ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 30, 2017

MBUNGE MGIMWA AMEKABIDHI MIFUKO 400 YA SARUJI NA BATI 150 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE NA ZAHATI ZA KATA YA MAPANDA

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa  akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
 Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa   amekabidhi  jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

“mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.

Obedi Madembo, Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.

“Hata ukiangalia mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda

Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.

“Wananchi kweli wananjitoa sana kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa wananchi wote” alisema Kalenga

MHE MWANJELWA ATOA SIKU MOJA KWA WAFANYABIASHARA WALIOFUNGA MAGHALA YA MBOLEA LA SIVYO KUNYANG'ANYWA LESENI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akikagua mbegu zilizohifadhiwa ghalani kabla ya kuanza kusambazwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge (Kulia) na Meneja uzalishaji Wakala wa Mbegu Ndg Charles Levi (Kushoto). Picha Zote Na Mathias Canal 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Wakala wa Mbegu Dkt Sophia Kashenge Kilenge alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo baada ya kukagua baadhi ya mashine za mbegu alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua namna mbegu za mazao mbalimbali zilivyohifadhiwa alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Leo 29 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa leo Disemba 29, 2017 amewaagiza wafanyabiashara wa mbolea kote nchini walioweka mgomo wa kupeleka mbolea kwa wakulima kufikia 30 Disemba 2017 wawe wamefungua maghala yao kwa ajili ya kuwauzia mbolea wakulima.

Alisema endapo wafanyabiashara hao wasipofanya hivyo serikali itawanyang'anya leseni zao haraka iwezekanavyo ili kuruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kufanya jukumu hilo pasina kuwaumiza wakulima kutokana na bei ghali ya mbolea.

Mhe Mwanjelwa ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Wakala wa mbegu za kilimo (Agricultural Seeds Agency-ASA) Mara Baada ya kubaini kuwa kuna wafanyabiashara ambao wameanza kufunga maghala kwa madai ya kupanda kwa mbolea katika soko la Dunia.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kuijaribu serikali kwani malalamiko yao ya kupanda kwa bei katika soko la Dunia hayana tija kwani mbolea zote zilipo nchini tayari wakishanunua kipindi soko likiwa kwenye unafuu mkubwa.

Alisema kuwa serikali ilitoa bei elekezi katika mbolea ya kukuzia na kupandia ikifahamu fikra kuwa kupitia gharama hiyo wakulima watanufaika lakini pia wafanyabiashara watanufaika kutokana na faida wanayoipata lakini wameamua kubadili utaratibu wa kutaka kupata faida kubwa zaidi pasina kujali wakulima wataumizwa na bei hiyo kwa kiasi gani.

Mhe Mwanjelwa ameitaka kampuni ya Premium ambayo ni moja ya kampuni zilizogoma kufungua maghala na kupeleka mbolea kwa wakulima kwa bei elekezi iliyotolewa na serikali.

Alisema kuwa wafanyabiashara hao kwa makusudi wameamua kufifisha juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ya kuwakomboa wakulima kupitia gharama nafuu ya mbolea hivyo kufikia kesho wasipofungua maghala hayo watanyang'anywa leseni zao ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa sheria.

MGODI WA ZEM WAPEWA SIKU SABA KUTOA VIFAA VYA KUJIKINGA

MGODI WA ZEM WAPEWA SIKU SABA KUTOA VIFAA VYA KUJIKINGA 
Serikali imetoa siku Saba kwa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM (T) Company Ltd wa Nyasirori Wilayani Butiama kuwapatia vifaa vya kujikinga kazini (safety gears) wafanyakazi wa mgodi huo vinginevyo mgodi utafungwa. 

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye mgodi huo kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na mgodi huo.

Wafanyakazi na wananchi wanaozunguka mgodi huo walimueleza Naibu Waziri huyo changamoto mbalimbali walizonazo kutokana na shughuli za mgodi ikiwemo mahusiano mabaya na wananchi, wafanyakazi kukosa vifaa vya kujikinga, mishahara midogo na manyanyaso ikiwemo kupigwa.

Akitoa tamko kuhusiana na hoja hizo zilizowasilishwa kwake, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kufanya shughuli zake kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria za Nchi.

Alisema haiwezekani wafanyakazi wakafanya shughuli mgodini hapo bila kuwa na vifaa vya kujikinga na aliiagiza Ofisi ya Madini Musoma kufuatilia suala hilo na endapo siku hizo zitapita bila vifaa hivyo kuletwa afunge mgodi.

“Ninawapa Siku Saba wawe wameleta vifaa na wasipofanya hivyo funga mgodi, ni lazima wafanyakazi wapatiwe vifaa vya kujikinga, kulingana na kazi wanazofanya,” alisema Nyongo.

Akizungumzia suala la mishahara, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kuhakikisha unafuata Sheria ya Madini inavyoelekeza kwa kuwalipa mshahara stahiki ambao alisema kima cha chini kuwa ni 400,000.

