ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 28, 2022

TANGA UWASA YATENGA MILIONI 900 KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI

 

Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Maji Cup yanayofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kombezi Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo  akizungumza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani

 

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Maji Cup





Na Oscar Assenga,TANGA.



MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) katika mwaka wa fedha 2022/2023 wametenga milioni 990 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha wanapambana na upotevu wa maji.

Hayo yalisemwa  na Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Maji Cup yanayofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kombezi Jijini Tanga.

Alisema fedha hiyo imetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali zikazopelekea kupunguza upotevu wa maji ambapo mwaka jana ulikuwa wastani wa asilimi 30 kwa kutekeleza hayo hiyo miradi wanaimani watapunguza upotevu huo hadi kufikia asilimia 26 June 2023.

Alisema kazi ambazo wanazilenga kuzifanya ni kuboresha miundombinu kwa ajili ya kuzibiti na kupunguza upotevu wa maji kutoka kwenye mabomba na watanunua na kufunga mita za malipo kabla hizo mita ni za aina yake na hivyo itakuwa mamlaka ya maji ya kwanza kuonyesha aina hiyo ya mita.



“Mita hizi tunatarajia tutaanza kuzifunga mwezi huu uzuri mita hizi kama kuna uvujaji mbele ya mita mteja anapata ujumbe kuna matumizi yanafanyika hebu fuatilia agizo hilo ni la wizara na sisi tunatekeleza kwa sababu tunataka kufunga mita ambazo ni rafiki kwa mtumiaji hiyo ni aina rafiki kwa sababu ina mjali mteja”Alisema



Kaimu Mkurugenzi huyo alisema wamekuwa wakipokea malalamiko bili kubwa na moja ya chanzo ni maji kuvunja mbele ya mita hivyo hilo litakwenda kutatua hilo tatizo ikiwemo kuendelea kuelimisha jamii juu ya udhibiti wa upotevu wa maji na utoaji wa taarifa kwa mamlaka.



“Tunamshukuru Rais kutoa fedha zilizowezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayolenga kuondoa kero ya maji nchini na nyengine nga imeshaleta mabadiliko makubwa ya utapatikanaji wa huduma ya maji nchini ikiwemo Jiji la Tanga ambapo kwa sasa imefikia asiimia 97”Alisema



Hata hivyo alisema Serikali itoa bilioni 13.31kwa ajili ya kujenga miradi ya maji kuhakikisha wananchi wa Jiji la Tanga wanapata huduma ya maji safi na salama.

Alisema pia wamepenga kutanua mtambo wa kusafisha maji eneo la Mowe ambapo wametenga Bilioni 9.1 na kwa sasa unaendelea na umefikia asilimia 62.

“Lakini pia tumeendeleza mtandao wa mabomba kilimota 17.6 maeneo ya Kichangani,Pongwe,Masiwani na Neema huu ni mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa Uviko na umekamilika asilimia 100 ulikuwa na thamani milioni 500”Alisema

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema licha ya hivyo serikali imewezesha fedha kujenga mradi wa maji kufikisha huduma maeneo ya Kibafuta,Mleni ,ndaoya,mpirani na chongoleani na kata ya chongoleani ni eneo pekee la Jiji la Tanga ambalo lilikuwa halina mtandao wa huduma ya maji sasa miundombinu imefika na wananchi na wameanza kupata huduma hiyo ya maji.

“Mradi hu wa kupelekea maji Chongoleani una thamani ya Milioni 918 na utekelezaji mradi umefikia asilimi 90 lakini pia kuna mradi wa kulaza bomba kubwa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo ”alisema

Alieleza hiyo inatokana na wananchi wa eneo la Chongoleani kupata maji kwa mgawo na serikali imetoa bilioni 2.7 kwa ajili ya kulaza bomba kubwa kutoka eneo la Amboni mpaka Chongoleani ili kuhakikisha wanapata maji muda wote.

DC MOYO :ZAIDI YA WANANCHI 48, 434 WAMEJITOKEZA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19

 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akishuhudia baaadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakipata chanjo ya UVIKO 19 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kuchanja inayoendelea nchini nzima.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akishuhudia baaadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakipata chanjo ya UVIKO 19 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kuchanja.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baaadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakati wa kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO 19 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kuchanja inayoendelea nchini nzima.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akishuhudia baaadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakipata chanjo ya UVIKO 19 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kuchanja.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akishuhudia baaadhi ya wananchi wa wilaya hiyo wakipata chanjo ya UVIKO 19 kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kuchanja.

