Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa zoezi la uhesabu kura.
Nafasi ya Mweka hazina imekwenda kwa Fred Katulanda aliyepata kura 28 aliyewaangusha Paulina David aliyepata kura 25 na Clara Matimo aliyeambulia kura 1.
Makamu Katibu mkuu imetwaliwa na bi Sheila Sezy aliyepita kwa kura za NDIYO 39 na HAPANA 14.
Nafasi ya Katibu Mkuu imekwenda kwa Jimmy Luhende aliyepata kura 27 akiwashinda Felista Kulijila kura 22 na Nashon Kenedy aliyeambulia kura 7.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imeenda kwa Flora Magabe aliyepata 29 dhidi ya wapinzani wake Rahabu Fred kwa kupata kura 27, ambaye hata hivyo hakuwepo uchaguzini kwenye mkutano huo kutokana na kuwa na udhuru.
Mwisho nafasi nyeti ya Uwenyekiti ilinyakuliwa kwa kishindo naye Deus Bugaiwa aliyetikisa kwa ushindi wa kishindo kwa kuzoa kura 41 dhidi ya Osoro Nyawangah aliyepata kura 15 za wanachama walioshiriki uchaguzi huo.
Wanachama mkutanoni.
Hapa wanachama walikuwa wakijinadi kupata ridhaa ya wadau kuwania nafasi tano za Ujumbe.