Naibu Waziri Nyongo vilevile aliuagiza mgodi huo kuandaa mikataba ya ajira na kwamba atakapofanya tena ziara mgodini hapo akute wafanyakazi wanayo mikataba ya ajira iliyoandaliwa kwa mujibu wa sheria. 

Aidha, aliuonya mgodi huo tabia ya kupiga wafanyakazi, alisema jambo hilo halikubaliki na ni kinyume na utu wa binaadamu na kwamba ikitokea mfanyakazi akapigwa, Ofisi ya Madini ifunge mgodi huo mara moja.

“Ni marufuku kupiga wafanyakazi, atakayepigwa aende Polisi na sisi tutaufunga mgodi. Mkuu wa Wilaya yupo hapa muwe mnamueleza matatizo yenu ili yapatiwe ufumbuzi,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Butiama kusimamia vyema masuala yote ya ulinzi na usalama, na ahakikishe anatembelea mgodini hapo ili kuzungumza na wafanyakazi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Vilevile Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kutofukuza mfanyakazi yoyote aliyeeleza changamoto zinazowakabili kwenye utekelezaji wa majukumu yao. “Usimfukuze mfanyakazi yoyote aliyetoa kero yake katika ziara hii, wako huru kuzungumza nami,” alionya Naibu Waziri Nyongo.

Kuhusu suala la mahusiano na wananchi, Nyongo aliuagiza mgodi huo kuajiri mtu maalum wa mahusiano atakayefanya mawasiliano ya mara kwa mara na wananchi ili kuboresha mahusiano na hapohapo aliiagiza Serikali ya Kijiji kufanya mikutano ya mara kwa mara na wanachi ili kuwapatia mrejesho wa masuala mbalimbali baina ya mgodi na maendeleo ya kijiji.

Friday, December 29, 2017

MGODI WA ZEM WAPEWA SIKU SABA KUTOA VIFAA VYA KUJIKINGA

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited alipofanya ziara mgodini hapo kujionea shughuli ziazoendelea na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka mgodi huo. Kulia ni Meneja wa Mgodi, Luo Guiquan.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kushoto) akitembelea Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited alipofanya ziara mgodini hapo kujionea shughuli ziazoendelea. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa tatu kulia) akitembelea Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited alipofanya ziara mgodini hapo kujionea shughuli ziazoendelea. Kutoka kulia ni Meneja wa Mgodi huo, Luo Guiquan na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Annarose Nyamubi.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) akielekeza jambo alipotembelea Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited wa Butiama ili kujionea shughuli zinazoendelea. Pembeni yake ni Kaimu Kamishna wa Madini, Kanda ya Ziwa Viktoria Mashariki, Mhandisi Nyaisara Mgaya.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited uliopo Butiama, Mkoani Mara (hawapo pichani) wakati wa ziara yake mgodini hapo. Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyasirori Wilaya ya Butiama, Mkoani Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) alipofanya ziara kwenye Mgodi wa Dhahabu wa ZEM Tanzania Company Limited uliopo katika kijiji hicho. 

Serikali imetoa siku Saba kwa Mgodi wa Dhahabu wa ZEM (T) Company Ltd wa Nyasirori Wilayani Butiama kuwapatia vifaa vya kujikinga kazini (safety gears) wafanyakazi wa mgodi huo vinginevyo mgodi utafungwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa agizo hilo Desemba 27, 2017 alipofanya ziara kwenye mgodi huo kujionea shughuli zinazoendelea mgodini hapo na kuzungumza na wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo jirani na mgodi huo.

Wafanyakazi na wananchi wanaozunguka mgodi huo walimueleza Naibu Waziri huyo changamoto mbalimbali walizonazo kutokana na shughuli za mgodi ikiwemo mahusiano mabaya na wananchi, wafanyakazi kukosa vifaa vya kujikinga, mishahara midogo na manyanyaso ikiwemo kupigwa.

Akitoa tamko kuhusiana na hoja hizo zilizowasilishwa kwake, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kufanya shughuli zake kwa kufuata utaratibu, kanuni na sheria za Nchi.
Alisema haiwezekani wafanyakazi wakafanya shughuli mgodini hapo bila kuwa na vifaa vya kujikinga na aliiagiza Ofisi ya Madini Musoma kufuatilia suala hilo na endapo siku hizo zitapita bila vifaa hivyo kuletwa afunge mgodi.

“Ninawapa Siku Saba wawe wameleta vifaa na wasipofanya hivyo funga mgodi, ni lazima wafanyakazi wapatiwe vifaa vya kujikinga, kulingana na kazi wanazofanya,” alisema Nyongo.

Akizungumzia suala la mishahara, Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kuhakikisha unafuata Sheria ya Madini inavyoelekeza kwa kuwalipa mshahara stahiki ambao alisema kima cha chini kuwa ni 400,000.

Naibu Waziri Nyongo vilevile aliuagiza mgodi huo kuandaa mikataba ya ajira na kwamba atakapofanya tena ziara mgodini hapo akute wafanyakazi wanayo mikataba ya ajira iliyoandaliwa kwa mujibu wa sheria.

