MAHAKAMA ya Katiba ya Korea Kusini imeafiki uamuzi wa bunge wa kumuondoa madarakani rais wa taifa hilo Park Geun-hye.
Katika
uamuzi wa kihistoria leo Ijumaa, Mahakama hiyo ya Katiba, ikiwa na jopo
la majaji wanane, imesema kuwa bi Park alikiuka sheria na kuvuruga
demokrasia
.
.
Park
ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa Korea Kusini
alihusishwa na kashfa ya ufisadi kutoka makampuni makubwa nchini kwa
kushirikiana na rafiki yake mkubwa Choi Soon-Sil. Wawili hao
wanakabiliwa na shtaka la kuchukua hongo kutoka mashirika makubwa
.
.
Bi
Park ameomba radhi kutokana na taathira za kashfa hiyo lakini
amekanusha kukiuka sheria. Rais huyo alipokonywa mamlaka yake mwezi
Desemba wakati bunge lilipomuuzulu lakini amekuwa akishikilia rasmi cheo
chake akisubiri uamuzi wa Mahakama ya Katiba. Hivi sasa kuna uwezekano
wa Park kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi
.
Hukumu hiyo imepokelewa kwa shangwe na wananchi ambao walitokeza
mitaani kuunga mkono uamuzi wa mahakama. Wafuasi wake pia walionekana na
kumekuwa na mzozano kati ya makundi hayo mawili. Uchaguzi wa urais sasa
utafanyika katika kipindi cha siku 60 .
.
Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi Han Min-koo amelitaka jeshi la nchi hiyo kuwa katika hali ya tahadhari kwani nchi jirani ya Korea Kaskazini inaweza kutumia vibaya hali iliyojitokeza. Korea hizo mbili zimekuwa zikihasimiana kwa muda mrefu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.