ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 11, 2023

HAIKUWA RAHISI KUFIKIA MAKUBALIANO MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI LAKINI KWA SAMIA IMEJIBU


 NA ALBERT G. SENGO/DODOMA

Haya yanafanyika wakati ambapo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiwa tayari amekwisha wasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 bungeni jana Februari 10, 2022.

SHIUMA WAALANI VURUGU ZILIZOTOKEA MWANZA


Naibu katibu mkuu wa machinga Taifa Joseph Mwanakijiji akiongea na waandishi wa habari mkoani Iringa juu ya kulaani vurugu zilizotokea jijini Mwanza Jana.



Na Fredy Mgunda, Iringa.

SHIRIKISHO la Umoja wa Machinga Taifa  (SHIUMA) limelaani vitendo vya vurugu vikivyofanywa na wafanyabiashara wadogo wadogo Jana jijini Mwanza kwa kusababisha hasara kwa baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na wananchi wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa,Naibu katibu mkuu wa machinga Taifa Joseph Mwanakijiji alisema kuwa wanalaani vikali uvunjifu wa amani ulitokea jijini Mwanza ulisababishwa na mgambo kuchukua hatua mkononi bila kufuata sheria walizojiwekea baina ya serikali na shirikisho hilo.

Mwanakijiji alisema kuwa wamekuwa wanafanya mazungumzo ya mara kwa mara na serikali juu ya namna bora ya kutafuta maeneo rafiki na wafanyabiashara wadogo wadogo lakini bado serikali imekuwa ikiwapangia wafanyabiashara hao maeneo ya mbali ambayo sio rafiki na biashara hiyo.





"Sisi kama Viongozi wa Taifa wa kundi hili la Machinga tunalaani vikali sana, uvunjifu uliofanyika Mwanza, maana sisi siyo wanaharakati wa kuhamasisha fujo, isipokuwa ni taasisi inayoshughulikia mambo yote kupitia meza za mazungumzo bila kuchoka"alisema mwanakijiji

Mwanakijiji alisema kuwa jana wameona kwenye mitandao ya kijamii au kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa , wafanyabiashara wakubwa wa maduka Mwanza,Wilaya ya Nyamagana, walifunga maduka baada ya Vurugu ambazo zilitokana na mgambo kuchukua bidha za machinga kwa kutumia nguvu.


"Moja ya taarifa zinazosambaa sana ni kwamba maduka yaliibiwa bidhaa na  magari kufanyiwa fujo kadhaa wa kadhaa,ikumbukwe Mwanza wapo watoto wa mitaani wengi Sana (uzurulaji) na kunawakati inapelekea kwenye mchangamano na wengine wanakuwa hawana nia njema, na inawezekana iyo imepelekea uvuninjifu kwa kiasi na kiwango kikubwa"alisema mwanakijiji

Alisema kuwa shirikisho hilo haliamini kuwa machinga ndio waliovunja maduka na magari na kuiba vitu vya watu,machinga wanabiashara zao na hawawezi kuwa wezi huo ni uzushi tu.

Mwanakijiji alisema kuwa machinga wanamahusiano mazuri na wafanyabiashara wakubwa kuanzia ngazi ya juu hadi huku chini hivyo hawawezi kuwavunjia na kuwaibia wafanyabiashara wenzao,wizi huo umefanywa na baadhi ya watoto wa mtaani.

"Sisi Machinga na wafanyabiashara wakubwa, tuna mahusiano mazuri na  makubwa sana, hasa kama viongozi Taifa na hata wasaidizi wetu tumewambia mara zote kwenye vikao vyetu vya Taifa wanaotoka kwenye Mikoa yote Tanzania na ieleweke kuwa wafanyabiashara na sisi tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana"alisema mwanakijiji


Mwanakijiji alisema kuwa shirikisho linatoa Pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa tatizo lilotokea na wamewaomba Machinga wote wa mwanza kuwa watulivu katika kipindi ambacho wanalitafutia ufumbuzi Jambo hilo.

Alimazia kwa kusema kuwa wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa namna anavyoendelea kuwashika mkono kwa kuhakikisha wanaimalika kiuchumi siku hadi siku

Itakumbukwa akiwa Geita kwenye ziara alitoa maelekezo Kwa wakuu wa Mikoa yote Tanzania kutoa kiwanja kwajili ya ujezi wa ofisi za Machinga kila Mkoa na pesa za ujezi alishatoa kiasi Cha shillingi million mia mbili na sitini 260,000,000 ambazo ni sawa na shillingi million kumi kila Mkoa 10,000,000=. Vile vile Billion arobaini na Tano 45,000,000,000 kama bajeti kupitia Bunge Kwa kundi hili na millioni mia Saba (700,000,000 za Iringa

DC MOYO ATOA MSAADA KWA FAMILIA 4 ZILIZO ATHIRIWA NA TEMBO

 

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi msaada kwa wananchi baada kupata athari za mnyama Tembo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi msaada kwa wananchi baada kupata athari za mnyama Tembo

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mohamedi Moyo leo amekabidhi msaada wa chakula jumla ya kilo 120 Kwa familia 4 zilizo hathirika na uvamizi wa Tembo katika kijijij cha Mwandila.


Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada uwo Dc MOYO ameeleza anafahamu juu ya Changamoto hiyo ya uvamizi wa Tembo katika mashamba na makazi ya wananchi hivyo ameguswa kutoa msaada uwo kwa familia ambazo hazina kabisa,Aidha Moyo ameeleza kuwa serikali inaendelea kuchua atua mbalimbali za kukabiliana na wanyama hao pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata chakula.


Wakizungumza kwa niaba ya familia hizo mwenyekiti wa kijiji hiko Rajabu Chitanda pamoja na diwani wa kata hiyo Ally Milile wamemshukuru mkuu wa wilaya huyo Kwa msaada uwo huku wakiomba serikali kuendelea na jitihada zaidi kwaajili ya kunusulu ari za wananchi.

Friday, February 10, 2023

TAASISI YA HABARI MTANDAONI YAZINDULIWA WAANDISHI WAASWA KUACHA KUTUMIKA VIBAYA

 NA ALBERT G. SENGO/DODOMA

Hii leo Msemaji wa Serikali ya Tanzania Geryson Msigwa amemwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye kuzindua Taasisi ya Waandishi wa Habari Mtandaoni (TOMA) . Katika uzinduzi huo uliofana ukifanyika jijini Dodoma na kuratibiwa na Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) na kuhudhuriwa na wanahabari toka maeneo mbalimbali nchini, mmoja kati ya masuala yaliyochomoza kwenye hotuba na nasaha za mgeni rasmi ni pamoja na:- "Tasnia ya habari iko mikononi mwa vyombo vya habari mtandaoni, twendeni tukaoneshe weredi wa hali ya juu. Hicho ndicho kitakachotufanya tuaminike na jamii" "Ni lazima tuangalie maadili ya uandishi wa habari yanasema nini, ni lazima tuangalie sheria za nchi yetu zinasema nini, hatuwezi kuwa waandishi wa habari za mtandaoni kwa kujikita tu kwenye kuzua taharuki, kuvunja sheria aun kuchonganisha jamii na jamii au jamii na serikali" Tumetoka tulipotoka vyombo vya habari vikimilikiwa na wanasiasa na wafanyabiashara, akija mmiliki anasema weka hiki usiweke hiki. Tuacheni kutumika, hapo ndipo heshima yetu itakuwepo, fanya kazi yako kwa weredi" . . . #ikulumawasiliano #samiasuluhuhassan #dodoma #TOMA @ikulu_mawasiliano @samia_suluhu_hassan @napennauye @jembenijembe @kikotifredy @jembefmtz ZAIDI SUBSCRIBE #YouTube CHANEL YETU ILI UWE WA KWANZA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI #Jembefmtz

NMB YAZINDUA UMEBIMA?

 

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB - Martine Massawe wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Umebima kwa Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar, Naima Said Shaame.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa, Mkuu wa Idara ya Bima wa Benki ya NMB - Martine Massawe, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na  Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Zanzibar- Naima Said Shaame katika picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni ya bima, mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Umebima visiwani Zanzibar.

 Wananchi viziwani Zanzibar wakiendelea kupata huduma mbalimbali baada ya uzinduzi wa kampeni ya Umebima.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Umebima visiwani Zanzibar.


Benki ya NMB ikiwa wasambazaji wa bidhaa mbalimbali za makampuni 10 ya bima, wamezindua rasmi kampeni ya 'Umebima - Teleza na Hii!' visiwani Zanzibar itakayowawezesha kutoa elimu na kuhamasisha mauzo ya bima mbalimbali zikiwemo za: Majanga, afya, moto, machinga, maisha, vikundi, vyombo vya moto, nyumba, biashara, kilimo, usafirishaji na kadhalika, zitakazosaidia kutoa fidia endapo majanga yatatokea.


Kampeni hii imezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi - Idrissa Kitwana Mustafa na Mkuu wetu wa Idara ya Bima wa NMB - Martine Massawe, huku Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Simai Msaraka na Meneja wa Biashara wa NMB Zanzibar - Naima Said Shaame wakishuhudia.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi  Bw.  Idrissa Kitwana Mustafa aliwaasa wananchi kuchukua juhudi ya kuzielewa aina zitolewazo za bima, ili waweze kukata kwani ni kwa manufaa yao ya sasa na hata baadae.


