Ni jamaa aliyehusika na kushiriki kikamilifu kuhakikisha jiji la mwanza linakuwa na utamaduni wa usafi kaya kwa kaya, mtaa kwa mtaa, kitongoji kwa kitongoji hali iliyopelekea jiji kutunukiwa mfululizo TUZO mbalimbali za usafi kitaifa na kwa Afrika Mashariki.
Mama wa Shilewa akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Pastory ambaye ndiye alikuwa mtoto wake wa kwanza.
Mke wa marehemu Teopista William Dodoma akiweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe.
Dada wa marehemu Pastory Shilewa wakiweka shada la maua katika kukamilisha mazishi yaliyofanyika kijiji cha mtakuja Wilayani Sengerema, ijumaa ya tarehe 17.december.2010
Wawakilishi kutoka ofisi ya jiji aliyokuwa akifanya kazi marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Pastory Shilewa.
Katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Monika Shilewa (dada wa marehemu), Grace Shilewa (dada wa marehemu), Mama Shilewa na ndugu wengine.
Wakifarijiana kwa kuondokewa na kipenzi chao, pichani kutoka kulia ni Mama Shilewa (mama wa marehemu), kwa ukaribu na Teopista William Dodoma ambaye ni mke wa marehemu na mwisho ni dada yake mke wa marehemu.
Baadhi ya watoto wa marehemu katika picha ya kumbukumbu pamoja na shangazi yao Monica (wa 3kulia). Marehemu Pastory alizaliwa mnamo tarehe 5 agust 1961 ameacha watoto 8 na mjane.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.