Katika kuitikia wito wa Clouds fm (X-MASS ZAWADI)wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuwawezesha kutabasamu hasa katika kipindi kama hiki cha kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa masia Yesu Kristo, Benki yako ya FBME kupitia tawi lake la Mwanza jana jioni imetoa zawadi ya krismasi na mwaka mpya kwa kituo cha watoto wanaoishi mazingira magumu cha 'Back Home Upendo Daima' kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza.
Afisa wa FBME BANK bwana Alawi Mdee akikabidhi sabuni kwa mlezi wa kituo cha 'Back Home Upendo Daima' Sister Monica.
Marry X-mass; Zawadi za mchele, mafuta, sabuni, chumvi, unga, sukari, unga wa ngano yaaaani....Ni tabasamu tu na vicheko kwa watoto!....AKSANTE FBME BANK!!!
Chakufurahisha Watoto hawa wamefundishwa kusaidiana na kuishi kwa upendo wa kumjua mungu, hivyo kila wanachokifanya wanafanya pamoja wakisaidiana kama ndugu wa tumbo moja.
Wadau wa FBME BANK walipata pia fursa ya kutembelea vyumba wanapolala watoto hao.
Ni vitanda vya juu na chini twaita Double deka vyenye kutosha watoto wote 30 wa kituo hiki, kila mtoto na kitanda chake. Nawapa shavu uongozi wa kituo hiki kwa kuwa na mazingira mazuri yenye kuzingatia usafi kama wa nyumbani kwa baba na mama.
Kuishi kunahitaji misingi bora na kanuni, si kwa mkubwa tu bali hata kwa mdogo.
Mama mlezi wa kituo hiki Anna Malima, akitoa maelezo jinsi watoto wanavyoishi na malezi kwa wadau wa FBME tawi la Mwanza.
Mlezi wa wa kituo cha 'Back Home Upendo Daima' sister Monica ametoa shukurani kwa benki ya FBME kwa msaada huo wa zawadi ya X-mass kwani ni nafasi inayowafanya watoto kama hao wajisikie vyema zaidi na kujiona nao ni sehemu katika jamii, aidha amewataka watu na mashirika mengine kuiga mfano huo wa FBME kwani watoto kama hao ni Watoto wetu sisi sote.
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania (taifa stars) Silvester Marsh kwaniaba ya kocha mkuu wa timu hiyo Jan poulsen (aliye mapumzikoni kwao Norway) amekitaja kikosi cha wachezaji 23 wa timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la Nile basin mashindano yanayotaraji kuanza kutimua vumbi rasmi tarehe 5 january 2011 nchini Misri.Tofauti na wengi tulivyozoea, Tukio hilo limefanyika leo katika eneo la wazi la uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo kocha huyo msaidizi yuko ziarani kwa ajili ya shughuli maalum huku likishuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa soka waandishi wa habari na wapenzi wa soka wa jiji la miamba.
KIKOSI KAMILI NI KAMA IFUATAVYO
GOALKEEPERS:-
1.JUMA KASEJA - SIMBA SC
2.SHAHBAN KADO -MTIBWA FC
3.SAID MOHAMED - MAJIMAJI SC
DEFENDERS:-
4.SHADRACK NSAJIGWA - YOUNG AFRICAN
5.MWASIKA STEPHANO - YOUNG AFRICAN
6.AGREY MORRIS - AZAM FC
7.KELVIN YONDANI - SIMBA SC
8.JUMA NYOSSO - SIMBA SC
9.NADIR HAROUB - YOUNG AFRICAN
MIDFIELDELS:-
10.IDRISSA RAJABU - SOFAPAKA
11.NURDIN BAKARI - YOUNG AFRICAN
12.SHAHBAN NDITI - MTIBWA FC
13.HANRY JOSEPH - NORWAY
14.JABIR AZIZ - AZAM
15.ABDI KASSIM - YOUNG AFRICAN
FOWARD PLAYERS
16.SALUM MACHAKU - MTIBWA FC
17.MRISHO NGASA - AZAM
18.NIZAR KHALFAN - CANADA
19.GODFREY TAITA - KAGERA SUGAR
20.ATHUMAN MACHUPPA - SWEDEN
21.JERRY TEGETE - YOUNG AFRICAN
22.SAID MAULID - ANGOLA
23.ALI AHMED SHIBOLI - SIMBA SC
Kocha huyo msaidizi amesema kuwa mazoezi ya Stars yataanza rasmi siku ya jumatatu ambapo kambi itakuwa uwanja wa karume jijini dar na tarehe 3jan 2011 wataanza safari kuelekea Misri. Tarehe 5jan2011 Stars kufungua na wenyeji. Wachezaji kama Erasto Nyoni, Mohamed Banka na Haruna Shamte hawajaachwa kutokana na viwango vyao kushuka bali ni kutokana na kuwa majeruhi. Kuhusu suala la kuwarejesha kikosini Machupa na Said Maulid Kocha Marsh amesema kuwa uamuzi huo umekuja kutokana na wachezaji hao kujaa uwezo kwa michezo ngazi za kimataifa.
