ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 24, 2014

NDIKILO KUONGOZA HARAMBEE YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA JAMII KATA YA NYAMSWA WILAYA YA BUNDA MKOA WA MARA ITAKAYO FANYIKA MWANZA JIONI YA LEO.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist ndikilo.
MKUU wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo hii leo anatarajiwa kuongoza harambee ya kuchangiaha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za jamii kwa kata ya Nyamswa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara itakayofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania - B.O.T tawi la Mwanza uliopo Capri Point wilayani Nyamagana.

Akizungumza na GSENGO blog Mwenyekiti wa Kamati Inayoandaa Harambee hiyo ya kuchagiza Maendeleo kata ya Nyamswa Bw. Juma Makongoro amesema kuwa nia ya kufanya tukio hilo ni kwaajili ya kuboresha huduma za kijamii kupitia changamoto zinazowakabili watu wa kata hiyo baada ya kuzibaini kuwa ni sugu zinazo rudisha nyuma maendeleo ya wakazi wa eneo hilo sambamba na kuzidi kuwadidimiza katika lindi la umasikini na kusababisha vifo vinavyoweza kuzuilika. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

Washiriki mbalimbali wamealikwa katika hafla hiyo wakiwemo:-
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Mhe. Wassira.
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baadhi ya Wanasiasa kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Wananchi, Vijana wa Kikizu na Nyamswa waliokuja kutoka Dar, Arusha, Mwanza nk.
Wakereketwa wa Maendeleo bila kujali kabila wala itikadi.
Wafanyabiashara na Wafanyakazi (mbalimbali).

MATARAJIO NA FAIDA
Uboreshaji wa Ujenzi wa Miundo Mbinu ya utoaji huduma za kijamii katika Sekta ya Elimu, Afya na Maji.
Kuboresha hali maisha kwa jamii ya wakazi wa wilaya ya Bunda hususani kata ya Nyamswa.
MICHANGO YOTE IELEKEZWE KATIKA A/C 30110000521 NMB-BUNDA MFUKO WA WAZEE WA MAENDELEO KATA YA NYAMSWA, M PESA 0753 520448

USIKU WA LEO JEMBE BEACH NI KAMA LISBON VILE

Kama uko jijini Mwanza hii leo (jumamosi 24/05/2014) basi ile Fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa kati ya Real Madrid na Atletico Madrid tutakwenda kuitizama pale JEMBE BEACH.
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo na mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani Gareth Bale watakuwepo katika timu ya Real Madrid itakayochuana na Atletico Madrid katika fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa hii leo jumamosi.
Ronaldo, 29, alikuwa amekosa kucheza mechi mbili akiuguza jereha sawa na mshambulizi Gareth Bale, 24, ambaye hakushiriki katika mazoezi siku ya jumanne.
Wawili hao kwa ushirikiano wamiefungia Real Madrid mabao 68 msimu huu.
Kocha Carlo Ancelotti, ambaye anapania kuwa mkufunzi wa pili katika historia ya mchuano huu kuwahi kushinda taji la ubingwa barani Ulaya mara tatu amethibitisha kuwa nyota hao wawili wakali kwa mashambuli watakuwepo
Real Madrid inapania kutawazwa mabingwa wa Uropa iwapo watawalaza washindi wapya wa ligi kuu ya Uhispania Atletico Madrid mbali na kusitisha ukame wa miaka 12 wa kombe hilo lenye umaarufu barani Uropa.
Atletico wamechuana dhidi ya Real Madrid mara nne msimu huu ,Real ikishinda mechi za kuwania kombe la Spanish kwa mabao 5-0 huku Atletico ikiibuka na ushindi katika mechi za ligi ya Uhispania .
Wakati huo huo nyota wa Atletico Madrid Diego Costa amerejea mazoezini leo kujifua tayari kwa fainali ya kombe la mabingwa bara Uropa dhidi ya Real Madrid baada ya kudaiwa kuwa alizuru Belgrade kupata utabibu kutoka kwa Muuguzi mmoja anayetumia kondo la nyuma kwa utabibu wake.
Costa aliumia mapema katika mechi ya kuamua mshindi wa ligi kuu ya Uhispania la liga ambayo Atleticoilitoka sare ya 1-1 na Barcelona na kutawazwa mabingwa.

