa hilo ni kuchukua hatua stahiki. hakuna namna Rais atamlinda Makonda na akabaki na sifa ya kuwa Rais anaesimamia haki na Usawa. Itafanya aonekane kama waliomizwa na ukali wake katika kusimamia sheria ni kwasababu hawakuwa na ukaribu nae na zaidi itafanya aonekane Rais wa kawaida sana kwa kulinda uovu kwa sababu za binafsi.Hivyo ukimya wa Rais unafanya dhamira yake ya uzalendo ihojike kwani sio kawaida yake.

"Mamlaka kama Sekretariet ya Maadili ya Uongozi ilipaswa kuwa imeshachukua hatua kuondoa wingu hili kwani kinachojadiliwa hapa mbali zaidi ya jinai pia kinahusu uadilifu wa Kiongozi(intergrity). ukimya wa taasisi hii ni mfano mbaya wa namna taasisi zinavopigwa ganzi pindi haki inapotakiwa kutendeka lakini inagusa maslahi ya Rais. huu ni uzoefu niliopata kuona hata kwenye sakata la Escrow.likitokea jambo ambalo Rais ana maslahi taasisi zetu zimekuwa nzito na kigugumizi kuchukua hatua ipasavyo.

"Chuo cha Uvuvi walichomsajili kwa cheti cha form4 ambacho anatuhumiwa kuwa sio chake pamoja na Chuo Kikuu ni taasisi ambazo mjadala huu unahusu heshima ya taasisi hizo. hivyo ilipaswa zijitokeze kuthibitisha au kukanusha. ukimya wao unaashiria hofu yao kwasababu kaguswa mtoto wa mfalme! Huu ni mfano mbaya kabisa kwa taasisi za taaluma kwamba zinaweza kuwa za hovyo kiasi hiki.

"Kibaya zaidi ni ukimya wa NECTA ambao ni mamlaka ya kutoa vyeti. sasa cheti kinachosumbua hapa ni cha form4 ambacho ni mali yao. lakn kwa woga wamekaa kimya kuficha ukweli na kuacha mjadala wa cheti uwe kati ya Askofu na RC na watanzania wakati wao ambao ni mamlaka sahihi kuondoa utata wamekaa kimya kwa hofu ya kugusa mtoto wa mfalme.. Hili ni fundisho la kwani nchi hii haiendelei kwasababu taasisi hizi haziko imara kutimiza majukumu yake kisheria bali zinafanya majukumu yake kwa kadiri ya mapenzi ya mteule wao."

Friday, March 10, 2017

MAHAKAMA YAMUONDOA MADARAKANI RAIS WA KOREA KUSINI.


MAHAKAMA ya Katiba ya Korea Kusini imeafiki uamuzi wa bunge wa kumuondoa madarakani rais wa taifa hilo Park Geun-hye. 
Katika uamuzi wa kihistoria leo Ijumaa, Mahakama hiyo ya Katiba, ikiwa na jopo la majaji wanane, imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuvuruga demokrasia 
.
Park ambaye alikuwa mwanamke  wa kwanza kuwa rais wa Korea Kusini alihusishwa na kashfa ya ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini kwa kushirikiana na rafiki yake mkubwa Choi Soon-Sil. Wawili hao wanakabiliwa na shtaka la kuchukua hongo kutoka mashirika makubwa 
.
Bi Park ameomba radhi kutokana na taathira za kashfa hiyo lakini amekanusha kukiuka sheria. Rais huyo alipokonywa mamlaka yake mwezi Desemba wakati bunge lilipomuuzulu lakini amekuwa akishikilia rasmi cheo chake akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba. Hivi sasa kuna uwezekano wa Park kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi 
.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe katika maeneo mbali mbali yaliyo na wapinzani wa rais huyo 

Wananchi wa Korea Kusini wakifurahia kuuzuliwa Rais Park.
Hukumu hiyo imepokelewa kwa shangwe na wananchi ambao walitokeza mitaani kuunga mkono uamuzi wa mahakama. Wafuasi wake pia walionekana na kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili. Uchaguzi wa urais sasa utafanyika katika kipindi cha siku 60 
.
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi Han Min-koo amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari kwani nchi jirani ya Korea Kaskazini inaweza kutumia vibaya hali iliyojitokeza. Korea hizo mbili zimekuwa zikihasimiana kwa muda mrefu

TAMASHA LA BATTLE ZONE LAJA MWANZA


Mkurugenzi wa Kampuni ya White Fish Entertainment (Katikati) Frank Mnubi akizungumza na wanahabari kuhusu Tamasha la Battle Zone katika Ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.



