ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 25, 2024

MWENEZI MRAMBA ASHUSHA NONDO KWA VIONGOZI WA TAASISI ZISIZOKUWA ZA SERIKALI


NA VICTOR MASANGU, PWANI
Katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM)  Mkoa wa Pwani David Mramba amewataka viongozi wa taasisi zisizokuwa za kiserikali kuachana na tabia ya kubezana na badala yake wanapaswa kuwa na umoja,mshikamano na kuwa wazalendo na Taifa lao.

Mramba ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu ambacho kimewakutanisha   taasisi mbali mbali zisozokuwa za kiserikali kwa ajili ya kujadili mambo pamoja kupewa elimu juu ya mambo mbali mbali mbali ikiwemo mambo ya mikopo,mahusiano, elimu ya uchaguzi wa serikali za mitaa,mizani ya kazi,pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Mramba alisema kwamba taasisi hizo zinapaswa kuweka mipango madhubuti katika kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujenga mahusiano mazuri na taasisi nyingine.

Pia alitaka taasisi hizo zifanye kazi kwa maslahi ya Taifa na sio kufanya kazi kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.

"Kitu kikubwa ambacho kinatakiwa kwa taasisi ni kuwa na umoja pamoja na kuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na mambo ya kubezana kitu ambacho sio kizuri na kuwahumiza kuzidi kushirikiana katika kila jambo,"alisema Mramba.

Aidha Katibu huyo alimpongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu kwa kuweza kutenga fedha nyingi kwa ajili wa utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa wananchi wake.

Alibainisha kwamba Rais amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo katika nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu,afya,maji miundombinu ya barabara pamoja na huduma nyingine za kijamii.

Katika hatua nyingine Katibu huyo ameagiza tasisi  zote ambazo sio za kiserikali katika   Mkoa wa Pwani kuhakikisha kwamba  zinajisajili zote  ifikapo Juni 30 mwaka huu ili ziweze kutambulika na kuweka mipango mikakati ya kufanya kazi.

Katika kikao hicho maalumu  kimehudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka taasisi 22  zisizokuwa za kiserikali sambamba viongozi wa (CCM) kutoka  mikoa ya Ruvuma,Morogoro,Dar es Salaam pamoja na wenyeji Mkoa wa Pwani.

Friday, May 24, 2024

DUH KUMBE HADI 'MAKAKA POA' NAO WAPO - KERO YA KUTAPAKAA KONDOM SHULE YA MSINGI KITANGIRI MWANZA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Baada ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Dkt Angeline Mabula kutoa malalamiko yake katika Bunge la 12 Mkutano wa 15, kikao cha 12 kuhusu changamoto zilizopo katika shule ya msingi Kitangiri ambayo inakutumika vibaya nyakati za jioni na 'madada powa' wakifanya biashara ya ngono kwenye eneo hilo na kuomba Wizara husika itenge fedha kwaajili ya ujenzi wa uzio kwa shule hiyo ili kuokoa maisha ya watoto wanaochezea 'kondomu' kama mpira. Wakati zoezi la ujenzi wa ukuta kwa shule hiyo likifanyika, hatimaye kipindi cha 'Drive Mix' kutoka radio Jembe Fm kinapata nafasi ya kuzungumza na diwani wa kata hiyo Mhe. Donard Ndalo Protas ambaye naye anatiririka haya akitusanua pia uwepo wa Makaka poa'. "Ilikuwa ni aibu kwasababu hawa madada powa na makaka powa walikuwa wakifanya biahsra yao ya kujiuza maeneo ya shule ndani ya shule, kwenye madarasa, kitu ambacho ni kibaya" "Ni kweli wale walinzi walituhumiwa kuwa na tabia ya kuwapokea hao 'Madada na Makaka poa' kama biashara, wale walinzi walikuwa wakinunua maboksi ya kondom na kuwauzia hao wateja wao, wakifanya biashara mbili, biashara ya kwanza kuwapatia chumba ambacho ni darasa wanalipia na biashara ya pili ni kondom" "Mbaya zaidi mipira hiyo ilikuwa inaachwa ikizagaa maeneo ya shule na watoto wetu walikuwa wakiiokota na kuipuliza, wakifanya mipita ya kuchezea na wengine kama maputo" "Kama kiongozikweli ukipata hii habari ba ukashuhudia mwenyewe kwa macho yako huwezi kuridhika nayo lazima upige kelele"

Taasisi ya CRDB Bank Foundation, UNFPA kushirikiana kuwainua vijana kiuchumi.

