Washindi wa Clean House wakabidhiwa zawadi zao toka Colgate Pamolive
Wakazi wa jijini Dar es salaam na mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya waliokuwa wakinunua bidhaa za Sta- Soft na Axion (sabuni ya kuoshea vyombo) zinazosambazwa na Colgate Pamolive wamekabidhiwa zawadi zao kupitia promosheni iliyokuwa ikiendeshwa na Colgate Palmolive.
Kampuni ya Colgate Pamolive imekuwa ikiendesha promosheni maalum ya CLEAN HOUSE kwa muda wa miezi miwili iliyokuwa na lengo la kuwafahamisha watanzania jinsi bidhaa zao za Sta- soft ambazo ni maalum kwa kufulia nguo na Axion maalum kwa usafi wa vyombo vya nyumbani. Bidhaa hizi ni maalum kwa kufanya usafi kwa ufanisi mkubwa.
Akieezea bidhaa hizo Afisa Masoko wa Colgate Pamolive Bw, Meshack Mdingi alisema “ Lengo la promosheni hii ni kuwajulisha wateja wetu jinsi wanavyoweza kuepuka magonjwa ya ngozi kwa kufua nguo zao na Sta- soft inayotunza nguo zako na kuziweka laini wakati wote na harufu nzuri na kusafisha vyombo vya ndani. Wateja wetu tunawashauri watumie bidhaa yetu ya Axion inayofanya vyombo vibaki na mng’ao wake mzuri siku zote”
Walioibuka washindi kwenye promosheni ya Clean House ni wale wote walionunua bidhaa hizi kati ya September na Oktoba ambapo walichaguliwa kupitia droo maalum iliyofanyika wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya walioibuka washindi kupitia promosheni hiyo ni Valeria Urio mkazi wa Dar Es Salaam, aliyejishindia Jiko la Gas cooker, Abeid Semira mkaazi wa Mwanza aliyejishidia Jagi la Kuchemsha maji, Hassan Ibraim mkaazi wa Tanga kati ya wengine 50.
Bw, Mdingi alisema hadi kufikia mwisho wa promosheni wameweza kuwaelimisha watu wengi kuhusiana na Usafi wa jamii, pia kurudisha faida wanazopata kwa jamii kwa kutoa zawadi ambapo jumla ya Majiko ya Gesi 3,Seti za Masufuria 8, Seti za jagi za maji 8, pamoja na mashine za umeme za kukausha mkate (Toaster) 8 za kisasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na zawadi nyengine ndogo ndogo.
Kupitia bidhaa zetu bado tutaendelea kuwafikia wateja wengi kwa kufanya promosheni kama hizi huku tukitoa elimu kuhusiana na usafi kwa jamii na kutoa zawadi tofauti tofauti ili kuwafaidisha wale wote wanatumia bidhaa zetu za Colgate Pamolive, alimazia Bw, Mdingi