Pichani ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika maandamano ya amani (Picha na Maktaba).
---
Watu
wengi kwa sasa wameibuka na kutokea kuipenda fani ya uandishi wa habari
bila kujua misingi na miiko ya uandishi wa habari. Tatizo moja ambalo
limeonekana ni kubwa sana ni utandawazi ambao umekuwepo na kutokea ibuko
la kila kijana kufungua gazeti tando (blog).
Hatukatai kuja kwa
magazeti tando ila naomba tujiulize, yanatumika ipasavyo ama ndiyo
limekuwa ni wimbi vamizi lenye kutoa ama kusambaza habari hata zile
zisizokuwa na vyanzo kamili na visivyojitosheleza.Kwa sasa imezuka tabia
ya wanaojiita wamiliki wa magazeti tando,wengi wao kukopi na kupaste
vitu wanavyoviokota katika mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter, facebook
na mingine mingi.
Sina nia ya kumsema
mtu bali napenda tuelimishane kama vijana wenzangu,ambao wametokea
kuipenda fani ya uandishi wa habari, wakumbuke kuwa fani ya uandishi wa
habari ina miiko na maadili yake, mfano. Katika kuandika habari za
mazingira, siasa, elimu, uchumi, michezo, burudani ukiangalia habari
hizi zote zina misingi na miiko yake. Leo hauwezi kumchukua mwandishi wa
habari za michezo ukamwambia aandike habari za uchumi kwa vile hatakuwa
na takwimu za uchumi na hata akiandika hiyo habari na kuisoma utakuwa
unajiuliza maswali mengi bila kupata majibu.
Vile vile ni vizuri
vijana wenzangu kutambua kuwa kila kazi ina mipaka na misingi yake,
juzi juzi nilisoma habari katika gazeti tando moja wapo ikisema,
'ALIYEONGOZA MAANDAMANO YA IRINGA MHESHIMIWA MCHUNGAJI MSIGWA ASWEKWA
NDANI' nilijiuliza maswali mengi ambayo kiukweli nilikosa majibu yake,
kuona huyu aliyeandika hiki kichwa cha habari kweli amepitia fani ya
uandishi wa habari ama ndio ule upepo vamizi?
Maana unapoandika
habari za mahakamani, polisi kuna misemo yake, hauwezi kumuhukumu mtu
moja kwa moja kwa kusema fulani ni mwizi, hata hao polisi ambao huwa
wanakwenda kukamata watu eneo la tukio hawawezi kusema fulani ni mwizi
mpaka apelekwe mahakamani ndipo sheria ichukue mkondo wake na kumbaini
huyo aliyekamatwa ni mwizi.
Naomba tufike
mahali tuheshimu utu wa watu na kuepuka udhalilishaji wa bila kujua
naamini baadhi ya vijana wengi walioamua kufungua magazeti hayo tando
ambayo yanatoa habari, hawana taaluma ya uandishi wa habari.
Napenda kuwapongeza
wale walioamua kufungua magazeti tando katika milengo yao tofauti
ikiwemo kutoa habari kwa njia ya 'kufundisha masuala ya urembo, mapishi,
kuwasaidia kuwatangaza vijana katika muziki na hata wale walioamua
kuandika habari zao binafsi.
Nayasema yote hayo
kwa vile kumezuka wimbi la vijana wanaotaka kuichafua fani ya uandishi
wa habari na ionekane si fani ya watu walioenda shule bali ni ya wahuni
tu wasiojua mambo, naomba vijana tuelimike na tujifunze kwa watu
wanayoyajua mambo ili tuweze kufika mbele zaidi.
Namalizia kwa kusema tusipoziba ufa tutajenga ukuta.
Asanteni sana kwa kusoma.
Imeandikwa na Cathbert A. Kajuna
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.