 

Dar es Salaam. Tarehe 23 Mei 2024: Katika kuongeza ujumuishi wa wananchi kiuchumi hasa makundi maalumu, Taasisi ya CRDB Bank Foundation imesaini mkataba wa makubaliano kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kuwawezesha kiuchumi vijana kuanzia miaka 18 hadi 24, waliopo shule na wale ambao wameacha shule kwasababu moja au nyengine.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya kutia saini mkataba huo wenye thamani ya dola 300,000 za Marekani, sawa na shilingi milioni 800, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa amesema ushirikiano huo unatokana na kufanana kwa malengo na mipango ya pande zote mbili katika kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi.
“Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2023, Taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation tumeelekeza nguvu kubwa katika kuanzisha programu za kuwawezesha vijana na wanawake kujumuishwa kwenye mfumo rasmi wa huduma za fedha, kuwapa mafunzo na mitaji wezeshi kupitia Programu yetu ya Imbeju. 

Ushirikiano huu na UNFPA unakwenda kuimarisha jitihada hizi na kuwezesha kufikia vijana wengi zaidi,” amesema Tully.

Kama ilivyo kwa CRDB Bank Foundation, UNFPA inatekeleza programu tofauti za kuwainua wananchi kiuchumi, kuwajengea uwezo wa kuzitambua haki zao, kupunguza migogoro ya kifamilia na kijinsia, pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa wanawake, mabinti na vijana azma ikiwa ni kujenga vijana wenye uwezo wa kiuchumi kuzikabili changamoto za kila siku.
Tully amesema ushirikiano huu unawalenga vijana walio masomoni na wale walioshindwa kuendelea na masomo kwasababu mbalimbali, walemavu pamoja na mabinti waliopata ujauzito wakiwa masomoni. Katika utekelezaji wake, amesema wanakusudia kupunguza changamoto za upatikanaji wa ajira, kuwapa elimu ya fedha, kuwapa elimu ya afya ili kupunguza mimba za utotoni, kupunguza ukatili wa kijinsia na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU), katika mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma.

“Ushirikiano wetu na UNFPA utajikita kwenye maeneo mawili ya msingi. Kwanza ni kutoa elimu na maarifa ya kujitambua kwa vijana walio shule na walioa nje ya shule itakayojumuisha mafunzo juu ya huduma rafiki za afya, unyanyasaji wa kijinsia, na jinsi ya kuepuka na namna ya kuishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi. Eneo la pili ni kutoa elimu ya fedha na ujasiriamali kwa vijana na mabinti ili kuwajengea mazingira ya kutekeleza majukumu yao kikamilifu,” amefafanua Tully.

Kwa upande wake, Mark Bryan Schreiner, Mwakilishi Mkazi wa UNFPA nchini amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi tofauti inayolenga kuwainua wananchi hasa wa makundi yaliyosahaulika katika jamii ili kuwa na uchumi jumuishi na wanufaika wakubwa wa programu zake ni wanawake, vijana wakiwamo mabinti wenye rika la balehe, na wahamiaji wanaoomba hifadhi kutokana na migogoro ya kisiasa na kijamii inayotokea kwenye mataifa jirani.

“Tukiangalia changamoto zinazowakabili vijana nchini ikiwamo upatikanaji  wa mitaji, ukosefu wa ajira na elimu  ya ujasiriamali, UNFPA inayo kila sababu ya kushirikiana na wabia wa kimkakati kusaidia kuwawezesha vijana nchini kushiriki kujenga uchumi wa taifa lao,” amesema Schreiner.
Kwa sasa, Schreiner amesema UNFPA inatekeleza programu yake ya tisa nchini inayohamasisha uzazi salama kwa kuitambua na kuikubali kila mimba inayopatikana, pamoja na kumwezesha kila kijana kutimiza ndoto za maisha yake.  “Lengo letu ni kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma hivyo tunashirikiana na wadau wenye mtizamo kama wetu kama ilivyo Taasisi ya CRDB Bank Foundation,” amesema Schreiner.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, zaidi ya nusu ya Watanzania ni vijana wenye umri chini ya miaka 24. Matokeo ya sensa hiyo yanaonyesha asilimia 44 ya watu wote ni watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 huku asilimia 19 wakiwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 mpaka 24. Hii ni idadi kubwa ya wananchi watakaoguswa na mradi huu wa kwanza wa ushirikiano kati ya CRDB Bank Foundation na UNFPA.








