ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 14, 2017

"ULIZENI TENA KWANINI NILIMKABIDHI BENDERA DIAMOND" WAZIRI NAPE

DAR ES SALAAM: Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye January 11, 2017 alimkabidhi nyota wa Afro Pop, Diamond Platnumz bendera ya Taifa ili kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye ufunguzi rasmi wa mashindano ya Africa Cup of Nation (AFCON) iliyofunguliwa Januari 14, 2017 nchini Garbon hivi karibuni.
Waziri Nape alisema haya siku ya kumkabidhi Diamond bendera ya taifa:

“Siku ya leo nina furaha  kumuaga ndugu yetu Diamond na kundi lake amabapo wamepata fursa ya kuipeperusha bendera ya nchi yetu kwa dunia nzima.

“Kama nilivyosema kuwa AFCON ni mashindano makubwa na yanaangaliwa na dunia nzima kwa hiyo kwa tukio hili inaonyesha ni jinsi gani sanaa yetu ya Tanzania imekuwa kubwa ndio maana leo nipo hapa kwa niaaba ya Serikali kumpongeza Diamond na kumkabidhi bendera ya Tanzania.‘” alisema Nape.
Wakati pazia la michuano hiyo likifunguliwa, ufunguzi huo uliambana na burudani kabambe ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa Afrika na nje ya Afrika. Diamond alitumbuiza kuiwakilisha nchi huku akiwa amevalia sare na wacheza shoo wake iliyoandaliwa kwa rangi za bendera ya taifa.

Baada ya uzinduzi huo kufanyika Waziri Nape ameandika haya katika mtandoa wa ‘Twitter’

“Ulizeni Tena Kwanini Nilimkabidhi Bendera Diamond”aliandika Waziri Nape



MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMPIGA MTOTO WAKE HADI KUFARIKI DUNIA WILAYANI ILEMELA.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 14.01.2017



·         MWANAMKE MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMPIGA MTOTO WAKE HADI KUFARIKI DUNIA WILAYANI ILEMELA.


KWAMBA TAREHE 11.01.2017 MAJIRA YA SAA 10:00HRS ASUBUHI KATIKA MTAA WA NSUMBA KATA YA KISEKE WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MWANAMKE MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JOYCE MATHAYO MIAKA 33, MKAZI WA MTAA WA NSUMBA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMPIGA FIMBO MTOTO WAKE AITWAYE MATHAYO MANIS MIAKA 12, MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUFARIKI DUNIA KWA KOSA LA UTORO SHULENI KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

INADAIWA KUWA SIKU YA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAREHEMU ALIMKATALIA MAMA YAKE KWENDA SHULE AKIDAI KUWA YEYE HATAKI TENA SHULE, NDIPO MAMA YAKE ALIPATWA NA HASIRA NA KUAMUA KUMPA ADHABU YA KUMCHAPA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE, NDIPO GHAFLA ALIBADILIKA HALI YAKE YA AFYA NA KUFARIKI DUNIA MUDA MCHACHE BAADAE, WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA MAPEMA ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.
MTUHUMIWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI HOSPITALI YA MKOA WA SEKOU TOURE TAYARI KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/ WALEZI AKIWATAKA WAWALEE WATOTO WAO KATIKA MAADILI MEMA NA NIDHAMU HUKU WAKIWAELIMISHA MAMBO MAZURI NI YAPI NA MABAYA, ILI KUEPUSHA ADHABU ZA VIPIGO KWA MTOTO PINDI ANAPOKOSEA ZITAKAZO PELEKEA MAJERA AU VIFO KAMA TUKIO HILI LILILOTOKEA KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