Tamasha la Battle Zone lafanyika Pasaka Rock City Mall
Na James Timber, Mwanza
Tamasha la Battle Zone lapangwa kufanyika Aprili 16, mwaka huu katika ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Rock City Mall Mkurugenzi wa Tamasha hilo kupitia Kampuni ya White Fish Entertainment Frank Mnubi alisema kuwa ameandaa tamasha kwa lengo la kuinua na kukuza vipaji kwa mkoani hapa na mikoa jirani.

Mnubi alisema kwa wale wanaotaka kujiunga na shindano hilo wafike katika ofisi ya White Fish Entertainment kwa ajili ya kujaza fomu ya ushiriki.

“Naomba vijana wafike katika ofisi ya White Fish Entertainment kwa ajili ya kuchukua fomu ya usajili, bila kujari jinsia wala sehemu atokayo,” alisema Mnubi.
Alisema kuwa wasanii wanaotakiwa wamegawanyika makundi mawili kundi la awali ni wanaofanya muziki wa kufoka (Hip Hop) na lingine ni kwa wale wanaocheza (Dancers).

Hata hivyo, alishukuru  Kampuni ya Simu ya Itel na kinywaji cha Coca cola kwa kudhamini tamasha hilo.

VIGOGO 11 CCM KUENGULIWA MABADILIKO YA CCM

Dar es Salaam/Dodoma. Wakati mabadiliko ya katiba yatawaengua vigogo 11 katika uongozi wa CCM walio na kofia zaidi ya moja, hatima ya idadi kama hiyo ya wanachama wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, itajulikana kesho.

CCM inatarajia kupitisha mabadiliko makubwa ya katiba, ambayo yatapunguza idadi ya wajumbe katika vikao vya juu na pia kupunguza kofia za uongozi mwanachama mwenye cheo ndani ya chama, ubunge au serikalini.

Mabadiliko hayo yalipendekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam Desemba 13 mwaka jana.

Mabadiliko hayo yalitangazwa kwenye vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM aliyemaliza muda wake, Nape Nnauye kwamba muundo wa chama umebadilika na mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi wa CCM, Toleo la 2012, Kifungu cha 22 na 23.

Nape alizitaja nafasi hizo kuwa ni mwenyekiti wa tawi, kijiji au mtaa, kata/wadi, jimbo, wilaya na mkoa. Wengine ni makatibu wa halmashauri kuu wa ngazi zote, mbunge, mwakilishi na diwani.

Mabadiliko hayo pia yamepunguza ukubwa wa Kamati Kuu kutoka wajumbe 34 hadi 24, hali inayofanya wanaoingia kwa kupigiwa kura kupungua hadi wanne kutoka kumi.

Pia nafasi za ujumbe wa Halmashauri Kuu zimepungua kutoka 388 hadi 158, huku wengi wakiingia kwa nafasi zao na wajumbe kutoka wilayani kuondolewa.

Kutokana na mabadiliko hayo, baadhi ya viongozi wenye kofia zaidi ya moja wameshaanza kutangaza kutotetea nafasi zao katika uchaguzi ujao wa viongozi wa CCM na jumuiya zake.

Wa kwanza alikuwa Sophia Simba ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba. Simba pia mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu.

Mwingine ni Abdallah Bulembo aliyetangaza kuwa hatagombea uenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM. Bulembo ameteuliwa na Rais Rais John Magufuli kuwa mbunge, jambo linalomfanya awe na kofia mbili.

Mbali na hao waliotangaza hadharani, wapo vigogo wengine ambao wana nafasi zaidi ya moja za uongozi, akiwamo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi ambaye mbali na uwaziri ni mbunge, mjumbe wa NEC na mjumbe wa Kamati Kuu.

