|
Baadhi ya
wacheza ngoma wa kikundi cha Rugu kutoka Karagwe mkoani Kagera wakishangilia na
kitita cha Shilingi 600,000/=mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za
mashindano ya Balimi Ngoma Mkoa wa Kagera yaliyofanyika katika Uwanja wa
Kaitaba Bukoba mjini.
|
|
Baadhi ya
washiriki na mashabiki wa Balimi Ngoma wakishuhudia fainali za mashindano ya
Ngoma mkoa wa Kagera yaliyofanyika
katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mjini.
|
Kikundi cha Ngoma cha Rugu-
Karagwe chatwaa ubingwa wa Mkoa Balimi Ngoma Kagera.
FAINALI
za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulikanazo kama “Balimi Ngoma Festival
2014” Mkoani Kagera kikundi cha Rugu chenye makazi yake Karagwe kimefanikiwa kuwa au bingwa wa Mkoa wa Kagera na kuzawadiwa fedha taslimu Shingi
600,00/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Kagera katika fainali za Kanda
zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014 Mkoani Mwanza.
Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Kikundi
cha Rugolo ile cha mjini Bukoba ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa katika fainali za Kanda.
Nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi
cha Abagambakamo cha Muleba ambacho kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Alute Continue
ambacho kilizawadiwa fedha taslimu shilingi 300,000/=.
Nafasi ya tano mpaka ya kumi ilichukuliwa na Uviti Ruzinga, Chupukizi, Kasharu, Kabete
cha Ihangilo, Jipe Moyo na Upendo Musira hivi vilizawadiwa kifuta jasho cha 150,000/=
kila kikundi. Jumla ya Vikundi 11 vilijitokeza kushiriki fainali hizo za Mkoa wa Kagera ngazi ya Mkoa kwa Mwaka
2014.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa
Kanda yaZiwa, Erick Mwayela alisema Sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano
ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni
sehemu yao ya kurudisha fadhila kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra
Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
Fainali za Mkoa wa Kagera zilifanyika katika Uwanja wa
Mkoa wa Kaitaba na fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa
kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza kwa kushilikisha vikundi viwili viwili
kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma
na Wenyeji wa mashindano Mwanza.