ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 15, 2012

DIWANI MATATA ATOA MSAADA KWA JAMII YAKE


Diwani wa kata ya Kitangili wilaya ya Ilemela jijini Mwanza leo ametoa msaada kwa jamii inayoishi kwenye mazingira magumu na wale wenye ulemavu na wasio jiweza.

Diwani Henry Matata wa Chadema amesema kuwa ameamua kutoa  msaada wa Nguo, Vyombo vya chakula, Mchele, Unga, Maharagwe, Viatu kutokana na ukali wa maisha unaowakabili baadhi ya wananchi wenye uwezo mdogo. 

Bw.Matata amesema kuwa katika kata 9 za wilaya ya Ilemela, Kata ya kitangili ndiyo yenye watu wengi wasiojiweza na waishio kwenye mazingira magumu yakiwemo makundi kama walemavu, wajane na waathirika waishio na virusi vya ukimwi.


Diwani akiendelea na zoezi la ugawaji.

Akinamama wakiwa kwenye mstari kupata msaada.

Moja ya masanduku ya nguo.

Nafaka kwaajili ya msaada.

Pamoja na kata ya Kitangiri kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za uhaba wa maji safi na salama, barabara nzuri kwa mitaa yake, madawati kwa shule zake, vyumba vya darasa kwa shule za msingi na umeme diwani huyo amesema kuwa bado ataendelea kuzitafutia ufumbuzi kwa kuhakikisha  zinatatuliwa kwa kipindi cha uongozi wake.

Wazee wakihusika na nafasi yao kupokea msaada huo.

Kusanyiko katika tukio hilo la ugawaji misaada katani humo.

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. Jamani muacheni huyo huyo mheshimiwa Matata aendelee na uongozi wake acheni tamaa ya madalaka na mambo hamuyawezi simuondoe acheni asaidie watu huyo sisi wazee tunamfahamu ana asili ya uongozi huko Mwanza sehemu za ilemela kitangiri mpaka mwanza airport mababu zake walikuwa watemi machief huko mwanza naomba msijenge hoja za uongo za kumsingizia mweshimiwa huyo watu wengi tunajiunga na chama kwa ajili ya mheshiwa huyo mpeni chance jamani

    ReplyDelete
  2. asante sana mrs Anthony karibu sana kwenye chama chetu cha Chadema tunaye mheshimiwa kuna watu wachache wanataka kukiharibu chama tukufu Chadema halafu tena wananjenga hoja za kashifa amabazo zinaleta chama kuzaraulika na vyama vingine na kuwapa chati ya kushinda katika uchaguzi mkuu Mheshimiwa Matata anakipenda chama chake sana na anaheshimu viongozi wake tunaomba wasimletdown mheshimiwa huyo kutokkana na usaidizi mkubwa unaonekana katika hizo picha

    ReplyDelete
  3. mimi nilikuwa sijaona jamani msimtupe huyo Diwani anafanya kazi kubwa ya nchi yake kitu namulaumu kwa asiwe Diwani wa cham cha mapinduzi CCM? ndio chama kilimlea hata asipochaguliwa kuwa Diwani afanyie kazi chama hicho aungane na wana CCM aisaidie Nchi yake Tanzania awaache watu wanohaja ya vyeo tu sio kusaidia wananchi bwana Matata chama chetu chamapinduzi chajenga nchi ndio tulikuwa tunaimba zamani wakati tuko wadogo sasa tumekuwa wazee tuendelee kudumisha chama hicho kwa kwasaidia watu nani anajua Chadema hehehehehehe jamani tudumishe chama chetu mungu akilinde na pia Mungu amlinde mweshimiwa Matatat

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.