Pia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ni mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu, kama ilivyo kwa Profesa Makame Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu wakati Shamsi Vuai Nahodha ni mbunge na mjumbe wa Kamati Kuu.

Mabadiliko hayo pia, yatawakumba wenyeviti wa CCM wa mikoa ambao kwa nafasi zao ni wajumbe wa NEC. Mmojawapo ni Kimbisa, ambaye ni mwenyekiti wa Mkoa wa Dodoma na mjumbe wa Kamati Kuu.

Wenyeviti wa mikoa ambao pia ni wabunge ni Joseph Msukuma (Geita), Martha Mlata (Singida) na Deo Simba (Njombe). Mwenyekiti wa CCM wa Mbeya, Godfrey Zambi pia ni mjumbe wa NEC na mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Mwingine anaonekana kuguswa na mabadiliko hayo ni Salma Kikwete ambaye ni mjumbe wa NEC anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini na ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais kuwa mbunge.

Bulembo ajiuzulu

Katika hatua nyingine, jana katika kikao cha Baraza Kuu Maalum la Jumuiya ya Wazazi, Bulembo alitangaza kutotetea nafasi yake ya unyekiti.

“Kila mmoja ni shahidi, wakati naingia, jumuiya hii ilikuwa inakwenda kufa, jambo lililosababisha aliyekuwa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kutaka kuifuta. Lakini nikamuhakikishia ataona mapinduzi akiniachia,” alisema Bulembo.

“Sasa natoka kifua mbele, yale yote niliyoyaahidi nimetimiza kwa asilimia 75. Tangu nimeingia hatujawahi kuomba hata shilingi moja kwa ajili ya uendeshaji,” alisema.

Hata hivyo, Bulembo alisema ataendelea na vikao vyote mpaka Oktoba atakapomkabidhi rasmi mwenyekiti mpya.

Alisema kwa sasa asiulizwe kwa nini amechukua uamuzi huo na kwamba hoja siyo kuteuliwa kwake kuwa mbunge bali ni utaratibu aliojiwekea katika maisha yake.

KAA Gent 2 - 5 KRC Genk ● MBWANA SAMATTA NA MAGOLI YAKE & Highlights ●UEFA Europa League 2017

MICHUANO ya Uefa Uropa Ligi imepigwa jana usiku kwa michezo mbalimbali,Manchester United imeambulia Sare na Fc Rostov bao 1-1 ,Apolia Nicosia wakiwa nyumbani wamechapwa na Anderletch bao 1-0.

Fc Copen hagen imetakata kwa bao 2-1,Celta vigo imeichapa Fc Krasnodar 2-1, Shakle imetoshana nguvu na Borussia Monchenglabach 1-1, KAA Gent imechapwa na KRC Genk 5-2, Lyon imeichapa As Roma 4-2 na Olympiakos imetoshana nguvu na Besktas kwa bao 1-1. Shuhudia video ya magoli ya mchezo baina ya KAA Gent v/s KRC Genk ambapo mtanzania Mbwana Samatta ameng'ara vilivyo kuisaidia timu yake ikaibuka na ushindi mnono.

MAGAZETI YA LEO: CCM MATUMBO MOTO DODOMA, LISSU AVUNJA UKIMYA UCHAGUZI MKUU TLS, ASKOFU GWAJIMA ARUSHIWA KOMBORA, TANESCO YAIPA ZNZ WIKI.


 CCM matumbo moto Dodoma, Lissu avunja ukimya uchaguzi mkuu TLS, Askofu Gwajima arushiwa kombora, TANESCO yaipa Zanzibar wiki 2.
 
RC Makonda azua balaa jipya, Lissu: Nitaomba kuwa sehemu ya kesi TLS, Dk. Shein: Zanzibar tukikatiwa umeme tutatumia vibatari. Pata yaliyojiri katika magazeti ya leo hapa.