Lakini pia, aliiipongeza NMB kwa ubunifu wa kampeni hii ambayo ni fursa nzuri ya maendeleo.


Aidha,  Mkuu wa Idara ya Bima wa benki hiyo, Bw. Martine Massawe, alisema timu ya NMB itakua mitaa mbalimbali visiwani Zanzibar kwa mwezi mzima kuhakisha wanatoa elimu ya bima na wanananchi wanaelewa ili waweze kuchagua ni ipi wanaihitaji. Bima hizi, mteja wa NMB na asiyekua mteja anaweza kuzinunua kutoka kwa matawi ya benki hiyo yaliyotapakaa nchi nzima.

Thursday, February 9, 2023

KAULI YA DKT MWIGULU ‘UGANGA WA KIENYEJI’ YAFUTWA KWENYE KUMBUKUMBU ZA BUNGE.

Dodoma. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amefuta katika kumbukumbu rasmi za Bunge kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba kuhusu wabunge kumuacha ajadili masuala ya uchumi na wao wajadili uganga wa kienyeji.


Dk Tulia ameyasema hayo leo Alhamis Februari 9, 2023 wakati akijibu utaratibu uliombwa na Dk Mwigulu wakati Mbunge wa Tandahimba (CCM) Katani Katani akichangia taarifa za kamati Februari 7, 2023.


Wakati akichangia taarifa za shughuli za Kamati wiki iliyopita Dk Mwigulu, alisema “Embu tujadili mambo mengine yanayohusu uganga wa kienyeji kwenye uchumi this is my profession (hii ni taaluma yangu), mnajadilije vitu ambavyo viko wazi”


Hata hivyo, Februari 7, 2023, Katani akichangia taarifa ya shughuli ya Kamati ya Hesabu za Serikali, (PAC) alisema kuwa waziri huyo amewatukana wabunge.


“Tunakwenda wapi. Mwigulu (Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba) umetutukana wabunge sana na unapaswa utafakari utakapokaa. Hakuna anayeweza kujadili waganga wakienyeji hapa. Haya tunayoyajadili ni maisha ya Tanzania na tumeletwa bungeni na Watanzania hata Iramba wanataka uwasaidie,”alisema Katani.


Kauli hiyo ilimfanya, Dk Mwigulu kuomba utaratibu ambapo alisema kanuni za Bunge zinazuia kusema uongo na mbunge anapojulisha Bunge kwamba yeye ametukana wabunge ni tuhuma kubwa.


“Bunge lako haliruhusu, mimi nisingeweza kutukana wabunge na kiti kikiwepo pamoja aepuke kuwajumuisha,”alisema Dk Mwigulu.


Akijibu kuhusu suala hilo, Dk Tulia amesema ni kweli Dk Mwigulu alitamka kauli hiyo bungeni, iliyowafanya baadhi ya wabunge kuirejea kwa mtazamo hasi.


Mbunge Katani afoka Bungeni "ulitutukana sana Wabunge" akimuunga Mpina ishu ya Bashe na Mwigulu

Hata hivyo, amesema kanuni ya Bunge ya 71 inataka wabunge kutumia lugha ya staha wakati wakiwa bungeni.


“Wabunge wakati mwingine tukichangia hatuendi na hoja bali mtu na yeye waziri ama naibu analazimika kwenda kwa mtu badala ya hoja. Kila upande ufanye kulingana na kanuni kuchangia kuhusiana na hoja na si mtu binafsi,”amesema.


Amesema lengo hasa la Dk Mwigulu lilikuwa ni kumjibu Mbunge wa Kisesa (CCM) Luhaga Mpina lakini baada ya maelezo mafupi baadaye akajikuta anasema kwa Bunge zima.


Amesema Katiba inalinda uhuru wa majadiliano na maoni ili mbunge aweze kuihoji Serikali na kuisimamia lakini kwa kuwa maneno yaliyosemwa na Dk Mwigulu yameendelea kusemwa bungeni ameagiza yafutwe kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge.

MELI KUBWA YA MV MWANZA HAPA KAZI TU KUSHUSHWA NDANI YA ZIWA VICTORIA KUENDELEA NA UKAMILISHWAJI WAKE

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Eric Hamissi amesema, Meli ya Mv Mwanza Hapa  ujenzi wake umefikia asilimia 82 hadi kukamilka kwake itakuwa imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 109 na inatajiwa kushushwa ndani ya ziwa Victoria siku ya  February 12 mwaka huu kwa ajili ya kuendelea na hatua mbalimbali za ukamilishaji wake ili iweze kukamilika na kuweza kuanza kutoa huduma za usafirishaji katika nchi ya Kenya, Uganda, Sudani ya Kusini na hapa nchini.