Thursday, May 23, 2024

UKINUNUA TV, GODORO, MABATI AU SARUJI NAKUPELEKEA KWAKO BURE DIWANI KATA YA KITANGILI MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Katika jitihada za kusaidia wananchi wake kujikwamua kiuchumi pamoja na kutatua changamoto ya kukosa usafiri kufuata tiba ya dharula kama mahitaji ya gari la wagonjwa hasa kwa akinamama wanaohitaji kujifungua na watoto wanaohitaji kuwahishwa kwenye vituo vya afya kupata tiba, Diwani wa Kata ya Kitangili mkoani Mwanza Donald Ndalo amekuja na mbinu hii.......

RFO PWANI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA WANAHABARI WA PWANI




NA VICTOR MASANGU,PWANI 

Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Pwani mrakibu Mwandamizi Jenifa Shirima  ametoa elimu kwa waandishi  habari wa Mkoa wa Pwani kuhusiana na masuala mbali mbali ya kuandika habari zinazohusiana na  kujikinga na majanga  mbali mbali ya moto.

Kamanda Shirima ameyasema hayo wakati aliposhiriki halfa ya  maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari ngazi ya Mkoa wa Pwani ambayo yamefanyika leo Mei 23 mwaka huu katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Kamanda Shirima alisema kwamba waandishi wa habari ni kiungo kikubwa  katika kuelimisha jamii juu ya kuweza  kukabiliana na majanga ya moto.

Aliongeza kuwa kama Jeshi la zima moto  wataendelea kutoa elimu katika makundi mbali mbali ikiwemo kundi la waandishi wa habari lengo ikiwa ni kuandika habari za kuwaelimisha wananchi kuhusiana na jinsi ya kujikinga na majanga ya moto.
 


Tuesday, May 21, 2024

KIKAO CHA KUTATHIMINI MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA CHAFANYIKA JIJINI TANGA

 

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Imani Clemence akizungumza wakati wa kikao cha kutathimini na kujadili utendaji wa Programu ya Utekelezaji wa Mradi wa Afya Hatua iliyopo chini ya Shirika la THPS na kufadhiliwa na Pepfar CDC kilichofanyika Jijini Tanga na kuhusisha wadau mbalimbali Mkoani Tanga wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya kutokana na mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa watumiaji kitaifa.


Mkurugenzi Mshirika wa Huduma za Jamii –Huduma za Kinga (THPS) Dkt Appolinary Bukuku akizungumza katika kikao hicho





Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba akizungumza jambo wakati wa kikao hicho






Na Oscar Assenga, TANGA.


KIKAO cha kutathimini na kujadili utendaji wa Programu ya Utekelezaji wa Mradi wa Afya Hatua iliyopo chini ya Shirika la THPS na kufadhiliwa na Pepfar CDC umefanyika leo Jijini Tanga na kuhusisha wadau mbalimbali Mkoani Tanga wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya kutokana na mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa watumiaji kitaifa.

Lengo kubwa la kuwaida wadau wa utoaji wa huduma za methadone kwa waraibu za Kulevya mkoani humo pia kilikuwa na lengo la kupitia na kujadili mafanikio ya utoaji wa methadone kwa waraibu na kujadili changamoto zinazoikabili huduma hiyo na kutengeneza mikakati ya kuboresha huduma kwenye mkoa huo.

Wadau wengine walioshiriki kwenye kikao hicho ni kutoka wizara ya Afya,wawakilishi wa Timu za wasimamizi za Afya ngazi ya mkoa na Halmashauri,Jeshi la Polisi,Asasi za Kiraia zinazowaibua waraibu wa dawa za kulevya na wadau wa THPS wanaoshirikiana na serikali katika kutoa huduma na kuziboresha katika kutoa mafunzo ya huduma za methanone ,wanasaidia vifaa mbalimbali vya kazi ,watumishi ,vikao ,wanajivunia mafanikio yaliyopo leo hii waraibu

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Imani Clemence alisema Serikali kushirikiana na wadau CDC kupitia THPS imeweka nguvu kubwa kuboresha huduma za waraibu kuhakikisha wanapata huduma bora ili afya za ziweze kuimarika na wafikie hali ambayo wanaweza kuisha maisha ya kawaida na kushiriki kujenga uchumi.