Friday, May 23, 2014

JUA LIMEZAMA WIKIENDI WAPI...?

EKACLIF Building Mwanza.
Barabara ya Pamba kuelekea Nyerere, Pepsi, Butimba, Nyegezi, Buhongwa......
Juu kwa juu.
Vilima na maajabu yake.
Kuelekea bandari ya Mwanza South Pole.
Ziwa victoria kwa chati na vivutio vya kitalii vilivyoko kandokando Yatch Club na Tilapia Hotel.
Barabara ndani kwa ndani Isamilo.
Tabia misitu na usalama wa uzio.
Eh bana jua lazama wIKieNdi wapiiiiiiiii!!!?
"Wapi tena zaidi ya Jembe"

GERMAIN KATANGA AHUKUMIWA JELA MIAKA 12

Kiongozi wa zamani wa wapiganaji waasi DRC Germain Katanga.
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imemhukumu kiongozi wa zamanai wa wanamgambo waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo, Germain Katanga, kifungo cha miaka kumi na miwili jela baada ya kumpata na hatia ya uhalifu wa kivita.
Bwana Katanga alipatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mamia ya wanavijiji katikaeneo la Ituri Katanga mwezi Machi mwaka 2003.
Jimbo la Katanga ni jimbo lenye utajiri wa madini ya dhahabu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo . Lakini kiongozi huyo wa waasi mwenye umri wa miaka thelathini na sita hakupatikana na hatia ya kuwatumikisha watoto vitani na makosa mengine ya ubakaji.
Chanzo BBC swahili.

NDOVU SPOTLIGH NIGHT

Mwongoza maada wa usiku wa Ndovu Spotlight, Gloria Mangi (kushoto) akiongoza maada wakati wa mdahalo kwa wadau mbalimbali uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa website, Laura Lyabandi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinjari, Andrew Mbona.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Fimbo Butallah (kutoka kulia), Meneja wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikuli na Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofrey Makau wakifuatilia maada wakati wa mdahalo wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Meneja wa kinywaji cha Redd’s, Victoria Kimaro (kutoa kushoto), Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofrey Makau, Meneja wa Bia ya Ndovu, Pamela Kikulina Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL), Fimbo Butallah wakifuatilia maada wakati wa mdahalo wa usiku wa Ndovu Spotligh tuliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia maada wakati wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wadau wakifuatilia maada wakati wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Mchekeshaji, Evance Bukuku (kulia) akichangia maada wakati wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Meneja wa Bia ya Castle Lite, Geofrey Makau (kushoto) akiwa na wadau wakipata vitafunwa mara baada ya mdahalo wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.
Mwongoza maada wa usiku wa Ndovu Spotlight, Gloria Mangi(kulia), mmilikiwa website, Laura Lyabandi (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinjari, Andrew Mbona wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mdahalo wa usiku wa Ndovu Spotlight uliofanyika katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana.

HOSPITALI YA NYAMAGANA KATA YA BUTIMBA YAKABIDHIWA VIFAA.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
HOSPITALI ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba jijini hapa, mkoani Mwanza, imepatiwa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya Idara ya Upasuaji na Wodi ya Wazazi wanaotaka kujifungua.



Msaada huo uliotolewa juzi na raia wawili kutoka nchini Canada baada ya kukutana na Meya wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula na kumweleza kusudio lao la kutaka kutoa msaada wa kijamii ikiwa ni vifaa vya hospitali kwa lengo la kuwasaidia wagonjwa wasioweza kuchangia gharama za matibabu.
Raia Susan Bibbings na mumewe Mark kutoka Jiji la West Voncover BC nchini Canada wakikabidhi vifaa hivyo, walieleza kusudio lao la kulisaidia zaidi Jiji la Mwanza kutokana na maaongezi ya kina waliyofanya na Meya Mabula na kuhamasika na hali halisi waliyoiona katika Hospitali hiyo baada ya kuitembelea.



