ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 24, 2013

WASTANI WA WAZEE 500 HUUAWA KILA MWAKA KUTOKANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA MIKOA YA KANDA YA ZIWA

Mratibu wa Hifadhi ya Jamii Julius Mwengela akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Tatizo la mauaji ya vikongwe katika mikoa ya Kanda ya Ziwa limeendelea kuwaumiza vichwa wadau mbalimbali wanao jihusisha na masuala ya maendeleo ya jamii hivyo kufanya jitihada kadhaa zinazolenga kutokomeza ukatili huo.

Shirika la MAPERECE lenye makao makuu yake wilayani Magu leo limeketi na waandishi wa habari jijini Mwanza kwa lengo la kuainisha masuala ya wazee ikiwemo changamoto wanazokumbana nazo mwisho wa siku yajulikane kwa mapana zaidi ikiwa ni pamoja na utatuzi wake.  
Wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kikazi zaidi.
Vitendo vya mauaji ya wazee vimezidi kuongezeka na kusambaa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania. takwimu kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na serikali zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 1998- 2001 kulikuwepo na matukio 17,220 ya kuwadhalilisha wazee namauaji 1,746 kutokana na imani za uchawi.

Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu ya mwaka 2009 ilionyesha kuwa wanawake wazee 2,583 walikuwa wameuawa katika mikoa minane ikiwa ni wastani wa mauaji 517 kila mwaka.

Taarifa kutoka mkoani Shinyanga pia zinatisha kwani wanawake wazee 241waliuawa mkoani humo pekee kati ya januari 2010 na juni 2011.

Wakati mauaji yaliyo mengi yanatokea mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Kagera Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa tatizo la mauaji linasambaa kwenye mikoa mingine ya Tanzania
Siyo sahihi kusema kuwa juhudi zote za serikalina wadau wengine hazina nguvu. Hata ahivyo ni ukweli kuwa jitihada hizi haziratibiwi na serikali na hivyo kukosa ufuatiliaji ambao ungeweza kuleta mahusiano baina ya wadau na kuleta uwajibikaji kwakutoa maamuzi kupambana na mauaji ya wanawake wazee.
Lengo kuu la kusanyiko hili ni kuwapa upeo waandishi wa habari juu ya masuala ya ukatili ufanywao kwa vikongwe nchini ili kutetea haki stahiki za wazee na watoto walio katika mazingira hatarishi wanayoishi pamoja na wazee.
Mapungufu mengine ni pamoja na:
Kukosekana na mipango, fedha na nguvu baina ya Wizara na mashirika yanayohusika na kukabiliana na mauaji ya Wazee.

Mauaji ya wazee kuchukuliwa kwa sura ya imani za uchawi na hivyo kujenga dhana kuwa haiwezekani kuyathibitisha pasipo shaka mahakamani kama ilivyo  kwa kesi nyingine za mauaji.

Mara nyingi viongozi wa serikali, wanasiasa na asasi za kiraia hubaki kimya wakati makosa makubwa dhidi ya binadamu yanapofanyika.

Mipango ya kukabiliana na tatizo hili kukosa uwezeshwaji (Fedha)

Kutotungiwa sheria kwa sera ya Taifa kwa wazee kwa miaka kumi sasa.

MAPENDEKEZO /JINSI YA KUKABILIANA NA TATIZO HILI
Bado tunaamini Serikali ikiwaratibu kikamilifu wadau wote patakuwepo na nia ya dhati na uwajibikaji wa taasisi zote za serikali zinazohusika pamoja na wadau wengine tutaweza kuleta mabadiliko yatakayoondoa kabisa mauajia ya wazee nchini.


"NI MUHIMU SANA..."

Ujumbe umefika.

NCHI SIO YA RAIS NI YETU SOTE TUMSAIDIE KIFIKRA


Wanamabadiliko.
Ndugu zangu kutokana na hali ya nchi yetu kukumbwa na changamoto mfululizo na lawama zote tunambebesha Rais kusema ni nchi yake peke yake tunakosea, tujitahidi kumpa mawazo nini kifanyike wapi parekebishwe ili kujenga nchi. Tukikaa kimya eti tunasubiri sijui chama tawala king`atuliwe madarakani hivi navyo tunakosea.

