MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku almaarufu 'Musukuma' amewaomba watanzania kusimama pamoja kuhakikisha Serikali inamaliza bila hasara kesi ya kushikiliwa moja ya ndege zake nchini Afrika ya Kusini.
Hatua hiyo inakuja saa chache baada ya kundi la Wananchi wameandamana hadi ubalozi wa Afrika kusini jijini Dar es salaam kushinikiza nchi hiyo kuiachia ndege ya ATCL inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama.
Aidha Musukuma amesikitishwa na vitendo vya baadhi ya Watanzania wanaofurahia jambo hilo kana kwamba ndege inayoshikiliwa ni mali ya mtu binafsi ile hali ni mali ya Taifa.
"Inavyoonekana mtaani ni kama imekamatwa ndege binafsi ya Mhe. Rais Magufuli, napenda kuwaambia watanzania wenzangu, wazalendo iliyokamatwa ni ndege yetu, mali yetu watanzania, iliyonunuliwa kwa kodi zetu na hiki ni kilio chetu" alisema Mbunge huyo wa Geita Vijijini kwa tiketi ya CCM
Musukuma amesema analijua 'genge la waovu' wanaoshiriki kuchochea yote haya na ameapa kwa kusema kuwa muda utakapofika atawataja mmoja baada ya mwingine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.