Alisema kwamba hadi kufikia Mwezi Mei 2023 Mkoa wa Tanga ulikuwa na waraibu 1094 ambao walishawahi kuanzishiwa Methadone na kati yao 683 ndio ambao bado wanaendela na dawa hao wengine wapo wapi wengine wahama na wengine wamefariki.

Alisema kwamba kwa kushirikiana na wadau CDC na Shirika la THPS wametoa mchango mkubwa na Serikali inatambua juhudi zao kwenye mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na huduma kwa waraibu .

“Tutaendelea kuwapa ushirikino katika miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani Tanga sisi tupo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha wakati wote mtakapokuwa mkiitaji na niwashukuru wadau wote tushirikiana nao kwenye pambano dhidi ya dawa za kulevya”Alisema

Awali akizungumza Mkurugenzi Mshirika wa Huduma za Jamii –Huduma za Kinga (THPS) Dkt Appolinary Bukuku alisema wanajadili changamoto za huduma za waraibnu wao kama sehemu ya wadau ili waweze kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi kwa jamii ya watanzania hasa huduma wanazozitoa za waraibu kwenye mkoa wa Tanga.

Alisema wamekusanyika na wadau mbalimbali hivyo kila mdau kuitwa ni muhimu kuchangia namna bora ya kuhakikisha huduma za waraibu walioathirika na dawa za kulevya zinakwenda vizuri na watapata watu wakaokwenda kufanya kazi kwenye jamii na kuchangia pato la taifa kama watanzania.

“tunatambua kuna watu wameingia huko na walikuwa na uwezo wa kufanya kazi kama sisi lakini kutokana na athari walizokutana nazo wameshindwa kufanya kazi na kutengwa na jamii huduma hizo zilikuwa zinatolewa na Serikali na wadau zitawasdia kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuchangia pato la Taifa”Alisema

Hata alisema wamekutana wao kama wadau wakiwa na asasi za kijamii na watu wanaotoa huduma kwenye kliniki za MAT lengo likiwa kupata changamoto kutoka wa wanufaika wa huduma pamoja na kusikia changomoto kwa wale wanaowahudumia.

“Sisi sote kwa umoja wetu tuweze kutoa mchango wa kuboresha hasa zile Asasi ambazo zinawaibua,vyombo vya ulinzi ambavyo vinawachukulia kama wahalifu lakini tunatambua jamii imewatenga na kuwaona watu ambao hawafai na wao wanawajibu wa kutoa elimu kwa jamii ili wawahudumie kwa upendo ili warudi kwenye hali ya kawaida tunaishuku mamlaka wanajitahidi zao“Alisema

Naye kwa upande wake Afisa kutoka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini Sara Ndaba alisema kwamba wanaishukuru Shirika la la (THPS) kwa kuandaa kikao hicho cha wadau kwani wamekuwa wakiwasadia kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya.

Alisema katika kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini,Jeshi la Polisi,Jeshi Magereza na Wizara ya afya wote wanapambana kwenye vita dhidi ya dawa za kulevya na mkoa umethirika na dawa za kulevya.

Hata hivyo alisema kwamba uwepo wao utasaidia kukabiliana na tatizo hilo na Tanga ikaondokana na tatizo la dawa za kulevya kwa maana hali bado so shwari kutokana na kwamba kituo cha Mat kinahudumia waraibu zaidi watu 1,113 mpaka sasa kutoka kwa Asasi za kiraia ambazo zimekuwa zikiwaibua na kuwapeleka kwenye kituo .

Benki ya CRDB yaendelea kusaidia jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya elimu nchini

 

 
Katika utekelezaji wa Sera yake ya Uwekezaji kwenye Jamii, Benki ya CRDB imeendelea kusaidia jitihada za Serikali kuboresha mazingira ya elimu nchini. 
 