Kocha Marsh Anauhakika na kikosi hicho alichokitaja kuwa cha ushindi akiwa na imani kubwa kuwa kila mchezaji atacheza kwa bidii na hatimaye kulipandisha soka la Tanzania katika viwango vya soka duniani.
TANESCO YATANGAZA MGAO WA UMEME NCHI NZIMA.
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) juzi lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.Tangazo hilo la mgawo ambalo limekuja katika kipindi ambacho mjadala wa jenereta za kampuni ya Dowans ukiwa umeibuka tena, linatarajiwa kuongeza gharama za maisha kutokana na ukweli kuwa viwanda vingi vitalazimika kutumia jenereta katika uzalishaji licha ya Tanesco kutangaza kuwa vitapewa umeme nyakati za mchana. Tangazo la Tanesco limetolewa wakati kukiwa na ahadi kemkem za kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme, huku Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwa imeliruhusu shirika hilo la umma kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.5. "Mgawo utahusisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa isipokuwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara." Kwa mujibu wa Badra Masoud, mgawo wa sasa umetokana na upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy, kuzimwa. Alisema kisima hicho kinachotoa gesi kimezimwa kwa ajili ya kukifanyia matengenezo ya kawaida, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40 za umeme zinazokwenda katika gridi ya taifa. Pan African Energy ni kampuni ambayo inachimba gesi hiyo eneo la Songo Songo, Kilwa na baadaye husafishwa na kusafirishwa na kampuni ya Songas ambayo huzalisha umeme wa megawati 180 eneo la Ubungo na kuiuzia Tanesco. Kwa mujibu wa makubaliano, Songas hutakiwa kuzalisha umeme kwa kiwango kilicho kwenye mkataba na ni jukumu la Tanesco kuutumia umeme huo wa gesi kulingana na mahitaji yake au kutoutumia. Tanesco huilipa Songas hata pale inapokuwa haitumii umeme wa kampuni hiyo.Badra alisema kuwa kiwango hicho cha upungufu wa umeme kinaweza kuongezeka hadi kufikia megawati 120 jambo alilosema likitokea, shirikma hilo litazidisha mgawo.
Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo huku maeneo yaliyopata umeme katika muda huo yakiukosa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku mara tatu kwa wiki. Kwa mujibu wa Badra, ratiba ya mgawo huo zitatangazwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari. Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo hayatakumbwa na mgawo huo akitaja baadhi kuwa ni hospitali, pampu za maji, migodi na viwandani ambako alisema vitakosa umeme usiku ili mchana viendelee kuzalisha. Alisema kuwa maeneo yanayopata umeme kutoka transoma ya Kipawa hawatakumbwa na mgawo huo, kutokana na kukamilika kwa matengenezo yake. Akizungumzia siku kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, Badra alisema Tanesco itajitahidi kuhakikisha wananchi wanasherehekea siku hizo bila kukosa umeme huku akiwaomba radhi kwa mgawo huo.
NIMEKUTANA NA BANGO HILI ASUBUHI YA LEO NIKAKUMBUKA MPANGO MWEMA UNAOENDELEA SASA WA CLOUDS FM JUU YA KUWAJALI WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU + X.MASS ZAWADI.AT THE SAME TIME - NIKAMKUMBUKA NDUGU YANGU fadhilimshairi.blogspot.com
NA KATIKA MOJA YA MASHAIRI YAKE (TENDA WEMA) ALIANDIKA.
Kuna wengi walimwengu, kujaa dunia nzima,
Muumba ni yeye Mungu, kila moja na karama,
Wenye maisha machungu, huhitaji tendwa mema,
Tenda wema nenda zako.
Wale walio shidani, kamwe sije watupa,
Waondoe majonzini, usijaribu wakwepa,
Wafanye was'ende chini, maisha wakaogopa,
Tenda wema nenda zako.
Wale walio na njaa, usisite kuwalisha,
Waso nguo za kuvaa, ukapate kuwavisha,
Waliokata tamaa, imani kuwahuisha,
Tenda wema nenda zako.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Southwark mjini London, Uingereza kuiamuru Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kulipa faini ya Paundi za kiingereza laki tano 500,000 kwa kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kihasibu kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni ya BAE Systems kwa Mfanyabiashara Shailesh Vithlani wa Tanzania miaka mitano iliyopita.
Serikali ya Tanzania,kupitia Ubalozi wetu nchini Uingereza imeomba taarifa rasmi kutoka Serikali ya Uingereza kuhusu uamuzi huo. Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.
Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems.
Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
22 Desemba, 2010
Tuesday, December 21, 2010
huzuni
Monday, December 20, 2010
HABARI