ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 17, 2011

BURUDANI ZAIDI NA BONANZA LA MIAKA 50 YA UHURU

Kulia Ali Choki na pale kati mtu mzima Banza Stone aka Mwalimu wa Walimu.

Safu ya Extra Bongo.

Safu ya dadaz.

Hadhira.

Dance la mayankiz.

Tamu ya burudani.

Pozi la leo.

We dada wewe!!!!!

Kunywa nimekunywa pakurara jeh!?

Me n' my Crew.

Wadau Namba moja wa Mwanza.

Ze graudi' at Furahisha Kirumba Mwanza

SIMBA YAIRARUA YANGA BONANZA LA TBL MWANZA

Maandamano kuelekea viwanja vya Furahisha.
Simba TBL ya jijini Mwanza asubuhi ya leo imeitandika Yanga bwiru bao 3-2 katika bonanza la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika mchezo wa dakika 30 magoli madogo uliochezwa katika uwanja wa furahisha.
Kikosi Simba
Licha ya kufungwa kwenye mchezo huo Yanga bwiru walionyesha kandanda safi la kuvutia kiasi cha kushangiliwa sana na mashabiki waliofurika asubuhi hii.

Niwakati wa kujuana.Jukwaa la wadau wa TBL na Wageni Mwanza.
Eh bana eeeh zimetulia!!!

Sehemu ya yetu.
Bonanza la Uhuru linaendelea ambapo kuna burudani za kufufuka mtu wakiwemo Wana Extra Bongo.

Friday, September 16, 2011

ZAIDI YA WANANCHI 100 KISEKE JIJINI MWANZA WAVUNJIWA MAKAZI YAO, ZOEZI LAFANYIKA CHINI YA AMRI YA MWENYEKITI

Zaidi ya wakazi 100 wa MTAA WA MIEMBE GIZA – KATIKA MLIMA WA KISEKE WILAYANI ILEMELA JIJINI MWANZA WAMEAPA KUTOHAMA KATIKA ENEO HILO KUTOKANA NA MWENYEKITI WA MTAA WA MIEMBE GIZA BWANA KAMANI KUVUNJA MISINGI YA NYUMBA 35 NA NYUMBA ZAIDI YA 100 WALIZOKUWA WAMEJENGA HIVYO KUWASABABISHIA HASARA NA UPOTEVU WA MALI ILE HALI BAADHI YA NYUMBA WANAZODAI KUWA NI ZA MATAJIRI ZIKIBAKIA KATIKA ENEO HILO BILA KUVUNJWA.

Wakizungumza na blogu hii katika eneo la tukio wananchi hao wamesema kuwa mnamo mwezi September 3 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni Mwenyekiti wa mtaa huo bwana Kamani akiongozana na watu wake kwa kutumia nguvu alibomoa nyumba na misingi ya nyumba za wakazi hao hali ambayo wanadai ni makosa na haikuwa sahihi.

Kupitia amri ya mwenyekiti wa kitongoji hicho nyumba nyingi zimebomolewa, mali kuharibiwa na nyingine kupora huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiachwa hawana mahala pa kujisitiri.

Babu Ntambi moja kati ya waliovunjiwa ameapa kutoliachia eneo lake kwani limemgharimu zaidi ya shilingi milioni 11 kulisawazisha na hatimaye kupata kiwanja ambacho alianza kujenga nyumba ambayo hata hivyo imebomolewa.

Ilikupata kiwanja imlibidi kusawazisha eneo kwa mawe na kujaza udongo kama inavyoonekana.

Wananchi hao wamehoji kuwa kama kweli eneo hilo limetengwa kwaajili ya hifadhi iweje zoezi hilo lifanyike kwa baadhi ya nyumba ile hali likiruka nyumba za marafiki wanaotajwa kuwa ni wa mwenyekiti waliogawiwa na kiongozi huyo maeneo.

Kwa upande wake Afisa ardhi wa jiji la Mwanza bw. Makusudi Bwabo amesema kuwa nyumba hizo zilizojengwa ndani ya hifadhi ya mlima huo wa Kiseke zimejengwa kimakosa kwa madai kuwa mlima huo umetengwa kisheria na uongozi wa jiji kwaajili ya hifadhi ya msitu na kwamba wale wote waliojenga kwenye msitu huo ni wavamizi hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 kifungu namba 8 na hatua inayofuata ni kubomoa nyumba zao.

Wakati yote hayo yakiendelea ndiyo kwaaanza ujenzi unaendelea tena baadhi ya wananchi wenye fedha wakijitengenezea viwanja kwa kuumega mlima huo.

Thursday, September 15, 2011

NEWS ANCHOR MOCKS KARDASHIANS!!!!!

