ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2019

SIKU YA KWANZA UTEKELEZAJI AGIZO KWA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI MWANZA YAFANYA HILI


Mongella ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaodhani inauzwa kwa gharama kubwa akisema nayo itashuka bei kama ilivyokuwa mifuko ya "Rambo" ambayo wakati inaanza kutumika ilikuwa ikiuzwa kwa gharama kubwa na baadae ikashuka.

Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza na kwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala ambapo wananchi na wafanyabiashara wamehimizwa kuendelea kusalimisha mifuko ya plastiki katika ofisi mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi amewahimiza wananchi wa Wilaya hiyo kuwa watiifu kutekeleza katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesema utekelezaji wa zoezi hilo utazingatia sheria hivyo wananchi waondoe hofu kwani zoezi hilo halitamuonea mtu yeyote na kwa wale ambao bado wana mifuko ya plastiki waendelee kuipeleka katika ngazi husika kama ilivyoelekezwa.
Afisa Mkaguzi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Abel Sembeka akizungumza wakati wa zoezi hilo ambapo amesema matumizi ya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa ni ile inayohusisha vibebeo kama vile "Rambo" na kwamba mifuko ya plastiki ya vifungashio kama karanga, binzari na miwa bado haijazuiliwa.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana, akitoa salamu zake kwenye zoezi hilo ambapo amesema Serikali itasimamia katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuzingatia sheria hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya Serikali yao sikivu.
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia zoezi la kuhamasisha katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki.
Wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wakifuatilia zoezi hilo.
Wadau wakiwa kwenye zoezi hilo.
Viongozi wa dini, wafanyabiashara wadogo na wananchi wakifuatilia zoezi hilo.
Wananchi na viongozi mbalimbali wa dini wakinyoosha mikono kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionyesha mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira inayopaswa kutumika.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya viongozi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akimsikiliza mmoja wa akina mama wanaouza mifuko mbadala jijini Mwanza ambapo Mongella amesema baada ya muda mfupi ujao, mifuko hiyo itaanza kuuzwa kwa gharama nafuu baada ya wafanyabiashara wakubwa kumaliza taratibu za kuitoa bandarini.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Meneja wa kiwanda cha Falcon kilichopo jijini Mwanza akionyesha baadhi ya bidhaa ikiwemo mbao zinazotengenezwa kwa kutumia mifuko ya plastiki ambapo amewahamasisha wananchi kukusanya mifuko hiyo na kwenda kuiuza kiwandani hapo badala ya kuitapanya ovyo na kuharibu mazingira.
Baadhi ya wajasiriamali wakisalimisha mifuko ya plastiki kwenye zoezi hilo ambapo kampuni ya kufanya usafi ya GreenWestPro ilitumia zoezi hilo kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kusalimisha mifuko ya plastiki.
Zoezi la kusalimisha mifuko ya plastiki likiendelea jijini Mwanza.
Wananchi wameshauriwa kusalimisha mifuko ya plastiki katika ngazi husika ikiwemo ofisi za Serikali za Mitaa badala ya kuitapanya ovyo na hivyo kuhatarisha mazingira.
Kampuni ya GreenWestPro ni mdau mkubwa wa mazingira ambapo inafanya shughuli zake za usafi na utunzaji wa mazingira katika majiji matatu nchini ambayo ni Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.
Kampuni ya GreenWastePro imetumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki na kujikita kwenye matumizi ya mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.

NEMC KUPIGA MZIGO HADI JUMAPILI.



Watendaji  wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (Nemc) wametakiwa kutokuwa na mapumziko siku ya kesho badala yake waende sokoni, madukani na magengeni kufuatilia utekelezaji wa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ameyaswema  hayo leo wakati akizungumza na wakazi wa Wilaya Temeke kwenye viwanja vya Zakhem Mbagala kuhusu utekelezaji wa katazo hilo.

Utekelezaji katazo la mifuko ya plastiki limeanza leo baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutangaza Bungeni kutangaza ifikapo Juni mosi mifuko ya plastiki haitakiwi kutumia na kosa kuingiza, kusambaza, kuzalisha na kuiuza.

Kabla ya kuzungumza na wananchi hao, Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli alifanya ziara ya kutembelea eneo la Kariakoo na kuzungumza na wafanyabiashara mbalimbali kuhusu matumizi ya mifuko mbadala.