 ·         WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA UHALIFU WA NJIA YA MTANDAO WILAYANI ILEMELA

MNAMO TAREHE 11.01.2017 MAJIRA YA 17:00HRS JIONI KATIKA HOTELI IITWAYO KINGDOM HOTEL ILIYOPO ENEO LA KONA YA BWIRU WILAYA YA ILEMELA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU WANAWAKE WAWILI NA MWANAUME MMOJA WALIOJULIKANA KWA MAJINA YA 1. EVELIN SILYVESTER MIAKA 39 MKAZI WA TABATA DAR ES SALAAM, MRANGI, 2.BEATRICE MATABA, MIAKA 36, MKEREWE MKAZI WA TABATA DAR ES SALAAM, NA 3.FITINA MILCHAEDES MIAKA 42, MUHA, MWANAMUME NA MKAZI WA BUSERESERE MKOANI GEITA, WOTE WAFANYA BIASHARA, WANASHIKILIA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTOA HUNDI HEWA KWA WAFANYABIASHARA WENYE MADUKA MAKUBWA NA MAKAMPUNI HAPA JIJINI MWANZA KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA JUU YA UWEPO WA WATU HAPA JIJINI MWANZA WANAOFANYA UHALIFU KWA NJIA YA MTANDAO KWA KUTOA HUNDI HEWA KWA WAFANYA BIASHARA WENYE MADUKA MAKUBWA NA MAKAMPUNI NA KUCHUKUA BIDHAA ZAO KISHA KUZIHIFADHI KATIKA STOO YAO NA BAADAE KUZIUZA.

ASKARI WALIFANYA UPELELEZI KUHUSIANA NA TAARIFA HIZO NA KUFANIKIWA KUWAKATA WATUHUMIWA WOTE WATATU KATIKA HOTELI TAJWA HAPO JUU, AIDHA KATIKA MAHOJIANO NA ASKARI WATUHUMIWA WALIKIRI KUHUSIKA KATIKA UHALIFU HUO WA MTANDAO KISHA WAKAWAPELEKA ASKARI KWEYE STOO ZAO ZILIZOPO MAENEO YA NYAMANORO WILAYANI IELEMELA AMBAPO ZILIKUTWA BIDHAA MBALIMBALI AMBAZO NI MABATI BUNDLE 20 ZA GEJI 30 YENYE THAMANI YA TSH 9,600,000/=, KATONI 75 ZA SABUNI YA UNGA AINA YA KLEED YENYE THAMANI YA TSH 6,200,000/=, PAMOJA NA MAFUTA YA KUJIPAKA AMBAYO THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.

POLISI WANAENDELEA NA UPELELEZI ILI KUPATA MTANDAO WA WAHALIFU HAWA  LAKINI PIA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA AMBAO TAYARI WAMEKAMATWA KWANI UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA WATUHUMIWA WAMEFANYA UHALIFU WA AINA KAMA HII MKOANI GEITA, MOROGORO NA MAENEO MENGINE, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI ILI WAHALIFU WAWEZE KUKAMTWA MAPEMA KABLA MADHARA MAKUBWA HAYAJATOKEA KWA WANANCHI, LAKINI PIA ANAWATAKA WAMILIKI WA NYUMBA ZA WAGENI KUTOA TAARIFA POLISI PINDI WANAPOPOKEA WAGENI AMBAO WANAWATILIA MASHAKA. AIDHA ANAWAKUMBUSHA WAFANYA BIASHARA KUWA MAKINI NA WAHALIFU WA AINA KAMA HII AMBAO WAMEJITOKEZA KATIKA MKOA WETU WA MWANZA.
IMETOLEWA NA,
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

BENKI YA NMB WACHANGIA UJENZI WA SKULI YA MSINGI NGAMBWA KISIWA CHA UZI WILAYA YA KATI UNGUJA.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Dunga.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (mwenye koti) akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya msingi Ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, mwenye tai kulia Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji na kushoto kwa Mwakilishi Sheha wa Ngambwa Ndg. Amour Ali Mussa na Mratibu wa Shughuli za Serikali SMZ  Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Khamis Foum. hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi Kilimo Gunga Wilaya ya Kati Unguja.

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja na kutowa shukrani kwa msaada wao huo kutowa kwa ajili ya jamii kuwapatia watoto wao majengo ya skuli katika eneo lao. Benk ya NMB itejenga jengo la Skuli hiyo katika Kijiji cha Ngambwe Uzi.

Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Waziri Barnabas akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya kati Unguja kuhusuana na kuguswa kwa hali ya kijiji hicho cha ngambwa watoto kupata elimu yao ya msingi masafa marefu na makazi yao. kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Ungja. 
 Afisa Elimu Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji, akitowa shukrani kwa uongozi wa Benk ya NMB kwa msaada wao huo kuwakumbuka Wakazi wa Ngambwa kuwapatia msaada kwa ajili ya kumalizia jengo la Skuli yao ya Msingi. ilioazwa msingi na wananchi wa kijiji hicho. 
Mratibu Shughuli za Serikali ya SMZ Wilaya ya Kati Unguja Ndg Khamis Foum akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi. na kutowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu kwa msaada wao kufanikisha shughuli hiyo ya ujenzi wa Skuli hiyo kuwapunguzia masafa marefu watoto wa ngambwa kufuati masomo katika eneo la uzi.
Maafisa wa Benk ya NMB wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakishuhudia hafla hiyo ya makabidhiano.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi zawadi ya embe za boribo za muyuni Kaimu Meneja Mkuu wa NMB Waziri Barnabas, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi cheki ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa.  


Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja Mhe, Simai Mohammes Said akimkabidhi zawadi ya mananasi ya Zenj Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg Waziri Barnabas, baada ya hafla ya kukabidhi cheki shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
Imetayarishwa na OthmanMapara. Blog.
Zanzinews.com
Mob. 0777424152. Or 0715424152.  

NAIBU WAZIRI AZINDUA MAZOEZI KWA WANANCHI ILEMELA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anstazia James Wambura (wa pili kutoka kulia) akikimbia mchakamchaka huku akiwa ameambatana na DC, OCD, Mhazina wa   Manispaa ya Ilemela kuboresha afya asubuhi ya leo.
NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AZINDUA MAZOEZI YA MWILI KWA WAKAZI WA WILAYA YA ILEMELA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia James Wambura leo tarehe 14.01.2017 ikiwa ni jumamosi ya pili ya mwezi amezindua mpango wa mazoezi kwa wananchi na wakazi wa Wilaya ya Ilemela ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amewataka wananchi na wakazi wa Ilemela ambao leo waliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dr. Leonard Masale, kufanya mazoezi ya mwili kama afanyavyo Rais mstaafu wa awamu ya Pili ambaye kwa sasa ana Zaidi ya miaka 90 na amekuwa akifanya mazoezi takribani saa moja kila siku, kwani mazoezi humfanya mtu kuwa mkakamavu na pia kuzifanya seli za mwili kuufanya mwili kutozeeka/kutochoka mapema.

Tukumbuke kuwa MAZOEZI NDIYO AFYA YAKO, NA AFYA YAKO NDIYO MTAJI WAKO, hivyo ukiwa unafanya mazoezi kutakufanya uwe na afya njema itakayokufanya ushiriki kikamilifu katika shughuli zako za kila siku zinazokuingizia kipato na ndiyo maana tunasema afya yako ndiyo mtaji wako.
Ukiugua magonjwa hasa haya ambayo si ya kuambukizwa kama vile Shinikizo la damu (pressure), Kiharusi au kisukari, ni magojwa ambayo yatakufanya kutofanya kazi kwa muda mrefu lakini pia utatumia gharama kubwa kujitibu, hivyo amewataka wananchi wote kwa ujumla kuyafanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Amesema pia, serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa ya kununua madawa na kutibu wananchi wake, fedha ambayo ingeweza kuwekwa katika shughuli nyingine za kimaendeleo endapo wagonjwa wa magonjwa haya yangeweza kuepukika kwa kufanya mazoezi.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Manispaa ya ilemela na wakazi/wananchi wa Wilaya hii, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Leonard Masale, kwanza amemshukuru Naibu Waziri kwa kuzindua mpango wa mazoezi katika wilaya ya Ilemela, na kuwaelekeza watendaji wa Kata washirikiane na waheshimiwa madiwani kuwaongoza na kuwahamisha wananchi walio katika kata zao kushiriki mazoezi hasa kila jumamosi ya pili ya kila mwezi. Lakini pia amehaidi mazoezi ya mwezi ujao yatashirikisha wananchi wengi kwani leo waliojitokeza wengi ni watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, na baada ya mazoezi hayo wananchi wote watakuwa wakifanya mazoezi katika kata zao.