News anchors are supposed to read the news, not make it. But we're more than happy to make an exception for two reporters from Philadelphia's Fox 29 morning show, "Good Day."Baada ya kufanya mahijiano hewani na ndugu wawili maarufu Kim Kardashian pamoja naye Kourtney Kardashian, watangazaji Mike Jerrick and Sheinelle Jones wakidhani kamera zimezimwa kumbe sivyo wakaanza kutimbwilika kuwabeza (CHEKI NA VIDEO)....... They hadn't.

As soon as they said their goodbyes to the Kardashians, who were promoting a line of clothes, the anchors began making fun of the two sisters. "Can they still hear us?" asks Jerrick. He then proceeds to mock the reality stars for their high-pitched voices and affinity for shoulder pads.

Jones half-heartedly attempts to defend the sisters, saying, "I think they're stunning." But even she can't keep a straight face as her cohort continues speaking in a nasally Kardashian-like voice, a bit like a Smurf who had inhaled helium.
Yes, yes, we know. Making fun of others is wrong. Except when it's the Kardashians. Then it's hilarious. Enjoy!

HAMAHAMA YA WAKUU WA MIKOA TANZANIA.

Na. JINA LA MKUU WA MKOA KITUO AENDAKO NA ATOKAKO
1. Bw. Saidi Mecki Sadiki DAR ES SALAAM RC - Lindi
2. Bw. John Gabriel Tupa MARA DC - Dodoma
3. Bw. Saidi Thabit Mwambungu RUVUMA DC - Morogoro
4. Kanali Joseph Simbakalia MTWARA RC Kigoma
5. Bi. Chiku S. Gallawa TANGA DC - Temeke
6. Bw. Abbas Kandoro MBEYA - Mwanza
7. Bw. Leonidas T. Gama KILIMANJARO DC - Ilala
8. Dkt. Parseko Ole Kone SINGIDA RC Singida
9. Eng. Stella Manyanya RUKWA - Mbunge V/Maalum
10. Bibi Christine Ishengoma IRINGA - RC Ruvuma
11. Dk. Rehema Nchimbi DODOMA DC - Newala
12. Bw. Elaston John Mbwillo MANYARA DC - Mtwara
13. Col. Fabian I. Massawe KAGERA DC - Karagwe
14. Bibi. Mwantumu Mahiza PWANI - Mbunge/NW Mstaafu
15. Bibi. Fatma A. Mwassa TABORA DC - Mvomero
16. Bw. Ali Nassoro Rufunga LINDI DC - Manyoni
17. Eng. Ernest Welle Ndikillo MWANZA DC - Kilombero
18. Lt. Col. Issa Machibya KIGOMA RC Morogoro
19. Bw. Magesa S. Mulongo ARUSHA DC - Bagamoyo
20. Bw. Joel Nkaya Bendera MOROGORO - Mbunge/NW Mstaafu
21. Bw. Ludovick Mwananzila SHINYANGA - Mbunge/NW Mstaafu

Wednesday, September 14, 2011

USAIN BOLT AVUNJA REKODI YA DUNIA ALIYOIWEKA

KUTOKA HUKO Zagreb, Croatia: Usain Bolt amefanikiwa kuvunja rekodi yake aliyoiweka kwenye mbio za mita 100 tangu alipowekwa kando kwenye michuano ya dunia iliyopita mara baada ya kukosa sifa na safari hii akishinda kwa kutumia sekunde 9.85 kwenye michuano ya dunia iliyofanyika jana mjini Zagreb. Bolt, who false-started in South Korea last month to end his hopes of retaining his world title, shaved 0.03 seconds off his previous fastest time this year — 9.88 at Monaco in June — on a warm, still night.

"It was a poor start," said Bolt, the world and Olympic record holder. "I kind of lost concentration and just went through the line. It was OK, I suppose, but I could have done better, especially with the weather like that."

Kim Collins of Saint Kitts and Nevis ran a season-best 10.01 seconds to finish second, ahead of Trinidad's Richard Thompson at 10.03.

There was standing room only at the 61st Boris Hanzekovic Memorial, where Real Madrid President Florentino Perez and club official Emilio Butragueno arrived in time to see Bolt run. Madrid leo jumatano inaanza kampeni yake katika Ligi ya Mabingwa dhidi ya Dinamo Zagreb.

WASHUKIWA WA2 WAKILI KUSHAMBULIA UGANDA

Wanaume wawili ambao walishtakiwa kwa kuhusika na ulipuaji wa mabomu mjini Kampala mwaka uliopita wamekiri makosa hayo. Wawili hao ni miongoni mwa washukiwa 14 ambao wanakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo mauaji ya watu 70 katika mashambulio hayo.

