ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 10, 2019

MWANZA YAZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI BURE VYANDARUA MASHULENI.


Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua rasmi zoezi la ugawaji bure vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu kwa wanafunzi wa Shule za Msingi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji afua mbalimbali za kupambana na Malaria.


Uzinduzi huo umefanyika Oktoba 10, 2019 katika Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza ambapo jumla ya Shule za Msingi 976 mkoani Mwanza zitafikiwa na zoezi hilo litakalodumu kwa muda wa wiki mbili kuanzia tarehe 09-23 Oktoba, 2019.


Muelimishaji akifundisha kwa vitendo namna ya kutundika na kuchomeka chandarua.
Vyandarua vilianza kutumika lini?
Vyandarua vilianza kutumika kuanzia katikati ya karne ya kumi na nane (mid-18th century), inasadikiwa kuwa hata yule malkia maarufu wa Misri Cleopatra alitumia chandarua. Vilevile vyandarua vilitumika wakati wa ujenzi wa mfereji wa suez baada ya malaria kutishia umaliziaji wa ujenzi wa mfereji huo.
Chandarua hutengenezwa kwa kutumia: pamba, polyester, polyethylene au nylon
Vyandarua vyenye dawa
Vyandarua vyenye dawa vilianza kutumika miaka ya 1980 kwa ajili ya kuzuia malaria. Na hadi sasa vyandarua hivi vinaanza kutumiwa kama mmbadala wa vyandarua vya zamani katika nchi nyingi, Tanzania ikiwa ni mojawapo ya nchi hizo.
Inaaminika kuwa vyandarua vyenye dawa vinafanyakazi maradufu ya vyandarua visivyo na dawa. Chandarua hutoa kinga ya asilimia 70 dhidhi ya malaria kulinganisha na kulala bila chandarua.
Katika tafiti iliyofanywa na Deswal na wenzake iliyochapishwa September 2004, katika kambi za jeshi katika mji wa Allahad, nchini India waligundua kuwa maambukizi ya malaria yalipungua kwa kiasi kikubwa baada ya kutumia vyandarua vyenye dawa, na mbu aina ya Anophiline walipungua kwa asilimia 67.8 wakati culex walipungua kwa asilimia 49. Na watumiaji hawakupata madhara yoyote. Na hivyo walithibitisha kuwa matumizi ya vyandarua vyenye dawa husaidia kupunguza malaria kwa kiasi kikubwa.
Kwa sasa vyandarua vingi huwekewa dawa aina zifuatazo: Deltamethrin na Permethrin. Kwa ufanisi mzuri wa chandarua chenye dawa, ni vyema kila baada ya miezi sita kukiwekea tena dawa,ili kiweze kufanya kazi vizuri.
Kwanini watu wengi hawatumii vyandarua vyenye dawa?
Tafiti mbalimbali zimeshafanyika kuhusiana na kwanini watu wengi hawatumii vyandarua vyenye dawa hata kama watapewa bure na serikali. Katika utafiti uliofanyika pembezoni mwa mto Imo, Nigeria iliyochapishwa machi 2010 “kuhusiana na mtazamo wa matumizi ya vyandarua vyenye dawa na athari yake katika kuzuia malaria kwa wakina mama wajawazito” uliofanywa na chukwuocha UM na wenzake waligundua kuwa mtazamo wa wananchi kuhusu malaria kuwa wanawake wajawazito na watoto wapo kwenye hatari zaidi ya kupata malaria kuliko wanaume na wanawake ambao hawana watoto kabisa kwa sababu miili yao ni dhaifu. Vilevile walipata sababu za kutotumia vyandarua vyenye dawa kuwa ni:
  • Gharama na upatikanaji wake
  • Vilevile wanaamini kemikali za dawa zinazowekwa zinamadhara kwa watu wazima,watoto na wanawake wajawawazito
  • Wengi walipata matangazo kuhusu umuhimu wa vyandarua vyenye dawa
  • Wengi waliamini dawa hizo zitumikazo kwenye vyadarua huleta madhara yafuatayo:
    • huathiri upumuaji hasa kwa wakina mama wajawazito na kama zinaua mbu basi zinaweza kuua hata binadamu.
    • Wapo pia watumiaji wengi walioripoti kuhisi joto kali na kukosa hewa ya kutosha wakiwa wamelala usiku.
Nini mtazamo wa matumizi ya vyandarua vyenye dawa katika nchi nyingi za afrika?
Kwa ujumla kuna imani na mitazamo mbalimbali kuhusiana na matumizi ya vyandarua vyenye dawa kikubwa kikiwa kuhusishwa na kupunguza nguvu za kiume na kuaminini kuwa zinaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu.
Hitimisho
Kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa zinathibitisha kuwa Hamna madhara kwa binadamu na matumizi mazuri ya vyandarua vyenye dawa hupunguza maambukizi ya malaria kwa kiasi kikubwa.
Nikisema matumizi mazuri namaanisha kuwa uhakikishe umelala katikati hamna ngozi inayogusa chandarua hasa kwa vile ambavyo havina dawa maana mbu huweza kukuuma, na kuhakikisha hakija chanika na kimechomekwa vizuri. Na kutosahau kukiwekea dawa tena baada ya miezi sita.

