ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 10, 2010

MISHEMISHE HAPA NA PALE.

KIJIJI NDANI YA JIJI.


UNAPOTINGA MUSOMA MKOANI MARA, LIPO ENEO MOJA MAARUFU SANA KWA MASUALA YA MAAKULI, MAPOKOPOKO NA MANJALI, ENEO LINAITWA MARA DISHES MISOSI AINA ZOTE, UJI FULL TIME HATA SAA TISA MCHANA UA SITA USIKU UNAKAMATA BAKULI LAKO SAAAFI... TEHE!

EEE KWA PEMBENI KUSHOTO HIVI SI MAKUFULI DIZAINI? ENHE! BASI HAPO HAPO NDO NAPIGA MZIGO CHAMAA LANGU..


KILICHOKUWA KITUO CHA EXPRESS ZIENDAZO NYEGEZI - BUHONGWA, JAMAA ALISHINDA KESI AKACHUKUA KIWANJA CHAKE TOKA MIKONONI MWA HALMASHAURI YA JIJI. KWA HIVI SASA HAKUNA KITUO KATIKATI YA JIJI..

WASHINDI WA KWEA PIPA WAPATIKANA MWANZA.

M1 WA WASHINDI WA TIKETI ZA KWEA PIPA NA COCA COLA JOHN SITTA MASANJA(KUSHOTO)TOKA WILAYA YA NGUDU MKOANI MWANZA AKIPOKEA MFANO WA TIKETI TOKA KWA MDAU WA NYANZA BOTTLING COMPANY LTD DEUS KADIKO.

MSHINDI MWINGINE WA KWEA PIPA CHARLES MATHEUS TOKA SHY (KUSHOTO) NAE AKIPOKEA TOKA KWA MWAKILISHI WA COCA COLA BW. MAGINGA.


PICHA YA PAMOJA. WENGINE ZAIDI KUPATIKANA ENDELEA KUBANDUA VIZIBO NA KUCHUNGULIA.

Friday, April 9, 2010

EH BANA DAH! EH BANA DUH!

WADAU WA TIGO THUMNI MITAANI KAMA ZAMANI VILE.

HIVI MAJUZI SEHEMU YA WAKAZI WA WILAYA YA ILEMELA MATHALANI. MISSION, MAKONGORO, KIRUMBA, KONA YA BWIRU NA BAADHI YA SEHEMU ZA KILIMAHEWA WALIKOSA MAJI KWA KIPINDI FULANI TATIZO LIKIWA NI KUPASUKA KWA BOMBA HILI KUU LINALOPITA KTK DARAJA LA MTO MILONGO ENEO LA KLINIKI MZ. TATIZO HALIKUDUMU KWANI WAHUSIKA WALITATUA KWA HARAKA HUDUMA IKAENDELEA.

LINAPOKUJA SUALA LA UCHAFUZI WA MAZINGIRA KUNA MENGI YAKUPIGIA KELELE. HUU NI MOSHI UNAOFUKA TOKA KIWANDA CHA NGUO MWATEX KILICHOPO IGOMA JIJINI MWANZA.

MZUKA WA INJILI TOKA KWA WATOTO WA MUNGU.


NI STAND YA AWALI KABLA HUJAFIKA ILE ILIYO KATIKATI YA MJI USIULIZE HAPA WAPI! SOMA BANGO.

MAKTABA YA MKOA WA MARA INAYOPATIKANA BARABARA YA MKENDO MJINI MSOMA.

Tuesday, April 6, 2010

MWANZA NA J3 YA PASAKA 2010.

MUACHENI MUNGU AITWE MUNGU NI TAMASHA LA PASAKA LILILOANDALIWA NA MSAMA PROMOTION NA KUDHAMINIWA NA ZAIN MWANZA, MMILIKI WA www.michuzijr.blogspot.com AKINESANESA PAMOJA NA INJINIA WA UPENDO GROUP BWANAAAAAAAA.........AGHH! limenitoka jina.