Washukiwa wa mashambulizi hayo walikuwa 19 lakini watano wakaachiliwa huru juzi na mahakama kuu mjini Kampala. Wengine miongoni mwao raia wawili wa Tanzania walikanuha mashtaka dhidi yao

Mbele ya hakimu Alfonse Owiny dollo walikuwa Edris Nsubuga a na Mohammoud Mugisha mbao walikiri kuhusika na mashambulizi ya mabomu mjini Kampala mwaka jana wakati wa fainali za kombe la dunia.

Nsubuga amekiri makosa matatu ikiwemo kutekeleza vitendo vya kigaidi kusafirisha na pia na kusambaza vilipuzi.Mwenzake Mugisha amekiri kosa la njama za kufanya vitendo vya kigaidi.

Baada ya kufikishwa mahakamani mshukiwa Nsubuga alinyoosha mkono wake na kumuomba jaji amukubalie kukiri makosa japo juzi alikuwa amekana makosa. Mshukiwa huyo aliambia mahakama kuwa jana alitishiwa na wenzake ambao walikuwa wamekana mashtaka na akaamua kukiri mashtaka.

Hapo juzi mahakama kuu ya Uganda ilimuondolea Muhamoud Mugisha makosa 76 ya mauaji na ila kosa la njama za kutenda visa vya ugaidi. Alenyo George William ni wakili anaeleza maana ya watu hawa wawili kukiri makosa yao.

Kesi hii ya shambulio la bomu mjini Kampala mwaka jana inaendelea ambapo washukiwa wengine wakiwemo raia sita wa Uganda Watanzania wawili na Wakenya Sita


CHANZO: bbc swahili

Tuesday, September 13, 2011

LINAPOKUJA SUALA LA NYWELE BANDIA - MWANAWANE WE UNASIMAMA WAPI?

Kupitia mtandao tulikuwa tukijadili suala la nywele kuweka dawa, nywele bandia na nakshi mbalimbali, 'SITAKI KUONGEZA CHUMVI' kazi kwako:- @Kama nimemwelewa vile boss, yeye anapenda nywele asilia na si za kuungaunga [ziwe na relaxer, curl au hata fupi]... i like the same, yaani mimi criteria ya kwanza ya kukimbia bibi ni nywele za kuunga au kushonea.
1. kwanza ukishika kichwa kinakua kama kina manundu nundu
2. pili most of them zinakua tofauti sana na original kiasi kwamba ukiangalia nyuma ya kichwa unakutana na kipilipili against indian hair za mbele [tetracycline!]
3. tatu wanawake wengi sana huonekana more cute wakinyoa nywele zao ila hawajui tu

big up to all women with their natural hair and no sugar added!!!

@Mwanamke wig bwanaaa....tena siku hizi kuna hizo wanaita lace wigs, shurti unatoka kama Beyonce banaa!mnh usuke mabutu utoke kama mrs Lawino, inahusuuuuu acheni kuwa conservative.

@Waache wachome mahindi Fab that doesnt stop us from looking fabulous wit 'fake' hair (lol)
I do keep mine clean though....tena kwa manufaa yangu binafsi!!!
Fab unajua kunayale feki na mengine orijino? feki bana mtu ni kama kasukia katani kichwani lol!!!!!!!!!!!!

@Nijuavyo mimi nywele za bandia ni kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa nywele za kichwani, mfano kuna watu wengine hawana nywele kichwani sehemu zote.
Hawa watu huwa wameliwa nywele kwa maradhi au kwa kuzaliwa hivyo hivyo pia kwa warembo wanaotaka kuonekana zaidi ya mungu alivyowaumba.
Usafi wake ni jukumu la mtumiaji.
Asanteni

@Halafu haya manywele ya bandia kama mtumiaji siyo msafi, huwa yananuka kweli kweli. Siku hizi wanawake wetu wanashindana kubandika manywele ya bandia ili wawe na nywele ndefu zilizodondokea mgongoni... but wapo watu,mimi nikiwemo huwa napenda kuona mwanamke akitoka na nywele zake fupi na kazisuka mitindo ya enzi na enzi.....very beautifull

@Mwana umegonga kunako, siku moja nusura nitapike katika daladala tulikuwa tumeshonana alafu bidada ndio yuko usoni kwangu, balaa mazeee!!
Jibu—“hahaha pole nadhani hiyo ilikuwa zazuuuuuu..”

@Lol....hivi bado watu wanaweka zazuuuu? Halafu kwanza zazuuu ni nini? inafanya nywele ziweje? nakumbuka miaka ya 80 zazuu ilikuwa kwenye chati sana...
Halafu nyie mnasahau how difficult to maintain that naturale hair...