Nchi ni yetu na sio ya mtu mmoja,  Rais tulimchagua wenyewe kwa mapenzi yetu, cha msingi katika hiki kipindi chake kilichobaki madarakani anahitaji msaada wa mawazo na sio lawama kama tunavyokesha kukilaumu chama tawala na uongozi wake.Kulaumu sio solution, solution ni kusaidiana wapi kakwama apate msaada na pindi tunapo fanikisha tumefanikiwa sote.

Lawama zisizokwisha kila kukicha hazisaidii ndugu zangu,Kikwete sio malaika wa kusema kila kitu anaweza na yeye ni binaadamu hajakamilika.

Nina imani kubwa hata hatakayekuja hataweza kuwaridhisha wanzatania wote mnavyotaka,cha msingi tuwe na tabia ya kutoa maoni nini kifanyike kwa viongozi wetu ili kujenga nchi na sio lawama ndugu zangu.

Nina Imani kubwa sana na watu wa jukwaa hili kwamba  wana fikra nzuri za kumshauri kiongozi yoyote yule ili kuleta maendeleo.Hata sisi kwenye jukwaa letu huwa tuna taratibu zetu tukiona kwamba fulani anakosea huwa tunajaribu kumrejesha kwenye njia iliyo sahihi na sio kumtupia lawama Moderator.

Nawaomba ndugu zangu kwa heshima zote na upendo wangu kwenu tujaribu kumsaidia huyu kiongozi wetu maana hata na yeye sidhani kama ana furaha na amani ndani ya nafsi yake kwa lawama za kila mtu.

Tujenge misingi ya kusaidiana kimawazo..najua wengi mmechoshwa na CCM na baadhi ya viongozi wao, sasa basi tujipange tusije kupoteza hata hiki tulichonacho wakati tukisubiri chama hicho kingine ambacho kitashika hatamu 2015, ila ninatoa angalizo, tusije tukaacha kuwasaidia hata hao watakaokuja kutuongoza kwa fikra kuwa wao tu ndiyo kila kitu.

Yangu ni hayo tu, nawatakia kila la heri.
                                                     Maganga One

Thursday, May 23, 2013

MOJA YA CHANGAMOTO ZA WAANDISHI WA HABARI



Zipo changamoto nyingi zinazowakabili wanahabari nchini tanzania, mbali na usalama wao pale wanapoibua mambo ndani ya mazingira yanayo wazunguka, wakisaka habari katika njia hatarishi na mambo kadha wa kadha lipo suala la kukosa ushirikiano kutoka kwa vyanzo vya habari ...dah kaazi kweli kweli.. chungulia kideo.

"!!.....SI UTANI AIRTEL YATOSHA....!!"

India inajulikana kwa lipi zaidi? Movies(Bollywood), shule bora au matibabu?? 

Sasa Airtel ya kuwezesha kulonga zaidi na walio india kwa bei nafuu, Kwa tsh 3000 tu utapata dakika 25, za kuwasiliana wiki nzima.

Kujiunga piga*149*13# upate kuwasiliana kwa bei poa ya shilingi 2 kwa sekunde.

 Airtel Yatosha!!

Wednesday, May 22, 2013

KWA NGUVU ZOTE MEYA WA JIJI LA MWANZA AHAIDI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA ELIMU NA AFYA KATA YA MKOLANI.

Ni vijana  wa darasa la saba shule ya msingi Nyasubi ambao leo wameanza mtihani wa moko wakiwa kwenye majadiliano, Shule hii ni moja kati ya shule za kata ya Mkolani ambazo Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula amefanya ziara ya ukaguzi kimaendeleo.


Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza na uongozi wa kata ya Mkolani ambapo alikutana na kamati ya Maendeleo ya Katanihumo WDC na kuelezea malengo ya ziara yake katika kukagua miradi ya maendeleo.


Kamati ya Maendeleo ya Katani humo (WDC) ikimsikiliza Mstahiki Meya aliyekuwa akielezea malengo ya ziara yake katika kukagua miradi ya maendeleo ikihusisha Sekta za Afya, Ekimu, Mazingira, miundombinu ya barabara, Maji na Umeme. 


Hapa Mstahiki meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akikagua Zahanati ya mtaa wa Mkolani.


Jengo la zahanati na huduma zikiendelea.


Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akisaini kitabu cha shule ya msingi Ibanda, moja ya kero kubwa shuleni hapa ni ukosefu wa vyumba vya madarasa, ofisi za waalimu na madawati.


Nyuma ya darasa ya moja kati ya madarasa shule ya msingi Mkolani ni mbao za madawati yaliyovunjika kwa kukosa matengenezo huku watoto wakibanana kwenye mabenchi wakitegemea mapaja kama meza.


Hali jinsi ilivyo...


Hatuna madawati...


Idadi ya madawati na wanafunzi haviuwiani.

Mstahiki Meya na wajumbe wa kamati ya maendeleo ya Kata na baadhi ya wajumbe wa kamati ya shule wakimsikiliza mwalimu wa shule ya msingi Mkolani akielezea changamoto zinazoikabili shule yake.


Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ameahidi kupambana kwa hali zote kuhakikisha mabadiliko yanafanyika ili kuboresha huduma zinazotolewa kata ya Mkolani.

AIRTEL YAZINDUA OFA KABAMBE KUPIGA SIMU KWENDA NJE

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano (kushoto) na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (wa pili kutoka kulia) wakizindua huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampun hiyo, Sunil Colaso.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice  Singano (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine   wanaofuatia ni Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Sunil Colaso na Meneja Biashara za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kutoka kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kupiga simu kwenda India kwa gharama nafuu. Wengine ni Meneja Biashara  za Kimataifa wa Kampuni hiyo, Prisca Tembo (kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Beatrice Singano na Balozi wa India hapa nchini, Debnath Shaw.

Airtel yazindua ofa kabambe kupiga simu kwenda nje ya nchi

•       Wateja kupata kifurushi cha dakika 25 kupiga simu kwenda India
•       Ofa hii inapatikana masaa 24 siku 7 za wiki,


Kampuni ya Bharti (“Airtel”) inayoongeza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na Asia leo imetangaza uzinduzi wa ofa itakayo wawezesha wateja wa Airtel Tanzania kupiga simu kwenda nje kwa gharam nafuu zaidi.

Ofa hii inaendelea kuonyesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuendelea kuwanganisha watanzania katika mtandao wa mawasiliano na kuwapa huduma  bora zenye gharama nafuu. Uzinduzi huu unafatia utambulsho wa huduma kabambe ya Airtel yatosha  iliyofanyika week chache zilizopita.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya, Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwn. Sunil Colaso alisema ”baada ya uzinduzi wa mafanikio ya  huduma yetu ya Airtel yatosha. leo tunazindua ofa ya mawasiliano ya  gharama nafuu  na kuwawezesha wateja wetu kuwasiliana na familia ,marafiki na washirika wa kibiashara walioko nje ya mipaka ya nchi.


Kwa kiasi cha chini cha hadi shilingi3, 000 sasa wateja wa Airtel  wanaweza kupiga simu India masaa 24 kwa siku 7 za wiki. Ofa hii itampatia mteja dakika 25 za muda wamaongezi kwa muda wa wiki nzima.

Aliongeza “Hii ni ya kwanza kutoka Airtel, na tunaendelea kuwahakikishia wateja wetu nchi nzima huduma bora, za uhakika na gharama nafuu za mawasiliano wakati wote. Tumesikiliza kile wateja wetu wanachokitaka na kutengeneza ofa inayokidhi mahitaji yao hivyo tutaendelea kutekeleza dhamira kwa watanzania ya kuleta huduma zenye ubunifu, bora na gharama nafuu ambazo kwa uhakika zitaleta uhuru wa kuongea nje ya mipaka. 


Ofa hii itawawezesha wateja wanaosafiri au kuwasiliana na India iwe kimasomo, kibiashara , wanaotembelea India kimatibabu kuwa na mawasiliano na familia zao kwa gharama za kiushindani zilizo nafuu zaidi. Uzinduzi huu ni mwanzo wa kuleta  mapinduzi ya mawasiliano katika soko la Tanzania.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania, H.E. Mr.Debnath Shaw alisema” Tunawapongeza Airtel kwa kuzindua ofa hii itakayoendelea kutuunganisha na kuendeleza ushirikiano wetu kati ya India na Tanzania. nchi hizi mbili zimekuwa na ushirikiano wa karibu si kibiashara tu bali katika sekta ya elimu, Afya na shughuli nyingine za kijamii. 