 

Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

ZAIDI ya wananchi 48,434 wa wilaya ya Iringa wamefanikiwa kuchanja chanjo ya UVIKO 19 kwa lengo la kuendelea kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Colona ambao umeshasababisha vifo vingi vya wananchi wa wilaya hiyo.

 

Akizungumza wakati wa kampeni ndogo ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO 19, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa hadi kufikia tarehe 26/7/2022 walikuwa wamewafikia jumla ya wananchi 48,434 ambao wamepata chanjo ya UVIKO 19 dozi ya pili ya chanjo ya Janssen ambayo ni sawa na asilimia 39.24 ya walengwa 123,418.

 

Moyo alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuhamasisha wananchi waliokuwa na miaka 18 na kuendelea waweze kupata chanjo ya UVIKO 19 katika kipindi cha kampeni ndogo inayoendelea hivi sasa katika wilaya ya Iringa.

 

Alisema kuwa kwa sasa wilaya ya Iringa imetenge jumla ya vituo 79 vinavyotoa huduma za chanjo pamoja na zoezi la uchanjaji katika vituo watoa huduma wanaotumia huduma za mkoba ili kuwafikia wananchi popote walipo.

 

Moyo alisema kuwa viongozi wa serikali, taasisi mbalimbali kama shule,vyuo, viongozi wa bajaji, daladala,bodaboda,saluni,vikoba, viongozi wa dini,siasa wadau wa afya,wazee mashuhuri na wazee wa kimila kuhakikisha wanashirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kuhamasisha jamii ili iweze kupata chanjo ya UVIKO 19.

Alisema kuwa wataalamu wa afya na jamii wanapaswa kupongezwa kwa namna ambavyo wamekuwa wanalishughulikia suala la kitaifa kwa kuwa inaonyesha kwa namna gani wanavyojitoa kutoa elimu kwa wananchi hadi wanachanja kwa hiyari chanjo ya UVIKO 19.

 

Moyo alisema kuwa anatarajia wananchi ambao hawajapata chanjo ya UVIKO-19 watashiriki kupata chanjo hiyo ambayo inaendelea kutolewa na wataalamu wa afya.

 

“Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiwaasa wananchi kushiriki kupata chanjo ya UVIKO-19 kwani maradhi hayo bado yapo nchini hivyo tushiriki kupata chanjo ya UVIKO-19,” amesema.

  

Moyo amesema baada ya maneno ya uongo na dhana potofu kuonekana kuwa ni propaganda zisizo na maana yoyote, wananchi wameamua kushiriki chanjo ya UVIKO-19 kwa manufaa yao.

 

“Mara nyingi kitu kigeni kikitokea kuna baadhi ya watu wanapotosha na kuzungumza ndivyo sivyo juu ya jambo hilo utadhani wanalitambua kumbe hawafahamu ila hili la UVIKO-19 wengi wao wamelitambua na kulielewa ndiyo sababu wamejitokeza kwa wingi kuchanja,” anasema Moyo

 

Mkazi wa kata ya Magulilwa John mwigane anasema wataalamu wa afya wamekuwa wanafika hadi vijijini na kutoa elimu kwa jamii kIsha kuwapatia chanjo hiyo ya UVIKO-19.

 

“Hadi hivi sasa elimu inaendelea kutolewa kwa jamii huku vijijini na wanaitikia ushauri wa kupatiwa chanjo ya UVIKO-19 kwani wanatambua kuwa ukipata maradhi hayo bila kuchanja utapata matatizo makubwa kwenye changamoto ya kupumua pindi ukiupata ugonjwa huo,” anasema.

 

Mkazi wa kijiji cha Ndiwili Hamisa Malima anasema kuwa viongozi na wananchi wa Wilaya ya Iringa kwa pamoja wameungana katika kuhakikisha wanapata chanjo ya UVIKO-19 ndiyo sababu ya wananchi kujitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO 19.