HISTORIA YA MAISHA YA HAWA NTAREJEA


Maisha ni mzunguko, Changamoto ni daraja la mafanikio, Mipango sio matumizi, Mvumilivu hula mbivu na Penya nia pana njia.  usilo lijua ni kama usiku wagiza!.  Karibu kwenye Historia ya 'Hawa Ntarejea'.

Majina yake kamili anaitwa Hawa Said lakini jina la usanii anaitambulika kama 'Hawa Ntarejea' Mnamo mwaka 1990 ilipofika tarehe 5/2 ndipo Hawa alipo zaliwa na kuanza kuishi maisha ya hapa Duniani. Kipindi hicho hakuweza kutambua kama Dunia inaweza kugeuka na kuwa chungu, kutokana na umri wake ulikuwa bado.  Kadri siku zilivyo zidi kwenda Hawa alizidi kukua na kuanza kujitambua. 

Bahati nzuri Mungu alimjaalia Hawa kipawa cha Sauti nzuri na uwezo wa kuitumia, hivyo ulipofika wakati Hawa akajitambua vizuri ndipo alipoanza kuusogelea Muziki.  Jamii ilimpokea kwa kishondo mara baada ya kushirikishwa kwenye wimbo wa Ntarejea na Diamond Platnumz, ambapo kila mmoja  alitambua Hawa ninani!  Kwenye wimbo alitoa sauti nyororo iliyo jaa simanzi kutokana na Ujumbe wa Wimbo huo.

Hivyo basi umaarufu wa wimbo huo ndio uliyo pelekea mpaka leo anaitwa Hawa Ntarejea.  Mbali na mahusiano ya kimuziki baina ya Hawa na Diamond Platnuz wawili hao walikuwa katiaka Mahusiano ya Kimapenzi. Na hata kabla ya kuimba pamoja walikuwa tayari ni marafiki.

Baada ya maisha ya muziki wa Ntarejea Hawa na Diamond Platnumz waliendelea kuishi kama mtu na Mpenzi wake, lakini tunakumbushwa tu kuwa hakuna marefu yasio na ncha,  Hivyo Penzi la Hawa na Diamond halikuweza kudumu.  Amini nakwambia upendo ukizidi kiasi huleta madhara, Hawa alikuwa na upendo uliyo pitiliza kwa Diamond Platnumz hali hiyo ilipelekea akawa na wivu uliopita kiasi mwisho Penzi likaangamia.

Pamoja na hayo yote msimamo wa Hawa katika ndoto zake ili kuwa ni kuja kuwa msanii mkubwa Duniani kote! Tukirejea kwenye utangulizi wangu hapo awali kuna msemo nimesema “Mipango sio matumizi” kumbe basi kuna vitu ambavyo vilibadilisha na kuharibu mtazamo wa ndoto za Hawa. Baada muda kidogo miaka ya 2015 -2016  Hawa alipata mwanaume wa kumuoa na ndoa ikafungwa  kutokana na tofauti zao za kidini Hawa alilazimika kubadili jina akaitwa 'Angel' Ndoa ilifanikiwa vizuri tena ni ile ya kupendana kwenye shida na raha.

