ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 28, 2019

SAA CHACHE BAADA YA MAANDAMANO YA WANANCHI KUHUSU NDEGE YA ATCL MBUNGE 'MUSUKUMA' ANENA HAYA


MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku almaarufu 'Musukuma' amewaomba watanzania kusimama pamoja kuhakikisha Serikali inamaliza bila hasara kesi ya kushikiliwa moja ya ndege zake nchini Afrika ya Kusini.

Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya kundi la Wananchi wameandamana hadi ubalozi wa Afrika kusini jijini Dar es salaam kushinikiza nchi hiyo kuiachia ndege ya ATCL inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama.

Aidha Musukuma amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya Watanzania wanaofurahia jambo hilo kana kwamba ndege inayoshikiliwa ni mali ya mtu binafsi ile hali ni mali ya Taifa.

"Inavyoonekana mtaani ni kama imekamatwa ndege binafsi ya Mhe. Rais Magufuli, napenda kuwaambia watanzania wenzangu, wazalendo iliyokamatwa ni ndege yetu, mali yetu watanzania, iliyonunuliwa kwa kodi zetu na hiki ni kilio  chetu" alisema Mbunge huyo wa Geita Vijijini kwa tiketi ya CCM

Musukuma amesema analijua 'genge la waovu' wanaoshiriki kuchochea yote haya na ameapa kwa kusema kuwa muda utakapofika atawataja mmoja baada ya mwingine.

Tuesday, August 27, 2019

MBUNGE RITTA KABATI TIMIZA AHADI YA KUKARABATI SHULE YA MSINGI KIHESA.

Diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametakiwa kutimiza ahadi ya kukarabati shule ya msingi Kihesa kama alivyowaahidi wakazi wa kata ya kisheza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika shule hiyo.

Akizungumza na blog diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani amemuomba mbunge huyo kutimiza ahadi aliyoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu katika kata hiyo.

“Naomba nimpongeze bwana Jose Mgongolwa kwa kusaidia kukarabati baadhi ya majengo ya madarasa kwa msaada wake wa kukarabati madarasa hayo katika shule ya msingi Kihesa” alisema Sawani

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amesema kuwa atatimiza ahdi hiyo mwezi wa tisa akitoka bungeni na kila kitu kipo sawa.

“Utaratibu wa sasa ukiomba pesa kwa wadau unatakiwa kutoa account ya Halmashuri ili kila kitu kinapitia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hivyo tayari wadau tayari wameshazitoa na zipo halmashuri” alisema Kabati

Aidha Kabati amesema anamifuko ya saruji zaidi ya mia saba kwa lengo la kukamilisha ahadi zote alizoahidi katika shule mbalimbali mkoani Iringa.

Mwezi wa tisa naanza kutekeleza ahdi zote kwa kuwa pesa ninazo hivyo ni jukumi la mkurugenzi kuninunulia mifuko hiyo ya sariji ili nianze kutimiza ahadi zote.

Sunday, August 25, 2019

UCHAMBUZI WA KITAALAMU KUHUSU TUHUMA ZINAZOMKABILI MWANDISHI JOSEPH GANDYE ANAYESHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA MADAI YA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO MTANDAONI.

Mwandishi wa Habari Joseph Gandye kutoka Watetezi TV"

Anaandika Mwandishi wa habari mwandamizi nchini, Dotto Emmanuel Bulendu.

Jioni ya leo baada ya ratiba ngumu,nimekutana na habari ya kukamatwa na kuendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa mwandishi wa Habari Joseph Gandye kutoka Watetezi TV".kwa kile kinachodaiwa kuandaa stori ya TV inayodaiwa kukiuka  sheria(Jeshi la Polisi ndiyo linamshikilia).

Gandye alikwenda mkoani Njombe kufanya stori ya TV juu ya tuhuma za unyanyasaji walizofanyiwa vijana na baadhi ya Askari na wakuu wa kiwanda walichokuwa wakifanyia kazi.

Nimeamua kuitafuta stori na kuipata,nimeiona nawe waweza itazama(nimekuwekea link-https://youtu.be/0LhQMsHSFWo)

Maoni yangu.
Stori hiyo haina tatizo lolote la kisheria,kiweledi na kitaaluma bali inachangamoto ya kimaadili kwa sehemu ndogo ambayo sidhani kama inaweza kuwa ni jinai.

Kwa nini nasema haya?

1.Stori imehusisha vyanzo vyote viwili,chanzo kitu (physical source) na chanzo mtu(human source)

2.Stori imebalansi uzania wa vyanzo kwa kuhusisha vyanzo vitatu kutoka chanzo mtu kwa maana ya mlalamikaji na mtuhumiwa,maana aliyelalamika yumo,aliyelalamikiwa pia yumo kwenye stori.

