Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akizungumza na wananchi wa kata ya Mganza wakati wa ziara yake Wilayani Chato ya kukagua utekelezaji wa uwekaji wa umeme vijijini(Rea awamu ya tatu) |
Waziri wa Nishati Dr,Medad Kalemani akiwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chato (Kulia)wakati alipokuwa akizungumza na wananchi. |
Mkuu wa wilaya ya Chato ,Shaaban Ntarambe akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyang’homango wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kwenye Wilaya hiyo. |
Wananchi wa kijiji cha Nyang’homango wakimsikiliza Waziri wa Nishati wakati wa ziara yake ya kikazi. |
Waziri wa Nishati,Medad Kaleman na Mkuu wa Wilaya ya Chato wakikagua kituo cha afya cha Kata ya Mganza wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Chato. |
Serikali inatarajia kujenga mradi
mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa mega
watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha miundombinu ya umeme na upatikanaji wa
uhakika kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara ya siku
moja ya kikazi Wilayani Chato Mkoani
Geita ilikuwa na lengo la kukagua na kujionea miundombinu ya umeme wa Rea awamu ya tatu ,Waziri wa Nishati ,Dr Medadi
Kalemani ,alisema kuwa hali ya umeme inaendelea kuimarika siku hadi siku na
kuna maeneo mengi yameanza kupata umeme wa kutosha.
“Hapo Nyuma mwezi Novemba tulikuwa
tunajitahidi kukarabati mahali ambapo kulikuwa na ubovu wa mitambo lakini kwa
sasa hali inaendelea vizuri maeneo mengi ya nchi yetu yanapata umeme kwa wingi na tunaanza kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme
wa maji wa mega watt 2100 kwenye
maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia
kuimalisha miundo mbinu ya umeme na
upatikanaji wa umeme hapa nchini”Alisema Kalemani.
Aidha Dr,Kaleman amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye
maeneo yao pindi kunapotoakea tatizo na kwamba wateja ambao wamelipia umeme kwa
mwaka 2017 ni vyema Tanesco wakahakikisha wanawaunganishia umeme haraka
iwezekanavyo kwani mwaka 2018 haitakiwi
kuwepo kwa mteja ambaye ajaunganishiwa huduma hiyo.
Kalemani ameendelea kutoa wito kwa
watendaji wa Tanesco kuhakikisha katika kipindi hiki cha msimu wa siku kuu ya
chrismas na mwaka mpya kuimarisha utoaji
wa umeme na uimalishaji wa miundombinu na kufanya patoro ya mara kwa mara
kwenye maeneo ambayo kuna shida ya umeme na kwamba suala hilo sio kwenye msimu
wa siku kuu tu ni wakati wowote hule kuhakikisha umeme unakuwepo kwenye maeneo
ya wananchi.
Elias Mahona ni mkazi wa Kata Mganza amesema kuwa endapo kama umeme utafika
kwenye maeneo ya vijiji utafungua uwigo mpana wa ajira za kujiajiri kwani
kwasasa vijana wengi wamekuwa wakikimbilia mijini kutokana na ukosefu wa ajira
hivyo umeme utaweza kufungua mirango ya kujiajiri kwa vijana wengi.
Bi,Zawad Nashoni mkazi wa kijiji cha Nyang’homango amemuomba
waziri wa nishati kusaidia umeme uweze kufika kwa haraka zaidi kwenye maeneo
yao kwani wamekuwa wakipata shida kutokana na kukosa umeme kwenye maeneo hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.