ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 27, 2013

H.BABA ATIKISA UZINDUZI WA ALBUM YA PASAKA


Ni makamuzi ya H. Baba katika kuusindikiza uzinduzi wa album ya mwana hip hop toka Mwanza Kala Jeremiah uliofanyika jana Villa Park Rock City.

KIKAO CHA KWANZA CHA HARUSI YA DANNY LAMECK CHAFANYIKA ROCK CITY

Mwenyekiti meza kuu Enrnest Nyambo akitoa tathimini ya kwanza ya kikao cha harusi ya Danny Lameck Airo kilichofanyika jana hotel Gold Crest.


Bwana harusi mtarajiwa Danny Lameck (kulia) akipewa maelezo na baba yake mzazi Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Lorya kwaajili ya marafiki na ndugu waliojitokeza kwenye kikao cha kwanza cha harusi kilichofanyika jana hotel Gold Crest Mwanza. Mr. Six wa Six Solution anaonekana pichani (mwenye mic mkononi) naye akitoa maelekezo kwa vijana wa kamati Erasto Airo.


'Mtu wa watu' Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula aliketi nasi kwenye meza hii.


Moja kati ya meza kwa akina mama ambapo kulia kabisa ni mama mzazi wa bwana harusi mtarajiwa.


Brothers.


Baba mzazi Mh. Lameck Airo ambaye ni mbunge wa Lorya (kushoto) aliweka utaratibu wa kupita meza hadi meza kusabahi ndugu na marafiki waliojitokeza kikaoni.


Mie na kaka zangu.


Kutoka kushoto waliosimama ni Mc Nyamhanga na Mc Bonke, walioketi ni Philbert Kabago na G. Sengo.


Wazee wa mji.


'Pamoja'
'Pia Mastori ya town... yalikuwepo'


Kutoka kushoto ni Waziri, Kabago na G. Sengo


Pia burudani ilikuwa na nafasi yake mara baada ya shughuli kumalizika.

MFUMO DUME BADO KIKWAZO KATIKA KAMPENI YA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO NA UZAZI WA MPANGO



Mhudumu wa Afya wa Kliniki ya Makongoro akimhudumia mama mjamzito Aprili 25,mwaka huu

Na Clara Matimo, Mwanza
KAMPENI ya kupunguza Maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto, “Prevention of Mother to Child Transmission”(PMTCT), na Ushiriki wa Wanaume katika Uzazi wa Mpango,unakwamishwa  na  tabia ya mfumo dume ulioota mizizi Kanda ya Ziwa, imefahamika.

Mratibu Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto Jijini Mwanza, Sarah Mahumbuga, amesema kwa miaka miwili ya 2011 na 2012, akina baba wachache walifika Kliniki na katika vituo vya Afya,ili kupima afya zao na kushiriki Uzazi wa Mpango.

Anasema,Shirika la Engender Health kupitia Mradi wa CHAMPION(Men Involvement), linalotoa huduma katika baadhi ya mikoa hapa nchini, Mkoa wa Mwanza ukiwemo,  wilaya za Ilemela na Nyamagana zinahusishwa na mradi huo.

Hospitali ya Nyamagana na Kliniki ya Makongoro  huhusishwa na mradi huo kwa nia ya kuwahamasisha  akina baba kushiriki Afya ya Uzazi na Maambukizi ya Ukimwi.
Sarah Mahumbuga amesema, katika kipindi cha mwaka 2011,wanaume walioshiriki kupima afya zao na Uzazi wa Mpango ni 3,370 sawa na asilimia 18  tu ya lengo lililokusudiwa, katika Jiji la Mwanza.


Mahumbuga anafanua kwamba, mwaka 2012  akina baba walioshiriki katika zoezi hilo muhimu ni 8,541 sawa na asilimia 43.

“Mwaka 2010 wanawake waliohudhuria Kliniki kwa mara ya kwanza walikuwa 18,952. Idadi ya waliopima virusi vya Ukimwi ni 12,057 sawa na silimia 63 ya akina mama wote waliohudhuria Kliniki kwa mara ya kwanza, na kati ya hao wanawake 756 sawa na asilimia 6.2 walikutwa na maambukizi ya Ukimwi”,Mahumbuga amesema.