Kuna wengine wanaweza wakasema ni mikosi lakini pengine si kweli bali ni mipango tu ya Mungu,  Ndoa ya Hawa ambaye kipindi hicho alikuwa ni Angel na Mumewe haikuweza kudumu pia!. Ilikuwaje ilikuwa hivi, Maisha ya ndoa ya Hawa hayakuchukua muda mrefu,  lakini ndani ya muda huo mchache kulikuwa na mikwaruzano ya hapa na pale baina ya ndugu wa Mume kwa Hawa yalizidi kuwekwa sawa na maisha mengine yakawa yanaendelea kama kawaida.

Sikumoja Mume akamwambia Hawa kuwa anataka kusafiri kwenda kutafuta maisha, lakini Hawa hakuvutiwa saana na safari hiyo maana hakukukubaliana naye yaani alikataa, kwa kumwambia kuwa “ Mbona mimi nalizika na tunacho kipata kwani nimesema siwezi kula ugali na mlenda au matembele? Kwani huko kuna kitugani cha ziada? Maswali haya ya Hawa hayakuweza kusaidia chochote kwasababu Mume alikuwa tayari kapanga plan zake! Hivyo aliaga kuwa anaenda Botswana Baada ya safari hiyo, Mume alikata mawasiliano kabisa kwa Hawa pia ndungu wa Mume hivyo hivyo, Hawa akabaki kwenye mataa mpaka hii leo 2019 toka 2015 – 2016 hana mawasiliano yeyote na Mumewe.

Kutokana na mgongano wa matukio yote hayo katika maisha ya Hawa yalipelekea akajikuta akiishi katika ndimbwi kubwa la mawazo. Hali hiyo ikasababisha ajikite zaidi kweye vilevi hasa pombe aina ya Gongo kwa kudhani kuwa itamsaidia kuondoa mawazo kumbe ndio alizidi kujiangamiza kiafya.  Lakini pia alikondeana sana kiasi cha kupoteza mvuto kwenye macho ya watu.

2018 ulikuwa ni mwaka wa Hawa kuteseka kiafya maana alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo,  madhara ambayo yalisababishwa na  Mawazo pamoja na Vilevi ambavyo alikuwa akitumia kwa kusudio la kupunguza mawazo. Amini na kwambia Ukitenda wema utatendewa wema, pamoja na kwamba Hawa alikuwa kwenye hali mbaya lakini Diamond Platnumz alitambua thamani ya Hawa kwa roho ya  huruma  alishirikiana na team yake ya WCB   kumpeleka India kwa ajili ya Matibabu ya Moyo, Baada ya matibabu Afya ya Hawa ilirejea vyema,  Mapaka sasa   Hawa anaendelea na Muziki na mashabiki wake bado wana upendo wa dhati kwa kile anacho kifanya.

Ukirejea tena kwenye uangulizi wangu nimesema “Changamoto ni daraja la mafanikio” hivyo basi kumbe huwezi kufanikiwa pasipo kupitia changamoto mbalimbali.  Kwa mambo ambayo ameyapitia msanii Hawa yanatosha kuukaribisha ulimwengu wa Mafanikio, lakini kupitia maisha yake naamni kuna mengi utakuwa umejifunza.

Note: Hawa ni msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye alifamika kwa wimbo wa 'Ntarejea' aliyo shirikishwa na Diamond Platnumz,  lakini ananyimbo zake zingine kama Kucheka na Shagala bagala kwa yote aliyo pitia ikumbukwe tu kuwa Hawa Ntarejea anyota ya Upendo pia anakipaji kikubwa anahitaji suport ya kila mmoja ili kutimiza ndoto zake alizo ahidi tangu alivyo kuwa mdogo!.

Wednesday, October 9, 2019

RATIBA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2019

                                                   

MTATURU AONYA MADIWANI NA VIONGOZI WA CHADEMA WANAOCHOCHEA WANANCHI KUTOCHANGIA MAENDELEO


NA MWANDISHI WETU, IKUNGI

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) amewaonya Viongozi na Madiwani wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Katika Kata zote za Jimbo hilo kuacha tabia ya kupita katika vijiji na Kata zao kuwahamasisha wananchi na viongozi kutomuunga mkono Mbunge huyo, kutoshiri na kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo atawaumbua kwa wananchi na kuwaomba wasiwasikilize hali washirikiane naye katika maendeleo.

