ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 13, 2016

"KAMA UNAMPANGO WA KUACHANA NA MWENZI WAKO SIKUSHAURI" LEMUTUZ AFUNGUKA NDANI YA KIKWETU YA JEMBE FM NATURE, OMMY DIMPOZ NDANI.

Natty E Brand na DvJ Benny Ndiyo wahusika wakuu wa kipindi cha KIKWETU ndani ya Jembe Fm Mwanza.
MAELEZO YA PICHA NYINGINE YAJA.......





 


Friday, February 12, 2016

HAPPY VALENTINES YOU ALL.

He!! Ndugu dam dam hawapendani? Msifanye hivyooo.
Ijumaa kama hii tukielekea siku kuu ya wapendanao duniani, Tarehe 14FEB2016 Enyi marafiki ndugu, jirani, wapenzi, waungwana tunaotakiana mema basi naomba leo GSengo Blog ipambwe na mwanangu kwa mdogo wangu anayeitwa Rainha D. Simba. 

Happy Valentines to you all.

HIKI NDICHO ALICHOANDIKA MHE. PROF JAY MARA BAADA YA KUFUTWA KESI YA UCHAGUZI DHIDI YAKE.

UKWELI UNA TABIA YA KUSHINDA SIKU ZOTE!!! Ndugu zangu wote wapenda HAKI na UKWELI napenda kuwatangazia rasmi kuwa ile kesi ya kupinga matokeo yangu ya ubunge wa jimbo la Mikumi IMEFUTWA RASMI baada ya mlalamikaji JONAS E. NKYA kushindwa kulipa gharama za dhamana ya kesi sh milioni 15 ndani ya siku 14 kama alivyotakiwa na mahakama kuu.

Hivyo basi mheshimiwa JAJI KITUTSI ameifutilia mbali na kumtaka mlalamikaji JONAS alipe na gharama zote zilizotokana na shauri hilo, Heshima kubwa sana kwa wakili Msomi sana TUNDU LISSU na Timu yake yote!!!
NB>Mtumishi wenu JOSEPH LEONARD HAULE Ndie mbunge halali wa jimbo la MIKUMI 2015-2020, Nawaomba sana ushirikiano zaidi na zaidi ili tuweze kuijenga MIKUMI yetu tunayoitaka yenye maendeleo kwa watu wote! ASANTENI SANA... MUNGU AWABARIKI SANA! !!

UFISADI WA SHILINGI MILIONI 20 WAZUA TAFRANI MSIKITINI.

Waumini wa dini ya Kiislam wakizozana nje ya Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam katika swala ya Ijumaa leo mchana, baada ya kutokea tafrani ya waumini hao dhidi ya viongozi wao ambao wanatuhumiwa kutafuna fedha zaidi ya sh.milioni 20 walizochanga kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.
Muumini wa Msikiti huo, Mbarouk Mohamed Makame (kushoto), akizungumza kuhusu fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao. Kulia ni mmoja wa wazee wa msikiti huo, Mzee Selasela.
 Mzee Selasela akionesha dari la msikiti huo lililochakaa ambapo fedha hizo zinazodaiwa kutumiwa vibaya na viongozi wao zingesaidia kuufanyia ukarabati.
Hapa mzee Selasela akionesha uchakavu wa kapeti.
Hapa akionesha vyoo vilivyo chakaa vya msikiti huo.
Mwonekano wa vyoo vya msikiti huo vinavyotumika.
Waumini wakiwa nje ya msikiti huo wengine wakiswali.
Waumini wakiwa mbele ya vibanda vya biashara vilivyopo nje ya msikiti huo.
Watoto wa shule ya awali katika msikiti huo wakiwa na mwalimu wao (kulia)

Na Dotto Mwaibale

TAFRANI kubwa imezuka katika Msikiti wa Masjidi Pelapela uliopo eneo la Mtakuja Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya viongozi wa msikiti huo kudaiwa kutafuna zaidi ya sh.milioni 20.

Fedha hizo imeelezwa kuwa  zilichangwa na waumini wa msikiti huo kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya baada ya unaotumika kuchakaa.

Imamu mkuu wa msikiti huo aliyetajwa kwa jina la Hamidu Mitanga alilazimika kutoweka ndani ya msikiti huo baada ya kuendesha swala ya Ijumaa iliyofanyika jana mchana kutokana na waumini kuwa na jaziba kufuatia imamu huyo kutamuka kuwa hakuhitaji kuulizwa maswali yoyote kuhusu upotevu wa fedha hizo na kuwa uongozi uliopo utaendelea kuwepo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msikitini hapo Dar es Salaam leo mchana wakati wa swala ya Ijumaa mmoja wa waumini wa msikiti huo Mbarouk Mohamed Makame alikiri kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za waumini zilizochangwa kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mpya.

