Wakati
kesho (TEREHE 7/12/2012) Treni ya abiria inataraji kuanza upya safari yake
kutoka jijini Dar es salaam hadi jijini Mwanza ikiwa ni kutekeleza kwa ahadi ya
serikali kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harson Mwakyembe aliyoitoa Bungeni wakati wa kupitishwa bajeti ya
wizara yake.
Jijini
mwanza blogu hii imeshuhudia mafundi pamoja na vibarua wa shirika la Railways
wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi sehemu mbalimbali
ikiwemo zile za kupumzikia abiria huku
pia abiria wakiendelea kukata tiketi zao kwa ajili ya safari ya kwanza tangu
kusitishwa takribani miaka mitano siku ya jumapili.
Kuanza
kwa usafiri huo kumerejesha matumaini kwa wananchi wanaotumia usafiri huo hasa
kwa wafanyabiashara wanaosafiri na kusafirisha bidhaa kwa wingi kila kukicha
kutokana na gharama zake kuwa nafuu zaidi ikilinganishwa na ile ya mabasi ya
abiria ya kutoka Mwanza hadi jijini Dar es salaam.
Bofya Play kusikiliza..
Hata
hivyo changamoto imejitokeza kwa abiria watakao tumia usafiri huo wa treni kwani
sasa watalazimika kuwa na vitambulisho au hati za kusafiria, kitambulisho cha
mpiga kura au barua ya mwenyekiti wa mtaa anapotoka abiria huyo ili kusaidia
kuweka kumbukumbu sahihi kwa abiria waliosafiri kwa siku husika kutambulika
pindi ajali au tatizo lolote
linapotokea.
Njia za treni na mafundi wake.
Mafundi.
Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.
Vibarua wa shirika la Railways wakifanya maandalizi ya mwisho kwenye njia za treni na usafi.
Mafundi wapaka rangi wakilikarabati eneo la kuketi abiria katika maandalizi ya mwisho.
Nao wadau wa usafirishaji barabarani kwa pikipiki maarufu kama bodaboda nao tayari wameanza kujongea eneo hili ambalo si muda mrefu litarejea kwenye shamrashamra zake kama siku za nyuma ilikuwa mishemishe mchana hadi usiku.