CCM imesema wabunge wa chama hicho aliowaita wenye nongwa kila Serikali inapotatua matatizo mbalimbali, ikiwemo kununua korosho watakuwa na hali ngumu 2020.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametoa kauli hiyo leo katika mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaotarajiwa kumaliza elimu ya juu mkoani Mtwara, Ambapo amewataka Wabunge kutafuta kazi nyingine.
Amesema wabunge wanaofanya hivyo wanapaswa kujipanga mapema, “Kama wewe ni CCM na unashiriki nongwa kwa jambo hili ambalo tumelifanya kwa uchungu mkubwa jipange mapema.”
“Jipange kwa sababu mimi na wenzangu kuanzia sekretarieti, kamati kuu na halmashauri kuu tupo kitu kimoja tumeweka mustakabali sawa kulinda utu na heshima ya wakulima.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.