Akilinganisha na akina baba waliopima virusi vya Ukimwi mwaka huo 2010 amesema walijitokeza akina baba 328 tu ambao ni sawa na asilimia 6.

Akaongeza kuwa mwaka 2011 wanawake waliofika kliniki kwa mara ya kwanza walikuwa 18,726; na kati yao waliopima Virusi vya Ukimwi ni 7,947 sawa na asilimia 42. Kati yao waliokutwa wakiwa na maambukizi ya virusi hivyo vya Ukimwi ni 506 idadi ambayo ni sawa na asilimia 6.3.

Mratibu huyo Msaidizi wa Afya ya Uzazi na Mtoto Jijini Mwanza, anasema katika mwaka huo 2011 wanaume waliofika Kliniki na wake zao na wakapima afya ni 374 sawa na asilimi 6.9.

Katika mwaka 2012,Mratibu huyo anabainisha kuwa wanawake waliohudhuria kliniki kwa mara ya mwanzo walikuwa 19,946; na kati yao waliopima afya zao ni 11,299 sawa na asilimia 57.Waliokutwa na maambukizi ya Ukimwi ni 523 sawa na asilimia 4.6.

Mratibu huyo amesema wanaume waliohudhuria kliniki mwaka 2012 walikuwa 596 ambao ni asilimia 2.1 tu
Baba akimshuhudia muhudumu wa afya akipima ujauzito wa mkewe katika Kliniki ya Makongoro, Mwanza

“Kama wanawake wanaohudhuria kliniki wangekuwa wanafika na wenzi wao na kupima, akina baba wangetambua umuhimu wa kushiriki zoezi hilo la kuokoa maambukizi kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto”, anafafanua.

Akizungumzia changamoto zinazokabili Kampeni hiyo ya Afya ya Uzazi na Mtoto,   katika utendaji wa kazi wa kila siku, ameseka kuna uhaba wa vitendanishi( HIV TEST KITS) , akatoa mfano kwamba kwa mwaka huu 2013 Jiji la Mwanza limepata kit 69 tu wakati vipo vituo 24 vinavyotoa huduma hiyo.     Kit moja ina vifaa 100 vya kupima ukimwi.

“Kufuatia hali hiyo, mwaka 2011 wanawake waliofika kliniki mara ya kwanza walikuwa 18,726,lakini waliopima walikuwa 7,947; hali hiyo husababisha waliobaki kukosa huduma kufuatia vifaa hivyo vya kupimia Ukimwi kuwa vichache”, alisisitiza.

Amewataka wanaume kujitokeza kwa wingi bila woga katika zoezi hilo ambalo lazima lihusishe baba, mama na mtoto kwa kuwa mtoto hapatikani bila ya wazazi wawili kushiriki tendo la ndoa.

“Wanaume wote wanapaswa kufika kliniki pindi wake zao wanapopata ujauzito; kwa sababu kuna faida nyingi; kujua mama ana tatizo gani wakati wa ujauzito,dalili za hatari; na ikitokea shida baba ajue cha kufanya ili kumsaidia mama mja mzito kujifungua salama”,

Hatari za akina baba kutoshiriki zoezi la upimaji wa afya ya uzazi  humfanya mama mjamzito kuathiriwa kisaikolojia,hususan anapopimwa na kubainika kuwa ameambukizwa.

“Wakipimwa pamoja wakagundua tatizo ina kuwa rahisi wote kwa pamoja kujua namna ya kumkinga mtoto aliyeko tumboni asipate maambukizi; na pia hujua namna ifaayo kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto”, Mratibu huyo amesisitiza.

 Imeelezwa pia kwamba,wanaume wengi wa Tanzania hawapendi kupima Ukimwi ukilinganisha na wageni wanaofika nchini, ambao Mratibu huyo wa Afya ya Uzazi na Mtoto amesema hawajifichi;lakini wanaume wa hapa nchini hawapendi kujitokeza kuzungumzia hali zao za kiafya kwa wataalam wa afya.

Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk.Kimaro Daniel anasema kuna wanaume wengi waliojitokeza kupima afya zao jijini Mwanza ukilinganisha na wanaume wa wilaya za Sengerema na Ukerewe.

"Wanaume wa jijini hapa wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika suala zima la afya ya uzazi  kwasababu elimu tunayowapatia wameielewa na kutambua umuhimu wake, japo elimu hii inapelekwa wilayani lakini kule ushiriki wa kule unakuwa mdogo kutokana na wanaume kujiona wao ni vichwa vya familia hivyo hawawezi kupangiwa na wake zao kwenda nao kliniki" anasema Dk. Daniel.

Akitoa taarifa kwa Naibu  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Seif Rashid,Siku ya Utepe Mweupe,Machi 15 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo amesema mkoa huu una jumla ya wakazi 2,571,402 kulingana na SENSA YA WATU NA MAKAZI ya 2012,ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 2.7.

Ndikilo anasema Mkoa wa Mwanza una watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja 106,360 na wenye umri wa chini ya miaka mitano 488,851; wakati akina mama wenye umri wa kuzaa ni 926,179.

Akizungumzia idadi ya hospitali na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto,Dk.Ndikilo amesema kuna vituo 353; na kati ya hivi vipo katika hospitali 14(mbili za rufaa);hospitali za wilaya,za binafsi na za mashirikika ya dini.

Kati ya vituo hivyo 353,vituo 326 sawa na asilimia 92 hutoa huduma ya afya ya mama na mtoto;wakati vituo 239 sawa na asilimia 73.3 hutoa huduma ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mhudumu wa Afya akiwapa huduma  mama wajawazito
         
Miongoni mwa akina mama 926,179 wenye umri wa kuzaa, akina mama 121,530 walipata ujauzito na kati yao  82,214 walipata huduma ya uzazi wakati wa kujifungua sawa na asilimia 67.6

Mkuu wa Mkoa anasema kiwango cha maambukizi ya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kimeshuka kutoka asilimia 5.2 mwaka 2011 hadi asilimia 4.2 mwaka jana.

Anasema kwamba vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi vimepungua kutoka  217 kati ya 100,000 hadi 95 kati ya 100,000 mwaka jana.

Mkuu wa Mkoa amesema mkoani Mwanza sasa vifo vya watoto walio chini ya mwaka mmoja ni 11 kati ya watoto 1,000 waliozaliwa hai.Kiwango hiki ni cha asilimia 14.
Kulingana na Mratibu wa Taifa wa Afya na Mama na Mtoto katika Wizara ya Afya, Dk. Koheleth Winani,akina mama wa Tanzania wangali wanakabiliwa na hatari ya maradhi yanayoweza kuzuilika.

Kiwango cha akina mama  wajawazito wanaofariki nchini 454 kati ya 100,000.Na watoto wanaokufa ni 26 kwa kila watoto 1000 wakati wanapozaliwa.

Kufuatia halihiyo, Mkurugenzi wa Afya wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani(USAID),Alisa Cameron alisema siku ya uzinduzi wa Kampeni ya Uzazi salama Jijini Mwanza kwamba Kampeni ya ‘Wazazi Nipendeni’ inayotangazwa na vyombo vya habari nchini iwafanye akina baba kuacha mfumo dume na kushiriki ipasavyo katika zoezi la uzazi wa Mpango na kupima virusi vya Ukimwi,ili kuokoa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa  mtoto.

“WAZAZI NIPENDENI” inalenga kuwezesha akina mama wajawazito na wenzi wao kuchukua hatua thabiti za uzazi salama, na kuzua maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT).

Sekamponge  Makuki (24)mkazi wa jijini  Mwanza ambaye  ni mjamzito, anasema yeye anafaraja sana kwa kipindi hiki cha ujauzito kwa kuwa yeye na mumewe walipanga kupata mtoto,na pia wote wanahudhuria klinik jambo linalowafanya kupata elimu ya pamoja kutoka kwa wataalamu wa afya,na pia mumewe anafundishwa jinsi ya kuishi nae kwa kipindi cha ujauzito.