"Suala la upotevu wa fedha hizo lipo na limeleta changamoto kubwa kwa waumini na kusababisha kuwepo kwa makundi mawili moja likiwa lile linalolalamikiwa kutafuna fedha hizo na lile linalotaka fedha hizo zitolewe maelezo zilipo" alisema Mzee Makame.

Mzee wa msikiti huo na Mwenyekiti wa Kamati ya watu 10 Saidi Ngubi alisema fedha zinazoshindwa kutolewa maelezo ya matumizi yake na viongozi wa msikiti huo zilitokana na mradi wa maji na michango ya waumini.

"Mimi ndiye niliyeanza kuuliza matumizi ya fedha hizo lakini viongozi hao wakawa hawana majibu na badala yake waliivunja kamati yetu na kuchagua nyingine jambo lililoleta sintofahamu" alisema Ngubi.

Imamu mkuu wa msikiti huo Hamidu Mitanda alisema fedha hizo zilitumika kwa ajili ya mchakato mzima wa kupata umiliki wa kiwanja ulipo msikiti huo na michoro ya ujenzi wa msikiti mpya na kuwa yeye ndiye aliyeanzisha mpango wa kupata msikiti ulio bora na si bora msikiti.

"Binafsi sina shida na cheo hiki cha Uimamu kwani nina shughuli zangu nyingi mkitaka kuniondoa fuateni taratibu kama zili zilizoniweka madarakani na sisi kama viongozi dhamira yetu ni kuwa na msikiti uliobora wa ghorofa na si bora msikiti" alisema Mitanga.

Mitanga alisema chokochoko hizo zilianza tangu mwaka 2007 ambapo tulikubaliana kila muumini kati ya waumini 205 achangie sh.5000 za ujenzi lakini waliochangia walikuwa ni waumini wachache ambapo zilipatikana sh.milioni moja tu.

Imamu huyo alisema uongozi unaoendesha msikiti huo hauko tayari kuachia madaraka kwa tuhuma hizo ambazo hazina ukweli alizodai zinachochewa na baadhi ya waumini.

BAADHI YA WAFANYAKAZI WA TRL WAFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Shirika la Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwafikishwa  katika  mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Dalaam tayari kwa kusomewa mashitaka 9 yanayo wakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. (PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA)

Baadhi wa wafanyakazi wa Kampuni ya Reli nchini Tanzania (TRL), wakiwa katika chumba cha mahakama ya Kisutu tayari kwa kusomewa mashitaka 9 yanayo wakabili likiwemo la  tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, wapili kulia ni aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika hilo,  Mhandisi Kapallo Kisamfu

TEKNO NA SEYI SHAY WAFANYA ZIARA JEMBE FM KUELEKEA MKESHA WA KUIKARIBISHA VALENTINES 13FEB 2016 AT JEMBE BEACH MWANZA.

Mkali wa muziki toka nchini Nigeria Tekno anayetamba na ngoma yake kali 'Duro', bigger than the rest and least of more to come akiwa katika studio za Jembe Fm Mwanza tayari kwa mahojiano na kituo hicho hii leo mchana.
Seyi Shay wamjua huyu ni mkali mwingine wa muziki toka nchini Nigeria akiwa katika studio za Jembe Fm Mwanza tayari kwa mahojiano na kituo hicho hii leo mchana.
Mbaba VC on the mic.
Tekno amekana kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi na ..........yule wa Bongo.SAUTI YA ENTERVIEW KUKUJIA HIVI PUNDE.


Nigerian singer, Seyi Shay ambaye tayari keshatua jijini Mwanza nchini Tanzania hapa akizungumzia juu ya performance yake ya kimalavidavi itakayofanyika kesho tarehe 13Feb2016 ikijulikana kama Muzika Festival akitumbuiza pamoja na mkali mwingine kutoka nchini Nigeria Tekno Miles na kutoka Tanzania ni Sir Juma Nature, Ommy Dimpoz, na wengine kibao eneo la tukio ni Jembe Beach.
Pia Seyi alipata nafasi ya kufunguka zaidi kuhusu album yake mpya ya sasa ‘Seyi Or Shay’ and her upcoming performance in the country.
Kutoka Jembe DjZ Deejay K-Flip akiuliza jambo kwa hewa.
Prizenta wa Jembe Fm Bonz (R) na Mbaba Vc (L).
Tekno akishow love na Jembe DjZ Criss The Dj.
Tekno si alilianzishaaaaaa......ikawa balaaaaa
Wacha waungwana wajiunge naye......Wayaaaaaaaa!!!!!
Mzigo woooote tisa 10 Jumamosi hii at Jembe Beach Resort Mwanza.
Upete (R) na wakishow Love na Tekno ndani ya studio za Jembe Fm Mwanza.
Seyi Shay
Tekno Miles
Gsengo Blog ikifanya yake.
Ha...ha..haaaaa!!
Team Jemba iki-show Love na Seyi Shay.
Tekno na Deeyjay K-flip 
Mkuu wa Production Oxy Okeleky akipata U-foto na Tekno.
"This is Tekno" Gsengo 
Pale penyewe.....
We.
Kuna kitu wakiteta....!!
Kutoka anga hizi...
Maandalizi ya selfie hapa zikidilitiwa pix ili kupata space kwa fONi.