“Tumetembelea kwenye Wodi za wagonjwa wanawake, wanaume, watoto na wazazi lakini tumeingia chumba cha Upasuaji, X-Ray, Maabara, Meno, Dawa, Masijara na Wodi ya Wamama wajawazito wanaosubiria kujifungua, tumeguswa na tumeahidi kureta misaada zaidi baada ya kurejea nyumbani Canada tutaanza kutafuta wafadhili mbalimbali kutuunga mkono,”alisema Susan.
Ni katika foleni ya kusubiri tiba Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyopo Kata ya Butimba.
Kwa upande wake Meya Mabula alisema kwamba, kutolewa kwa vifaa hivyo kutaongeza chachu ya madaktari na wauguzi kutoa huduma kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo, pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali zilizopo katika hospitali hiyo tunaendelea kuzifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanaofika kupata huduma kwa wakati ikiwa na kupata dawa.

“Marafiki zetu hawa wameamua kutusaidia baadhi ya vifaa katika maeneo ya Upasuaji, Wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiria kujifungua, lakini wametuahidi msaada mkubwa ambapo wameeleza kuwa wataleta Kontena la vifaa mbalimbali vikiwemo vifaa btiba na wameonyesha kuguswa na mapungufu waliyoyaona katika hospitali yetu,”alisema.
Aidha Mabula aliwahakikishia Wahisani hao kwamba watakaporeta Kotena la vifaa vya msaada kwa ajili ya hospitali hiyo Halmashauri ya Jiji iko tayari kulipia gharama za Bandarini na usafirishaji hadi jijini hapa ili kuhakikisha masaada huo unaanza kutumika haraka kwa wananchi wa Wilaya na Jiji la Mwanza.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Ngaila amewashukuru raia hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia vyema ili kusaidia wagonjwa ambao baadhi yao hutibiwa bure ikwemo wazee, watoto na wanawake wanaojifungulia katika hospitali hiyo.
“Vifaa hivi vina ubora unaokubalika na vitatuwezesha kutoa huduma nzuri na imepunguza pengo la vifaa tiba vinavyohitajika ikilinganishwa bado kuna changamoto nyingi kutokana na Bajeti yetu pia kuwa ndogo jambo ambalo hupelekea baadhi ya vifaa tiba kuwa na upungufu kiasi,” alisema Dr. Ngaila.

Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa kwanza kushoto) akiwa na marafiki ambao ni  Raia Susan Bibbings na mumewe Mark kutoka Jiji la West Voncover BC nchini Canada kwakiagana kutoka hospitalini hapa mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya afya.

Thursday, May 22, 2014

FLAVIANA MATATA, AY WASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 18 AJALI YA MV BUKOBA JIJINI MWANZA.

JANA ilitimia miaka 18 tangu ndugu zetu walipopata ajali na Meli ya MV. Bukoba 21 May 1996, na wengi kupoteza maisha! Ni tukio kubwa lililoua mamia ya watu na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania.
Miss Universe tanzania 2007 na mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata jana alijumuika na wananchi wengine wa mkoa wa Mwanza katika ibada maalum ya kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya waliopoteza maisha yao baada ya ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba yapata miaka 18 sasa.
Flaviana Matata (mwenye gauni la bluu kulia) akiwa amesindikizana na jamaa, ndugu na marafiki akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu mama yake mzazi aliyefariki kupitia ajali hiyo.
Akiwa ameambatana pia na mwanamuziki wa kimataifa Ambwene Yesaya 'AY' (mwenye kofia nyeusi), mwanamitindo Flaviana Matata alishirikiana na wadau hao pamoja na wananchi wengine kuwasha mishumaa kama sehemu ya ibada kwa marehemu hao walio fariki dunia yapata miaka 18 sasa.
"Tutawakumbuka daima"
Ajali ya kuzama kwa Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamotarehe 21/05/1996 nakupoteza maisha ya zaidi ya watu 1000.
Mwanamuziki wa kimataifa Ambwene Yesaya 'AY' (mwenye kofia nyeusi kulia) ni mmoja kati ya marafiki waliofika eneo hili la makaburi ya waliokufa katika ajali ya Mv Bukoba, na kushiriki ibada maalum ya kuwaombea wote walio tangulia mbele za haki. 
Misa hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa dini, ndugu wa karibu wa Flaviana akiwemo baba yake mzazi, marafiki zake wanamchi mbalimbali na pia viongozi wa Serikali, na viongozi na wafanyakazi wa Marine Services Co. LTD. 
Ni tukio kubwa lililoua mamia ya watu na kuacha huzuni kubwa kwa Watanzania, nayo miili ya watu kwa mamia imelala hapa. Eh Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema twakuomba uwarehemu watu wako.
Amen.

