Mwandishi
Mathias Canal akionyesha cheti cha ndoa aliyoifunga Jumamosi tarehe 18 Agosti
2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo
Farasi Jijini Dar es salaam na mkewe Bi Elizabeth Chagamba.
Mwandishi Mathias Canal na mkewe Bi Elizabeth Chagamba (walioketi)
pamoja na watumishi wa Wizara ya Kilimo wakiongozwa na waziri wa wizara hiyo
Mhe Dkt Charles Tizeba, Watumishi kutoka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) wakati wa hafla ya jioni baada ya ibada ya ndoa Takatifu tarehe 18
Agosti 2018 katika eneo la Urafiki Social Hall Ukumbi wa Nyangumi Jijini Dar es
salaam.
Mwandishi
Mathias Canal akivishwa Pete na mkewe Bi Elizabeth Chagamba wakati wa ibada ya
ndoa Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania
(KKKT) usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Mwandishi
Mathias Canal akimtambulisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji
J. Mtaturu wakati wa tafrija iliyofanyika eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa
Nyangumi baada ya ibada ya ndoa Takatifu iliyofanyika
katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) usharika wa Mabibo
Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Bwana harusi Mathias Canal na Bi harusi
Elizabeth Chagamba wakicheza wimbo maalumu ulioimbwa na msanii wa midondoko ya
(RnB) Elias Barnabas maarufu Barnaba Boy Classic wakati wa tafrija iliyofanyika
eneo la Urafiki Social Hall ukumbi wa Nyangumi baada ya ibada ya ndoa
Takatifu iliyofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT)
usharika wa Mabibo Farasi jijini Dar es salaam tarehe 18 Agosti 2018.
Na
Mwandishi Wetu, Wazohuru Blog
Mwandishi na mchambuzi wa Habari nchini
Tanzania ambaye ni Afisa Habari Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula
(NFRA)-Wizara ya kilimo ameingia kwenye historia ya vijana wachache waliofanya
maamuzi ya busara na tija katika mustakabali wa maisha mema katika jamii kwa
kufunga ndoa Takatifu.
Ibada ya ndoa Takatifu ilifanyika siku ya
jumamosi tarehe 18 Agosti 2018 kuanzia majira ya saa sita na nusu (6:30) mchana
mpaka saa nane na nusu (8:30) mchana katika kanisa la Kiinjili La Kilutheli
Tanzania-Usharika wa Mabibo Farasi Jijini Dar as salaam.
Mathias Canal amefunga ndoa na Binti
mstaarabu, wenye nidhamu na busara huku akiwa mcha Mungu Bi Elizabeth Chagamba
mzaliwa wa Tanga ambaye kihistoria tangu kufahamiana urafiki wao umedumu kwa
takribani miaka sita mpaka kufikia maamuzi ya kufunga ndoa Takatifu.
Ibada hiyo ya ndoa Takatifu iliendeshwa na
Mchungaji Remmya Chuma kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi
ya Mashariki ya Pwani Usharika wa Kawe Jijini Dar es salaam ambapo aliwataka
Bwana Harusi Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kuishi kwa kuzingatia
misingi ya ndoa na agano Takatifu baina yao na Mungu kwani ndoa yao
imeshuhudiwa na watu duniani lakini shahidi pekee mwenye maono zaidi ya ndoa
hiyo ni Mungu mwenyewe.
Mchungaji Chuma aliwakumbusha waumini
wengine katika ibada hiyo kumshukuru Mungu kwa kila hatua wanazopita huku
akiwasihi waumini hususani vijana ambao hawajafunga ndoa Takatifu kuingia
katika tendo hilo muhimu machoni pa wanadamu na Mungu wa Mbinguni. Na kuongeza
kwa kunukuu Kitabu cha Mathayo 19:5 kisemacho, "Kwa sababu hiyo mtu
atamwacha Baba na Mama yake ataambatana na Mkewe na hao wawili watakuwa mwili
mmoja"
Mara baada ya Ndoa Takatifu kati ya Afisa
Habari NFRA Ndg Mathias Canal na Bi Elizabeth Chagamba kukamilika kanisani
ilihudhuriwa na tafrija fupi iliyofanyika katika eneo la Urafiki Social Hall
katika ukumbi wa Nyangumi ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na mamia ya wananchi
huku viongozi mbalimbali wa Chama na serikali wakihudhuria.
Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi ndoa
hiyo ilihudhuriwa na Timu ya uenezi kutoka Chama Cha Mapinduzi
Taifa, Mohammed Alliyan Kaimu Katibu wa Idara ya oganaizesheni na
uhusiano wa kimataifa Umoja wa Vijana (UVCCM) Makao makuu pamoja na
wasaidizi wa Mwenyekiti na Katibu Mkuu UVCCM Taifa.
Kwa upande wa serikali hafla hiyo
ilihudhuriwa na Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ambaye katika
salamu alizozitoa kwa niaba ya Wizara yake alisema kuwa Ndoa ni muunganiko wa
kiagano wa kudumu kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja wenye kuishi na kuwa
mume na mke. Neno agano ni neno muhimu sana kwa sababu agano ni patano la
milele ambaye shahidi yake ni Mungu mwenyewe wala si mwanadamu hivyo kuwataka
sana ndoa hao kuwa waaminifu milele.
Aidha, alitaja umahiri katika utendaji
unaofanywa na wasaidizi wake akiwemo Mathias Canal pamoja na mwenzake Innocent
Masaka kuwa ni wadogo sana kwake kiumri lakini wamekuwa msaada mkubwa katika
kutekeleza majukumu ya serikali yakiwemo na yale ya Chama cha Mapinduzi.
Katika hafla hiyo Mhe Dkt Tizeba alisema
kuwa Fungate ni jambo muhimu baada ya ndoa Takatifu hivyo akatoa ofa maalumu
kwa maharusi hao kwenda mapumzikoni Mjini Unguja-Zanzibar huku akisema kuwa
gharama zote za siku tano atagharamia yeye. Pia Dkt Tizeba ametoa ofa ya
mapumziko ya siku tano kwa Ndg Mathias Canal ambaye muda wake wa mapumziko
ulikuwa umemalizika hivyo kuendelea na mapumziko ya siku tano.
Tayari Mathias Canal na Mkewe Bi Elizabeth
Chagamba wamewasili Mjini Unguja-Zanzibar ambapo katika mapumziko hayo
wamesafiri na wapambe 10 waliohudumu katika sherehe yao (Maids) ili kufurahi
kwa pamoja katika mapumziko hayo.