MHE. LUHAGA MPINA VUUUUP HADI KITUO CHA AFYA FUONI KIBONDENI.

Kituo cha Afya kilioko Fuoni Kibondeni ambacho kilitembelewa na Mhe Luhaga Mpina katika Jimbo la Dimani kikiwa ni moja ya kero kwa Wananchi wa kituo hicho kwa kudai kiko mbali na njia yake kuwa mbaya na shinda kufika Wananchi kupata huduma za afya kituoni hapo na kumuomba Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mizingira kuwafanyia utaratibu wa kuwatengenezea barabara hiyi kuwa rahisi kufika Wananchu kupata huduma za Afya na kupatiwa vifaa kwa ajili ya kituo hicho, Kikiwa na Hudumna zote za Uzazi kulaza waginjwa na jengo la kuhifadhia maiti.Kituo hicho kilizinduliwa na Aliyekuwa Waziri Kiongozi Mstaaf Mhe Shamsi Vuai Nahodha mwaka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe, Luhaga Mpina akitembelea kituo hicho na kupata maelezo kutoka kwa Daktari Dhamani Ndg Said Amour wakati alipofika kituoni hapo akiwa katika ziara yake.

Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira. Mhe Luhaga Mpina wakiwa katika chumba cha kuzalia Wakinamama katika Kituo hicho lakini hakifanyi kazi kwa kukosa Vifaa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira akitembelea jengo la Kituo cha Afya Fuoni Kibondeni Zanzibar.
 Naibu Waziri akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed, alipofika kukitembelea kituo hicho cha Afya na Mbunge wa Jimbo hilo la Dimani Mhe Hafidh Ali Tahir.

Mhe Luhaga Mpina akipata maelezo alipotembelea jengo la kuhifadhia maiti la kituo hicho cha Afya Fuani Kibondeni.
  Jengo la kuhifadhia maiti la kituo hicho cha Fuoni Kibondeni.
Maofisa wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakiwa katika msafara wa Mhe Naibu Waziri 
Mkurugenzi Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Ndg Bakari Rajab akijitambulisha kwa Wananchi wa Jimbo la Dimani wakati wa ziara ya Naibu Waziri katika Jimbo hilo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Dimani alipofika kuwatembelea na kuagalia Kituo chao cha Afya kuona namna ya kukisaidia Kituo hicho kwa ajili ya kuimarisha utowaji wake wa huduza za Afya kwa Wananchi wa Jimbo hilo na jirani na kuahidi kukiimarisha  kwa kukipatia baadhi ya vifaa kuweza kutowa huduma.kwa ufanisi zaidi. 
Baadhi ya Wananchi wa Jimbo la Dimani wakimsikiliza Naibu Waziri alipofika kuwatembelea wakati wa ziara yake Zanzibar.
Afisa wa Wizara ya Afya Zanzibar Ndg Fadhil Mohammed, akitowa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina wakati alipofika katika Skuli ya Msingi ya Fuoni Kitogani ikiwa ni moja ya Ahadi za Rais Mstaaf wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete alipofika katika Skuli hiyo na kutowa ahadi ya kumalizia Ujenzi wa Madarasa ya Skuli hiyo. 
Mbunge wa Jimbo la Dimani Mhe Hafidh Ali akitowa maelezo ya Jimbo hilo akiwa na ramani ya Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA ya uchimbaji wa Visima viwili ambavyo tayari vimeshachimbwa na kutoa huduma kwa Wananchi wa maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akitowa maelezo kwa Wananchi wa Jimbo la Dimani wa Kamati ya Skuli ya Kitongani Fuoni baada ya kupokea maelezo yao ya Ahadi ya Rais Mstaaf  wa Tanzania Dk JK alipofika katika Skuli hiyo, wakati wa ziara yake Zanzibar. Naibu Waziri amesema atazishughulikia kero zao hizo, baada ya kusema kero zao ni barabara kisima kwa ajili ya skuli hiyo na kituo cha afya. 
Afisa wa Mamlaka ya Maji Zanzibar akimuonesha sehemu ya eneo hilo lililochimbwa visima viwili kwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo hilo 
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.
Zanzinews.com