"Mtanisamehe sana kesho hakutakuwa na mapumziko  wala sherehe baada jambo hili kuonyesha mafanikio. Msione kazi imeisha mambo ndio kwanza yameenza.

TANZIA: AJALI YAMPOTEZA MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL



Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Sevilla Jose Antonio Reyes, amefariki kwa ajali ya gari leo asubuhi. Ajali imeripotiwa kutokea eneo la Utrera nje kidogo ya mji wa Seville. Reyes mwenye miaka 35, alikuwa akichezea Extremadura inayoshiriki ligi daraja la kwanza Hispania.

WABUNGE WENYE NONGWA CCM WAONYWA.


CCM imesema wabunge wa chama hicho aliowaita wenye nongwa  kila Serikali inapotatua matatizo mbalimbali, ikiwemo kununua korosho watakuwa na hali ngumu 2020.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametoa kauli hiyo leo katika mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaotarajiwa kumaliza elimu ya juu mkoani Mtwara, Ambapo amewataka Wabunge kutafuta kazi nyingine.

Amesema wabunge wanaofanya hivyo wanapaswa kujipanga mapema, “Kama wewe ni CCM na unashiriki nongwa kwa jambo hili ambalo tumelifanya kwa uchungu mkubwa jipange mapema.”

“Jipange kwa sababu mimi na wenzangu kuanzia sekretarieti, kamati kuu na halmashauri kuu tupo kitu kimoja tumeweka mustakabali sawa kulinda utu na heshima ya wakulima.”

RAIS MSTAAFU MWINYI AKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI KURANI KIKWAJUNI

 Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Kumi na Tano, Abdallah Hassan, akibeba zawadi ya televisheni aliyokabidhiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (watatu kushoto), wakati wa fainali za mashindano yaliyofanyika leo  katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Mpigapicha Wetu
 Rais  Mstaafu  wa  Awamu  ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi  Mshindi  wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah  wakati  wa fainali za mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja  vya  Mapinduzi, Visiwani  Zanzibar.Wakwanza  ni  Mbunge wa  Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi  Hamad Masauni. Picha na Mpigapicha Wetu
 Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya  Abdallah akisoma  Kurani  wakati  wa  mashindano  hayo  yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.Picha na Mpigapicha Wetu
 Mbunge  wa  Jimbo  la  Kikwajuni, Mhandisi  Hamad  Masauni (kulia), akimkabidhi  zawadi  Mgeni Rasmi  katika  Mashindano  ya  Kuhifadhi  Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji  Ali Hassan  Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.Picha na Mpigapicha Wetu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Mjiini, Twalib Ali Twalib  akikabidhi msaada  wa  vitabu  vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani  Zanzibar  kwa  Mgeni Rasmi  katika  Mashindano  ya  Kuhifadhi Kurani, Rais  Mstaafu  wa  Awamu  ya  Pili, Alhaji  Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano  ya  Kuhifadhi  Kurani  yaliyofanyika  leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor JazzeraPicha na Mpigapicha Wetu

Friday, May 31, 2019

HAZINA YAKABIDHIWA KILO 324.96 ZA DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 27 NA FEDHA TASLIMU MILIONI 305



Kilo 325 ya dhahabu, fedha taslimu Sh305 milioni na magari mawili yaliyotaifishwa na Mahakama baada ya washtakiwa kutiwa hatiani kwa makosa ya rushwa na kusafirisha dhahabu kinyume cha sheria imekabidhiwa Hazina.


Makabidhiano hayo yamefanyika leo Mei 31, 2019 jijini Mwanza baina ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), Biswalo Mganga na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango aliyewakilishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khatibu Kazungu.



Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Biteko amewasihi wachimbaji na wafanyabiashara wa madini nchini kuachana na utoroshaji wa madini kwani biashara hiyo kwa sasa ni zilipendwa hivyo wafanye shughuli zao kwa kuzingatia sheria.


`



Naye DPP Biswalo Mganga amesema mali zilizotaifishwa ni Dhahabu kilo 324.96 yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 27, Fedha taslimu shilingi milioni 305, Mzani wa kupimia ubora wa madini, mizani ya kupimia madini pamoja na magari mawili ambapo vyote kwa pamoja vilikamatwa mwezi Januari mwaka huu wilayani Sengerema. Aidha ameongeza kwamba dhahabu kilo tano iliyokamatwa mkoani Geita nayo imekabidhiwa Serikalini baada ya kutaifishwa pia.