“Tangu tulipofunga ndoa na mume wangu,tumekuwa tukishirikiana nae katika masuala yote ya afya ya uzazi,hivyo na huu ujauzito nilionao tulipanga kwamba tazae,hata kabla ya kupata ujauzito tulipima afya zetu na baada ya ujauzito tulipima pia kwa pamoja, namshukuru MUNGU hatukupatikana na maambukizi ya ukimwi  anasema na kuongeza kuwa “lakini kwa kuwa tunashirikiana hata kama majibu yangekuwa mabaya tungeyapokea kwa pamoja,ni vizuri akisikia mwenywe  majibu kutoka kwa mtaalamu wa afya kuliko kumwambia mimi’’”anaeleza Makuki.

Mhudumu wa Afya akiwahudumia watoto katika Kliniki ya Makongoro

Mwanaume anayeshiriki katiaka suala zima la Uzazi wa Mpango katika kliniki ya makongoro iliyopo jijini Mwanza,Abel Luzibila (30)mkazi wa Bwiru jijini Mwanza anasema amekuwa akienda kliniki na mke wake tangu mwanzo wa ujauzito ili kufahamu maendeleo ya afya ya mke wake, kama wataalamu wa afya watabaini tatizo lolote kutoka kwa mke wake wajue watajipanga vipi kiuchumi katika kulitatua.

Luzibila, amesema kwamba mara ya kwanza alipofika Kliniki na mkewe ambaye ni mjamzito, alisema alivutiwa na somo la namna  inavyopasa kumsaidia mama mjamzito.
“Kwa mfano,leo(Aprili 25 mwaka,2013) tumejifunza somo la unyonyeshaji, tumefundishwa lishe bora wakati mama anaponyonyesha na sitabishia Bajeti inayotukabili kwa sababu tayari nimeshiriki mafunzo hayo na najua umuhimu  na athari za kukosa lishe bora”, Luzibila anasema.

Ofisa Mawasiliano wa Mradi  wa CHAMPION unaoshughulikia Ushiriki chanya wa Wanaume katika Mkakati wa kitaifa wa kupambana na Maambukizi ya  Virusi vya Ukimwi na Ukimwi (Engender Health),Muganyizi Mutta, anasema akina baba wanaposhiriki kikamilifu katika Uzazi wa Mpango watawezeshwa kupanga idadi ya watoto wanaowataka.

Mutta pia amesema baba na mama wakishiriki kwa pamoja katika zoezi hilo watapata njia za uzazi wa Mpango zinazofaa, na kuwa na familia zilizo bora.

“Shirika la Engender Health,kupitia Mradi wa CHAMPION(Men Involvement) limetenga Dola za Kimarekani milioni 16 kwa ajili ya kuhamasisha akina baba kushiriki kikamilifu katika mkakati huu kitaifa wa kupambana na virusi vya Ukimwi kutoka ,mradi ni wa miaka  mitano unaomalizika Septemba mwaka huu”, Mutta amesema

AFRICA SUPER MIDDLEWEIGHT ON THE LINE AS MASHALI ATTEMPTS TO GRAB THE CROWN


FRIDAY 26, 2013 - Dar Es Salaam - Reeling from the recent defeat in the hands of the German strongman Uensal Arik , TEAM Francis Cheka is back on the drawing board as it attempts to defuse negative impact of the loss in their forthcoming rumble against the man of the people and dreadlock Thomas MashaliThe duo is competing for the “IBF Continental Africa Super Middleweight Title” as optional defense for Cheka.ients
Francis Cheka (right) and Uensal Arik (left)
 
 
The tournament slated for 1st May, 2013 (May Day) has elicited a lot of excitements from thousands of boxing stakeholders in Tanzania and the whole of East African region. Thomas Mashali is the East & Central African Middleweight Champion and the biggest crowd puller in the region todate.