Thursday, March 9, 2017

MAZINGIRA YA BARABARA YA MISHENI KIRUMBA JIJINI MWANZA NA DHAHMA YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

 Ni barabara ya Misheni Kirumba kushuka kuelekea CCM Kirumba, pembezoni mwa Villa Park, The Kiss Club kulia nako kushoto ni uwanja wa Furahisha, Studio za ABC na maduka, hali ya mazingira mara baada ya mvua kubwa kunyesha jana jijini hapa.
 Askari Polisi kikosi cha usalama barabarani Afande Mama Kothecha akijaribu kurudisha magari yasipite barabara ya Misheni Kirumba kushuka kuelekea CCM Kirumba mara baada ya mvua kubwa kunyesha jana jijini hapa. PICHA NA ZEPHANIA MANDIA.
  Ni barabara ya Misheni Kirumba kushuka kuelekea CCM Kirumba, pembezoni mwa Villa Park, The Kiss Club kulia nako kushoto ni uwanja wa Furahisha, Studio za ABC na maduka, hali ya mazingira mara baada ya mvua kubwa kunyesha jana jijini hapa.
  Ni barabara ya vumbi pembezoni mwa uwanja wa Furahisha eneo la gereji.
 Hali tete.
 Uwanja wa Furahisha ambako kulikuwa na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia,viwanja hivi vilikuwa katika hali hii.
Huwezi kutofautisha wapi barabara na wapi mtaro ukijitusu imekula kwako.

NAPE AHAIDI KUWALINDA WAWEKEZAJI TASNIA YA HABARI.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, ameahidi kulinda uwekezaji wa mmiliki wa kituo cha Redio EFM na Tv E, Francis Ciza, maarufu Dj Majizo.


NAPE alitoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea makao makuu ya kituo hicho cha redio katika eneo la Kawe, Dar es Salaam.

Katika hotuba yake fupi aliyoitoa mbele ya watumishi wa redio hiyo jana, Nape alisema yeye ndiye waziri mwenye dhamana ya habari, hivyo ana wajibu wa kulinda habari na wawekezaji katika tasnia hiyo.

“Nataka nikuhakikishie mimi ndie waziri mwenye dhamana ya habari, kuilinda habari na tasnia yenyewe, lakini kuwalinda wanaowekeza kwenye tasnia hii, kwa sababu uwekezaji kama huu ulioufanya katika tasnia hii, ndio unanifanya mimi kama waziri niendelee kuwapo.
55
“Lakini ndio unaoifanya Serikali na Tanzania kuendelea kuwa nchi njema ya watu waendelee kuishi, kazi yako ni nzuri na nyinyi kwa kuwa mnasikika sana Dar es Salaam, mchango wenu wa kuifanya Dar es Salaam kuwa njema ni mkubwa na hauwezi kupuuzwa hata kidogo.

“Kwa mtu yeyote mwenye mapenzi mema na Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla atawalindeni, atawalinda na kuhakikisha mnapata ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yenu,” alisema.

Nape pia alimpongeza Majizo kwa uwekezaji mkubwa alioufanya na kuahidi kwamba serikali itampatia ushirikiano na msaada anaouhitaji ili kuhakikisha uwekezaji wake unasonga mbele.

“Kama Serikali na kama waziri mwenye dhamana ya habari, nimeshuhudia kwa macho yangu uwekezaji uliouweka hapa, tutalinda uwekezaji uliouweka usiharibiwe ovyo.

“Si Watanzania wengi wenye maono haya, najua umeanza mbali mpaka kufika hapa, si kazi rahisi, ndiyo maana nasema ukiona mtu kasimama si vizuri kwenda kumparamia ovyo.

“Ni vizuri kuheshimu kazi ambayo amehangaika nayo, jasho si la bure, uwekezaji huu ni mkubwa sana, labda iwe hujui alichowekeza, hujui kapambana kiasi gani kufika hapo ndiyo unaweza kufanya unachotaka,” alisema Nape.

 Nape alisema katika dunia yenye ushindani vita ni kubwa, hivyo akamtaka mwekezaji huyo asikatishwe tamaa na kelele za barabarani kwa sababu Serikali iko pamoja naye.

Aliwaeleza pia watumishi wa redio hiyo kwamba wasiwe na hofu kwa sababu kazi wanayoifanya ina baraka za Mungu, hivyo hawapaswi kuvunjika moyo.