Baada ya kupokea mali hizo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Khatibu Kazungu ametoa shukrani kwa mamlaka zote zilizofanikisha kukamatwa, kutoa ushahidi na kutaifishwa na kwamba zitatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Thursday, May 30, 2019

SERIKALI YANUSURU ANGUKO LA BEI YA PAMBA


MWANZA. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ana imani kuwa ununuzi wa zao la pamba utaanza mara moja kwa bei ya sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo. Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya bei kwa takriban ya wiki nne tangu bei elekezi ilipotangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga kwamba bei hiyo ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019.

Alikuwa akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao cha dharura kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Kilimo na Viwanda, Makatibu Wakuu wa Kilimo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na  Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Wengine ni wawakilishi wa Wabunge wa mikoa hiyo, Makatibu Tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya zote za mikoa hiyo, na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hizo. Pia kilihudhuriwa na wanunuzi wa pamba, wakulima na maafisa wa benki kadhaa.

Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali bado inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuwakutanisha wadau wa mazao ya kibiashara ili yaweze kuwa na tija kwa wakulima. Alisema kazi hiyo inafanywa wa Wizara ya Kilimo. Mazao hayo ni pamba, chai, kahawa, korosho, tumbaku na chikichi.

Pia alisema Bodi ya Pamba iachiwe jukumu la kutoa leseni za ununuzi wa zao hilo na kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wakifanya kazi hiyo waache mara moja.

Mwenyeji wa Kikao hicho Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akiongoza utaratibu wa uwasilishaji mijadala kwa wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini hapa.
Mfanyabishara mkongwe Mzee Christopher Mwita Gachuma akiwakilisha maoni ya wafanyabishara katika kusanyiko hilo la wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini
Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicha cha dharura....
Kuhusu ubora wa pamba, Waziri Mkuu alitaka wananchi waelimishwe ili waache kuweka maji au mchanga kwenye pamba kwa minajili ya kuongeza uzito kwani kwa kufanya hivyo wanachafua jina la Tanzania pindi inapopelekwa kuuzwa nje ya nchi.
Pia alitaka vyama vikuu vya ushirika vijiridhishe kuhusu ubora wa maghala ya kuhifadhia pamba kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia wakulima wauze mapema pamba yao mara baada ya kuivuna.

DIKTETA ADOLF HITLER: KIJANA KATILI ALIYEFELI SHULE, LAKINI AKATAWALA DUNIA.


Adolf Hitler katika maisha yake hasa mwaka 1906 alitamani sana kuwa msanii na alianza kupeleleza nafasi za kusomea uchoraji, na Ilipofika mwaka 1907 aliomba kujiunga katika chuo cha sanaa mjini Vienna, lakini nako alishindwa tena. #HISTORIAYAADOLFHITLER Baada ya Kifo cha Mama yake Desemaba 1907, Hitler aliishi maisha ya kuhama hama na ilipofika Januari 1908, Hitler alianza kutumia urithi wa mama yake aliyefariki kwa ugonjwa wa Saratani kuhamia Vienna alipokaa hadi 1913.

HISTORIA YA CHIFU MKWAWA / WAZUNGU WANAYOIFICHA!


HISTORIA YA CHIFU MKWAWA / WAZUNGU WANAYOIFICHA! Wahehe walimuita Mkwawa mtwa, waswahili wakamuita mfalme, Unyanyembe wakamuita mtemi, waha wakamuita Mwami na shuleni tukamuita Chifu Mkwawa, mwanaume pekee aliyewanyoa nywele wazungu bila maji. Huyu mwanaume kiboko ya Wajerumani ni uzao wa yule jiniazi kutoka nchi ya Uhabeshi, Ethiopia ya leo, aliyefika katika ufalme wa Mwamududa miaka 1700 akiwa na teknolojia ya kuwinda kwa mbwa.

RAIS MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA ZIMBABWE.




Rais John Magufuli arejea nchini kutoka Zimbabwe ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jen.  Venance Mabeyo.