@Is it easy to maintain fake hair? C'mon on now....just a few days ago this one girl told me she wants to workout so she can tone (whatever that is) but she doesn't want to sweat coz that's gonna mess up her hair... I think every week or every other week she goes to get her hair done (and yes it's treated with a whole bunch of chemicals)....so how easy is that?
Its easy to maintain natural hair shem.....compared to 'fake' hair

@Nywele za bandia zenyewe ni ghali na matunzo ni ghali pia, na zinakufanya mtumwa wake kweli kama hapo kwenye red. (binafsi nimuathirika wa hilo...siendi swimming nikiwa na fake hair) kwa wale wanaosema zinanuka, si kweli hata natural hair inanuka kama haisafishwi. Nywele bwana zinahitaji usafi wa hali ya juu usijindanganye eti hiz ni asili so sioshi mpaka miezi sita maana zita'shrink'

@Mimi nikimmega dem huwa napenda kushikilia nywele zake, dem akiwa na bandia utaona ananikataza nisishike, kuna dem mmoja alijisahau...nywele zilitoka zikabaki mikononi kwangu....nilimuona mbaya ajabu… dah! Ilikuwa noma lakini ilitokea nikajikaza kisabuni…

@Dada Mmoja akiwa na nywele zake bandia huku aki drive kwa manjonjo na minato kama anapark vile pale kitaani kwetu akatoa kichwa dirishani…. Mama yangu wigi silikaenda na upepo…. Mtumeeee!!! Dada ana bonge la kipara yaaani full udang’a …tehe..tihi!!

Monday, September 12, 2011

WAZAMIAJI WA SOUTH AFRIKA WAWASILI ZANZIBAR KUTAFUTA MILI YA WALIOZAMA

Watu wakijaribu kutambua miili ya watu waliofariki katika ajali.

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wazamiaji 12 kutoka nchini Afrika ya Kusini, wamewasili usiku huu mjini Zanzibar kuungana na wazamiaji wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini ili kufanya uhakiki wa kujua kama bado kuna mili iliyokwama kwenye Meli ya MV Spice Islander iliyozama chini ya bahari eneo la Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja usiku wa Jumamosi wiki iliyopita.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Aboud Mohammed, amesema kuwa wazamiaji hao wamewasili wakiwa na zana za kisasa za uzamiaji na kwamba kazi ya kwanza itakayofanywa na timu hiyo ni kuhakikisha kuwa wanaifikia meli hiyo iliyozama umbali wa karibu nusu kimometa kwenye mkondo mkubwa wa maji na majabali.


Bado Serikali na wananchi mbalimbali wanadhani kuna miili ya watu waliokwama katika vyumba vya meli hiyo tangu ilipozama usiku wa Jumamosi Septemba 10 mwaka huu ikiwa na idadi ya watu isiyojulikana.

Makundi ya wananchi wamekuwa wakitaja idadi ya ndugu na jamaa waliosafiri na Meli hiyo na ambao hawaja patikana wakiwa hai ama miili yao kiasi cha kutia shaka kuwa huenda bado wamenasa ndani ya vyumba vya meli hiyo iliyozama chini ya kina kirefu cha mkondo wa bahari ya Hindi.

Tangu kuokolewa kwa abiria 619 na kuopolewa kwa miili ya watu 197 hadi jana jioni, hakujapatikana mtu hai ama mwili wa abiria aliyekufa maji ukielea juu ya maji ama kukokotwa kupelekwa mwambao mwa nchi kavu.

Katika eneo ilipo Meli hiyo zipo Meli nyingine za MV Kasa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na MV Mamba ya Jeshi la Polisi ambazo zote ziliwasili alfajiri siku iliyotokea tukio hilo la kuzam,a kwa MV Spice Islander.

Sunday, September 11, 2011

JUMUIYA YA WATANZANIA UINGEREZA YATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Kwa niaba ya jumuiya ya watanzania waliopo nchini uingereza chini ya Mwenyekiti wa TANZ- UK taifa imesikitika sana na kuwapa pole watanzania wenzetu wa zanzibar kwa msiba mkubwa uliolikumba taifa. Watanzania wote tulio hapa tunaungana nanyi kwa pamoja katika wakati huu mgumu na pia tuko tayari kushirikiana kwa hali na mali kuwafariji ndugu na jamaa kwenye msiba huu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

Mwenyekiti TANZ- UK.
Dr John Lusingu

SALHA ISRAEL ATWAA TAJI LA VODACOM MISS TANZANIA 2011

Salha Israel akiwapungia mkono mashabiki wa urembo duniani kote ishara ya kuwashukuru kuchaguliwa kuwa mrembo wa Taifa.Salha ataiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya dunia.zawadi ya salha hii hapa chini(jeep).

Mikogo ndani ya Vazi la Ubunifu.

Safu ya wanyange one.

Safu ya wanyange two.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya 5 bora ya Vodacom Miss Tanzania 2011 wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kushoto ni Miss Sports Woman Loveness Flavian, Miss Photogenic Tracy Mabula, Jenifa Kakolaki, Miss Personality, Alexia Willium na Salha Izrael.

Ni Vodacom Miss Tanzania 2011.