 

“Mtu anaona atapata maambukizi ya UVIKO-19 yeye mwenyewe na hayo ni maradhi ambayo hayana matibabu hivyo ameona hawezi kupata tatizo kisa kutochanjwa kwa kutosikiliza wataalamu wa afya na kuwasilikiza wazushaji,” anaeleza

 

Hivi karibuni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza hivi karibuni kwenye tamasha la MZIKI MNENE lililofanyika uwanja wa Nangwanda Mkoani Mtwara amesema imethibitika kuwa njia ambayo ni salama ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 ni kupata chanjo kwani ukichanja utakuwa umejikinga na kuikinga jamii ya watanzania.

 

Waziri Ummy amesema Serikali inaendelea kuwalinda wananchi wake katika maambuzi ya magonjwa mbalimbali kwa kutoa chanjo ikiwemo ya UVIKO-19.

 

“Sisi kama Wizara ya Afya tutatumia mbinu mbalimbali ambazo zitakazowafikia wananchi kama tunavyotumia matamasha haya kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kupata huduma ya chanjo ya UVIKO-19,” anamaliza kwa kusema Waziri Ummy.

TUTAISHANGAZA DUNIA -TIMU YA JUMUIYA YA MADOLA

 

Na John Mapepele, Birmingham - Uingereza

Kocha Mkuu Timothy Kingu wa kikosi cha ndondi kinachoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yanaanza rasmi leo Julai 28,2022 amemhakikishia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania wote kurejea na medali za ushindi kwenye mchezo huo kwa kuwa wamepata maandalizi ya kutosha.

Akizungumza katika kambi ya wachezaji hao jijini Birmingham, Uingereza amesema wachezaji wake wamepikwa vizuri na watapata hamasa ya kutosha tayari kwa ajili ya pambano lililopo mbele yao.

Aidha, amesema hamasa kubwa inayotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri anayesimamia Michezo nchini, Mhe Mohamed Mchengerwa na wadau mbalimbali kwa sasa zinawafanya wawe na ali na nguvu zaidi ya kushindana kufa na kupona kwenye mashindano haya.

Hadi sasa, tayari Mabondia wawili wa Tanzania Yusuf Changarawe na Kassim Mbundwike wameingia robo fainali za mchezo ya Jumuiya ya Madola inayoanza rasmi leo jijini Birmingham, Uingereza.

Bondia wa tatu wa Tanzania, Alex Isinde sio tu ataanzia mzunguko wa kwanza bali pia atakuwa ndiye Mtanzania wa kwanza kutupa kete kwenye mashindano haya ya 48 ya nchi zilizopata kutawaliwa na Uingereza kesho Julai 29, 2022. 

Isinde atapambana na bondia kutoka Antigua & Barbuda aitwaye Alston Ryan. 

Endapo Isinde atashinda ataungana na wenzie katika robo fainali ambapo mshindi anabeba medali ya shaba.

Endapo wakishinda robo fainali wataingia nusu fainali ambako watawania kunyakua angalau medali za fedha.

Michezo ya Jumuiya ya Madola 2022 inazinduliwa rasmi leo saa mbili usiku kwa saa za huku (Tanzania iko mbele kwa saa mbili).

Tanzania itatupa tena kete zingine siku ya Jumamosi Julai 30, 2022 wakati wanariadha wanne wa mbio ndefu (Marathon) wanawake na wanaume wataingia kuchuana.

Wanariadha hao wa marathon ni Alphonce Simbu, Hamisi Misai, Jakline Sakilu na Failuna Matanga.

Kwenye michezo hiyo Tanzania inawakilishwa na wanariadha tisa, mabondia watatu, wacheza judo wawili, waogeleaji wawili na mnyanyua vitu vizito kwa walemavu (Para-Powerlifting) mmoja.

Tuesday, July 26, 2022

WAZIRI MCHENGERWA AONGOZA KIKAO CHA UJUMBE WA TANZANIA BIRMINGHAM UINGEREZA

 


Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe,  Mohammed Mchengerwa  ameongoza kikao cha maandalizi ya ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Mawaziri wa Michezo wa Jumuiya ya Madola kitakachoanza leo Julai 26 mjini Birmingham, Uingereza. 


Kikao hicho ni maandakizi mahususi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu yanayofanyika nchini Uingereza huku Tanzania ikiwa imeshiriki katika michezo hiyo.

Katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza Serikali imetoa  motisha kubwa kwa wachezaji watakaofanya vizuri na kurejea na tuzo nchini.

Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha   michezo inatumika kikakamilifu kuitangaza Tanzania kimataifa.

Aidha, amesema michezo ni ajira na uchumi mkubwa ambapo amesisitiza wachezaji wote kuwa wazalendo kujituma kufa na kupona kwa ajili ya taifa la Tanzania.

Amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuleta mapinduzi  makubwa kwenye sekta za michezo katika kipindi kifupi iliyopo madarakani.

Miongoni mwa motisha hizo amesema  Serikali itatoa kiasi cha  dola  10,000 za kimarekani kwa mchezaji atakayerejea na medali ya dhahabu, dola 7000 kwa medali ya Shaba na dola 5000 kwa medali ya fedha.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt, Asha-Rose Migiro, Mhe. Mussa Sima ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Ndugu Saidi Yakubu pamoja na wajumbe kutoka Tanzania.

Monday, July 25, 2022

BALOZI WA UJERUMANI ATEMBELEA TENDAGURU NA KUSHUHUDIA MFUPA WA MJUSI

 

Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Regine Hess akiwa ameshikilia moja ya mfupa wa mjusi wakubwa wanaopatikana Tendaguru, Lindi alipotembelea eneo hilo Balozi wa Ujeruman nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess na mumewe Collins Davidson wakiwa wameshikilia moja ya mfupa wa mjusi mkubwa walioishi eneo la Tendaguru, Lindi miaka zaidi ya miaka milioni 150 iliyopitaBalozi wa Ujeruman nchini Tanzania Mhe. Regine Hess katika picha ya pamoja na wenyeji wa vijiji vinavyozunguka Tendaguru alipotembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki.


Na Mwandishi Wetu, Lindi

Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe.Regine Hess ametembelea eneo la Kipalaentolojia la Tendaguru, Mkoani Lindi ikiwa ni ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Malikale yanayopatikana kusini mwa Tanzania. 

Katika ziara yake kwenye Hifadhi ya Tendaguru, Balozi Hess alifurahishwa na historia ya eneo hilo ambalo masalia ya Mijusi mikubwa aina ya Dinosaria waliopata kuishi takribani miaka milioni 150 iliyopita imekuwa ikipatikana katika eneo hilo. 

Hifadhi hiyo ya Tendaguru ambayo inasimamiwa na Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania (NMT) ni moja ya maeneo muhimu sana Dunia na ilitangazwa kwenye gazeti la Serikali kuwa Urithi wa Taifa mnamo mwaka 1937. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi alishuhudia mfupa ya Masalia ya Mijusi wakubwa takribani kilo 7 hadi 10 na zana za mawe za kati katika eneo hilo la Uhifadhi.

Itakumbukwa ya kwamba kati ya mwaka 1905-1913 takribani tani 225 ya mifupa ya Mijusi ilichimbwa katika eneo hili na kusafirishwa kwenda Ujerumani.

Pamoja na changamoto ya barabara kuelekea katika Hifadhi hiyo, Balozi wa Ujerumani amewapongeza Makumbusho ya Taifa Tanzania (NMT) kwa kazi nzuri ya ujenzi wa kituo cha taarifa eneo la Mkwajuni ambacho kitatoa taarifa juu ya historia ya hifadhi ya Tendaguru pamoja na kuweka maonesho kwa wageni watakaotembelea eneo hilo.

Balozi Hess ambaye pia alipokelewa na viongozi wa vijiji vya Mkwajuni, Mnyangala na Mipingo amepongeza mpango wa Makumbusho ya Taifa Tanzania (NMT) wa kuweka vibao vya maelezo katika hifadhi hiyo ya Tendaguru na kusisitiza juu ya kufanyika kwa utafiti zaidi katika eneo hilo na kuboresha miundombinu kwa ajili ya kupata watalii zaidi katika eneo hilo muhimu kwenye historia ya Dunia. 

Aidha, wakaazi wa maeneo hayo wakiongozwa na viongozi wao, walimuomba Balozi wa Ujerumani kuwasaidia kuboresha miundombinu kwa ajili ya eneo hilo kuweza kufikika kirahisi wakati wote wa majira ya mwaka.