Pamoja nae, kamanda wa polisi wa Wilaya ya Ilemela, Mrakibu wa Polisi, Evodius Kasigwa, amesema wao polisi wamekuwa wakifanya mazoezi haya kila jumamosi ya wiki.

Mazoezi haya yalianzia katika kiwanja cha Furahisha kwa kutembea matembezi ya Kilomita 3 kwa kupitia mtaa wa Ghana, Kitangiri na kisha kurudi katika uwanja wa Furahisha na kufanya mazoezi ya viungo.

Imetolewa na:
Kizito Bahati
Afisa Michezo

Manispaa ya Ilemela.

Diamond Platnumz - GABON #AFRCON2017

 Diamond Platnumz keshatua nchini Gabon kutuwakilisha.....

MAGAZETI YA LEO: MARUFUKU KUTIMUA WANAFUNZI VILAZA, KAMBI YA LIPUMBA YAMSHTUKIA MTATIRO, MIZIGO YA ABIRIA YATEKETEA KWA MOTO UWANJA WA NDEGE DAR.


Marufuku kutimua wanafunzi vilaza, Kambi ya Lipumba yamshtukia Mtatiro, Mizigo ya abiria yateketea kwa moto uwanja wa ndege Dar. 

Kauli ya JPM nzito, Mawaziri wajifungia kujadili muungano, Sumaye adai mwisho wa CCM 2020, JPM mbinoni kutumbua magazeti mawili. Habarika na dondoo hizi hapa; 

AZAM FC NDIYO MABINGWA MAPINDUZI CUP 2017 KWA KUINYUKA SIMBA 1-0

Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.

Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.

Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.

Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.

Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.

Friday, January 13, 2017

WATANZANIA WATANO WACHAGULIWA KUWA MABALOZI WA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI DUNIANI

“BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.
Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.

Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassan Mohamed Toziri, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo. 

Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.  

Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.


https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

KADA WA CCM BUCHOSA AWASHIKA MKONO VIJANA WA KATA YA KATWE.

Awali kada huyo wa CCM aliwakabidhi mabati mia moja vijana wa kijiji cha Mwagika ili waweze kuwekeza kwenye mradi wa kuwaingizia kipato.
 NA:- ZEPHANIA MANDIA.
Wakazi wa kata ya katwe halmashauri ya wilaya Buchosa mkoani Mwanza wametakiwa kutatua changamoto zinazokikabili kituo cha afya cha mwangika ikiwemo ufinyu wa wodi ya uzazi pamoja jengo la upasuaji badala ya kuisubiri serikali.


Wito huo umetolewa na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ESTON KASIKA ambaye ameahidi kuwaunga mkono wananchi hao kwa kutoa vifaa vya ujenzi ikiwemo mbao, misumari pamoja na mabati mia moja huku akiwataka kufyatua matofali,kusomba mawe na mchanga.
 Kituo cha afya cha mwangika halmashauri ya wilaya buchosa mkoani Mwanza kinakabiliwa na ufinyu wa wodi ya uzazi pamoja na ukosefu wa huduma ya upasuaji na hivyo kuzorotesha utoaji wa huduma kwa akinamama wajawazito.

Wakizungumza na vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kata ya Katwe wameiomba serikali kuboresha utoaji wa huduma ya uzazi katika kituo hicho ili kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto vinavyotokea wakati wa kujifungua.