HUU HAPA WIMBO MAHUSUSI KWA KOMBE LA DUNIA 2014


La La La (Brasil) wimbo wake mwanamama Shakira ndiyo utakuwa wimbo maalum kwaajili ya Kombe la dunia la FIFA 2014.

Hii si mara ya kwanza kwa Shakira kwani mnamo Tarehe 10 mwezi Juni 2010 njini Soweto, Shakira na Freshlyground walitumbuiza wimbo maalum katika tamasha la uzinduzi kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la dunia.

Nyimbo kadhaa zisizo rasmi tayari zimesikika sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ule ulioimbwa na John Barnes Kwa fainali za Kombe la dunia mwaka 1990, World in Motion by New Order.

Wimbo rasmi wa mwisho wa England katika Kombe la Dunia ulioitwa "World At Your Feet" wa kundi la Embrace ulikamata nafasi ya tatu katika chati za muziki mwaka 2006. Pia mwanamuziki Tony Christie na Crazy Frog walifanya jitihada kadhaa za kutoa nyimbo za kuhamasisha kampeni ya England.

Mwaka 2002, wimbo "We are on the ball" ulirekodiwa na watangazaji wa Tv, Ant na Dec.

Mwaka 1998, kundi la Spice Girls waliimba wimbo (How Does it feel To Be) on Top Of The World, ulioandikwa na Endo na ian McCulloch wa kundi la Bunnymen.

TAHADHARI: UGONJWA WA DENGUE WATINGA MWANZA

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (L) akitoa taarifa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza ambapo hadi sasa amepatikana mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo, kulia ni Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza valentino Bangi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Bangi akielezea jinsi walivyobaini ugonjwa wa Dengue kupitia mtu aliyefika katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure na kuthibitika kuwa na ugonjwa huo ambapo pia alitilia msisitizo njia za kuuthibiti ugonjwa katika jamii. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa Sekou Toure Dr. Onesmo Rwakyendela ametoa wito kwa wananchi hususani wa visiwani kwa sababu ugonjwa huu una dalili kama za maleria basi wanapo jihisi kuwa dalili hizo wakimbilie hospitali kupata vipimo na hatimaye wapate tiba. 
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa umakini utolewaji wa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza ambapo hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo.
Ni mazingira ya nje Hospitali ya Rufaa ya Sekou-toure mahali alipolazwa mtu mmoja mtumishi mstaafu mwenye umri wa miaka 62 mkazi wa Kilimahewa wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza, ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa wa Dengue.

 KUWEPO KWA UGONJWA WA DENGUE   KATIKA MKOA WA MWANZA

TAARIFA  KWA  UMMA

Ndugu, Waandishi wa habari, wawakilishi wa vyombo vya habari na wananchi wote. Napenda kutoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa Dengue katika Mkoa wa Mwanza. Hadi sasa kuna mgonjwa mmoja katika Hospittali ya Rufaa ya Sekou-toure ambaye amethibitika kuwa na ugonjwa huo.  Kufuatia taarifa hii  napenda wananchi wafahamu machache kuhusu ugonjwa wa Dengue. Ugonjwa wa Dengue husababishwa na VIRUS vinavyoitwa “Dengue Virus”  na vinaenezwa na mbu aina ya Aedes.

Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au kwenye vyombo vya kuhitadhia maji majumbani.

JINSI UGONJWA WA HOMA YA DENGUE UNAVYOENEZWA

Binadamu hupata ugonjwa huu baada ya kuumwa na mbu wa aina ya Aedes aliye na Virusi vya ugonjwa huu.  Mbu  hawa hupendelea kuuma wakati wa mchana.

Ugonjwa huu huwapata wetu wa rika zote aidha watoto wenye umri chini ya miaka mitano na mama wajawazito huathirika zaidi.

Ndugu wananchi

Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Dengue

Asilimia 90 ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huu uonyesha dalili awali kuanzia siku ya 3 hadi 14 baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi vya ugonjwa huu dalili hizi ni kama zifuatazo:
·        Homa kali ya ghafla
·        Kuumwa kichwa hususani sehemu za machoni
·        Maumivu makali ya misuli pamoja na viungo vya mwili
·        Kichefuchefu au kutapika
·        Kuvimba tezi
·        Kupatwa na harara
Asilimia 10 ya wagonjwa hupatwa na dalili kali kama kutokwa na damu kwenye sehemu za uwazi za mwili mfano mdomoni, masikioni pamoja na sehemu za kutolea haja ndogo na kubwa.

Ndugu wananchi,
Njia za kujikinga na Homa ya Dengue
Ugonjwa wa dengue unazuiliwa kwa njia zifuatazo:-
·        Kuangamiza mazalio ya mbu
·        Kufukia madimbwi ya maji au nyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
·        Kuondoa  vitu vyote vinavyoweza kuwa mazalia ya mbu kama vile vifuu vya nazi, makopo, chupa na magurudumu ya gari ambavyo vinaweza kufanya maji kutuama karibu na makazi.
·        Kufyeka nyasi na vichaka vilivyo karibu na makazi.
·        Kuhakikisha maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
·        Kufunika mashimo ya maji taka kwa mfuniko
·        Kusafisha mitaro na  gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.

Kuzuia kuumwa na mbu kwa:-
·        Kutumia dawa za kufukuza mbu  (Repellents)
·        Kuvaa nguo ndefu
·        Kuweka wavu wa kuzuia mbu kwenye madirisha na milango
Kwa kufanya hayo, tunaamini tunaweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu yasiendelee kutokea.  Naomba kila mmoja atimize wajibu wake.

Asanteni kwa kunisikiliza,



Baraka M. Konisaga
KAIMU MKUU WA MKOA
MWANZA


AIRTEL YAJA NA 'SWITCH ON' Intaneti maalum kwa simu unayotumia.

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Levi Nyakundi akizungumza na wadau mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla hiyo ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana usiku katika  Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi wa Huduma mpya ya Airtel ya ‘SWITCH ON’ wasanii maarufu Ney wa Mitego, Vannessa Mdee na Barnabas wakiwa wameshikilia mabango yenye kuonyesha namba ya kujiunga na huduma hiyo ya intaneti wakati wa hafla ya uzinduzi wake uliofanyika jana usiku kwenye kiota cha Maraha cha Club Rouge ndani ya Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Msaanii maarufu kwa kumiliki jukwaa na balozi wa huduma ya Airtel SWITCH ON Vanesa Mdee akiwa na wacheza shoo waki wakitoa burudani kali kwa wageni waalikwa  waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana usiku katika  Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Msaanii maarufu na mwenye uwezo wa kutumia gitaa na kuimba pia ni Balozi wa Airtel SWITCH ON barnabas  akitoa burudani kali kwa wageni waalikwa waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel kwa watumiaji wa Internet hapa nchini ijulikanayo kama SWITCH ON. hafla ya uzinduzi ilifanyika jana usiku katika  Hoteli ya Hyatt Agengy The Kilimanjaro,Jijini Dar es Salaam.
Airtel yaja na SWITCH ON, Intaneti maalum kwa simu unayotumia