Cheka’s recent defeat was kind of embarrassment as he took the fight as a warm up but alas, things turned bitter as the Germany strongman Uensal Arik sent him reeling to the floor before Thomas Mtua threw out the towel as SOS for the Tanzanian slugger! It was a defeat from “Manna”as this kind of taught Cheka a lesson or two about taking boxing serious as there is nothing as a small fight in boxing.

Adam Tanaka of Mumask Investment and Gebby Presure LTD, the man of the hour promoting this fight has been working over drive to have all the details finalized. Of the top priority is the arrival of the ring officials (all coming outside Tanzania) who have been summoned to preside over the rumble. This is so because Adam want to avoid complaints from either boxer should the decision goes against their expectations.

"The poster in Kiswahili language tells it all"

 
The man who has been charged with the responsibility to stand in as “the third man in the ring” is no other than the Zambian Army Officer, John Shipanuka who himself looks like a heavyweight boxer in refereeing uniform. Shipanuka’s body language and impatiality with boxers in the ring has illuminated his CV and make him one of the most sort-out ring officials in Sub Sahara Africa.
Arusha Mayor (left) and IBF/AFRICA' Onesmo 
Ngowi (right) crowing Cheka after his last 
 defense 12/26/12


To assist him would be two Sedentary Generals of; Uganda Professional Boxing Commission (UPBC), master Simon Katogole and Daudi Chikwanje of Malawi Boxing Association (MBA). These two gentlemen would be in the company of one of the most experienced judges in East Africa Alhaj Ismail Sekisambu also from Uganda.

So, “the chickens have finally come home to roost" as any of the two has to face the consequences of his mistakes in the ring on that particular day.

So, as the clock ticks to the morning hours of May Day 2013, Dar Es Salaam landscape may turn into a “quicksand” for the two gladiators as fans from all walks of life jams the PTS Social Hall to witness yet another rumble of the year!
 
Nothing has been left to chances as the World's premier professional boxing “top dog” the IBF has already given its blessing by sanctioning for the title!
 


Friday, April 26, 2013

MTEULIWA WA TUZO ZA KILI MUSIC 2013 KALA JEREMIAH KUZINDUA ALBUM YAKE LEO VILLA PARK JIJINI MWANZA

Kala jeremiah wrote: MWANZA KWANZA UZINDUZI WA ALBUM YANGU YA PASAKA YENYE JUMLA YA NYIMBO 23 UTAFANYIKA LEO IJUMAA JIJINI MWANZA TAREHE 26 MWEZI WA 4 NDANI YA UKUMBI WA VILLA PARK KWA KIINGILIO CHA TSH 5000/= TU.  PIA ALBUM ITAUZWA KWA TSH 5000/=. KARIBUNI SANA WASANII KIBAO WA MWANZA WATASINDIKIZA. BILA KUMSAHAU RAIS WA MATEJA KITALE. NA MWANADADA DAYNA NYANGE WA NIVUTE KWAKO. BONGE LA SHOW NITACHANA NGOMA ZOOTE UNAZOZIJUA...

Kwenye interview Kitale alinyunyiza ucheshi studioni ...basi kila mmoja kwe-kwe-kwe.

Kitale akiendelea kunyunyiza mbwembwe....huku Mwanahip hop mteuliwa tuzo za Kili Kala Jeremiah akiangua kicheko...

Prizenta wa kipindi cha 'Michano Time' Passion Fm Philbert Kabago akihojiana nao.

Kutoka kushoto ni Kala Jeremiah, Kitale, Producer Tiddy wa One Love Production na mwenzake Shaib'


Wameiona kamera ya G. Sengo...!!!!

Ramani ya eneo la tukio.
Msanii bora wa hiphop
Fid Q,
Joh Makini,
Kala Jeremiah,
Profesa J,
Stamina

Wimbo bora wa Mwaka: 
Dear God Kala Jeremiah,
Leka Dutigite Kigoma All Stars,
Mapito - Mwasiti Ft Ally Nipishe,
Me and You -Ommy Dimpoz Ft Vanessa Mdee
Pete - Ben Pol.

Msanii bora wa Kiume 
Ben Pol,
Diamond,
Linex,
Mzee Yusuf 
Ommy Dimpoz.