Kada wa chama chamapinduzi (CCM) ESTON KASIKA akiteta na wananchi wenzake.
Kwaya ya AIC Nyahunge.
Timu ya soka wakazi wa kata ya Katwe imepokea vifaa vya michezo ikiwemo mipira.
 Kilio cha wakazi hao kimemgusa kada wa chama chamapinduzi(CCM)na mkazi wa kijiji cha mwangika ESTON KASIKA ambaye amewataka wananchi kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho cha afya.

JPM AAGIZA UONGOZI WA MKOA WA SHINYANGA KUFUTA USAJILI WA MRADI WA TRIPLE S.

????????????????????????????????????
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoawa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.
Agizo hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupomkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
“Futeni usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji hakashindwa kuendesha kiwanda kwazaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha
kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.
Akizungumzia sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.
Aliongeza kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.
Rais Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene.  

NJIA 10 ZA KUPUNGUZA MAGONJWA YA KUKU

Mlipuko wa Magonjwa
Moja ya sababu za hasara kubwa kwa wafugaji ni vifo vingi vinavyotokea wakati mmoja .pindi mfugaji anapokumbwa na janga la vifo vya ndege kabla ya kufikia mwisho wa mzunguzo wa uzalishaji hivyo basi asitarajie kupata faida nzuri baada ya mauzo.


Hasara itokanayo na vifo inaweza kuepukika au kupunguzwa na kutokea kwa kiasi kidogo.Hili linawezekana,ifuatayo ni namna ya kufanikisha.

Thursday, January 12, 2017

SAMBURU RESIDENTS HOLD DEMOS TO PROTEST KILING BY ELEDPHANT.

Residents of Kirimon area in Samburu central Sub County have vowed not live with elephants in the region again. This was after elephants killed 3 people in a week. The residents held demos to protest the killing. They claimed that their efforts to have the issue resolved have not borne fruits. Laikipia Kenya Wildlife 

VIONGOZI WA MADAKTARI NCHINI KENYA KUKAMATWA.

Mgomo wa madaktari nchini Kenya.
Mahakama nchini Kenya imetoa hati ya kukamatwa viongozi wa chama cha madaktari, kutokana na kutokuwepo mahakamani wakati ikitolewa hukumu iliyowatia hatiani ya kuingilia maamuzi ya mahakama

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa wakati, serikali ya kitaifa nchini Kenya ikiendelea na jitihada za kufanya majadiliano na madaktari ili kumaliza mgomo wao uliodumaza kabisa huduma za afya katika sekta ya umma.

MABONDIA MFAUME MFAUME NA MUDDY MATUMLA WATAMBIANA KUZIPIGA FEB 5 TAIFA.

Bondia Mfaume Mfaume kushoto akitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni mratibu wa mpambano uho Chese Masanja.
Mratibu wa mpambano wa masumbwi Chese Masanja kulia akimwinua mkono juu bondia Manyi Issa kwa ajili ya kumtambulishe mbele ya wahandishi wa habari kuhusu mpambano wake wa Feb 5 na Iddi Mkwela raundi kumi utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa.

Mratibu wa mpambano wa masumbwi Chese Masanja kulia akimwinua mkono juu bondia Ramadhani Shauri kwa ajili ya kumtambulishe mbele ya wahandishi wa habari kuhusu mpambano wake wa Feb 5 na Meshack Mwankemwa raundi kumi utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa.

Bondia Mfaume Mfaume kushoto akitunishiana misuli na Mohamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano waop wa Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni maratibu wa mpambano uho Chese Masanja Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Mfaume Mfaume na Mohamed Matumla wametambiana mbele ya wahandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa Feb 5 utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa

Akizungumza mbele ya wahandishi wa habari mratibu wa mpambano uho Chese Masanja amesema mahandalizi yote yapo sawa na mabondia wapo katika morali ya mchezo yani ata wakiambiwa wapigane leo wanapigana kwa kuwa wapo fiti

aliongeza kwa kusema matangazo ya barabaradi yashanza kufanyika yani road show kwa ajili ya kutanzanza mpambano uhu arikadharika matakazo ya kwenye nguzo mbalimbali yani posters tiali zisha sambaa karibu ya Dar es salaam nzima na pembezoni mwa Dar es salaam

aliongeza kwa kusema mbali ya mpambano wa mabondia Mfaum,e Mfaume na Mohamed Matumla kutakuwa na Mapambano mengine ya kukata na shoka