Ninayofuraha kuona Airtel ikiwa mstari wa mbele kuleta gharama nafuu katika soko la Tanzania. Nchini India Airtel ni mtandao  unaoongoza uliowekeza katika technologia ya hali ya juu, mtandao bora na unaotoa huduma bora za gharama nafuu kwa wateja wake. Ninayofuraha kuona huduma za mawasiliano zinabadilika kwa kasi na kufanana kama za India katika soko la Airtel barani Afrika.”
“Tunaamini hii ni fulsa pekee kwa wafanyabiashara , wanafunzi waliko India na wengine wanaotembelea India kwa sababu mbalimbali kuwasiliana na familia, marafiki na washirika wa kibishara waliko Tanzania kwa
gharama nafuu

Akifafanua kuhusu ofa hii Meneja wa biashara za kimataifa wa Airtel bi Prisca Tembo alisema” ofa hii inapatikana katika kifurushi cha muda wa maongezi ambapo kwa bei moja ya shilingi 3000 mteja atapata dakika 25  atakazozitumia masaa 24 kwa siku 7. Kifurushi hiki kitatozwa kwa sekunde na kudumu kwa muda wa wiki nzima. Sambamba na hilo, Simu zitakazopigwa kwenda nchi nyingine nje ya ofa hii zitatozwa kwa bei ya kawaida”

“Ili kujiunga na ofa hii mteja anatakiwa kupiga*149*13# na kuweza kufurahia ofa hii. Na huduma hii ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima” aliongeza Tembo

Hivi karibuni Airtel ilizindua huduma ya Airtel yatosha inayotoa ofa  ya vifurushi vya muda wa mongezi, ujumbe mfupi na internet zinavyomuwezesha mteja kuwasiliana na mtandao wowote nchini. Ikiwa katika mwendelezo wake wa kuboresha huduma zake Airtel imezindua ofa mpya ya kupiga simu kwenda nje ya nchi inayompatia mteja kifurushi cha  muda wa maongezi kupiga simu kwenda India. Ili kupata huduma hii  piga *149*13# na unganishwe sasa.

FANI YA UANDISHI WA HABARI IMEVAMIWA, TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA.

Pichani ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani (Picha na Maktaba).
 ---
Watu wengi kwa sasa wameibuka na kutokea kuipenda fani ya uandishi wa habari bila kujua misingi na miiko ya uandishi wa habari. Tatizo moja ambalo limeonekana ni kubwa sana ni utandawazi ambao umekuwepo na kutokea ibuko la kila kijana kufungua gazeti tando (blog).

Hatukatai kuja kwa magazeti tando ila naomba tujiulize, yanatumika ipasavyo ama ndiyo limekuwa ni wimbi vamizi lenye kutoa ama kusambaza habari hata zile zisizokuwa na vyanzo kamili na visivyojitosheleza.Kwa sasa imezuka tabia ya wanaojiita wamiliki wa magazeti tando,wengi wao kukopi na kupaste vitu wanavyoviokota katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, facebook na mingine mingi.

Sina nia ya kumsema mtu bali napenda tuelimishane kama vijana wenzangu,ambao wametokea kuipenda fani ya uandishi wa habari, wakumbuke kuwa fani ya uandishi wa habari ina miiko na maadili yake, mfano. Katika kuandika habari za mazingira, siasa, elimu, uchumi, michezo, burudani ukiangalia habari hizi zote zina misingi na miiko yake. Leo hauwezi kumchukua mwandishi wa habari za michezo ukamwambia aandike habari za uchumi kwa vile hatakuwa na takwimu za uchumi na hata akiandika hiyo habari na kuisoma utakuwa unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.

Vile vile ni vizuri vijana wenzangu kutambua kuwa kila kazi ina mipaka na misingi yake, juzi juzi nilisoma habari katika gazeti tando moja wapo ikisema, 'ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA IRINGA MHESHIMIWA MCHUNGAJI MSIGWA ASWEKWA NDANI' nilijiuliza maswali mengi ambayo kiukweli nilikosa majibu yake, kuona huyu aliyeandika hiki kichwa cha habari kweli amepitia fani ya uandishi wa habari ama ndio ule upepo vamizi?