Ushushwaji wa Meli ni zoezi nyeti sana tumepata msaada mkubwa kutoka kwa Jeshi la Wananchi la Tanzania,Kamandi ya Wanamaji, Polisi Marine,Jeshi la Zimamoto na baadhi ya wastafu ambao wako ktika taaluma hiyo ili kuhakikisha ili zoezi linafanyika kwa hali ya usalama kabisa nichukue nafasi hii kuwashukuru wadau wote serikali ya mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Adam Malima,Jeshi la Wananchi wa Tanzania pamoja na Jeshi la PolisI, Eric Hamissi - Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, MSCL.

Ujenzi wa Meli Duniani una hatua kubwa tatu, hatua ya kwanza ni kuweka msingi wa meli, hatua ya pili ndio hii tutaiona siku ya February 12, 2023, ya kushusha sasa meli kutoka kwenye chelezo kuweka kwenye maji na hatua ya tatu itafuata baadae baada ya miezi sita itakuwa ni kujaribu mitambo ya meli na kufanya safari za majaribio kabla ya kuanza safari rasmi, Eric Hamissi - Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini, MCSL


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini, Eric Hamissi  katika tukio la ushushwaji wa meli mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa, pamoja na wakuu wa mikoa yote inayozunguka kanda ya ziwa Victoria wakiwemo wakuu wa mikoa ya Kigoma na Tabora huku akiwaalika wakazi wote wa kanda hiyo kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria la ushushwaji wa meli hiyo.

Meli ya Mv Mwanza Hapa kazi tu, ambayo ni kubwa kuliko zote katika ukanda wote wa maziwa makuu na itakuwa na uzito wa tani elfu tatu mia tano, itakuwa na urefu wa mita 92.6, pia itakuwa kuwa na kimo cha ghorofa 4 na upana wa mita 17, ina uwezo wa kubeba abiria elfu moja mia 2,mizigo tani 400 na magari kuanzia 20 kwa maana ya meli hiyo nchi yetu ya Tanzania inavunja rekodi ya kuwa na meli kubwa ambayo itaelea katika ziwa Victoria, Eric Hamissi, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini, MSCL.


BALOZI WA DENMARK AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA MATOKEO MAZURI YA FEDHA.

 


Balozi wa Denmark nchini, Mette Nørgaard Dissing-Spandet (wapili kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wakwanza kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipomtembelea ofisini kwake kujadili uwekezaji wa DANIDA ndani ya benki hiyo na Mkakati mpya wa Miaka Mitano wa Biashara wa Benki ya CRDB wa 2023/2028.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wakwanza kulia) akimwelezea Balozi wa Denmark nchini, Mette Nørgaard Dissing-Spandet (wapili kushoto) juu ya Mkakati mpya wa Miaka Mitano wa Biashara wa Benki ya CRDB wa 2023/2028 wakati ujumbe wa Benki hiyo ulipotembelea katika Ubalozi wa Denmark kujadili mafanikio ya uwekezaji wa DANIDA ndani ya benki hiyo. Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (wapili kushoto), pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Prof. Neema Mori (hayupo pichani), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (watatu kushoto), na Katibu wa Kampuni Benki ya CRDB, John Rugambo.

Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Benki ya CRDB kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela umekutana na Balozi wa Denmark nchini, Mh. Mette Nørgaard Dissing-Spandet kujadili uhusiano baina ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na benki hiyo.

Hakuna wakati mzuri wa kujadili uhusiano huo wa kihistoria kama kipindi hiki ambacho benki hiyo kinara wa utoaji huduma za kifedha nchini, imetoka kupata faida kubwa kwa mwaka uliopita.

Ikiivunja rekodi yake yenyewe iliyoiweka kwa mwaka 2021 ya faida baada ya kodi ya takriban Sh268 bilioni na kufikia faida ya Sh353 bilioni kwa mwaka 2022.

Mafanikio hayo yanaelezwa kutokana na jitihada za makusudi za benki hiyo kukuza vyanzo vya mapato yasiyotokana na riba ambapo yaliongezeka kwa asilimia 13 mwaka hadi mwaka na kufikia kiasi cha Sh400 bilioni kutoka Sh354 bilioni.

Nsekela, akifafanua rekodi hiyo, alisema imechagiwa na ongezeko la ufanyaji miamala ya fedha hususan kupitia njia za kidijitali.

Kiujumla, wanahisa wa benki hii, DANIDA akiwa mmojawapo akishirikiana na Serikali ya Tanzania, wanaendelea kuona fahari ya kuwa sehemu ya uwekezaji wa benki inayofanya vizuri kwa kuwa wana uhakika gawio lao litaongezeka maradufu.

Balozi Dissing-Spandet akizungumza na viongozi wa Benki ya CRDB alisema amefurahishwa na matokeo mazuri ya Benki ya CRDB kwa 2022 na ni kiashiria kizuri kwa matokeo yajayo.