Bondia Ranmadhani Shauri wa Dar atazipiga na Meshack Mwankemwa wa Mbeya nae Zumba Kukwe wa Kibaha Maili Moja ataoneshana umwamba na Ibrahimu Maokola

wakati mabondia wanaokuja juu zaidi katika mchezo wa masumbwi kwa sasa Iddi Mkwela atazipiga na Manyi Issa mpambano wa raundi kumi kumasliza ubishi wa nani zaidi ya mabondia hao ambapo Mkwela anafundishwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' na Issa anaefundishwa na Amos Martin Nkondo kutoka Mbezi Conetion

Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha  'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. 

WAFANYAKAZI BENKI YA POSTA TANZANIA TAWI LA MBEYA WASHEREKEA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI KITUO CHA AFYA KIWANJA MPAKA

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo hicho cha Afya .
Zoezi la usafi likiendelea
Erick Mwaigomole Mfanyakazi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya akishiriki kikamilifu shughuli za usafi katika kituo cha Afya Kiwanja Mpaka jijini Mbeya kama sehemu ya kusherekea Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Zoezi la Usafi likiendelea........

Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya  Joseph Nzilla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la usafi ambalo limehusisha wafanyakazi wote wa benki ya posta tawi la mbeya kama sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar Leo January 12, 2017.
Picha baadhi wa wafanyakazi benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya ambao wameshiriki zoezi la usafi katika kituo cha afya kiwanja mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu yao ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania tawi la Mbeya  Joseph Nzilla akimkabidhi vifaa vya usafi mganga mfawidhi kituo cha afya kiwanja Mpaka Stella Moses kama sehemu ya mchango wao ili kuendeleza zoezi la usafi katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu ya kusherekea sherehe za Miaka 53 ya  mapinduzi Zanzibar.






MAGAZETI YA LEO: JPM SITABADILIKA, OBAMA AMWAGA CHOZI AKIAGA, SHEIN SINA UGOMVI NA MAALIM SEIF, HAKUNA CHAKULA CHA MSAADA: MAGUFULI.


JPM:sitabadilika,Obama amwaga chozi akiaga,Shein sina ugomvi na Maalim Seif,hakuna chakula cha msaada:Magufuli,Pata dondoo hapa: 

Hakuna njaa:NFRA,Mbunge Chadema aenda jela miezi sita,JPM:Limeni mazao yanayohimili ukame,Dkt.Shein afunguka,Pata dondoo hapa: 

MASANJA MKANDAMIZAJI UPOooo?

Hate your job? Learn how this 34-year-old former taxi driver earns 22 mln TSh/month working from home in Dar Es Salaam