Msanii bora wa kike
Isha Mashauzi,
Khadija Kopa,
Lady JayDee,
Mwasiti
Recho. 
Msanii bora wa kiume Bongo Fleva: 
Ally Kiba,
Ben Pol,
Diamond,
Linex
Ommy Dimpoz

Msanii bora wa kike Bongo Fleva: 
Linah, 
Mwasiti
Recho
Shaa

 Msanii bora anaechipukia:
Ally Nipishe,
Angel,
Bonge la Nyau,
Mirror
VanessaMdee

Video Bora: 
Baadae - 
Ommydimpoz 
Kamili gado - Profesa_Jay
Marry me - Rich Mavoco,
Nichum -Bob Jr
Partyzone  -AY

Mtunzi bora wa mashairi Bongo Fleva: 
Ally Kiba,
Barnaba,
Benpol,
Linex
Ommydimpoz

Mtunzi bora wa mashairi Hiphop:  
FidQ
Joh Makini,
Kala Jeremih,
MwanaFA
Stamina

Mtunzi bora Mashairi kwenye Band: 
Chaz Baba,
Greyson Semsekwa,
Jonico Flower
Jose Mara
Khaleed Chokoraa

Mtayarishaji bora muziki wa kizazi kipya: 
Bob Juniour,
C9,
Imma the Boy,
Man Water,
Maneke, Marco
Marco Chali
Mensen Selekta

Wimbo bora wa Bongo Pop  
Aifora - Linex,
Baadae - Dimpoz,
Chuki Bure-Sharo,
Marry me-Mavoco
Me & You Ommy Ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa kushirikiana:
Chuki bure -Sharo Milionea Ft Dully Sykes
Mapito-Mwasiti Ft Ally Nipishe
Me & You, - Ommy Dimpoz Ft Vanessa mdee
Sihitaji marafiki  - Fid Q Ft Yvinne Mwale
Single boy - Ally Kiba Ft Jaydee

Wimbo bora wa Hiphop: 
Alisema -Stamina,
Bum Kubam -Nikki wa II,
Dear God -Kala Jeremiah,
Nasema nao  - Nay
Sihitaji Marafiki - Fid Q

Wimbo bora Afrika Mashariki: 
Fresh all day - Camp Mullah
Make you dance - Keko
Maswali ya polisi - DNA
Still a Liar - Wahu
Valuvalu -Jose Chameleone

Wimbo bora wa Zouk/Rhumba: 
Gubegube -Barnaba,
Mapito - Mwasiti
Nashukuru umerudi - Recho
Ni wewe - Amini
Sorry - Barnaba.

Bendi bora ya Mwaka: 
The African Stars Band,
Mapacha Watatu,
Mashujaa Band
Mlimani Park Orchestra (Sikinde)
Msondo Ngoma Music Band.

MAAMBUKIZI YA VVU TOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO YANAWEZA KUEPUKWA



MAAMBUKIZI YA VVU  TOKA KWA MAMA  MJAMZITO KWENDA  KWA MTOTO  YANAWEZA KUEPUKWA
Edwin Soko
Mwanza
Tafiti  zinaonyesha  kwamba kuna uwezekano  mkubwa wa mama  mjamzito   kumwambukiza mwanae Virusi  Vya Ukimwi (VVU),  endapo mama  atakuwa  anaishi na Virusi  Vya  ukimwi  kama  hakutakuwa na mipango  mathubuti  ya kimkinga mtoto aliye tumboni kupitia mpango wa kuzuia  maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi toka  kwa  mama mjamzito kwenda  kwa  mtoto(PMTCT). 

Baba ana nafasi ya kumpenda mkewe akiwa mjamzito
Mganga  mkuu wa mkoa wa Mwanza, bwana Valentino  Bangi,  alisema kuwa, virusi vya ukimwi vinaweza kusambazwa kutoka kwa mama mjamzito aliyeambukizwa, hadi kwa mtoto tumboni kwa njia kuu tatu. Njia ya  kwanza  wakati mtoto yungali tumboni mwa mama, ambapo virusi vinaweza kusambaa kutoka kwa mama hadi kwenye nyumba ya uzazi. 

