Wakizungumza na blogu hii katika eneo la tukio wananchi hao wamesema kuwa mnamo mwezi September 3 mwaka huu majira ya saa 10.30 jioni Mwenyekiti wa mtaa huo bwana Kamani akiongozana na watu wake kwa kutumia nguvu alibomoa nyumba na misingi ya nyumba za wakazi hao hali ambayo wanadai ni makosa na haikuwa sahihi.
Kupitia amri ya mwenyekiti wa kitongoji hicho nyumba nyingi zimebomolewa, mali kuharibiwa na nyingine kupora huku baadhi ya wakazi wa eneo hilo wakiachwa hawana mahala pa kujisitiri.
Babu Ntambi moja kati ya waliovunjiwa ameapa kutoliachia eneo lake kwani limemgharimu zaidi ya shilingi milioni 11 kulisawazisha na hatimaye kupata kiwanja ambacho alianza kujenga nyumba ambayo hata hivyo imebomolewa.
Ilikupata kiwanja imlibidi kusawazisha eneo kwa mawe na kujaza udongo kama inavyoonekana.
Wananchi hao wamehoji kuwa kama kweli eneo hilo limetengwa kwaajili ya hifadhi iweje zoezi hilo lifanyike kwa baadhi ya nyumba ile hali likiruka nyumba za marafiki wanaotajwa kuwa ni wa mwenyekiti waliogawiwa na kiongozi huyo maeneo.
Kwa upande wake Afisa ardhi wa jiji la Mwanza bw. Makusudi Bwabo amesema kuwa nyumba hizo zilizojengwa ndani ya hifadhi ya mlima huo wa Kiseke zimejengwa kimakosa kwa madai kuwa mlima huo umetengwa kisheria na uongozi wa jiji kwaajili ya hifadhi ya msitu na kwamba wale wote waliojenga kwenye msitu huo ni wavamizi hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 kifungu namba 8 na hatua inayofuata ni kubomoa nyumba zao.
Wakati yote hayo yakiendelea ndiyo kwaaanza ujenzi unaendelea tena baadhi ya wananchi wenye fedha wakijitengenezea viwanja kwa kuumega mlima huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.