Jitihada hizo zimefanyika mkoani Manyara, katika Wilaya za Mbulu na Babati, siku chache kabla ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki ya CRDB uliofanyika jumamosi ya tarehe 18 Mei 2024

Baadhi ya shule zilizonufaika na uwezeshaji huo ni  Shule za Msingi shikizi Muungano ya Babati Mjini iliyokabidhiwa madarasa Mawili na Ofisi ya Walimu na shule ya Endagikot iliyoko wilayani Mbulu iliyokabidhiwa Darasa na madawati kwaajili ya Watoto wenye uhitaji malumu.
Misaada ya madarasa kwa shuke za msingi shikizi Muungano yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon tarehe 14 Mei 2024 na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga ambaye aliishukuru Benki ya CRDB kwa msaada huo unaounga juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu nchini.

Aidha, tarehe 15 Mei 2024, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo alikabidhi darasa kwa ajili ya Watoto wenye mahitaji maalumu kwa Shule ya Msingi Endagikot iliyopo wilaya ya Mbulu na kupokelewa  na Mkuu wa Wilaya wa Manyara, Mhe. Lazaro Twange ambaye  alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara ambaye aliishukuru Benki ya CRDB kwa mara nyingine kuchangia ukuaji elimu katika Mkoa wa Manyara.
Ujenzi wa madarasa hayo ni sehemu ya utekelezaji wa sera yetu ya uwekezaji kwa Jamii (Policy) inayotenga asilimia moja ya faida ya benki kila mwaka kuwezesha miradi ya maendeleo katika jamii.

Benki pia inatekeleza mradi wa Keti Jifunze unaolenga kutatua changamoto za elimu zinazojumuisha upungufu wa madarasa na ofisi za walimu, madawati, vyoo na miundombinu mingine muhimu.









 

Monday, May 20, 2024

DIDDY AOMBA MSAMAHA KWA TABIA YAKE 'ISIYO NA SABABU'

. 

Sean "Diddy" Combs ameomba msamaha kwa tabia yake "isiyo na udhuru" baada ya CCTV kuonekana kumuonyesha akimshambulia mwimbaji Casandra "Cassie" Ventura.

Akiongea kwenye video iliyotumwa kwenye ukurasa wake wa Instagram, nyota huyo wa rap alisema aliwajibika kikamilifu kwa matendo yake kwenye klipu hiyo.

Kanda hiyo, iliyorushwa hewani na CNN mapema wiki hii, ilionekana kumuonyesha Bw Combs akimpiga teke na kumsukuma mpenzi wake wa zamani kwenye njia ya ukumbi wa hoteli.

"Nilichukizwa nilipofanya hivyo. Nimejichukia sasa," alisema katika taarifa yake. "Nilienda na nikatafuta usaidizi wa kitaalamu.

Niliingia kwenye matibabu, kwenda kituo cha kupata usaidizi. Ilibidi nimuombe Mungu rehema na neema zake. Samahani sana." BBC haijaithibitisha kwa uhuru video hiyo, ambayo inaonekana kuwa ni mkusanyiko wa video za uchunguzi wa tarehe 5 Machi 2016.

Kulingana na CNN, ilirekodiwa katika Hoteli ya InterContinental ambayo sasa imefungwa huko Century City, Los Angeles


WANAHISA WA BENKI YA CRDB WAIDHINISHA MALIPO YA GAWIO LA SHILINGI 130.6 KWA MWAKA WA FEDH WA 2023

 

Arusha 18 Mei 2024 - Wanahisa wa Benki ya CRDB wameidhinisha kwa kauli moja mapendekezo ya Bodi ya Wakurugenzi kuhusu malipo ya gawio la Shilingi 50 kwa kila hisa jambo linalofanya jumla ya thamani ya gawio la mwaka wa fedha 2023 kufikia Shilingi bilioni 130.6, sawa na 30.9% ya faida halisi.

Katika taarifa yake wakati wa Mkutano Mkuu wa 29 wa Benki hiyo uliofanyika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Dkt. Ally Laay alisema gawio lililoidhinishwa kwa kila hisa ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganishwa na Shilingi 45 kwa kila hisa iliyotolewa jana, ikiashiria ukuaji mkubwa wa mapato kwa kila hisa kufikia Shilingi 161.9 ikilinganishwa na Shilingi 134.1 mwaka 2022.
"Kwa mara nyingine tena, tunafuraha kuwatoa thamani endelevu kwa wanahisa wetu. Utendaji wa Benki mwaka 2023 ulikuwa mzuri, ikiwa ni uthibitisho wa mafanikio ya mkakati wetu mpya wa miaka mitano wa muda wa kati wa 2023 - 2027. Benki yetu na kampuni zake tanzu ilipata faida halisi ya Shilingi 422.8 bilioni, ongezeko la 20.3%," alisema Dkt. Laay.

