ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 9, 2019

WAJUMBE SADC WATEMBELEA VIWANDA 21, WAKOSHWA NA JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA VIWANDA
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa. 

“Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.Katika ziara hiyo Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu,huku ikionesha pia ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.

Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakharesa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Biotan Group Limited,Bahati Mayoma akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.

Akizungumzia kuhusu soko,Mayoma alibainisha kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.Alisema kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka. 
Baadhi akina mama wakibangua korosho ndani ya kiwanda cha BIOTAN,kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.Picha na Michuzi JR.

*Wengine wasifu teknolojia ya hali ya juu walioyoina kwenye viwanda vya Tanzania
  
*Wakiri Tanzania inaweza kuliteka solo la Jumuiya ya SADC ,waona fursa lukuki


 Na Ripota, Michuzi TV 

WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa  Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea  viwanda 21vinavyofanya uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo  Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.

 Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.
  
Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia   katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.

Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.
  
Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani  ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia  mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.
  
Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.
  
"Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi
  
"Lakini  uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.
  
Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.

Akitoa maelezo kuhusu  uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.
  
“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Bhachu na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.
  
Hata hivyo katika ziara hiyo, wajumbe wa SADC pia walipata fursa kutembelea kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
  
Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonyesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu pia ulionyesha ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.

Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakhresa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.
  
“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
  
“Katika kuhakikisha tunakuza ajira na kuongeza tija katika uzalishaji, kwa asilimia kubwa malighafi zetu zinatoka Tanzania. Tuna ardhi kubwa inayotuwezesha kukusanya matunda kila kona ya nchi, tunayasindika na kuuza nje ya nchi kwa kiwango cha kutosha. Asilimia 15 ya bidhaa zetu tunazisafirisha nje ya Tanzania hasa hizi nchi za SADC,” ameeleza.
  
Akizungumza katika kiwanda hiki, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amesema watahakikisha wanasimamia haki za msingi za kampuni hiyo kwa sababu imewapa heshima kubwa katika Mkoa wa Pwani kutokana na kupata ajira nyingi za vijana.
  
Pamoja  na mambo mengine wajumbe wametembelea pia kiwanda cha kusindika korosho cha Biotan kilichopo wilayani Mkuranga ambapo  Katika kiwanda hiko wajumbe walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.
  
Akizungumza kiwandani hapo Bahati Mayoma ambaye ni  Mkurugenzi wa Biotan Group Limited amefafanua kampuni yao kwa kiasi kikubwa kinamilikiwa na raia kutoka Australia, ndiyo maana hata bidhaa zao zinazingatia viwango vya hali ya juu kwa kuwa wanazisafirisha katika nchi za Ulaya.
  
Ameongeza kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.

“Bidhaa zetu tunazipeleka Denmark, Sweden, Ujerumani, Australia na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Lakini kwa sasa soko letu jipya tunaangalia hizi nchi za SADC,” amesema Mayoma.

 Amesema kwamba kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka.
  

Kwa kukumbusha tu SADC ni jumuiya ya kimaendeleo ya kiuchumi inayohusisha nchi wanachama 16 ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ushelisheli, Comoro, Botswana, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Afrika Kusini, Mauritius na Namibia. Kwa mwaka huu mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utafanyika Tanzania kuanzia Agosti 17 hadi 18 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC).

KAMA UKO MWANZA - HII HAPA NJIA RAHISI YA KUSAJILI BIASHARA YAKO AU JINA LA BIASHARAKatika kuwahakikishia wajasiliamali na wawekezaji sekta ndogo na kubwa ya viwanda kwamba wanatekeleza shughuli zao kwa ufanisi na tija kwa taifa kupitia Sera inayosimamiwa na Serikali ya awamu ya tano inakuza uchumi kupitia viwanda, wakala wa  usajili wa biashara na leseni (Brela), msimu huu wa Nanenane wanamiliki banda lao la huduma kwenye maonesho hayo yenye msisimko yanayofanyika pia mkoani Mwanza katika viwanja vya Nyamhongolo wilayani Nyamagana.

Brela imeweka utaratibu mzuri ulio rahisi kwaajili usajili wa makapuni na viwanda.

ZAIDI BOFYA PLAY.

Thursday, August 8, 2019

SAVE THE CHILDREN YAADHIMISHA WIKI YA UNYONYESHAJI DUNIANI MKOA WA DODOMA

Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto la Save The Children kupitia mradi wake wa Lishe Endelevu unaolenga kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano limeadhimisha wiki ya Unyonyeshaji duniani mkoani Dodoma.


Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children yamefanyika leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma.


Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Dodoma Benety Malima alisema maadhimisho hayo ya wiki ya unyonyeshaji ni sehemu ya utekelezaji wa mradi Lishe Endelevu unaofadhiliwa na Mfuko wa Watu wa Marekani 'USAID'.


Malima alitumia fursa hiyo kuwahimiza waajiri kwenye mashirika na taasisi mbalimbali kutenga chumba maalumu kwa ajili ya akina mama kuwanyonyesha watoto wao.
Alisema siku 1000 za lishe ya mtoto zinaanzia tumboni na na kuwasisitiza akina mama wajawazito kula vyakula vyenye lishe kabla na baada ya kujifungua.

Malima alisema kwa mujibu wa takwimu za hali ya lishe kutoka taasisi ya chakula na lishe kuwa katika mikoa minne ya Dodoma, Rukwa, Iringa na Morogoro ambako shirika lao linafanya nao kazi hali ya lishe hairidhishi.

Malima aliwasisitiza wanaume kushirikiana na akina mama katika suala zima la kunyonyesha na kuongeza kuwa wakati mwingine wa baba ni chanzo wa mama kutopata maziwa kutokana na ugomvi hivyo ni vyema wanaume wakawapenda wake wao.
Aidha alisema lishe kwa wanawake wajawazito inachochea hatari ya kujifungua watoto njiti , waliodumaa au kuharibu mimba.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa alisema takwimu za hali ya ulishaji watoto wachanga na wadogo katika mkoa wa Dodoma takribani asilimia 97 ya watoto wenye umri wa miaka miwili,wananyonyeshwa maziwa ya mama, idadi ya watoto wanaoanzishiwa maziwa ya mama kwa wakati sahihi katika kipindi sahihi kisichozidi saa moja baada ya kuzaliwa ni asilimia 57.

"Idadi ya watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama pekee bila kupewa maji, vinywaji na vyakula vingine katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo baada ya kuzaliwa ni asilimia 47.7, idadi ya watoto wenye umri wa miezi 6-23 wanaolishwa chakula kinachokidhi vigezo cha ubora kiliishe ni asilimia 35.9 na idadi ta watoto wanaoanzishiwa vyakula cha nyongeza kwa wakati sahihi katika umri wa miezi 6 hadi 8 ni asilimia 85.7,'' alieleza.

Alibanisha kuwa changamoto ya matumizi ya chumvi yenye madini joto, ni asilimia 81 ndio wanatumia chumvi yenye madini joto la kutosha, mama mjamzito anatumia chumvi siyo na madini joto, hivyo afya ya mtoto inaathiriwa sana kwani anaweza kuzaliwa akiwa na udumavu wa ubongo au ulemavu wa viungo.

''Nitoe rai kwa wazazi na walezi kutafuta taarifa sahihi kuhusu unyonyeshaji unaofaa kutoka kwa mtoa huduma ya kiafya katika jamii, mtaalam wa afya kipindi cha ujauzito hili likienda sambamba na kuhudhuria kliniki mapema pindi tu mama anapojigundua ni mjamzito,'' alisema Mkurugenzi huyo.

Aliwataka akina baba kuwasindikiza wenza wao kliniki ili kuhakikisha kwamba mume/mwenza na familia wana taarifa kuhusu malengo ya unyonyshaji ili waweze kutoa msaada , pia aliwasisitiza kina mama wanaonyonyesha kuainisha msaada wa vitendo unaohitajika na kuomba msaada kutoka kwa mume/mwenza, familia na ndugu wengine ili kupata msaada.

Nao baadhi ya akina mama waliohudhuria katika maadhimisho hayo akiwemo Sikitu Damian Lyimo aliwataka akina mama wote nchini kula vyakula vyenye lishe ili kuweza kuzaa watoto wenye afya njema na akili timamu.

Aliongeza kuwa wamepata elimu ya kutosha Shirika la Save the Children hivyo watahakikisha wanaitumia ipasavyo kwa kuwa vyakula vyote vyenye lishe bora vinapatikana kijijini hapo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma. 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Dodoma Benety  Malima (mwenye tisheti nyekundu kulia) akiwa kwenye Kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children leo Agosti 7,2019 katika kijiji cha Kingale wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma.  
Zoezi la upimaji wa hali ya lishe kwa watoto wa miezi 6 hadi 59 likiendelea.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa akishuhudia mafunzo ya upishi wa chakula cha watoto kwa wanajamii hususani akina mama.