Utakumbuka May 28 mwaka huu ndipo Rais Magufuli aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe Jijini Harare nchini Zimbabwe na kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa.
Rais Magufuli akiwa nchini Zimbabwe 

Serikali yakanusha kuwalazimisha wafanyakazi wake kuwa na laini ya TTCL





Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema hakuna agizo la Serikali linalolazimisha mfanyakazi wa Serikali kuwa na laini ya TTCL isipokuwa viongozi wanaowekewa vocha za Serikali kwamba ni muhimu kuwa na laini hizo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo amesema taarifa inayosambaa kwenye mitandao kuhusu hilo ni ya upotoshaji na kuwataka wananchi kuipuuza.

"Hakuna agizo la serikali linalolazimisha mfanyakazi wa serikali kuwa na laini ya TTCL, isipokuwa viongozi wanaowekewa vocha za serikali ni muhimu kuwa na laini hizo." amesema.

 Chini taarifa hiyo iliyokanushwa.



MWANZA. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ana imani kuwa ununuzi wa zao la pamba utaanza mara moja kwa bei ya sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo. Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya bei kwa takriban ya wiki nne tangu bei elekezi ilipotangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga kwamba bei hiyo ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019.

Alikuwa akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika hapo jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Kilimo na Viwanda, Makatibu Wakuu wa Kilimo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na  Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Wengine ni wawakilishi wa Wabunge wa mikoa hiyo, Makatibu Tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya zote za mikoa hiyo, na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hizo. Pia kilihudhuriwa na wanunuzi wa pamba, wakulima na maafisa wa benki kadhaa.

Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali bado inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuwakutanisha wadau wa mazao ya kibiashara ili yaweze kuwa na tija kwa wakulima. Alisema kazi hiyo inafanywa wa Wizara ya Kilimo. Mazao hayo ni pamba, chai, kahawa, korosho, tumbaku na chikichi.

Pia alisema Bodi ya Pamba iachiwe jukumu la kutoa leseni za ununuzi wa zao hilo na kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wakifanya kazi hiyo waache mara moja.

Kuhusu ubora wa pamba, Waziri Mkuu alitaka wananchi waelimishwe ili waache kuweka maji au mchanga kwenye pamba kwa minajili ya kuongeza uzito kwani kwa kufanya hivyo wanachafua jina la Tanzania pindi inapopelekwa kuuzwa nje ya nchi.

Pia alitaka vyama vikuu vya ushirika vijiridhishe kuhusu ubora wa maghala ya kuhifadhia pamba kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia wakulima wauze mapema pamba yao mara baada ya kuivuna.

Wednesday, May 29, 2019

Four Ways na Girls Queens kuingia kambini rasmi kujiandaa na Castle Africa 5s 2019.




Balozi wa Castle Lager  Africa 5s, Ivo Mapunda (kushoto) akizungumza na wachezaji wa timu ya Four Ways Fc ya Kinondoni na Girls Queens ya Msimbazi Kariakoo zinazo wakilisha nchi kwenye fainali za mashindano ya Castle Africa 5s wakati wa uzinduzi wa Kambi maalumu ya maandalizi  wa mashindano hayo yanayo tarajiwa kufanyika Juni 7 na 8,2019 katika Uwanja Taifa wa Zamani jijini Dar esSalaam.

 Jumla ya Nchi nane(8) zinatarajiwa kushiriki fainali hizo mwenyeji akiwani Tanzania.


Wachezaji wa Four Ways Fc  ya Kinondoni na Girls Queens ya Msimbazi Kariakoo zote za jijini Dar es Salaam wakifanya mazoezi wakijiandaa na fainali za mashindano ya Castle Africa 5s yanayotarajiwa kufanyika Juni 7 na 8,2019 katika Uwanja Taifa wa Zamani jijini Dar esSalaam. Jumla ya Nchi nane(8) zinatarajiwa kushiriki fainali hizo mwenyeji akiwa ni Tanzania.



Four Ways na Girls Queens kuingia kambini rasmi kujiandaa na Castle Africa 5s 2019.
Na Mwandishi Wetu.