·        Airtel yazindua huduma ya kipekee ya vifurushi vya data maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.
·        Airtel kuwapa suluhisho bora wateja katika huduma ya Internet
·        Wateja wa Airtel kufurahia inteneti bora kwa gharama nafuu

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel leo imezindua huduma kabambe ya Intaneti itakayojulikana kama SWITCH ON. Huduma hiyo ni maalum kwa watumiaji wa huduma za Interneti Tanzania ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kufuruhai huduma ya kipekee ya vifurushi vya data/intaneti maalum kwa simu na mahitaji ya kila mteja.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel  Tanzania Bw, Levi Nyakundi alisema “ ulimwengu wa leo matumizi ya huduma za intaneti/data au mtandao hayaepukiki, ukitaka kujua kinachoendelea duniani kwa haraka basi intaneti ndio suluhisho au jawabu linapopatikana, lakini kumekua na changamoto nyingi sana hasa pale tunapohitaji intaneti bora ya kutuwezesha kufanya fasta mawasiliano na tuwapendao au tunapotaka kuunganishwa na taarifa za mambo muhimu yanayoendelea dunia kote, inawezekana kila wakati umekua ukijiuliza ni MB au GB au kifurushi gani kitakuwezesha kufanya mambo yako kuwa poa zaidi, hili ndilo lililotusukuma Airtel kukuletea wewe mteja wetu huduma hii ya kisasa na ndio maana tunakuambia SWITCH ON”

“Ukiwa na Airtel ‘SWITCH ON’ watumiaji wa huduma za Intaneti Tanzania sasa wanakila sababu yakufurahia kujipatia huduma bora zaidi kwa gharama nafuu na kufanya chaguo la kufurushi utakacho MAALUM kwa simu yako. Hii ni huduma inayoenda na wakati, inazingatia utamaduni wetu kwa kuwa ni ya kukutoshelezea hitaji lako, na gharama ni nafuu kuliko zote huku ikikuhakikishia mteja Non-stop intaneti - yaani fulu makamuzi kwa wewe mtumiaji kutokupimiwa. Huduma hii ya pia inamuwezesha mteja kuwa na chaguo la kifurushi iwe kwa SIKU, WIKI auMWEZI”

“Airtel Tanzania tumejipanga zaidi kuhakikisha tunaendelea kuwa wabunifu na kuwapatia huduma bora ya mawasiliano ya internet. Tutaendelea kufanikisha  hili kwakuwa Airtel Yatosha, Airtel Money nusu gharama, au Bure Pack ni vielelezo vya huduma bora na nafuu tunazowapatia wateja wetu kwa sasa na kuwafaidisha wateja kila siku. Hivyo leo hii SWITCH ON nimuendelezo wa kuwahudumia watumiaji wa Internet nchini Tanzania kwa kuwapa wanachokitaka bila kikwazo yaani Fulu makamuzi” aliongeza Nyakundi 
 Kwa upande wake Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo akielezea jinsi ya kutumia huduma hiyo alisema “Ni rahisi sana mteja wetu kujiunga, unatakiwa tu kupiga *148*22# ikiwa tu una simu yako yenye uwezo wa kutumia intaneti /Data kisha utaweza kujichagulia aina ya kifurushi kinachokufaa kutokana na mahitaji yako kwa kuwa vifurushi ni maalum kwa simu au kifaa utakachotumia yaani iwe unasimu ya Feature phone, au Simu mpapaso (Smart phone au Tablet sisi Airtel tumekuwekea kifurishi cha intaneti maalum kwa kila simu”

‘Vilevile kwa wale wateja wote wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha pia bado wananafasi ya kujiunga na vifurushi vya intaneti vya Yatosha na ikiwa wamemaliza Data /intaneti na wanapenda kujiunga na Data pekee basi wanaweza pia KU-SWITCH ON na kuendela na makamuzi” alimalizia kusema Prisca.