Mtaturu alitoa onyo hilo jana alipokuwa akihutubia mamiaa ya wananchi waliofulika kwenye mkutano wake wa hadhala uliofaanyika senta ya Kata ya Makiungu, ambapo aliwataka wananchi kuwapuuza kwa kile wanachowahamasisha kwa kuwa yeye ndo Mbunge halali wa Jimbo hilo aliyekwisha apishwa.

"Msiwasikilize na muwakatae kwa kusambaza uongo na hawawatakii mema kwani wao mliwachagua washirikiane na wananchi kuhakikisha kero za majisafi, afya, elimu, umeme na miundombinu ya barabara ikiwemo na mawasiliano ya mitandao ya simu za mkononi zilizopo katika vitongoji, vijiji na Kata zinapatiwa ufumbuzi wa haraka lakini kwa wanavyofanya ni kuwachelewesha na kusababisha miradi ya maendeleo kukwama kutekelezeka kwa kukosa Madiwani wa kuisemea Halmashauri na hata Bungeni," alisema.

Mbunge Mtaturu alisema wananchi waache ushabiki wa vyama vya siasa kwa kufananisha na ushabiki wa timu za mpira wa miguu kwa kuwa siasa ni maisha hivyo lazima wawe makini kuchagua viongozi wa watakaokuwa wawakilisha wa wananchi watakaowaunganisha katika maendeleo bila kuwabagua katika itikadi za vyama vya siasa, rangi, dini na makabila yao bali wawaunganishe kushirikiana pamoja kujiletea maendeleo.

"Mimi ndo Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa mujibu wa Katiba, Sheria na taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano hivyo hivyo wanaota ndoto kudhani kuwa tunacheza na kuigiza watambue kuwa kazi iliyopo ni kuhakikisha kero zote zinafikishwa serikalini na kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kama mnavyojua tayari Rais aliagiza na Wizara ya Maji wametupatia Sh bilioni 2 za kutekeleza mradi wa majisafi Wilaya ya Ikungi yenye majimbo mawili baada ya Mimi kutaka kuomba Bungeni baada ya kuapishwa na Spika Job Ndugai kunipa nafasi ya kuuliza swali ninyi ni mashahidi mliona," alisema.

Mbunge Mtaturu aliwaeleza wananchi hao kwamba miradi ambayo serikali haikuitekeleza kwa miaka tisa kwa kukosa mtu wa kuisemea Mbungeni sasa atahakikisha inatekelezwa ili wananchi wapate huduma bora katika sekta za Afya, Elimu, Majisafi, Umeme, Miundombinu ya barabara na mawasiliano ya mitandao ya simu sanjali na kuwa na uhakika wa pembejeo za kilimo na mifugo ili wananchi waweze kuongeza kipato cha familia na maendeleo kwa ujumla.

Mkutano huo wa Mbunge uliohudhuliwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo ambayo alionya viongozi wa vyama vya siasa wanaopita kupanga njama za kuwahamasisha wananchi kuvuruga uchaguzi wa serikali za Mitaa watakumbana na mkono wa serikali ambapo watakamatwa na kuchukuliwa hata za kisheria hivyo aliwataka wananchi kuwa watulivu nawajipange kuchagua viongozi watakaowaunganisha, kuwaongoza na kushirikiana nao katika maendeleo kwenye maeneo yao ya vitongoji na vijiji pasipo kuwabagua.

Katika Mkutano huo viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji wakiwemo wanachama wa vyama vya upinzani 40 kutoka Chadema walibwaga manyanga na kujivua uanachama na kurejesha Kadi zao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakiongozwa na Ayubu Mohamed Mwenyekiti wa Kata hiyo, baadhi ya waliokuwa makada kindakindaki wa Chadema ni Maiko Mahiki, Maiko Mathias, James Emmanuel, Gaspary Majoa, Miraji Seleman, Eliabu Aloyce, Abudallah Lessolesso, Hamisi Kinyori, Shaban Selema, Laurence Fransis, Gaza Boy, George Yunde na Maiko Ghamaa ambapo walisema wanamuunga mkono Mbunge Mtaturu kwa kupambania maendeleo ya Jimbo hilo ambapo waliomtangulia waliendekeza kuwagawa kwa itikadi za kisiasa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Makiungu ulipofanyikia mukitano huo, Hamis Haji alisema wananchi wa Kata hiyo wameteseka kwa miaka tisa bila kutekelezewa miradi ya maendeleo na mara nyingine ukosekanaji wa huduma ya majisafi ilisababisha ndoa nyingi kuvunjika huku wawakilishi wao ambao ni aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Tundu Lissu kabla ya kutenguliwa na Spika na Madiwani waliendekeza na kuwachochea kubaguana na kuwazuia wananchi kuchangia miradi ya maendeleo hali iliyopelekea Jimbo hilo kudumaa kimaendeleo hivyo kumpata Mtaturu wameona ni Jembe jipya linalowapa matumaini mapya ya maendeleo na kutekelezeka kwa miradi.