Kulia ni Mtaalamu wa afya akionesha aina mbalimbali za za vyakula lishe vinavyopatikana katika mkoa wa Dodoma.

VIDEO:- WAZIRI MKUU AONGOZA UJUMBE WA SERIKALI YA TANZANIA MAZISHI YA MKE WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI


HATIMAYE Mwili wa Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi umezikwa leo majira ya saa nane mchana nyumbani kwake, Luchelele, wilayani Nyamagama mkoani Mwanza.

 Viongozi mbalimbali wamejitokeza leo Jumatano Agosti 7,2019 katika ibada hiyo inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala.

Akiongoza ujumbe wa Serikali Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa dini na wadau mbalimbali kumuombea Professa Kilangi na familia yake kwa kuwa wanapitia katika kipindi hiki kigumu hasa ikizingatiwa kuwa mkewe ndiye aliyekuwa tulizo kwa Profesa Kilangi ambaye amekuwa mshauri mkubwa wa Serikali katika harakati mbalimbali za  Maendeleo. 

TAASISI ZILIZOSAJILIWA KAMA KAMPUNI NA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA NGO, KUANZA KUSAJILIWA UPYA MWANZA.


Erasto Ching'oro ambaye ni msemaji wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Idara Kuu Ya Maendeleo ya Jamii  amesema kuanzia KESHO Alhamisi Agosti 8, 2019 unaanza usajili wa taasisi zilizosajiliwa kama kampuni lakini zinatekeleza majukumu ya taasisi zisizo za kiserikali (NGO).

Amesema usajili huo umegawanywa katika kanda tano ili kurahisisha mchakato huo.

Ching'oro ametoa kauli mapema hii leo  katika mkutano na wandishi wa Habari kwa ajili ya kutoa taarifa ambayo imenuiwa kuwafikia wadau husika wa maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Katika Bunge la bajeti lililomalizia Juni 28, 2019 ulipitishwa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2019 uliokuwa na marekebisho ya sheria nane, zikiwemo Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (sura ya 56) na Sheria ya Makampuni (sura ya 212).

Muswada huo ambao umeshapitishwa bungeni miezi miwili iliyopita inazitaka kila asasi za kujisajili upya badala ya awali kusajiliwa na taasisi nyingine ikiwemo Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (Brela).

Msemaji huyo wa Wizara ya Afya amefunguka zaidi kwa kusema kuwa fomu za maombi ya usajili huo zitapatikana katika ukumbi maalum ulioteuliwa katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza nao wadau wa BRELA kuwepo tayari na endapo muombaji akikamilisha taratibu zake kwa ufanisi ndani ya siku 14 atakabidhiwa cheti chake cha usajili ili atekeleze majukumu yake kwa ufanisi.

Wednesday, August 7, 2019

WAZIRI MKUU AONGOZA UJUMBE WA SERIKALI YA TANZANIA MAZISHI YA MKE WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

HATIMAYE Mwili wa Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi umezikwa leo majira ya saa nane mchana nyumbani kwake, Luchelele, wilayani Nyamagama mkoani Mwanza.

 Viongozi mbalimbali wamejitokeza leo Jumatano Agosti 7,2019 katika ibada hiyo inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala.

Akiongoza ujumbe wa Serikali Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa dini na wadau mbalimbali kumuombea Professa Kilangi na familia yake kwa kuwa wanapitia katika kipindi hiki kigumu hasa ikizingatiwa kuwa mkewe ndiye aliyekuwa tulizo kwa Profesa Kilangi ambaye amekuwa mshauri mkubwa wa Serikali katika harakati mbalimbali za  Maendeleo. 

Baadhi ya viongozi wa kisiasa na kiserikali waliohudhuria ibada hiyo ni; Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally.

Natalia ambaye ni mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi alifariki Jumamosi iliyopita ya Agosti 3, 2019 saa 7 mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa akiendelea na matibabu ya ugonjwa wa kiharusi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally akitoa heshimaza mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Wilaya yaNyamagana Dkt Philis Nyimbi akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
 Akiwa ameambatana na bintiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Pia anayefuata nyuma (kijana mdogo) ni mtoto wa marehemu...Ni huzuni tupu imetawala hapa.
Pole rafiki.
 Mtoto wa kwanza wa marehemu.
Ibada ya mazishi inaendelea.
Safu ya watumishi wa Mungu.


1 THE. 5:18 SUV


Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.