ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 7, 2019

BAKWATA YARIDHISHWA MAANDALI YA MAULIDI IKIWATAKA WAISLAMU KUSHIRIKIANA NA WAUMINI WA DINI ZINGINE

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke, jana akiwaonyesha Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Sheikhe Hamis Mattaka (mwenye koti) na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma (wa tatu kutoka kulia) eneo la viwanja vya Furahisha Ilemela litakalotumika kwa ajili ya Maulidi ya kitaifa mapema mwaka huu.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Sheikhe Hamis Mattaka (wa tatu kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma ( wa tatu kutoka kulia) jana, wakiongozwa na Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Hasani Kabeke (wa pili kulia) kukagua eneo la viwanja vya Furahisha litakalotumika kwa maadhimisho ya Sherehe za Maulidi mwaka huu.
4.Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke ( wa pili kulia) akifafanua jambo jana kwa viongozi wa BAKWATA wakati wakikagua eneo la viwanja vya Furahisha Manispaa ya Ilemela litakolotumika kwa sherehe za Maulidi Novemba mwaka huu.
Baadhi ya wajumbe jana wakimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA taifa Sheikhe Hamis Mattaka (aliyevaa koti) wakati wa ukaguzi wa eneo zitakakofanyika sherehe za Maulidi mwaka huu jijini Mwanza
kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke akisistiza jambo kwa wajumbe na viongozi wa BAKWATA Taifa , Sheikhe Hamis Mattaka (mwenye koti) na Sheikhe Nuhu Jabir Mruma, aliyevaa suti wa pili kutoka kulia) wakati wa ukaguzi wa viwanja vya Furahisha Mwanza , jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Sheikhe Hamis Mattaka,jana  akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo la viwanja vya Furahisha jijini Mwanza zitakakofanyika sherehe za Maulidi mwaka huu, kushoto kwake ni katibu Mkuu wa Baraza hilo Sheikhe Nuhu Jabir Mruma na kushoto wa kwanza ni Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hasani Kabeke.

Picha na Baltazar Mashaka

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
HALMASHAURI Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka waumini wa dini hiyo kuhakikisha wanashirikiana na dini zingine kufanikisha Maulidi ya kihistoria Mtume Muhhamad S.A.W.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa BAKWATA, Sheikhe Hamis Mattaka alisema jana wakati wa kukagua maendeleo ya maandalizi ya sherehe hizo za maulidi zitakazofanyika kitaifa jijini Mwanza.

Alisema Waislamu kwa umoja,ushirikiano na uhusiano uliopo na waumini wa dini zingine wahakikishe wanafanikisha kufanyika kwa maulidi ya kihistoria ya nusu karne baada ya BAKWATA kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1968.

Sheikhe Mattaka alisema BAKWATA kwa wiki nzima kwenye maualidi hayo, itaonyesha na kuelezea shughuli na miradi mbalimbali ya huduma za kijamii zinazofanywa na baraza hilo ikiwemo miradi inayohusu UKIMWI,Kumlinda Mtoto wa Kike,Kuendesha na Kusaidia Familia masikini (duni kwa kipato). 

Alisema uongozi wa BAKWA Mkoa wa Mwanza chini ya Sheikhe Kabeke (Hasani) unastahili pongezi kwa ubunifu ambao haujawahi kufanyika wa kuwakusanya na  kushirikisha waislamu wa Kanda ya Ziwa kuona hilo ni jambo lao na kwa hali na mfumo huo Waislamu wanaweza kufanya makubwa kwa kushirikishana.

“Niupongeze uongozi wa Sheikhe Hasani Kabeke kwa ubunifu walioufanya wa kuandaa Maulidi hii kubwa ya kihistoria ya nusu karne ya pili ya uhai wa Baraza Kuu la Waislamu ambalo mwaka jana limetimiza miaka 50.Mwanza imepata fursa ya kuanza safari hiyo chini ya falsafa ya Jitambue,Badilika, Acha Mazoea.Itakuwa Maulidi yakukusanya na kufanya shughuli za kijamii,”alisema.

Sheikhe Mattaka alisema Maulidi ya mwaka huu anaamini itahudhuriwa na wageni wengi kutoka nchi nyingi za Afrika Mashariki kutokana na unyeti wake na kutoa wito kuwa wanadamu wanao udugu, wa kwanza ni ubindaamu wao na ndio maana BAKWATA inaishi kwa amani na watu wa dini zote na kuleta utengamano wakiwa wamoja.

“Wasio na dini na wenye dini tunakaa pamoja, tunaishi pamoja katika ubinadaamu wetu.Kwa pamoja tukidhamiria tunaweza kufikia maendeleo chanya kwa jamii ya Watanzania wasio waislamu kwa sababu ya  udugu wa ubinadaamu wetu,”alisema Mwenyekiti huyo wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Taifa.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa BAKWATA Sheikhe Nuhu Jabir Mruma alisema kuwa, eneo Maulidi hiyo itakakofanyikia Jiografia yake inaridhisha, linafikika kwa urahisi,lina usalama na lina faa kwa sababu huduma mbalimbali za kijamii zinapatikana na lina uwezo wa kumudu watu watakaohudhuria hapo.

“Hamasa yenyewe kwa kuwa kutakuwa na watu wengi tulikuja kujiridhisha kuona maandalizi haya ya Maulidi ambayo ni mwanzo wa kuwapeleka Waislamu kwenye maendeleo.Ni eneo sahihi la kueleza mipango waliyo nayo Waislamu, changamoto na mafanikio.Tofauti ni kuwa gharama zake hazitalingana na yale yatakayofanyika kwa miaka mingi,”alisema.

Katibu Mkuu huyo wa BAKWATA alieleza kuwa ili kujenga maendeleo ya Waislamu aliwataka waislamu wote kuungana na waandaaji wa Maulidi hiyo kwa kutoa michango yao ya hali na mali pamoja na mawazo ili kufanikisha kumshangilia Mtume Muhhamad S.A.W.
Kwa mujibu wa Sheikhe Kabeke Maulidi hiyo ya kihistoria inafanyika Mwanza kitaifa ikiwa ni baada ya miaka 20 tangu yalipofanyika mara ya mwisho mkoani humu mwaka 1990.ssss

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.