Maana unapoandika habari za mahakamani, polisi kuna misemo yake, hauwezi kumuhukumu mtu moja kwa moja kwa kusema fulani ni mwizi, hata hao polisi ambao huwa wanakwenda kukamata watu eneo la tukio hawawezi kusema fulani ni mwizi mpaka apelekwe mahakamani ndipo sheria ichukue mkondo wake na kumbaini huyo aliyekamatwa ni mwizi.

Naomba tufike mahali tuheshimu utu wa watu na kuepuka udhalilishaji wa bila kujua naamini baadhi ya vijana wengi walioamua kufungua magazeti hayo tando ambayo yanatoa habari, hawana taaluma ya uandishi wa habari.

Napenda kuwapongeza wale walioamua kufungua magazeti tando katika milengo yao tofauti ikiwemo kutoa habari kwa njia ya 'kufundisha masuala ya urembo, mapishi, kuwasaidia kuwatangaza vijana katika muziki na hata wale walioamua kuandika habari zao binafsi.

Nayasema yote hayo kwa vile kumezuka wimbi la vijana wanaotaka kuichafua fani ya uandishi wa habari na ionekane si fani ya watu walioenda shule bali ni ya wahuni tu wasiojua mambo, naomba vijana tuelimike na tujifunze kwa watu wanayoyajua mambo ili tuweze kufika mbele zaidi.
Namalizia kwa kusema tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Asanteni sana kwa kusoma.
Imeandikwa na Cathbert A. Kajuna

HUDUMA ZA NIC BANK ZAZIDI KUPAA KANDA YA ZIWA SASA ZAIMARIKA AFRIKA MASHARIKI


Mkurugenzi wa NIC Bank James Muchiri akiitambulisha safu wa watendaji wa benki hiyo kwa makao yake makuu hapa nchini yaliyopo jijini dar  kwa wafanyabiashara, wawekezaji na wateja wa NIC mkoa wa Mwanza, katika hafla ya chakula cha jioni ilifanyika katika ukumbi wa Nyerere Gold Crest Hotel jijini humo. 


NIC Bank imekuja na program mpya ya T24, mfumo mpya wa kisasa wa kikopyuta unaorahisisha uendeshaji wa shughuli za kibenki ambao unawasaidia wateja wao kuwahudumia kwa haraka na kwa muda muafaka.  


Meneja wa Tawi la Mwanza Richard Donatus akiitambulisha safu ya wafanyakazi wa NIC Bank tawi la Mwanza na vitengo vyao husika.


Kwa mpango huu NIC Bank ndani ya soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki inatoa tafsiri ya kujizatiti na kujiimarisha kiutendaji kwa kutoa huduma kwa eneo lote bila usumbufu hivyo kuwa tegemeo linapokuja suala la huduma za kibenki. 


Wateja wa benki ya NIC wakiwa ndani ya ukumbi wa Nyerere Gold Crest Hotel kwaajili ya kupata chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo.


Wateja ambao ni wafanyabiashara wa jijini Mwanza wakijadiliana ndani ya Hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NIC.


Wadau wa biashara wamekutana kwenye Hafla hii kwa mazungumzo mafupi na kubadilishana uzoefu.


Wadau wa NIC Benk. 


Moja kati ya faida ya huduma mpya ya T24 ni kuwa, kupitia mtandao (On line banking) mteja anaweza kukaa nyumbani au kuwa mahali popote pale akapata huduma za kibenki kupitia SMS banking. 


Ushauri wa sisi kwa sisi wateja wa NIC.


Ni moja kati ya meza waliyokaa wafanyabiashara maarufu jijini Mwanza.


"Temenos T24 is comprehesive business functionality with an advanced, secure, scalable technology and market challenges of today and tomorrow" Said 'Mc Stopper' 


Wadau wakijipatia chakula kizuri kilichoandaliwa na NIC Bank kwenye hafla na wateja wake jijini Mwanza.


Samaki au kuku?


Chakula time.


Starter ...


Futher to embracing technology advancement, within the last 12 months the bank has opened two additional branches. Its 5th branc in Kahama town Shinyanga Region and a 6th branch in Kariakoo along Sikukuu Street in Dar es salaam.