Historia ya DANIDA na Benki ya CRDB

Uhusiano wa DANIDA na Benki ya CRDB haujaanza leo, mizizi yake ilipandwa kupitia uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Denmark.

Tanzania imekuwa mnufaika wa misaada ya kimaendeleo kutoka kwa Denmark kupitia DANIDA kwa miongo kadhaa iliyopita ikitekeleza miradi ya afya, uchumi, utafiti, ujasiriamali nk.

Wakati Benki ya CRDB ikijulikana kama Cooperative Rural Development Bank, ilipitia nyakati ngumu kiasi cha kushindwa kujiendesha hatua iliyopelekea Serikali kuiomba DANIDA kupitia wake Mfuko wa Uwekezaji wa Denmark (DIF) kuinasua benki hiyo.

Kuingia kwa DIF kama mwekezaji kuliweza kuleta mageuzi katika benki hiyo ambayo ilipelekea kuzaliwa upya kama Benki ya CRDB. Miaka kadhaa baadaye Benki ya CRDB ilifikia hadhi yakuweza kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Uwekezaji wa hisa na urudishaji kwa jamii

DIF ilianza kwa kuwekeza hisa 247,014 mwaka 2002 ambazo zimeongezeka na kufikia hisa 548,067,648 mwaka 2021 ambazo ni sawa na asilimia 21 ya hisa zote za Benki ya CRDB.

Katika upande wa gawio, DIF na Serikali ya Tanzania, zilipata kiasi cha Sh247 milioni mwaka 2002 na Sh19.7 bilioni mwaka 2021.

Uhusiano huu wa aina yake baina ya DANIDA, Serikali na Benki ya CRDB umekuwa na maana kubwa katika kuifanya benki hii kuendelea kufanya vyema kila mwaka na kupata faida katika biashara yake.

Serikali ya Denmark imeendeleza ushirikiano wake na Benki ya CRDB na sasa imewekeza kupitia Mfuko wake wa Uwekezaji unaoitwa Investment Fund for Developing Countries (IFU), kwenye Kampuni tanzu ya CRDB Bank nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa kuwa DANIDA ni mdau wa maendeleo nchini, inaelezwa kuwa Denmark ilikuwa miongoni mwa waasisi wa Fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja (HBF) mwaka 1999 na imekuwa ikiendelea kuchangia katika mfuko huo. Kwa mwaka huo pekee, ilichangia kiasi cha DKK 60 milioni.

Kupitia mchango wake katika fedha za mifuko ya afya ya pamoja kwa bara na visiwani, Danida imekuwa ikitumia fedha zake za uwekezaji kusaidia kuboresha mifumo ya afya, ubora wa huduma za afya, huduma za afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana.

Kwa mantiki hiyo, ili DIF inayoshirikiana na Serikali, iweze kuendelea kusaidia upatikanaji wa huduma za afya katika jamii zenye uhitaji mkubwa inalazimika kutenga kiasi cha gawio litokanalo na faida ya uwekezaji wake kila mwaka kwa Benki ya CRDB kufanikisha jitihada hizo.

Kwa kuwa mfuko huo na mingine bado inategemea michango kutoka kwa wadau wa maendeleo, Benki ya CRDB inabaki kuwa tegemeo la wadau wengi ambao wanachangia katika mfuko huo kupitia gawio inaloligawa kila mwaka baada ya kuwekeza hisa zao.

Ni sahihi kusema kuwa benki hiyo imekuwa ikisaidia moja kwa moja katika HBF kupitia wanahisa wake wanaopata gawio kila mwaka, kwa mantiki hiyo, ina dhima kubwa ya kuendelea kuhakikisha inakuja na mikakati bora ya kuiwezesha benki kufanya vizuri kwa mwaka huu na inayofuata na wanahisa wake kuchangia zaidi.

Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kuwa wadau wa HBF walikubaliana kuchangia kiasi cha Sh98.1 bilioni kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

“Fedha zinazoingizwa nchini kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za afya tunapenda ziingizwe kwenye Mfuko wa Afya wa pamoja ili tuweke kushirikiana kufanya kazi pamoja na kupata matokea ya haraka kwa pamoja. Mapendekezo yetu wadau wengine wachangia kupitia mfuko huo kwani tumeona mafanikio makubwa" amefafanua Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha Waziri Ummy Mwalimu amesema upo umuhimu kwa wadau wa maendeleo kuchanga fedha kwa pamoja na kuweka kwenye Mfuko wa Afya wa pamoja na kusema kuwa kufanya hivyo ni kuzingatia Mifumo na taratibu za Serikali za kutoa fedha kwa ajili ya Huduma za Afya nchini pamoja na kuwekeza fedha kwenye maeneo ya vipaumbele vya Serikali.