CHINA YAKOSOA HATUA YA MAREKANI VIKWAZO DHIDI YA MAKAMPUNI YAKE.

China imeitaka Washington kuondoa vikwazo vyake vipya dhidi ya kampuni za tekenolojia za China.

 Wizara ya mambo ya kigeni ya China kupitia msemaji wake Geng Shuang imekosoa vikali hatua ya karibuni ya Marekani ya kuyaingiza kwenye orodha mbaya makampuni makubwa ya kijasusi ya taifa hilo kwa kusema ni uingiliaji kwenye masuala ya ndani ya China.

Hata hivyo China haikusema iwapo itajibu hatua hizo. Kwa upande mwingine wizara ya biashara ya China imesema ujumbe wa mazungumzo ya kumaliza vita vya kibiashara na Marekani unaoongozwa na makamu waziri mkuu Liu He utaenda Washington tayari kwa majadiliano siku ya Alhamisi licha ya mzozo huu unaoibua wasiwasi.

Monday, October 7, 2019

PICHA :- RAIS MAGUFULI ALIVYOWASILI UWANJA WA NELSON MANDELA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Sumbawanga mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa mpira wa Nelson Mandela kwa ajili ya kuwahutubia

ZAIDI YA WAKAZI MILIONI 1 6 KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA MKOA WA MWANZA


KAMATI ya ulinzi na usalama za wilaya mkoa wa Mwanza zimetakiwa kuhakikisha zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa linafanyika kwa ufanisi ili kutimiza azma ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanaojitokeza kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura linafanyika kwa amani na utuli bila bugdha yoyote huku akionya kwa yeyote atakaye kwamisha zoezi hilo kuchukuliwa hatua za kisheria kwa muujibu wa katiba ya nchi. 
Rai hiyo imetolewa mapema hii leo na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza John Mongella,  wakati akifungua kikao cha wasimamizi kamati mbalimbali za ulinzi na usalama kwa wilaya zote 7 na halmashauri zake 8.

Jeh mkoa wa Mwanza umejipanga vipi katika zoezi hilo la uandikishaji linaloanza rasmi kesho (8 -October- 2019) kwenye kata mbalimbali? 


Jeh mkoa wa Mwanza unamalengo ya kuandikisha wananchi wangapi? 


Kanuni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa ngazi ya vijiji, vitongoji na mtaa za mwaka 2019 nchini Tanzania zimeainisha aina nane za vitambulisho ambavyo msimamizi wa kituo cha uchaguzi anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe ili kujiridhisha na jina kama ndilo liko katika orodha ya mpiga kura.
Kanuni hizo zimetolewa tangu Agosti 23 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Seleman Jafo jijini Dodoma mbele ya viongozi mbalimbali wa mikoa na wadau wa siasa.
Kanuni hizo zimetaja vitambulisho hivyo ni kitambulisho cha mpiga kura, cha kazi, hati ya kusafiria, kadi ya bima ya afya, cha shule au chuo, cha mfuko wa hifadhi ya jamii, leseni ya udereva na kitambulisho cha Taifa.
Kanuni hiyo ya 33 kifungu cha pili kinasema, "Msimamizi wa kituo anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe kitambulisho kitakachoonesha kuwa jina la mpiga kura huyo ndio lililomo kwenye orodha ya wapiga kura."

Sehemu ya wajumbe wa mkutano wa kamati ndogo na kubwa za ulinzi na Usalama toka halmashauri mbalimbali za wilaya mkoa wa Mwanza. 
Sehemu ya wajumbe.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro (kushoto) ni sehemu ya wajumbe wa mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Mwanza, Emmanuel Stenga, (kushoto) yu sehemu ya wajumbe wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa kusanyiko hilo.