MIE NA MKALI WA INJILI KUTOKA JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA WATU WA KONGO SOLOMON MKUBWA.

ROSE MUHANDO NA KUNDI LAKE NDANI YA TAMASHA LA PASAKA JUMATATU MWANZA CCM KIRUMBA PALITIKISIKA BILA NYUFA.

WAU! NYUSO ZA TABASAMU! WAPI SAMADU ABDUL MWANA WA 88.1

WADAU WA GOSPEL NA MAVAZI NADHIFU.

SEHEMU YA UMATI NA ULINZI WA KUTOSHA NDANI YA CCM KIRUMBA.

MC JOB AKA BABA PAROKO ASISIKIE CHOCHOTE, MACHO MBEEELE KWAMAKIIINI..

ALIYENACHO ATAZIDI KUONGEZEWA SOLOMON AKIWATUNUKISHA BURUDANI WAKAZI WA MWANZA NI KTK WIMBO MUNGU NI MWAMINIFU AMBAPO ALIWAANDAA MASHABIKI KABLA YA TAMASHA KILA MMOJA KUJA NA KITAMBAA CHEUPE.

HII NI ZAIDI YA UPAKO! MBLOGISHAJI MAARUFU NCHINI MICHUZI JR (MWENYE TSHIRT ORANGE)AKICHEZA.

UPENDO GROUP SAAAAFI! HAWA MABWANA KAMA NI SAUTI ZA UKWELI WANAZO, HAPA NI KTK WIMBO 'HALELUYAH AAAH, HALELUYAH AAAH!' ZAIN WAKIWA WADHAMINI.

UPENDO NKONE AKIIMBA HUKU KAMERA YA STAR TV IKICHUKUA TUKIO. HUYU SISTER ANAITWA NANI?

KKKT BUGANDO NAO ZAMU YAO ILIFANA SANA!

VIJANA ANGLIKANA NYAMANORO NAO WAKISISIMUA.

Monday, April 5, 2010

PASAKA NA WAKAZI WA SHINYANGA .

KIVUTIO KIKUBWA MWIMBAJI ASIYE NA MASIHARA KATIKA JUKWAA ROSE MUHANDO AKIFANYA KILE KILICHOKUWA KIKINGOJEWA KWA HAMU NDANI YA TAMASHA LA PASAKA SHINYANGA LILILOANDALIWA NA MSAMA PROMOTION YA JIJINI DAR-ES-SALAAM.

ILIKUWA NI SHANGWE KWA KILA MMOJA KWA WALIOTHUBUTU KUFIKA CCM KAMBARAGE SHY TOWN.

SOLOMON MKUBWA THE GREATEST MAN KUTOKA NCHINI CONGO AMBAYE KTK TAMASHA HILI ANAZINDUA ALBUM HAPA AKIIMBA MOJA KATI YA ZAKE ZITIKISAZO WIMBO UNAOPENDWA NA WENGI MUNGU NI MWAMINIFU.

USAFIRI MKUU MJINI SHINYANGA NI BAISKELI HIVYO KULIKUWA NA PAKING TULIVU JUKWAA KUU. HEHEE MAMBO YA UPAKO!

WAPAMBE WA MUIMBAJI MAHIRI WA MUZIKI WA INJILI NCHINI ROSE MUHANDO WAKIWA SHUGHULINI...

EEEH! NA SARAKASI ZIMO? MUIMBAJI MAGIDA AMBAYE NI ALBINO WENGI NAYE AKIWA YU MMOJA WAPO HUPENDA KUMWITA MZUNGU, HAPA AKILITAWALA JUKWAA...

WAKAZI WA SHINYANGA WAKIJUMUIKA NA MPAKWA MAFUTA WA BWANA MTUMISHI WA MUNGU MWIMBAJI UPENDO NKONE AMBAYE ALIFURUMISHA INJIRI KISAWASAWA KWA NJIA YA UIMBAJI.