Pili  ni  wakati wa kujifungua, ambapo mtoto anaweza kuingiwa na majimaji ya ukeni au majimaji mengine kutoka kwa mama.  Tatu ni  wakati wa kunyonyesha, ambapo virusi vinaweza kuambukizwa kupitia maziwa anayonyonya mtoto. 
 
Kwa mujibu wa UNICEF, uwezekano wa kumwambukiza mtoto  wakati wa kujifungua ni mkubwa zaidi kama mama ana ujazo mkubwa wa virusi mwilini mwake na kinga yake tayari ni dhaifu. 

Kabla ya mwanamke aliyeambukizwa kupewa usaidizi wowote wa kimatibabu kwanza atafanyiwa uchunguzi wa damu kuona kima cha virusi ndani ya mwili na hali yake ya kinga kwa ujumla. Kama kinga yake itakuwa thabiti na idadi ya virusi ni ndogo mwilini, huenda hatahitaji dawa mpaka kipindi cha mwisho mwisho cha uja uzito yaani baada ya wiki ya 24.

Lakini kama ujazo wa virusi ni mkubwa na kinga mwili ni dhaifu, huenda italazimu kutumia madawa maalumu  ya kupunguza makali ya ukimwi, mapema ili kupunguza uwezekano wa kumwambukiza mtoto.

Tanzania  ni  moja  kati  ya nchi  zilizo mstari wa mbele  kutekeleza mkakati wa kuzuia  maambukizi   ya  Virusi  Vya  Ukimwi  toka kwa mama  mjamzito kwenda  kwa mtoto(PMTCT) kupitia  huduma zitolewazo na mkakati huo. Hali  hiyo imepelekea  kushuka kwa maambukizi   toka  kwa mama  kwenda  kwa mtoto sanjali na vifo  vya  kina mama wajawazito

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alibainisha kwenye  maadhimisho ya siku  ya  utepe mweupe  yaliyofanyika  duniani kote  na kitaifa  kufanyika mkoani Mwanza     machi 15 mwaka huu   kuwa, vifo  vya kinamama  vinavyotokana  na  uzazi  vimeshuka  kutoka  200 kwa mwaka 2006  hadi  kufikia   vifo 160 kwa mwaka  2012. Hali  hiyo  imsababishwa na kuongezeka  kwa huduma  ya PMTCT.

Nchini Tanzania kwa mujibu wa kituo  cha kuzuia  maambukizi toka  kwa mama mjamzito kwenda  kwa mtoto, kiliainisha takwimu zinaonyesha kuwa, wanawake wajawazito wanaopata huduma ya PMTCT  imeongezeka  toka 34% kwa mwaka 2007 hadi  80% kwa mwaka 2012. Nchini  Kenya  kwa mujibu wa UNICEF pia idadi  imeongezeka toka  56%  kwa  mwaka 2008  hadi 74% kwa mwaka 2008. Nchini Uganda ungezeko ni 27% kwa mwaka 2007 hadi 50% kwa mwaka 2011, kwa mujibu wa ripoti ya wizara  ya  afya ya Uganda.

Dira   ya maendeleo  ya  Taifa 2025 kipengele cha tatu cha  ustawi wa jamii kinasisitiza kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na lengo  la tano la malengo  ya millenia  linasisitiza  kuimarisha huduma za kinamama wajawazito, lengo hilo   zikitekelezwa vyema  ni wazi kwamba hatari ya kumwambukiza mtoto virusi vya ukimwi inaweza kupunguzwa hadi kufikia kati ya asilimia, moja na asilimia mbili tu kama hatua zifuatazo zitazingatiwa. Kupata  matibabu ya  kupambana  na virusi  vya  ukimwi, kuzaa kwa njia  ya  upasuaji na kutonyonyesha kama  mama atabainika kuwa na maambukizi ya virusi  vya ukimwi. 