Tuesday, May 21, 2013

LEO NI MIAKA 17 TANGU AJALI YA MV BUKOBA NI TAREHE SAWA NA SIKU ALIYOZALIWA KALA JEREMIAH

Siku hii yenye historia ya majonzi yaani Tarehe 12 mwezi May vilevile ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa msanii anayewania tuzo za Kili 2013, Kala Jeremia (Pichani), yeye katika siku hii huwa aisherehekei bali  hutenge muda kwa sala na maombi

Tarehe 21/may/2013 Tanzania imeadhimisha miaka 17 tangu meli ya MV BUKOBA kuzama ndani ya ziwa Victoria na kusababisha taifa kupoteza raslimali watu ambapo zaidi ni ya watu ELFUMOJA wanatajwa kufa maji kwenye ajali hiyo iliyoiletea simanzi kubwa taifa la Tanzania.
Hivi karibuni wasanii wazawa wa jiji la Mwanza walio nyumbani na wale walio mikoa ya mbali walirejea nyumbani na kujumuika na wenzao kufanya usafi kwenye makaburi ya watu waliofariki dunia kwenye ajali ya Mv. Bukoba kama sehemu ya shughuli za jamii. Pichani ni H.Baba na Mwanachemba Squard Dark Master.

Wananchi wa kanda ya ziwa leo wanajumuika pamoja na marafiki waliopoteza ndugu na jamaa zao katika makaburi hayo maalum ya marehemu hao yaliyoko eneo la Igoma jijini Mwanza kwa ajili ya Ibada ya kumbukumbu. 

Mwenyezi mungu ndiye mpangaji wa yote, jina lake lihimidiwe.

Monday, May 20, 2013

VIONGOZI WA MANCHESTER UNITED KUTETA NA AIRTEL JUMATANO HII JUU YA MRADI WA AIRTEL RISING STARS


Viongozi wa Man U kuteta na Airtel Jumatano juu ya mradi wa Airtel Rising Stars  nchini

Viongozi wawili kutoka Manchester United -- Anthony Benerjee, Mkurugenzi wa Uhusiano na Michael Higham, Meneja Uhusiano -- wanatua jijini Dar es Salaam Jumatano hii kufanya manzungumzo na viongozi wa Airtel Tanzania namna bora ya kuendesha michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando amesema mkutano huo utakao jumuisha wadau mbalimbali utafanyika makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam na kutathimini ARS ya miaka miwili iliyopita ili kuona namna nzuri ya kuendesha michuano siku za usoni kuanzia mwaka huu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni moja ya wadau wataoshiriki mkutano huo ili kutoa mchango wao hasa katika masuala ya kifundi kama vile upangaji wa ratiba ya mashindano. Ratiba ya kuanza kwa ARS 2013 inatarajiwa kutangazwa mwezi huu.

Michuano ya soka Airtel Rising Stars ilizinduliwa hapa nchini Tanzania na sehemu nyingine barani Afrika mwaka 2011 ikiwa na lengo mahsusi la kusaidia kuvumbua vipaji vya wanasoka chipukizi na kuwafanya waonekane kwa makocha na mawakala wa kusaka vipaji vya wachezaji nyota.

Mashaindano haya huanzia ngazi ya chini ambapo timu za sekondari ngazi ya mkoa huchuana ili kupata wachezaji nyota wa kuunda kombaini inayowakilisha mkoa husika kwenye mashindano ya Taifa ambayo hufanyika jijini Dar es Salaam. Jumla ya timu 48 zimepata fursa ya kushirikia ARS katika miaka miwili iliyopita.

Katika mwaka wa uzinduzi  2011 mashindano ya ARS ngazi ya Taifa yalifuatiwa na kliniki ya kimataifa chini ya usimamizi wa makocha kutoka Manchester United iliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushirikisha wavulana na wasichana kutoka nchi za
Kenya, Malawi, Sierra Leone na mwenyeji Tanzania..

Mwaka jana fainali za taifa za ARS zilifuatiwa na michuano ya kimataifa ya ARS zilizofanyika jijini Nairobi zikishirikisha nch  ambazo kampuni ya Airtel hufanya biashara. Vile vile kliniki ya mwaka jana ilifanyika Nairobi chini ya usimamizi ya makocha wazoefu kutoka shule za mafunzo ya soka ya vijana za Manchester United ambapo vijana walipata fursa ya kujifunza mbinu mbalimbali za soka.