VIFARANGA VYA KUKU KUTOKA NJE YA NCHI MWISHO JULAI 30

 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), akizungumza kwenye kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma na kuweka wazi kuwa baada ya tarehe 30 mwezi huu, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini kutoka nje ya nchi na kwamba serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo ili kuzuia ugonjwa mafua ya ndege na kulinda wazalishaji wa vifaranga wa ndani ya nchi. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Stephen Michael ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko akizungumza kwenye kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma ambapo amesema katika Mpango Kabambe wa Sekta ya Mifugo wa Mwaka 2016 umefanya tathmini na kuainisha kuwa hadi kufikia Mwaka 2031 kutakuwa na upungufu wa nyama kwa tani milioni 1.8 hivyo tasnia ya kuku ni rahisi ikitiliwa mkazo itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa nyama nchini. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Bw. Evance Ntiyalundura akiwa kwenye kikao cha wadau wa tasnia ya kuku jijini Dodoma ambapo amefafanua hatua mbalimbali katika kukuza tasnia hiyo ikiwemo ya kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na wadau wa tasnia. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Hezron Nonga, akiwa mmoja wa washiriki katika kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma na kuelezea umuhimu wa wadau kujisajili kwenye mfumo ili kutambulika kisheria na namna serikali inavyotoa vibali mbalimbali vya kusafirisha mifugo kikiwemo cha kuku. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Nyanda za Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo Dkt. Asimwe Rweguza akifafanua umuhimu wa matumizi ya vyakula bora vya mifugo hususan vya kuku na kuwakumbusha wazalishaji wa vyakula hivyo kutumia maabara ya Wakala ya Veterinari Tanzania (TVLA) kuhakiki ubora wa vyakula wakati aliposhiriki kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)


Msajili wa Bodi ya Nyama nchini Dkt. Daniel Mushi akitolea ufafanuzi ombi la wafugaji wa kuku kuwepo kwa machinjio ya kuku kila wilaya ili kuzuia uuzwaji holela wa kuku na kuwepo kwa bei elekezi ya kuku sokoni, wakati aliposhiriki kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)



Katibu wa Chama cha Wadau wa Kuku Tanzania (PAT) Bw. Manase Mrindwa akielezea changamoto za chakula cha kuku kuwa kumetokea ongezeko la bei ya chakula cha kuku hadi kufikia Shilingi Elfu 80 kwa mfuko mmoja kwa mwezi wa Julai kutokana na ongezeko la bei ya mahindi na mashudu ya soya kwenye soko la Tanzania pamoja na kuelezea uwepo wa uhaba wa vifaranga, wakati akisoma taarifa ya chama hicho kwenye kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichofanyika jijini Dodoma. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)

Muonekano wa washiriki katika kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo kimejumuisha menejimenti ya wizara Sekta ya Mifugo, wazalishaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na wafugaji wa kuku ambapo wametoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha tasnia hiyo na kuomba kuwepo kwa vikao vya namna hiyo mara kwa mara lengo likiwa ni kukuza tasnia. (Picha na Edward Kondela, Afisa Habari - Wizara ya Mifugo na Uvuvi)





Na. Edward Kondela 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema baada ya tarehe 30 mwezi huu, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na kwamba serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo (22.07.2022) jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo ambapo lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akizungumza wakati akifunga kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Mhe. Ulega amesema ni mategemeo kuwa serikali haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi na kutaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi.” Amesema Mhe. Ulega

Awali Naibu Waziri Ulega akizungumza wakati akifungua kikao hicho cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku amesema tasnia hiyo imekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo kwa soko linalotokana na ongezeko la watu na kipato, ongezeko la uwekezaji na uwepo wa mazingira bora ya uwekezaji katika tasnia ya kuku, urahisi wa kufuga kuku na uwezekano mkubwa wa kuwamiliki kuliko wanyama wakubwa.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Bw. Stephen Michael akizungumza kwenye kikao hicho amesema kutokana na umuhimu wa tasnia ya kuku katika Mpango Kabambe wa Sekta ya Mifugo wa Mwaka 2016 umefanya tathmini na kubainisha kuwa hadi kufikia Mwaka 2031 kutakuwa na upungufu wa nyama kwa tani milioni 1.8 hivyo tasnia ya kuku ni rahisi ikitiliwa mkazo itasaidia katika kuongeza uzalishaji wa nyama nchini.