Sera  ya Taifa  ya  kuthibiti  ukimwi (2001)  katika  lengo  lake  la kwanza inasisitiza juu  ya  kuzuia na  kuenea  kwa ukimwi, hivyo  basi  ni wajibu  baba na jamii  nzima kuzuia  maambukizi  toka kwa mama  kwenda  kwa mtoto ili kuwaokoa watoto wasiambukizwe virusi  hivyo.

Sera ya afya ya Taifa  ya mwaka 2007 moja ya lengo lake kati ya malengo tisa ni kupunguza maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto na kuongeza umri wa kuishi. Huenda  lengo  hili likawa linatia  matumaini kupitia  takwimu, kwani  Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF linabainisha kwamba, maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto yamepungua  kwa  24%  katika nchi ishirini na mbili na nyingi kati ya hizi ni zile ambazo ziko Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mkakati wa Pili wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (2008-2012) umehusisha mchakato wa Ushirikiano wa wadau mbalimbali, kama mashirika  asasi  na watu  binafsi katika kupunguza maambukizi  ya  Virusi  vya  ukimwi.

Shughuli  nyingi za kuzuia  maambukizi  toka  kwa mama  kwenda  kwa  mtoto (PMTCT) nchini Tanzania zimekuwa vikiungwa mkono  na mfuko wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupunguza maambukizi  ya  Virusi  Vya  Ukimwi( U.S President’s Emegence Plan for  AIDS Relief ) kupitia shirika  la Engender health  ambalo  umekuwa  ukitoa elimu  kuhusiana na  afya  ya  uzazi wa mpango, kutoa  mafunzo kwa wadau  juu  ya  afya ya uzazi  wa mpango na uzazi  salama.

Mkakati  huo unatukumbusha wajibu wa baba, mama na jamii nzima kushirikiana na kutumia huduma ya kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) ili kuwakinga watoto wasipate maambukizi hayo. Huduma za  PMTCT  ni pamoja na ushauri na upimaji wa Virusi Vya Ukimwi.  Pia ushauri kuhusu ulishaji wa mtoto aliyezaliwa na mama aliyeambukizwa Virusi Vya Ukimwi, matumizi sahihi ya dawa (ARV) za kuzuia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi; huduma bora na salama wakati wa kujifungua na ufuatiliaji wa mama na mtoto baada ya kujifungua.

Katika  kujali  hilo Tanzania tarehe 1 Desemba 2012 mheshimiwa  Rais Jakaya  Mrisho Kikwete  alizindua  mpango wa kupunguza  maambukizi ya VVU toka kwa mama kwenda  kwa mtoto kwa mwaka  2012 – 2015. Mpango huo una lengo la kupunguza maambukizi mapya  kwa watoto  na kumfanya  mama kuendelea  kuishi salama.

Kuhakikisha programu ya kuzuia  maambukizi ya Virusi  Vya Ukimwi  toka kwa mama kwenda kwa mtoto  (PMTCT)  inafanikiwa ni lazima hatua zote muhimu zifuatwe, kama kuhudhuria kliniki, kupatikana kwa vipimo,  kukubali kupima,kupata majibu, kupatikana kwa dawa, kukubali dawa, kumeza dawa, dawa kwa mtoto na lishe salama

Hatua mbalimbali za kufuatwa ili kukamilisha programu ya PMTCT)

Makala  haya  yameandaliwa kwa msaada mkubwa  wa sera  ya  Afya  ya Taifa (2007),Sera  ya Taifa ya kuthibiti ukimwi(2001), Dira  ya  maendeleo  ya  Taifa (2005), Mkakati wa pili wa kuthibiti  UKIMWI(2008-2012), Mkakati wa PMCT wa Kenya, Malengo ya Millenia 2015, Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania. Mkakati wa kutathimini  hali  ya  PMTCT  Tanzania . Mpango  wa  Uganda wa  kupunguza  maambukizi  mapya  miongoni mwa watoto ifikapo  mwaka 2015 na kuwaweka mama zao  salama.

Kwa maoni na ushauri juu ya makala hii wasiliana na mwandishi 
kupitia Simu No.0754 551 306