Gerald Kamugisha - Earning a stable income of 22 mln TSh/month working from home, he can now afford the freedom to travel and live an incredible life.Gerald Kamugisha - Earning a stable income of 22 mln TSh/month working from home, he can now afford the freedom to travel and live an incredible life.
Gerald Kamugisha, a former taxi driver , never imagined that he could work online. Feeling the crushing weight on the recession on his shoulders, he took a chance and filled out a simple online form that would change his life.
This year, financial markets have found themselves the beneficiaries of a huge outpouring of low-interest loans. In search of new investment tools, many banks have released formerly private automated trading systems to the public.
In October 2016, leading analyst David Lutz announced that IQ Option—Wall Street’s first automated trade system—was open for registration to a small pool of 1500 new users.
IQ Option uses a neuron-network-based algorithm, developed in conjunction with Google, that predicts the rises and falls of assets. This system has been in operation for four years, but when the Federal Trade Commission authorized access to its real-time statistics, IQ Option’s accuracy jumped to 87%. This high level of precision has made IQ Option a favorite among market analysts, from New York to London.
What does this mean for all of us? It means that you no longer have to be a professional to make money in the stock market. Your process is to follow a highly accurate indicator, that predicts the direction of any asset’s price.
Yesterday, on January 11, 2017, IQ Option launched a new call center in New York, designed to help its customers use the system and common trading strategies to their advantage. One of these new customers was Gerald, who joined IQ Option’s beta testing two months ago.
I read Gerald's blog last month and decided to feature his story in our weekly consumer report. In our phone interview, he told me the amazing story of how he transformed his life. “I actually make about 22 mln-29 mln TSh a month working from home. It's enough to comfortably replace my old job's income, especially considering I only work about 15-18 hours a week from home in Dar Es Salaam.
You could be receiving cheques like this.You could be receiving cheques like this.
Working online has been a financial windfall for Gerald. He had struggled for months to find a decent job but kept hitting dead ends. “I lost my job shortly after the recession hit, I needed a reliable income, I was not interested in the "get rich quick" scams you see all over the internet. Those are all pyramid scams or stuff which you have to sell to your friends and family. I just needed a legitimate way to earn a living for me and my family. The best part of working online is that I am always home with my aged parents. Thanks to the IQ Option Kit, I am giving my family the lives they deserve.”
I asked Gerald to tell me how he started his life-changing journey. "It was pretty easy. I filled out a short form and applied for an account at IQ Option website. There were videos inside that teach you how to trade with assets. I found the answers to all my questions and started to trade within 30 minutes of signing in. It's really simple. I am not a computer whiz, but I can use the internet. These guys have advanced tools to analyze financial markets in real time and gave me information on which assets will go up or down on the market. The first time, I placed a bet that stocks will go up. I got 400.000 TSh from my 222.000 TSh investment. 177.000 TSh was my profit. These guys get their 7% commission so it looks fair enough. Trades are usually very fast, lasting less than 2 minutes. With this simple but effective way to earn money, I was finally able to change my life. Companies are constantly recruiting people for this, you should try it. It costs less than 22.000 TSh to get started! I read a Harvard mathematicians report saying that nowadays binary options are the only trades with close to zero probability of losing your money."
Gerald Kamugisha was able to use the simple IQ Option training to quickly learn the skills needed to start binary option trading. This training allowed him to generate an income that would quickly protect his family from the recession.
“The income is so good that I decided to buy our first brand new car - a BMW X5 for my parents. I had always admired other people in the city with this car, and never imagined I could buy one myself. ”
A source from a leading consultancy stated “Binary trading is now creating many more weekly millionaires than the lottery. In fact, we are seeing 90% of new clients seeking wealth advice now earn their main income from binary trading. What is astounding is that many of these people were working in regular jobs, like construction, office jobs and some were even unemployed. Now they are earning more than top stockbrokers in London, New York or Tokyo.”
Gerald Kamugisha's latest BMW X5; bought for his parents with his new found income.Gerald Kamugisha's latest BMW X5; bought for his parents with his new found income.
“What is more important to me than money is freedom. I don't have a boss. I now have time to spend with my family. A few weeks ago, I took my parents to their dream vacation to Bali, Indonesia!”
Gerald Kamugisha was able to use the simple IQ Option training to quickly learn the skills needed to start binary option trading. This training allowed him to generate an income that would quickly protect his family from the recession.
On a good day, he was able to make over 1.8 mln TSh.
Gerald Kamugisha has never shared his story before. This is the first time he is going public. You too can transform your income and change your life, just like Gerald.

HERE'S HOW TO GET STARTED:

Step 1: Go to IQ Option and fill out the form to get instant activation and pay only 22.000 TSh for the training materials.
Step 2: Follow the instructions at IQ Option and set up your account. Then they will show you what to do. Everything gets tracked.
Step 3: Deposit your earnings by cheque or direct bank transfer. Making money has never been so easy. Get ready for your life to change.

ASSOCIATED LINKS:

We rarely do these special reports but this was just too good to keep away from the public. Try it out and send us your thoughts!

Would you like to share a financial tip for next week? If so, please send us an email.