Bw. Michael ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uzalishaji na Masoko katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, amesema ufugaji wa kuku ni njia rahisi na ambayo haihitaji maeneo makubwa na miundombinu mingi tofauti na mifugo mingine hivyo kikao hicho ni muhimu kwa kuwa kimeunganisha wadau wa tasnia hiyo pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwa kuzingatia uwepo wa taasisi mbalimbali zinazotoa mikopo kwa vijana na akina mama na vikundi mbalimbali ambao wengi wamejizatiti katika biashara ya kuku.

Naye Katibu wa Chama cha Wadau wa Kuku Tanzania (PAT) Bw. Manase Mrindwa amebainisha changamoto za chakula cha kuku kuwa kimefikia hadi Shilingi Elfu 80 kwa mfuko mmoja kwa mwezi wa Julai ambapo kunatokana hasa na ongezeko la bei ya mahindi na mashudu ya soya kwenye soko la Tanzania.

Bw. Mrindwa amebainisha pia changamoto ya kutokea kwa uhaba wa vifaranga kwa wakati fulani wa mwaka, huku mitaani bado viko vifaranga visivyo bora ambavyo vinawafikia wafugaji hususan wafugaji wadogo.

Kikao cha wadau wa tasnia ya kuku kilichoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kimejumuisha menejimenti ya wizara Sekta ya Mifugo, wazalishaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na wafugaji wa kuku ambapo wametoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha tasnia hiyo na kuomba kuwepo kwa vikao vya namna hiyo mara kwa mara lengo likiwa ni kukuza tasnia hiyo kwa kuirasimisha na kuwepo kwa machinjio maalum kwa ajili ya kuku na bei elekezi ya kuku sokoni.


RC PWANI AFUNGA MICHUANO YA UMISHUMTA.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akibabidhi kombe kwa Baadhi ya timu ambazo zimefanya vizuri katika michuano hiyo.

Na Victor Masangu, Pwani

MKUU wa mkoa Pwani Abubakari  Kunenge amewataka wanamichezo wa Umitashumta Mkoa wa Pwani watakaokwenda kushiriki katika kivumbi Cha  michezo ya Umitashumta kitaifa mkoani Tabora kuhakikisha wanaupeperusha vema Mkoa na sio kufanya vinginevyo.


 Kunenge ametasema  hayo leo katika mashindano ya ufungwaji wa Umitashumta Mkoa Pwani yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kibaha iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani hapa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na wanafunzi kutoka wilaya zote Saba za Mkoa wa Pwani.


 Aidha mkuu huyo amesema kwamba wanamichezo watakaoenda Tabora hasa wasichana wajiepushe na vitendo vyote vichafu kwani wakifanya hivyo watajiletea aibu wao wenyewe, wazazi wao na Mkoa Pwani kwa ujumla.


 'Kikubwa zaidi nawataka wanamichezo wote wa Mkoa wa Pwani mtakaochaguliwa kutuwakilisha Mkoa nendeni mkapamnane na mkashindane na mrudi na ushindi mkubwa na si kwenda kujiingiza kwenye mambo yote machafu", 


    "Kwa jinsi mlivyojiandaa kuanzia leo nitakuwa mlezi wa timu hii ila kikubwa nasisitiza nidhamu pindi mtakapokuwa uko katika michuano hasa nyie wanamichezo ambao no waluvana wavulana nendeni mkawalinde madada zenu,"akisema KUNENGE.


Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa huyo ameuomba uongozi wa Mkoa kupitia kwa Katibu Tawala kukaa na kuangalia ni kwa namna gani wataweza kuinua michezo mkoani Pwani.


   "Tumeweza kukaa na kuboresha elimu tukapata wawekezaji na sasa ni zamu ya kuona ni namna gani tutaweza kwenye michezo", alimaliza Kunenge


Kwa upande wake Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta alisema kuwa lengo kubwa kwa mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanaibuka kidedea katika michuano ya Taifa katika kushinda katika michezo mbali mbali.


Aidha Buleta aliwaomba wadau na viongozi mbali mbali kushirikiana bega kwa bega kuisapoti timu ya Mkoa kwa Hali na Mali ili kuwawezesha wachezaji wote kuwa na molali ya kuibuka na ushindi katika kivumbi Cha michuano hiyo ngazi ya Taifa.