3.Stori imezingatia msingi mkuu haki za binadamu (haki ya kusikilizwa kabla ya kuhukumiwa),kwani mwandishi ameweza kutoa nafasi kwa Uongozi wa kiwanda pamoja na Jeshi la Polisi(ambao ni watuhumiwa)waweze kujibu tuhuma hizo maana RPC katumika kwenye stori na kiongozi wa kiwanda).

Udhaifu upo wapi?

Binafsi nauona udhaifu kwenye eneo la maadili baada ya mwandishi kuacha baadhi ya maneno ambayo yana ukakasi kidogo kutumika maana kwenye uandishi tunaambiwa tujitahidi kupunguza ukali wa maneno (ila siyo sheria ni suala la maadili).

MSIMAMO WANGU.

Jeshi la Polisi muachieni Joseph Gandye maana amefanya stori kwa kuzingatia misingi ya Habari ni nini?na amezingatia misingi yote ya kisheria ya matakwa ya uandaaji wa Habari.Katumia vyanzo vyote vinavyotakiwa.Kuendelea kumshikilia Gandye ni kuendeleza kile kinachohisiwa kuwa kuna ubinywaji wa Uhuru wa Vyombo vya Habari na waandishi wa Habari.

Wasalaaam
Bulendu E.D

MKURUGENZI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA APONGEZA MAFANIKIO YA TASAF.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi. Anne Kabagambe (aliyeshika mkoba) akilakiwa na Mmoja waMaafisa wa TASAF, Bi. Tatu Mwaruka wakati wa ziara ya kukutana na Walengwa wa TASAF katika Mtaa wa Keko Machungwa wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam. 

Na Estom Sanga -TASAF 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Bi.Anne Kabagambe amepongeza mafanikio ya Serikali ya Tanzania Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF katika kuboresha maisha ya Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

Bi. Kabagambe ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kikazi , ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na TASAF,na kujionea bidhaa wanazozalisha katika Mtaa wa Keko Machungwa ,Wilaya Temeke, mkoani Dar es salaam. 

Amesema kutokana na ubora wa Utekelezaji wa Miradi ya TASAF, Benki ya Dunia imekubaliana na Serikali ya Tanzania kuidhinisha kiasi cha Shilingi Trilioni Moja kwa ajili ya Utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Sehemu ya Pili , fedha ambazo amesema zitasaidia zaidi juhudi za Serikali katika kuwahudumia Wananchi wanaokabiliwa na Umaskini. 

‘’Tumejiridhisha pasi na mashaka kuwa utekelezaji wa Shughuli za TASAF katika awamu zote tatu umekuwa wa mafanikio makubwa hivyo Benki ya Dunia imeamua kuendelea kusaidia juhudi hizi’’ amesisitiza Bi.Kabagambe. 

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika amesema kiasi hicho cha fedha kitatolewa mwezi Ujao wa Septemba na kuwataka Walengwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kuendelea kuboresha miradi ya kiuchumi ili kuongeza tija na hatimaye waweze kuboresha zaidi maisha na kuondokana na umaskini wa kipato. 

Kwa Upande wao Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wameishukuru Serikali kupitia TASAF kwa jitihada za kuwaondolea kero ya umaskini wa kipato na kuomba juhudi zaidi zielekezwe katika kuwapatia elimu ya Ujasiliamali ili waweze kuboresha shughuli za uzalishaji mali na kukuza kipato chao. 

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF umekuwa ukitekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao unahudumia takribani Kaya Milioni Moja na Laki Moja Kote Tanzania Bara,Unguja na Pemba na hivi sasa uko katika maandalizi ya utekelezaji wa Sehemu ya Pili ya Mpango inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni baada ya taratibu muhimu kukamilika.


Bi. Anne Kabagambe (picha ya juu na chini) akiwa katika mkutano na walengwa wa TASAF katika mtaa wa Keko Machungwa ,wilaya ya Temeke, jijini Dar es salaam. 

Baadhi ya Walengwa wa TASAF wakiwa na bidhaa walizozitengeneza baada ya kupata ruzuku kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini-PSSN. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bi. Anne Kabagambe akikagua bidhaa zilizotengenezwa na Walengwa wa TASAF mtaa wa Keko Machungwa,Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DuniaBi. Anne Kabagambe katika picha na Walengwa wa TASAF baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato kkupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini. 