ZAIDI YA WANAFUNZI 50 WATEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII NYANDA ZA JUU KUSINI.

 

Afisa kutoka ofisi ya utalii Kanda ya Iringa Hoza Mbura akiwa na kundi la baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Iringa wakati walipotembelea vivutio vya utalii vya ndani vya nyanda za juu kusini vilivyopo mkoa wa Mbeya na Njombe.
Afisa kutoka ofisi ya utalii Kanda ya Iringa Hoza Mbura akiwa na kundi la baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Iringa wakati walipotembelea vivutio vya utalii vya ndani vya nyanda za juu kusini vilivyopo mkoa wa Mbeya na Njombe


Na Fredy Mgunda,Iringa.


Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Iringa inashirikiana na chuo cha Iringa kupitia kitivo cha utalii na anthropolojia katika kuvitangaza vivutio vya utalii pamoja na kuhamasisha wananchi kupenda kutembelea vivutio vya ndani.

Akizungumza na waandishi wa habari,afisa kutoka ofisi ya utalii Kanda ya Iringa Hoza Mbura alisema kuwa zaidi ya wanafunzi 50 wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha utalii na anthropolojia wamefanikiwa kutembelea vivutio vya utalii wa ndani vya nyanda za juu kusini mwa Tanzania ambavyo vitawasaidia katika masomo yao.

Mbura alisema kuwa wamefanya kampeni ya kuhamasisha wanafunzi kutembelea vivutio vya utalii vya ndani ili kuongeza idadi ya wananchi ambao hawajui umuhimu wa utalii.

Alisema kuwa wamefanikiwa kutembelea vivutio vya mkoa wa Njombe na Mbeya ambavyo ni vivutio vya utalii vya Mpanga kipengere,Ziwa Ngosi,Fukwe za Matema pamoja na daraja la Mungu ambavyo vinavutia wananchi wote wa ndani na nje ya nchi.

"Faida kubwa waliopata wanafunzi kwanza ni kujifunza juu ya vivutio vinavyopatikana kusini mwatanzania,Pia wameondoka na  experience isiyosahaulika kwani wengi ndio mara ya kwanza kufika katika vivutio hivyo"alisema Mbura

Mbura alisema kuwa faida waliyoipata kujifunza kwa vitendo juu ya vivutio vya utalii vya ndani na kulinganisha na kile wanachofundishwa darasani   na uhalisia wake katika mazingira husika ambayo itawasaidia katika masomo yao. 

"Lengo nikuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni maalumu ya shule za msingi sekondari na vyuo vya elimu"

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imehitimisha kampeni ya kutangaza,na kuhamasisha utalii wa ndani kupitia vivutio vya utalii vilivyopo Njombe na Mbeya ambapo zaidi ya wanafunzi 50 wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha utalii na anthropolojia walihamasika kutembelea vivutio hivyo wakiwa sambamba na maafisa wa ttb kanda ya iringa.

Wametembelea vivutio vya daraja la mungu God's Bridge,daraja kubwa la asili lililounganishwa na kingo mbili za mto kiwira wilaya ya Rungwe takribani kilometa 10 upande wa magaharibi mwa tukuyu,


Wednesday, February 8, 2023

CHANJO YA COVID 19 SASA NYUMBA KWA NYUMBA - NI HIYARI ELIMU YATOLEWA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Kupitia Jembe Fm ndani ya kipindi cha Drive Mix ungana na mtangazaji wako Mc Suzuki akiwa na wadau wa Afya Elimu ya UVICO 19 waliofanya nasi mahojiano.

WAWILI WANASWA NA JESHI LA POLISI VURUGU ZA MACHINGA MWANZA LEO

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

JESHI la polisi mkoani Mwanza linawashikilia vijana wawili ambao imeelezwa walikuwa vinara wa kuhamasisha maandamano na kupelekea vurugu katika maeneo ya Makoroboi, Nyerere Square na Lumumba wilayani Nyamagana mkoani Mwanza. Akitoa taarifa juu ya vurugu hizo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza WILBRAD MUTAFUNGWA amesema jeshi hilo linaendea pia kuwafuatilia na kuwabaini kundi la vijana wadogo waliojichanganya na baadhi ya machinga waliofanya maandamano hayo. Amesema vurugu hizo zimepelekea madhara mbalimbali lakini si madhara ya kibinadamu ambapo mpaka sasa mitaa hiyo imedhibitiwa na hali ni shwari kwa muktadha wa usalama. AIDHA KAMANDA MUTAFUNGWA AMESEMA JESHI HILO LIMEJIPANGA KUHAKIKISHA KUWAKAMATA WALE WOTE WANAOTAKA KUJARIBU KUFANYA VURUGU YOYOTE #samiasuluhuhassan #mwanza #VuruguMwanza #VuruguMachingaMwanza

WATEJA 7 WA NMB MASTABATA KOTE KOTE WAJISHINDIA SAFARI KWENDA DUBAI.

