ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 4, 2013

PROF. LIPUMBA AONGOZA MIKUTANO YA NDANI MJADALA KWA MAENDELEO YA WOTE MWANZA.


Mwenyekiti wa chama cha CUF Ibrahimu Lipumba akiwasilisha mada mbalimbali kwa wadau wapatao130 kutoka makundi mbalimbali ya jamii taasisi za kiserikal, viongozi wa dini, mashirika na vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo.

Mkutano huu umekuja ukiwa na maudhui ya kuimarisha mfumo wa demokrasia ndani ya vyama vya siasa na kukuza mijadala baina ya vyma, wapiga kura na taasisi mbalimbali za kijamii.

Mada zilizowasilishwa na kujadiliwa ni pamoja na :
1.Sekta ya madini na maendeleo ya wananchi wa mikoa ya ukanda wa ziwa na mchangowake katika madnelao ya taifa.

2Changamoto zinazowakabili wakulima wadogo wadogo katika sekta ya kilimo cha pamba, mazao ya chakula na sekta yaufugaji katika mkoa wa Mwanza.

3. Matatizo yanayoikabili sekta ya uvuvi na matumizi sahihi ya ziwa Victoria kwa maendeleo ya wananchi wamikoa ya kanda ya ziwa.

4.Rasilimali ya maendeleo ya watu elimu ya awali, msingi na sekondari pamoja na huduma za Afya. 

Washiriki wakifuatilia kwa makini mada ziwasilishwazo.

Washiriki eneo jingine kusanyikoni.

Umakini kwa washiriki huku wakitafakari mada.

pia washiriki walipewa fursa kuwasilisha michango yao kuishauri serikali nini kifanyike ili kuboresha huduma mbalimbali na utendaji kazi kwa jamii.

Mwenyekiti wa chama cha CUF Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kujibu maswali na kuelezea ujumbe wa mkutano huo.

Engo nyingine.

Mkutano huu umefanyika ndani ya ukumbi wa JB Belmount jijini Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.