Alibainisha zaidi kuwa kampuni tanzu za Benki ya CRDB zilitoa mchango chanya kwa mwaka uliopita. CRDB Bank Burundi ilipata ukuaji mzuri wa 30.7% katika Faida Baada ya Kodi, na kufikia Shilingi 30.2 bilioni. Amesema pamoja na kampuni za CRDB Bank Congo na CRDB Insurance Company Ltd kutotengeneza faida, kampuni hizo zimeonyesha mwanzo mzuri unaoashiria kuwa na mchango mkubwa katika siku za usoni. Jumla ya mchango wa kampuni tanzu kwenye Faida Baada ya Kodi ulikuwa 6%.
"Ninafurahia kuona juhudi zetu za upanuzi za kikanda zinaleta matokeo chanya. CRDB Bank Burundi imefanikiwa kuongoza kwa faida katika soko la nchi hiyo katika kipindi cha robo ya kwanza ya 2024. Zaidi ya hayo, kampuni yetu ya nchini DRC imepokelewa vizuri nchini humo tangu kuanzishwa kwake mwezi Julai 2023, na kuvutia wateja na biashara nyingi nchini humo,” aliongeza.
Afisa Mkuu wa Fedha, Fredrick Nshekanabo, aliripoti kuwa Mizania ya Benki ya CRDB na kampuni zake tanzu imeendelea kuimarika ikishuhudia ukuaji wa mwaka wa 14.5% kutoka shilingi trilioni 11.6 mwaka 2022 mpaka shilingi trilioni 13.3 mwaka 2023. Ukuaji huo ulichangiwa zaidi na ongezeko la 22.8% la mikopo kufika shilingi trilioni 8.4 ikichangiwa na ongezeko la amana za wateja zilizopanda kwa 8.0%, mikopo kwa 73.9%, na kukua kwa mtaji wa wanahisa kwa 20.4%. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesisitiza kuwa mkakati mpya wa biashara umekuwa muhimu kwa mafanikio ya benki, ukifanya kazi kama ramani ya kuboresha utendaji kazi. Amesema kwa sehemu kubwa Benki ya CRDB ilijikita katika uwekezaji kwenye mifumo ya kidijitali, huku akieleza kuwa benki imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa mradi wa mfumo mkuu mpya wa uendeshaji wa benki (CBS).

Nsekela pia alisema kuwa Benki ya CRDB imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kukuza ujumuishi wa kifedha, kwa wajasiriamali na wafanyabiashara. Kupitia mpango wa IMBEJU taasisi ya CRDB Bank Foundation imeboresha uwezeshaji kwa vijana na wanawake. Zaidi ya hayo, Benki imeunda ushirikiano wa kimkakati ili kufadhili vyema miradi ya maendeleo nchini.
Nsekela alielezea mipango ya siku za usoni ya Benki ya CRDB na kampuni zake, akisisitiza kuongeza kwa mchango wa kampuni tanzu zilizoanzishwa, kuboresha huduma kwa wateja na kuwekeza zaidi katika ubunifu wa kidijitali. Kadhalika, amesema Benki hiyo itaendelea kuongeza usimamizi mkubwa katika vihatarishi, na kuhakikisha inaendana na mabadiliko ya usimamizi, na kuhakikisha utawala bora.

Kwa upande mwingine, Wanahisa wa Benki ya CRDB waliidhinisha kampuni ya Price Water Coopers (PWC) kama Wakaguzi wa Nje wa Benki kwa mwaka wa fedha wa 2024. Wanahisa wa Benki pia walichagua tena Wajumbe wawili wa Bodi, Prof. Faustine Bee kuwakilisha wanahisa wenye umiliki chini ya 1%, na Gerald Kassato kuwakilisha wanahisa wenye hisa kati ya 1% na 10%.
Akizungumzia malipo ya gawio hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei, alieleza kufurahishwa kwa wanahisa kwa kuendelea kupata ongezeko la gawio, akibainisha kuwa hisa za benki hiyo zimebakia kuwa chachu ya wawekezaji kwasababu benki haijawahi kushindwa kulipa gawio kwa wanahisa wake.