MAKUNDI YA UCHAGUZI UKARA UKEREWE YALIIANGUSHA CCM DHIDI YA CHADEMA







Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (katikati) akiteta jambo na Katibu wa Wilaya ya Ukerewe Peter Mashenji, wakiwa kwenye kivuko cha MV. Ukara wakielekea kwenye ziara ya kikazi kisiwani Ukara wilayani Ukerewe jana.Kulia ni Diwani wa Viti Maalum Ukara Fausta Masondole.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na wanachama wa CCM (hawapo pichani) wa Kata ya Bwisya Tarafa ya Ukara wilayani Ukerewe jana.


Wana CCM wa Kata ya Bwisya, Ukara katika Wilaya ya Ukerewe (kulia) wakimsikiliza Katibu wa Chama wa Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, (kushoto) wakati wa ziara ya kikazi kisiwani humo jana.




Salum Kalli ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, akisisitiza jambo alipokutana na wana CCM wa Kata ya Bwisya Ukara katika Wilaya ya Ukerewe jana.

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Bwisya Ukara pamoja na watumishi wa serikali wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli aliyesimama  kushoto.


Wana CCM wa Kata ya Nyamanga katika tarafa ya Ukara (kulia) wakismikiliza Katibu wa Chama Mkoa wa Mwanza Salum Kalli (kushoto) alipofanya ziara ya kikazi jana kwenye kata hiyo wilayani Ukerewe.



Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli akisistiza jambo alipozungumza na wana Chama wa Kata ya Nyamanga jana wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Kanisa Katoliki, Nyamanga Parish jana.


Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli, akisaini kitabu cha wageni katika Kata ya Bukiko Ukara jana alipokwenda kwa ziara ya kikazi kisiwani humo.Kata ya Bukiko mwaka 2015 iliangukia mikononi mwa CHADEMA baada ya mgombea wake Josephat Mkundi ambaye amerudi CCM kushinda kwenye uchaguzi kwa nafasi ya ubunge na udiwani.Anayeshudia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Januari Magati (kulia)

Wana Chama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwemo watumishi wa serikali Kata ya Bukiko katika Tarafa ya Ukara wilayani Ukerewe, wakimsikiliza Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli (hayupo pichani) jana.


Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli, akizungumza na wana Chama wa Kata ya Bukiko (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa cha Ukara jana.Kulia ni Januari Magati ambaye ni mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo.



Katibu wa CCM wa Wilaya ya Ukerewe Peter Mashenji akizungumza na wana CCM wa kata ya Bukungu katika Tarafa ya Ukara jana usiku.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli, akizungumza na wanachama katika Kata ya Bukungu wakiwemo watumishi wa serikali jana usiku katika ziara ya kikazi kwenye kata hiyo wilayani Ukerewe.

Picha zote na Baltazar Mashaka

NA BALTAZAR MASHAKA, UKARA
MAKUNDI ya viongozi wasaka vyeo wakiwemo wanachama  ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Ukerewe, yaliigharimu kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu wa 2015.Imebainika

Pia wana CCM na wananchi wa Kisiwa cha Ukara na wa Wilaya ya Ukerewe kwa ujumla wao walipokea na kubeba msiba usio wao uliosababisha baadhi ya vitongoji, vijiji,kata na Jimbo la Ukerewe kuangukia mikononi mwa chama wasichokijua undani wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu MKuu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli, alipozungumza kwa nyakati tofauti na wana CCM wa kata nne za Bwisya,Nyamanga, Bukiko na Bukungu kisiwani Ukara.

Alisema kwenye chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa 2015 CCM iliangushwa na makundi ya wasaka vyeo waliokosa kura kutosha, kwenye uchaguzi wa ndani hivyo walinuna na kugeuka makuwadi wa CHADEMA na kusababisha  CCM ikapoteza jimbo, baadhi ya kata, vijiji na vitongoji.

Alisema wanachama wa CCM wenyewe waliamua kuwapa kura CHADEMA wakishirikiana na wananchi wasio wana CCM kuuza jimbo kwa kumchagua mgombea wa CHADEMA ambaye hata hivyo alipokosa pa kuzikia msiba huo aliamua kuwaachia mliomsaidia kuubeba na kurejea CCM.

Kalli alidai CCM iliadhibiwa na wanachama wake walioshindwa kwenye kura za maoni kwa msemo wa bora tukose wote akaonya mwaka huu asitokee mtu ambaye  kura hazitatosha aseme bora amwage mboga, yeye abaki na ugali, cha moto atakona kwa dhamana waliyo nayo wana CCM ni vitendo si maneno.

Katibu huyo wa CCM Mkoa aliwataka wanachama wa  Chama Cha Mapinduzi  na wananchi wa Kisiwa cha Ukara pamoja na Wilaya ya Ukerewe kutofanya makosa yaliyopita ya kukumbatia makundi ya wasaka vyeo badala yake washikamane na CCM kwa kuchagua watu wa kuwaletea maendeleo na kuachana na wasaka vyeo.

