BAADA ya kutamba na wimbo wake wa Nai Nai Msanii anaekuja juu kwa kasi na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz anataraji kuzindua Single yake mpya ya Baadae katika ukumbi wa Club Bilcanas jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mtandao huu wa Kijamii, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika nay a kuvutia.
Mubenga amesema Ommy Dimpozy anataraji kuzindua wimbo huo aliofanyiwa kazi na Mwandaaji wa muziki Man Water huku spoting ya wimbo huo ikifanywa na mwanadada Angel.
Aidha Mubenga amesema Dimpoz atasindikizwa na wakali wa Bongo Fleva, Diamond, Ben Pol pamoja na msanii Alawi Jr pamoja na Ma DJ wakali wa Bongo kutoka kundi la Super Deejayz.
Tayari Dimpoz ameshaanza kuwasikilizisha wimbo huo baadi ya mashabiki wake wa mikoa ya Mwanza na Moshi wakati wa Ziara ya Wakali wa Kili Music Awartd 2012 inayoendelea ambapo leo atakuwa Mbeya chini ya Bia ya Kilimanjaro.
“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva make tayari kwa singo hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya redio na kumbi za burudani nchini kote baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
Mungenga amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club ya Bilcanaz katikati ya jiji la Dar es Salaam jumapili.