Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah wakati wa fainali za mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Mpigapicha Wetu
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya Abdallah akisoma Kurani wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.Picha na Mpigapicha Wetu
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.Picha na Mpigapicha Wetu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mjiini, Twalib Ali Twalib akikabidhi msaada wa vitabu vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani Zanzibar kwa Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani yaliyofanyika leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor JazzeraPicha na Mpigapicha Wetu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.