“Simlaumu Mbunge, kura alizopata wana CCM walimpa wenyewe kwa sababu ya makundi ya wale ambao kura hazikutosha.Walihangaika na kuwa makuwadi wa vyama vingine, mchana walikuwa CCM,jioni NCCR-Magauni (Mageuzi) usiku CHADEMA.Ndiyo yaliyotokea Bukiko Ukara na Ukerewe,”alisema Kalli.

Alisistiza kuwa misiba waliyoibeba ya kuchagua wagombea nje ya CCM ilisababisha Mbunge huyo wa CHADEMA Josephat Mkundi aliuachia msiba huo katikati ya safari baada ya kubaini alidanganywa akajiunga na CCM.

“Nguvu kubwa ya wana CCM ilimsaidia kumbeba Joseph Mkundi kushinda Ubunge Ukerewe lakini kwenye tukio la ajali hakuna kiongozi wa chama chake alishiriki na kujikuta akipwaya.Pia kasi ya maendeleo ya Rais John Magufuli na nguvu kubwa CCM iliyombeba,aliamua kujiunga na timu ya kuleta maendeleo,”alisema Kalli.

Aidha, baadhi ya wana CCM akiwemo Mwenyekiti wa Kata ya Nyamagana walisema kuwa makundi yanayotokana na uchaguzi wa ndani bado yapo ili kushinda lazima makundi hayo yaliyokigharimu Chama 2014 na 2015  yatafutiwe dawa na yavunjwe, kwani tunahitaji maendeleo ili kupiga hatua.

Pia walisema wana CCM si wavumilivu, ni wagumu wa kutafuta kura zingine kutoka nje lakini pia uhusiano duni ndani na nje ya CCM, kuishi kwa kujibagua na kujitenga na jamii ni changamoto. ssss

KAMPUNI YA PUMA YATOA ZAWADI KWA SHULE NA WANAFUNZI WALIOSHINDA MASHINDANO YA UCHORAJI WA MICHORO YA ELIMU YA USALAMA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti wa  Taifa  wa Baraza  la  Usalama  Barabarani  Nchini, Mhandisi  Hamad Masauni (katikati), Mkurugenzi Mtendaji  wa  Kampuni  ya  Mafuta  ya Puma, Dominic  Dhanah (watatu  kushoto)  na Mrajisi  wa  Jumuiya  sisizo za  Kiserikali  Zanzibar, Ahmed  Khalid  Abdullah (watatu kulia) wakikabidhi  mfano  wa  Hundi  ya  Shilingi  Milioni  Nne  kwa  Uongozi  wa Shule  ya Msingi  Mkunazini  baada  ya  mwanafunzi Raya Zubeir Hemed(kulia), kuibuka  mshindi wa  kwanza  kwenye  Shindano  la  Uchoraji  wa  Michoro  ya  Elimu  ya Usalama Barabarani  kwenye  hafla  iliyofanyika  Visiwani  Zanzibar.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti wa  Taifa  wa Baraza  la  Usalama  Barabarani  Nchini, Mhandisi  Hamad Masauni, akimpa zawadi mwanafunzi wa Shule  ya Msingi Mkunazini, Saidat Jumbe zawadi baada ya kujibu swali lililohusiana na Kanuni za Uvukaji wa Barabara ili kuepuka ajali.Hafla hiyo  iliyoandaliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma ya kukabidhi zawadi  kwa washindi wa Shindano  la  Uchoraji wa  Michoro  ya  Elimu  ya Usalama  Barabarani  iliyofanyika  Visiwani  Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi, ambae  pia  ni  Mwenyekiti wa  Taifa  wa Baraza  la  Usalama  Barabarani  Nchini, Mhandisi  Hamad Masauni, akimkabidhi kikombe mshindi wa kwanza  wa Shindano  la  Uchoraji  wa  Michoro  ya  Elimu  ya Usalama Barabarani  mwanafunzi wa Shuke ya Msingi Mkunazini Rayah Zubeir Hemed.Kulia  ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya  Puma,Dominic Dhanah.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya  Puma,Dominic Dhanah, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili Salum Ali Khatib baada ya kushika nafasi hiyo katika  Shindano  la Uchoraji  wa  Michoro  ya  Elimu  ya Usalama  Barabarani  lililodhaminiwa na kampuni hiyo.Hafla hiyo imefanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mrajisi wa  Jumuiya  sisizo za  Kiserikali  Zanzibar, Ahmed  Khalid  Abdullah akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kisiwandui,Salma Ali Seif baada ya kujibu swali lililohusiana na usalama barabarani, wakati wa Hafla iliyofanyika Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.