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi (wa pili kushoto) na mwanahabari - Millard Ayo (wa pili kulia), wakibonyeza kitufe cha kompyuta wakati wa droo ya kutafuta washindi saba wa ‘Grand Finale’ ya kampeni ya NMB MastaBata Kote Kote. Wakishihudia ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa NMB - Philbert Casmir (kushoto) na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) - Upendo Mfuru.

KAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya NMB mastercard na QR Code 'Lipa Mkononi' iitwayo NMB MastaBata 'Kote Kote', imefikia ukomo kwa wateja 7 na wenza wao kujishindia safari ya Dubai kwa siku nne inayogharamiwa kila kitu na Benki ya NMB.

Kampeni hii imeendeshwa kwa miezi  mitatu na kutoa zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh. Mil. 350 kwa washindi.

Akizungumza katika droo hiyo ya fainali Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB - Filbert Mponzi aliwataja washindi hao kua ni: Upendo Yohana Msanjila (Dar), Edwin Sett Mwakabage (Kilimanjaro), Benigna Xaveria Hyera (Dar), Nazia Abdulsatar Lakha (Dar), John Wayne Lubisha (Dodoma), Chintan Chandrakant Kamania (Dar) na Qamara Rose Aloyce (Arusha)


Kampeni ya NMB MastaBata 'Kote Kote' msimu wa nne ilizinduliwa Oktoba 28 mwaka jana ili kuchagiza matumizi yasiyohusisha pesa taslimu 'cashless'

Kabla ya 'grand finale' hiyo, jumla ya washindi 750 walishinda pesa kiasi cha Sh.100,000 kila mmoja, wengine 98 wakizawadiwa Sh. Mil. 1 kila mmoja, huku washindi 12 wakitwaa bodaboda moja moja zenye thamani ya Sh. Mil. 3 kwa kila moja na washindi wengine wanne wakijishindia safari ya Zanzibar kuhudhuria Tamasha la NMB Full Moon Party.


Kampeni hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kubadili tamaduni za matumizi ya kadi na QR Code ambayo ni salama, rahisi na nafuu zaidi.

HIVI NDIVYO UZI MPYA WA SIMBA ULIVYOZINDULWA

 

UZINDUZI wa uzi mpya wa Simba wenye nembo ya Visit Tanzania amao utatumika kwenye mechi z kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi

Tuesday, February 7, 2023

SHABIKI WA YANGA ALIYETOKA MWANZA KWA BAISKELI ATINGA MOROGORO.

 Majaliwa Update 👉Uongozi wa tawi la Yanga Dumira Morogoro umempokea  ndugu Majaliwa kutoka mwanza kwa baiskeli  kwasasa  analala hapa Dumira,   ðŸ–Š️ By Hashim Omary

AGIZO LA WAZIRI AWESO LATEKELEZWA MWANZA.


Uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba la maji ukiendelea eneo la Buswelu Mkoani Mwanza Ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Jumaa Aweso ya kutanua mtandao wa maji.

 Na Mohamed Saif 


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameielekeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kuanza mara moja kuongeza mtandao wa usambazaji maji Kata ya Buswelu Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza. 

Ametoa maelekezo hayo Februari 4, 2023 alipofanya ziara kwenye tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa  lita milioni 3 la Buswelu Mkoani Mwanza.

Akiwa katika mradi huo wa tenki, Waziri Aweso alielezwa kuwa licha ya tenki hilo kukamilika maeneo pekee yanayonufaika kwa sasa ni Buswelu, Bujingwa, Buhila, Buyombe na Mwashosha na kwamba bado kuna maeneo ambayo hayajafikiwa na miundombinu ya maji.

"Haileti maana kuona tenki hili limekamilika lakini baadhi ya wananchi hawana huduma ya maji, dhamira ya Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kumtua Mama ndoo kichwani na hapa bado Mama hajatuliwa ndoo kichwani," amesisitiza Waziri Aweso.

Kufuatia maelezo hayo, Waziri Aweso aliiagiza Wizara ya Maji kuipatia MWAUWASA kiasi cha shilingi milioni 500 ili kuhakikisha maeneo yanayopaswa kunufaika na tenki hilo yanafikishiwa miundombinu ya maji mara moja.

"Sisi Wizara hatutakuwa kikwazo kwa wananchi wa Buswelu kupata maji, MWAUWASA nataka kuona utekelezaji wa mradi huu unaanza mara moja ili kuwaondolea adha wananchi wa Buswelu," ameelekeza Waziri Aweso.

Awali kabla ya ziara yake kwenye tenki hilo, Waziri Aweso alikutana na Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya MWAUWASA ambapo alielekeza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma ya maji inaimarika kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake.

