Mkurugenzi wa Kampuni ya White Fish Entertainment (Katikati) Frank Mnubi akizungumza na wanahabari kuhusu Tamasha la Battle Zone katika Ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza. |
Tamasha la Battle
Zone lafanyika Pasaka Rock City Mall
Na James
Timber, Mwanza
Tamasha la
Battle Zone lapangwa kufanyika Aprili 16, mwaka huu katika ukumbi wa Rock City
Mall jijini Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Rock City Mall Mkurugenzi wa Tamasha
hilo kupitia Kampuni ya White Fish Entertainment Frank Mnubi alisema kuwa
ameandaa tamasha kwa lengo la kuinua na kukuza vipaji kwa mkoani hapa na mikoa
jirani.
Mnubi
alisema kwa wale wanaotaka kujiunga na shindano hilo wafike katika ofisi ya
White Fish Entertainment kwa ajili ya kujaza fomu ya ushiriki.
“Naomba
vijana wafike katika ofisi ya White Fish Entertainment kwa ajili ya kuchukua
fomu ya usajili, bila kujari jinsia wala sehemu atokayo,” alisema Mnubi.
Alisema kuwa
wasanii wanaotakiwa wamegawanyika makundi mawili kundi la awali ni wanaofanya
muziki wa kufoka (Hip Hop) na lingine ni kwa wale wanaocheza (Dancers).
Hata hivyo,
alishukuru Kampuni ya Simu ya Itel na
kinywaji cha Coca cola kwa kudhamini tamasha hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.