MAKAMISHNA WA NNE TOKA JESHI LA POLISI WAKIONGONZWA NA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI) ROBERT BOAZ WAMETEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME KATIKA MTO RUFIJI.


 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, akiongoza kikao cha Maafisa na Wahandisi wa Ujenzi wa Mradi Mkubwa wa kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo. (PICHA NA JESHI LA POLISI)
 Makamishna wa Polisi wakiongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz, katikati na kulia kwake ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Maabara na Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban hiki na kushoto kwa CP Boaz ni Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo wakiwa katika picha ya pamoja na Wahandisi wa Ujenzi wa mradi wa Umeme Rufiji baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.(PICHA NA JESHI LA POLISI)



Mhandisi Manda akitoa maelekezo juu ya Ujenzi mradi wa uzalishaji Umeme katika Mto Rufiji kulia kwake ni Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai CP Charles Mkumbo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz wa kwanza kutoka kulia ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas (PICHA NA JESHI LA POLISI)

BAKWATA YARIDHISHWA MAANDALI YA MAULIDI IKIWATAKA WAISLAMU KUSHIRIKIANA NA WAUMINI WA DINI ZINGINE

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke, jana akiwaonyesha Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Sheikhe Hamis Mattaka (mwenye koti) na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma (wa tatu kutoka kulia) eneo la viwanja vya Furahisha Ilemela litakalotumika kwa ajili ya Maulidi ya kitaifa mapema mwaka huu.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Sheikhe Hamis Mattaka (wa tatu kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma ( wa tatu kutoka kulia) jana, wakiongozwa na Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasani Kabeke (wa pili kulia) kukagua eneo la viwanja vya Furahisha litakalotumika kwa maadhimisho ya Sherehe za Maulidi mwaka huu.
4.Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke ( wa pili kulia) akifafanua jambo jana kwa viongozi wa BAKWATA wakati wakikagua eneo la viwanja vya Furahisha Manispaa ya Ilemela litakolotumika kwa sherehe za Maulidi Novemba mwaka huu.
Baadhi ya wajumbe jana wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikhe Hamis Mattaka (aliyevaa koti) wakati wa ukaguzi wa eneo zitakakofanyika sherehe za Maulidi mwaka huu jijini Mwanza
kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke akisistiza jambo kwa wajumbe na viongozi wa BAKWATA Taifa , Sheikhe Hamis Mattaka (mwenye koti) na Sheikhe Nuhu Jabir Mruma, aliyevaa suti wa pili kutoka kulia) wakati wa ukaguzi wa viwanja vya Furahisha Mwanza , jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Sheikhe Hamis Mattaka,jana  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo la viwanja vya Furahisha jijini Mwanza zitakakofanyika sherehe za Maulidi mwaka huu, kushoto kwake ni katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma na kushoto wa kwanza ni Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke.

Picha na Baltazar Mashaka

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
HALMASHAURI Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka waumini wa dini hiyo kuhakikisha wanashirikiana na dini zingine kufanikisha Maulidi ya kihistoria Mtume Muhhamad S.A.W.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa BAKWATA, Sheikhe Hamis Mattaka alisema jana wakati wa kukagua maendeleo ya maandalizi ya sherehe hizo za maulidi zitakazofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Alisema Waislamu kwa umoja,ushirikiano na uhusiano uliopo na waumini wa dini zingine wahakikishe wanafanikisha kufanyika kwa maulidi ya kihistoria ya nusu karne baada ya BAKWATA kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1968.

Sheikhe Mattaka alisema BAKWATA kwa wiki nzima kwenye maualidi hayo, itaonyesha na kuelezea shughuli na miradi mbalimbali ya huduma za kijamii zinazofanywa na baraza hilo ikiwemo miradi inayohusu UKIMWI,Kumlinda Mtoto wa Kike,Kuendesha na Kusaidia Familia masikini (duni kwa kipato). 

Alisema uongozi wa BAKWA Mkoa wa Mwanza chini ya Sheikhe Kabeke (Hasani) unastahili pongezi kwa ubunifu ambao haujawahi kufanyika wa kuwakusanya na  kushirikisha waislamu wa Kanda ya Ziwa kuona hilo ni jambo lao na kwa hali na mfumo huo Waislamu wanaweza kufanya makubwa kwa kushirikishana.