Aidha, mapema hivi leo Februari 6, 2023 ikiwa ni siku mbili tangu MWAUWASA kupokea maelekezo ya Waziri Aweso, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Meck Manyama ametembelea eneo hilo ili kujiridhisha na juu ya kuanza kwa  utekelezaji wa maelekezo ya Waziri. 

Akiwa katika eneo hilo, amekuta kazi za uchimbaji mitaro ya kulaza mabomba ya mtandao wa usambazaji maji zikiendelea kutekelezwa na baada ya kujiridhisha kuwa kazi inakwenda vizuri na kwa kasi Manyama ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maji hususan Mhe. Waziri Aweso kwa kuipatia MWAUWASA fedha haraka ili kuongeza mtandao wa usambazaji maji kutoka kwenye mradi wa tenki la maji Buswelu kwa kuhakikisha wananchi wa Kata ya Buswelu wanapata huduma ya majisafi na salama. 

"Tumepokea  maelekezo ya Mheshimiwa Waziri na  tumeanza kuyatekeleza, ninaahidi kuwa maelekezo aliyotoa Waziri wetu wa Maji yanatekelezwa na kukamilika kwa wakati kwani tayari uchimbaji wa mitaro umeanza na baadhi ya bomba zimefika na ulazaji wake unafanyika, tunachimba na kulaza bomba vyote vinakwenda kwa pamoja," amesema Manyama.

Manyama ametaja mitaa ya Kata ya Buswelu itakayonufaika kuwa ni Kadinda, Kigala, Buhila, Majengo na Halimashauri  ambapo amesema zaidi ya wananchi 40,000 kutoka maeneo hayo watanufaika.

"Niwasihi wananchi wa maeneo ya mradi kuhakikisha wanatunza na kulinda miundombinu hii ambayo imeigharimu fedha nyingi Serikali yetu. Tunapenda kuona wananchi wanapata huduma endelevu," amesema Manyama.


Monday, February 6, 2023

NI VILIO TU.

 Vilio simanzi na uzuni zimetanda kwa wananchi wa wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wakati wa shughuli za kuaga miili ya watu 12 waliofariki kwa ajali ya gari Februari 3 mwaka huu katika eneo la Magira Gereza wilayani Korogwe mkoani Tanga wakati wakielekea Rombo kwa mazishi ya Atanas Mrema.


 "Msiba huu ni mkubwa ambao hauwezi kuelezeka hivyo niwape pole wananchi wa Rombo hasa wanafamilia kutokana na kuondokewa na ndugu zenu niwaombe mjipe moyo katika kipindi hiki kigumu" Nurdin Babu RC Kilimanjaro.


 "Tunayo majonzi makubwa wanakilimanjaro na tunachopaswa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi na tuwaombee ndugu zetu wapumzike mahali pemapeponi" Nurdin Babu RC Kilimanjaro.
 "Niwaombe viongozi wa dini kufanya maombi makubwa katika nyumba za Ibada ili kuepusha ajali zinazopeleka vifo vya watu" Nurdin Babu RC Kilimanjaro.

 "Jeshi la Polisi endeleeni kutoa elimu kwa madereva kufuata sheria za barabarani kwani wapo baadhi ya madereva wamekuwa hawafuati alama na sheria za barabarani hali inayopelekea vifo vya watu kutokana na ajali" Nurdin Babu RC Kilimanjaro.


POLISI SHINYANGA WAKAMATA WATU 9 TUHUMA ZA UJAMBAZI.

 

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limewakamata watu tisa wanaosadikiwa kuhusika katika tukio la ujambazi lililotokea Februari 4, 2023 katika kambi ya Wachina wanaojenga reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR eneo la Old-Shinyanga katika Manispaa ya Shinyanga.


Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao kufuatia msako na doria zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Magomi amesemna pamoja na watuhumiwa hao jeshi hilo limekamata pesa za kigeni za nchi mbalimbali ambapo amesema uchunguzi unaendelea na kwamba watuhumiwa watafikishwa mahakamani wakati wowote.

Kamanda Magomi ameendelea kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutojihusisha na hujuma dhidi ya mradi wa reli ya Kisasa ya Mwendo kasi SGR pamoja na uhalifu mwingine.

Kamnada huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga amesema kuhujumu miundombinu katika mradi wa SGR na miradi mingine ni kurudisha nyuma juhudi za serikali ambayo imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.

CHARLES HILARY ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI YA ZANZIBAR.

 


Charles Hilary

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Charles Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali. Charles Hilary ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu, Zanzibar.

Ikumbukwe Charles Hilary ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi nchini Tanzania.


Cheo hicho hakikuwahi kuwepo ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk Salmin Amour

Sunday, February 5, 2023