Aidha, aliuonya mgodi huo tabia ya kupiga wafanyakazi, alisema jambo hilo halikubaliki na ni kinyume na utu wa binaadamu na kwamba ikitokea mfanyakazi akapigwa, Ofisi ya Madini ifunge mgodi huo mara moja.

“Ni marufuku kupiga wafanyakazi, atakayepigwa aende Polisi na sisi tutaufunga mgodi. Mkuu wa Wilaya yupo hapa muwe mnamueleza matatizo yenu ili yapatiwe ufumbuzi,” alisema Naibu Waziri Nyongo.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Butiama kusimamia vyema masuala yote ya ulinzi na usalama, na ahakikishe anatembelea mgodini hapo ili kuzungumza na wafanyakazi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Vilevile Naibu Waziri Nyongo aliuagiza mgodi huo kutofukuza mfanyakazi yoyote aliyeeleza changamoto zinazowakabili kwenye utekelezaji wa majukumu yao. “Usimfukuze mfanyakazi yoyote aliyetoa kero yake katika ziara hii, wako huru kuzungumza nami,” alionya Naibu Waziri Nyongo.

Kuhusu suala la mahusiano na wananchi, Nyongo aliuagiza mgodi huo kuajiri mtu maalum wa mahusiano atakayefanya mawasiliano ya mara kwa mara na wananchi ili kuboresha mahusiano na hapohapo aliiagiza Serikali ya Kijiji kufanya mikutano ya mara kwa mara na wanachi ili kuwapatia mrejesho wa masuala mbalimbali baina ya mgodi na maendeleo ya kijiji.

SERIKALI KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI

Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akizungumza na wananchi wa kata ya Mganza wakati wa ziara yake Wilayani Chato ya kukagua utekelezaji wa uwekaji wa umeme vijijini(Rea awamu ya tatu)

Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akiwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chato (Kulia)wakati alipokuwa akizungumza na wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Chato ,Shaaban Ntarambe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyang’homango wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kwenye Wilaya hiyo.

Wananchi wa kijiji cha  Nyang’homango wakimsikiliza Waziri wa Nishati  wakati wa ziara yake ya kikazi.

Waziri wa Nishati,Medad Kaleman na Mkuu wa Wilaya ya Chato wakikagua kituo cha afya cha Kata ya Mganza wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Chato.

Na,Joel Maduka,Chato

Serikali inatarajia kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme  wa maji wa mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha  miundombinu ya umeme na upatikanaji wa uhakika kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya  kikazi Wilayani Chato Mkoani Geita ilikuwa na lengo la kukagua na kujionea miundombinu ya umeme wa Rea  awamu ya tatu ,Waziri wa Nishati ,Dr Medadi Kalemani ,alisema kuwa hali ya umeme inaendelea kuimarika siku hadi siku na kuna maeneo mengi yameanza kupata umeme wa kutosha.

“Hapo Nyuma mwezi Novemba tulikuwa tunajitahidi kukarabati mahali ambapo kulikuwa na ubovu wa mitambo lakini kwa sasa hali inaendelea vizuri maeneo mengi ya nchi yetu yanapata umeme kwa wingi  na  tunaanza kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa  mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji  ambao utasaidia kuimalisha  miundo mbinu ya umeme na upatikanaji wa umeme hapa nchini”Alisema Kalemani.

Aidha Dr,Kaleman  amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye maeneo yao pindi kunapotoakea tatizo na kwamba wateja ambao wamelipia umeme kwa mwaka 2017 ni vyema Tanesco wakahakikisha wanawaunganishia umeme haraka iwezekanavyo kwani mwaka 2018 haitakiwi  kuwepo kwa mteja ambaye ajaunganishiwa  huduma hiyo.

Kalemani ameendelea kutoa wito kwa watendaji wa Tanesco kuhakikisha katika kipindi hiki cha msimu wa siku kuu ya chrismas na mwaka mpya kuimarisha  utoaji wa umeme na uimalishaji wa miundombinu na kufanya patoro ya mara kwa mara kwenye maeneo ambayo kuna shida ya umeme na kwamba suala hilo sio kwenye msimu wa siku kuu tu ni wakati wowote hule kuhakikisha umeme unakuwepo kwenye maeneo ya wananchi.

Elias Mahona ni mkazi wa Kata  Mganza amesema kuwa endapo kama umeme utafika kwenye maeneo ya vijiji utafungua uwigo mpana wa ajira za kujiajiri kwani kwasasa vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutokana na ukosefu wa ajira hivyo umeme utaweza kufungua mirango ya kujiajiri kwa vijana wengi.

Bi,Zawad Nashoni  mkazi wa kijiji cha Nyang’homango amemuomba waziri wa nishati kusaidia umeme uweze kufika kwa haraka zaidi kwenye maeneo yao kwani wamekuwa wakipata shida kutokana na kukosa umeme kwenye maeneo hayo.