“Niupongeze uongozi wa Sheikhe Hasani Kabeke kwa ubunifu walioufanya wa kuandaa Maulidi hii kubwa ya kihistoria ya nusu karne ya pili ya uhai wa Baraza Kuu la Waislamu ambalo mwaka jana limetimiza miaka 50.Mwanza imepata fursa ya kuanza safari hiyo chini ya falsafa ya Jitambue,Badilika, Acha Mazoea.Itakuwa Maulidi yakukusanya na kufanya shughuli za kijamii,”alisema.

Sheikhe Mattaka alisema Maulidi ya mwaka huu anaamini itahudhuriwa na wageni wengi kutoka nchi nyingi za Afrika Mashariki kutokana na unyeti wake na kutoa wito kuwa wanadamu wanao udugu, wa kwanza ni ubindaamu wao na ndio maana BAKWATA inaishi kwa amani na watu wa dini zote na kuleta utengamano wakiwa wamoja.

“Wasio na dini na wenye dini tunakaa pamoja, tunaishi pamoja katika ubinadaamu wetu.Kwa pamoja tukidhamiria tunaweza kufikia maendeleo chanya kwa jamii ya Watanzania wasio waislamu kwa sababu ya  udugu wa ubinadaamu wetu,”alisema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa BAKWATA Sheikhe Nuhu Jabir Mruma alisema kuwa, eneo Maulidi hiyo itakakofanyikia Jiografia yake inaridhisha, linafikika kwa urahisi,lina usalama na lina faa kwa sababu huduma mbalimbali za kijamii zinapatikana na lina uwezo wa kumudu watu watakaohudhuria hapo.

“Hamasa yenyewe kwa kuwa kutakuwa na watu wengi tulikuja kujiridhisha kuona maandalizi haya ya Maulidi ambayo ni mwanzo wa kuwapeleka Waislamu kwenye maendeleo.Ni eneo sahihi la kueleza mipango waliyo nayo Waislamu, changamoto na mafanikio.Tofauti ni kuwa gharama zake hazitalingana na yale yatakayofanyika kwa miaka mingi,”alisema.

Katibu Mkuu huyo wa BAKWATA alieleza kuwa ili kujenga maendeleo ya Waislamu aliwataka waislamu wote kuungana na waandaaji wa Maulidi hiyo kwa kutoa michango yao ya hali na mali pamoja na mawazo ili kufanikisha kumshangilia Mtume Muhhamad S.A.W.
Kwa mujibu wa Sheikhe Kabeke Maulidi hiyo ya kihistoria inafanyika Mwanza kitaifa ikiwa ni baada ya miaka 20 tangu yalipofanyika mara ya mwisho mkoani humu mwaka 1990.ssss

Sunday, October 6, 2019

WAJERUMANI WAVUTIWA NA MATUMIZI SAHIHI FEDHA ZA MIRADI YA SERIKALI YA JPM KUENDELEA KUWEKEZA MWANZA



Naibu Waziri Mhe.Jumaa Aweso mwishoni mwa wiki amendelea kuongoza ziara ya Ujumbe wa kamati ya Mazingira na maji ya Bunge la Ujerumani, ambao pia umekagua mradi wa majisafi na majitaka sehemu za milimani jijini Mwanza.

Aidha miongoni mwa wajumbe hao alikuwepo mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na maji Mhe. Mgimwa.




PICHA: WACHEZAJI WA NGORONGORO HEROES WAWASILI SALAMA NCHINIBAADA YA KUNYAKUA UBINGWA.







TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' leo imerejea ikiwa na ubingwa na kupokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe.

Ngorongoro imetwaa ubingwa huo jana kwenye michuano hiyo iliyofanyika nchini Uganda kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya.

Tanzania haikupoteza mchezo hata mmoja kwenye michuano hiyo ililazimisha sare ilipocheza na Kenya kwenye hatua ya makundi.

Ilikuwa kundi B lenye timu nyingine za Zanzibar, Ethiopia, Kenya.


Mabingwa wa CECAFA U20 Timu ya Vijana U20 Tanzania Bara wamewasili salama na kupokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.