|
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando(aliyekaa katikati) akiongea na wandishi wa habari (hapo pichani) wakati wa droo kubwa ya mwisho ya kumtafuta mshindi wa shilingi million 50 wa promosheni ya Amka millionea ambapo bwana Layakal Akbar Thawer mkazi wa Dar es salaam aliibuka mshindi wa promosheni hiyo. Kushoto ni mshindi wa million 15 wa promosheni ya Amka milionea bwana Juma Ibrahim Hiza mkazi wa Dar es Saalam na kulia ni mshindi mwingine wa shilingi milioni 15 Bwana Adnan Ayub Khan mfanyabiashara Simiyu. |
Airtel yatangaza mshindi wa million 50 wa promosheni ya Amka millionea
· Zaidi ya washindi 1458 wazawadiwa pesa taslimu zenye thamaniya shilingi million 626 Hadi mwisho wa promosheni hii
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imechezesha droo ya mwisho ya promosheni ya Amka millionea na kumzawadia mshindi wa droo hiyo kitita cha shilingi million 50.
Droo hiyo kubwa na ya mwisho ilifanyika katika makao makuu ya Airtel morocco na kushuhudia na waandishi wa habari ambapo mkazi wa Kariakoo Dar es Salaam Bwana Layakal Akbar Thawer mwenye umri wa 60 mafanyabiashara wa duka la rangi aliibuka kuwa mshindi wa millioni 50 na kutangazwa rasmi kuwa mshindi.
Akiongea wakati wa droo hiyo, Mkuu wa kitengo cha Masoko wa Airtel Levi Nyakundi alisema, Mpaka sasa Airtel kwa kupitia promosheni ya Amka millionea imewazawadia watanzania na wateja wengi nchini. leo tunashuhudia bwana Akbar akiibuka kuwa mshindi wa pesa taslimu shilingi million 50 kupitia promosheni hii ya Amka millionea na Airtel.
Hii inathibitisha thamira yetu ya kutuoa huduma bora na bei nafuu huku tukiendelea kuwazawadia watanzania na wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali ikiwemo hii ya Amka millionea
Tunaahiidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuhakikisha tunawafikia watanzania wengi zaidi, mpaka sasa kwa kupitia huduma ya Airtel yatosha wengi wamepata unafuu wa gharama za mawasiliano na kuwezeshwa kupiga simu kwenda mitandao yote nchini na kushuhudia kuwa kweli Airtel yatosha.
Tunaamini kwa kuendelea kuongeza ubunifu katika huduma zetu na kuwazawadia wateja wetu kwa kupitia promosheni mbalimbali pamoja na huduma bora zikiwemo za kibenki kupitia Airtel money na huduma ya internet ya kasi zaidi ya 3.75G wateja wataendelea kupata suluhusho la mawasiliano na za kimtandao zilizo bora , za uhakika na gharama nafuu aliongeza Nyakundi.
Akiongea kwa njia ya simu mshindi wa shilling million 50 bwana Layakal Akbar Thawer alisema “ mimi nimekuwa mteja wa Airtel kwa miaka 7 sasa na nafurahia huduma zao, napenda kuwambia watanzania washiriki promosheni hizi nao wananafasi ya kuibuka washindi.
Promosheni ya Amka milionea ilizinduliwa rasmi mwenzi December mwaka jana na kuongezewa muda wake mwenzi machi mwaka huu, mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi million 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.
Mshindi mwingine wa shilingi million 50 alipatikana na kuzawadia mwenzi watatu naye ni Mwalimu wa shule ya msingi na mkazi wa manyara kiteto bwana Grayson Safieli Kabora , huku washindi wa shilingi million 15 wakiwa ni pamoja na Juma Ibrahim Hamza umri wa miaka 30 na mkazi wa kawe Dar es Saalam na Adrian Ayub khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara Simiyu