TIMU Four Ways Park Fc yenye makazi yake Kinondoni jijini Dar es Salaam na Girls Queens yenye makazi yake Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam wameingia kambini leo rasmi kujiandaa na mashindano ya Castle Africa 5s(5 – aside) yanayotarajia kuanza kutimua vumvi Juni 7 na 8,2019 katika Uwanja wa Taifa wa Zamani(Shamba la Bibi) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Balozi wa Castle Lager Africa nchini Tanzania, Ivo Mapunda alisema timu zote ziko vizuri tayari kwa kuwakilisha Watanzania katika fainali za Kimataifa na ushindi ni lazima kulingana na maandalizi waliyonayo na watakayoendelea nayo.

Mwaka huu Tanzania tutawakilishwa na timu ya Wanaume kutoka Four Ways ya Kinondoni na timu ya Wanawake ya Girls Queens kutoka Msimbazi Kariakoo kwa ujumla timu zote ziko sawa na ziko tayari kwa fainali hizo na leo rasmi sasa wanaingia kambini kwa kujiandaa na fainali hizo.

Nae Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alizitaji Nchi shiriki zinazotarajiwa kushiriki mashindano hayo ya Africa 5s kuwa ni Africa Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lethoto, Uganda, wenyeji Tanzania na chi alikwa ya Nigeria.

Kikuli alisema Nchi hizo zikiwakilishwa na timu ya Wanaume na Wanawake zinatarajiwa kuwasili nchini Juni 5,2019 tayari kwa fainali za Castle Africa 5s.

Juni 6,2019 timu zitakabidhiwa vifaa vya michezo katika Hoteli ya Lamada jijini Dar es Saalaam tayari kwa kuanza mashindano rasmi Juni 7 na 8,2019.

Tunawaomba watanzania wapenda michezo wajitokeze kuja kuzishangilia timu zao zinazowakilisha nchi katika Fainali hizo za Castle Africa 5s.

Mwisho Kikuli alisema fainali hizo zinatarajiwa kuhudhuria na Balozi wa Castle Africa 5s, Samwel Eto’o hivyo tujitokeze kwa wingi kuja kumshuhudia mchezaji mkongwe wa Zamani pamoja na kupiga nae picha.

wameibuka mabingwa katika Bonanza kubwa la Soka  lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Posta Kijitonyama kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager na hivyo kuzawadiwa Kikombe, Medali za dhahabu, Pesa taslimu shilingi 1,500,000/=, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na kuwakilisha nchi katika fainali za Caslte Africa 5s zinazotarajiwa kufanyika mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Four Ways Park Fc waliutwaa ubingwa kwa point 7 wakifuatiwa na Jacks Pub Fckwa pont 4 ambao walizawadiwa Medali za Silva, Catoni ya bia ya Castle Lager na pesa taslimu Shilingi 900,000/=

Mshindi wa tatu ni katika fainali hizo ni Meeda Night Club Fc ambao walipata pointi 3 na hivyo kuzawadiwa medali feddha, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na pesa taslimu Shilingi 600,000/=

Akizungumza na wachezaji, waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye Bonanza hilo, Menager Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli alianza kwa kuwapongeza mabingwa Four Ways Park Fc kwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ikiwa ni mara ya pili sasa kufanyika kwa Tanzania  na akawaomba zawadi walizopata zikawe chachu ya maandalizi bora ya fainali za Castle Afica 5s ambazo zinatarajiwa kufanyika nchini Tanzania.

Kikuli pia aliwapongeza timu ya pili nay a tatu kwa ushindi na akato pongezi kwa timu shiriki zote kwa kujitoa kwao katika fainali hizo na kwa jinsi hiyo wakajiandae kwa mashindano mengine mwakani.

Pamela aliutaja mchakato ulivyokuwa wa kuzipata timu ambao ulianzia kwenye Baa 60 za jijini Dar es Salaam ambapo Bar zilishindana kwa kununua Bia za Castle Lager na kukusanya vizipo na mwisho tukapata timu 32 zilizoongoza na ndizo zimeweza kushiriki Bonanza mpaka kumpata Bingwa ambaye ni Four Ways Park Fc.

Nae Balozi wa Bia ya Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapundaaliishukuru Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kwa uratibu mzuri wa mashindano ya Castle Africa 5s mwaka huu kwani yamekuwa na hamasa ya hali ya juu na kuwaomba waendelee kudhamini mashindano hayo kwani kupitia Bonanza hili wapo waliopata marafiki na mambo mengine mengi kwa sababu ya Bonanza hili kupitia Bia ya Castle Lager ambayo imetuunganisha pamoja.