“Mkiona mti unaotupiwa mawe ni ule wenye matunda, kwa miaka mitatu mafanikio mliyoyapata ni makubwa sana, lazima yatamtisha yule aliepo sokoni, kwahiyo mkiona kuna vita basi mjue ni kwa sababu kasi yenu ni kubwa mno kiasi kwamba inawatia joto wengine.

“Mtu mmoja aliwahi kuniambia wakati naanza siasa kwamba ukiona watu hawakuzungumzii jiulize kama bado unaishi au umeishakufa, ukiona watu wanakuzungumza ujue umewazidi,” alisema Nape.

Majizo ni mmoja wa watu waliohusishwa na dawa za kulevya katika kampeni iliyokuwa ikiendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

UMOJA WA AZAKI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI VIPAUMBELE VYAO KATIKA BAJETI YA 2017/2018

  Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) akizungumza kwenye kongamano la vijana kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Geofrey Adroph
 Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine (CCM) akizungumza na vijana kwenye kongamano lililoandaliwa na Asasi ya Dira ya Vijana (TYVA) kwa kushirikiana na asasi za mbalimbali za vijana katika kujadili vipaumbele vya vijana katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuhusu namna ambavyo wabunge wanajaribu kupigania maslahi ya vijana kwenye bajeti. 

Mbunge wa viti maalum wa Katavi, Rhoda Edward Kunchela(CHADEMA) akizungumza na vijana kuhusu mchakato wa bajeti unavyofanyika kutoka ngazi ya chini mpaka ya juu kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ukumbi wa Wanyama jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa AZAKI akizungumza na vijana kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo.
 Mratibu wa Mtandao wa Vijana na Bajeti, Saddam Khalfan akizungumzia suala la bajeti ya taifa hasa kwa bajeti ya mwaka 2017/18 kuwa ni sera na sheria mama ya masuala ya mapato na matumizi ya serikali hivyo serikali ni lazima ifahamu umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya vijana na ushirikishwaji wao katika mipango ya maendeleo kwenye kongamano lililowakutanisha vijana leo katika ukumbi wa hoteli ya Wanyama jijini Dar.
Majadiliano yakiendelea kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha  2017/2018 hasa kwa bajeti inayowahusu vijana lililoandaliwa na Asasi ya Dira Vijana (TYVA) kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za vijana kwenye hotel ya Wanyama leo jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye kongamano lililowakutanisha ili kujadili masuala ya bajeti hasa bajeti ya mwaka 2017/18 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo( katikati) akiwa kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ukumbi wa hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Victoria Mwanziva ambaye ni mtafiti wa masuala ya Demokrasia na Maendeleo. 
 Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine (CCM) akichokoza mjadala wa bajeti kwa vijana
Baadhi ya vijana wakichangia mada juu ya bajeti kwa vijana pamoja na upatikanaji wa ajira
Mshauri wa Demokrasia na utawala bora, Frederick Fussi akitoa mada kwenye mkutano huo
 Baadhi ya vijana wakiwasilisha maoni
Mbunge Viti Maalum CHADEMA, Anatropia Theonest akifunga kongamano la vijana lililokuwa linajadili mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Vuma Augustine akizungumza na waandishi wa habari na waandishishi wa habari kuhusu ukusanyaji wa maoni kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye bujeti ya mwaka 2017/2018.
  Mbunge wa viti maalum wa Katavi Rhoda Edward Kunchela(CHADEMA) jinsi alivyoshiri kwenye mchakato wa vijana kutaka kujua ni kwa jinsi gani vijana wanaweza kunufaika na bujeti ya Taifa.
Makamu wa Rais wa DARUSO, Shamira Mshangama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bujeti zinazowekwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja changamoto wanazozipata katika upatikanaji wa fedha za mikopo zinazotengwa na serikali katika bajeti yake.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo (TYVA), Dianarose Lyimo akizungumza na waandishi wa habari kuhusi taasisi ya Vijana ya TYVA inavyojihusisha na mijadala pamoja na makongamano kwa vijana kutambua umuhimu wa bajeti hasa bajeti ya Vijana.
Picha ya Pamoja